Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,942
- 6,860
You have no idea how imperative and critical what you are pointing out is.
Tanzania hakuna records (hata hati ya Muungano imepotea). Rekodi zenyewe ndio hizi za simulizi simulizi. Nina hakika mbeleni huko kuna vizazi vitakuja kutafiti haya tunayoandika humu (thanks to Invisible and cohort) in order to piece together our history. Sasa wakikuta mwandishi mmoja ambae ana hold sway kubwa sana anasema vitu oulandish vya ajabu halafu hawi called out tutaoneka kizazi chote ma heathen!
Ila nichaoomba kukuuliza sio kuhusu mtu mmoja, ni kuhusu jamii ya Watanzania kwa ujumla.
Hivi unadhani ni kwa nini FMES na uongo wake wote huu bado an garner support ya watu wanaosubiri dataz zake? I mean kuna watu kabla ya kuchangia kitu huwa wanaandika "FMES njoo utupe dataz kwenye hii mada..." na vitu kama hivyo.
Ni kwamba watu hawaijui Bongo na siasa kiasi hicho, au ? Fundi, hear me out on this, Field Marshall anasema, kwa mfano, mafao ya safari za nje za viongozi kama vile kwenda kutibiwa yamo kwenye Katiba! Hivi unahitaji kuwa constitutional scholar kugutuka kwamba safari za Rais mstaafu zitaingiaje kwenye Katiba?
Au ni watu kuhofia hivyo vigezo vya ukaribu na Wakubwa, kusaidiwa kubatiziwa watoto wake na kina Asha Migiro, kama anavyodai. Lakini, mmmh! Angalia hili, anasema anakutana na kina Rupia na Mke wake wanampa dataz, halafu anawaalika nao wajiunge JF. Kwa maneno mengine, Rupia na Mkewe wanajua kwamba analeta hizo data JF. Think about it, Rupia na Mkewe wakijua kwamba huyu Mja tukimpa dataz anapeleka kwenye public forum halafu anatutaja kwamba ni sisi tumempa unadhani kweli, Fundi, huyo Rupia na Mke wake na kina Migiro na wengine ni wapumbavu kiasi gani mpaka wawe wanaendelea kumpa FMES dataz? Au, kwenye sakata la Ballali akasema ameongea na dada yake mjane, na akaonyesha anataka privacy yake. Lakini akaendelea kuja na dataz kutoka kwa hao hao wanaomwambia wanataka privacy halafu anawaanika hapa, na saa nyingine anawachana na kuwachana. Ina maana hawezi tena kurudi kwa hao Wakubwa kuchukua dataz kwa sababu baadae anawatandika shutuma na kuwaanika, sasa watakuwa vipi kila siku wamuibie siri za serikali ? Kiongozi hawezi kuwa mjinga kiasi hicho kumpa dataz mtu kama FMES, hata awe karibu nae kivipi, hata awe Mama wa Ubatizo wa wanae, hata awe baba yake mzazi.
Sasa kwanini Umma unashindwa kuona kwamba FMES anatengeneza data mwenyewe?
Eti Katiba inasema viongozi wakatibiwe nje...! How preposterous is that.
Mimi naamini wako wengine, kwa lugha ya mtaani, wanamsanif! They can't be for real!!!
Kuna wakati ( alipokuwa akiandamwa Masha) nilimshauri kuwa he (kama ni he) is not doing them any favours kwa kusema kuweka wazi ukaribu wake. Hakunielewa. Akadai namuonea wivu! Mtu ambae hata simjui!
Sasa amekuja na hilo la katiba! Worse still ( kwa mtazamo wangu) ni hapo anaposema yeye ana facts on the ground kwa hiyo tuziamini kuliko hiyo Act ambayo anakiri hajaisoma! Lord have mercy!
Lakini huu ndiyo uzuri wa www. It is a jungle! Enter at your own risk.
Amandla........ Boss!
Juha Fundi Mchundo!