Mishahara ya viongozi wa Tanzania

1.
Mkuu Mndundu,
Humu jamvini kuna watu wamejenga kitabia cha kutaka kuaminiwa kwa kila jambo ili mradi kasema yeye. Humu jamvini wengi hatufahamiani kwa hiyo mimi nikisema hii ishu niliambiwa na Mheshimiwa jana hatuna namna ya kuthibitisha. Kuna wachache wenye ujasiri wa kuweka majina yao na hao tutawaamini kutokana na kujua nafasi yao, ingawa ukweli ni kuwa hata hao hatuna uhakika nao maana watu wanaweza kutumia jina lolote.
Kwa bahati mbaya, inaelekea utomasi haukubaliwi na baadhi yetu kiasi kwamba ukihoji wanachokiita dataz basi utatafutwa hata huko ulikojificha, hata kama ni Harlem kwa Clinton.

Hapa fourm ni mahali pa kuelimishana na kuhabarishana, sasa kama hatuna uhakika na habari basi ni kutafuta ukweli kwanza badala ya kurusha maneno ya mitaani, na kama huna ukweli dawa ni kunyamaza kuwaachie wenye ukweli maana siku zote hwua wapo, ila wanaogopeshwa na hivi vitisho vyenu na mnaishia kuharibu mijadala tu, kwa sababu kwenye hii topic sijaona mwenye kujaribu kuleta ukweli zaidi ya ule nilioutoa, sijaona mwenye facts au sheria, badala yake naona maneno mengi yasiyokuwa na ukweli, kama una ukweli zaidi uweke then unawez akuwa na right ya kudai umedanganywa.

2.
Tofauti katika hii ishu ni simpo. Kuna mmoja amesema yeye anajua stahili za viongozi wastaafu kwa sababu yu karibu nao! Huyu muungwana anafikia hatua ya kusema kuwa hana hata haja ya kusoma waraka wa katiba ( anajaribu ku'cover all bases' maana kitu kama hicho hakipo) maana yeye anayaona. Anachosahau ni kuwa si kila kitendachwo ni halali au kimeidhinishwa. Mengi yanafanywa kwa kuoneana aibu au kuheshimiana tuu lakini hatuwezi hata siku moja tukasema ni stahili (Kwa mfano leo wajane wa viongozi wetu wanaendelea kutunzwa ingawa sidhani kama kuna sheria inayosema kuwa hiyo ni haki yao).Kuna sheria inayoongoza stahili za mafao za viongozi wastaafu na ni hii peke yake ambayo inaainisha mafao ya haki ya hawa wakuu wetu na si kingine. Mimi nimeisoma kitambo lakini uwezo wa kuitundika humu ndani sinao. Nimeyasema ninayoyakumbuka lakini kama kuna mtu anajua kuwa sheria inasema tofauti I stand to be corrected. Ninachokataa ni huu ubabe wa kulazimishana na inaposhindikana kutumia personal attacks ambazo hazina msingi maana huyo anayenidhania ndiye, siye. Ni haki yangu ya msingi kubakia anonymous kama ilivyo kwa mchangiaji yeyote. Na ni haki yangu ya msingi kupinga hoja au kauli ambayo naona haijakaa sawa. Ninachotarajia ni kuwa nitajibiwa kwa lugha ya kuheshimiana ( hata katika utani) maana kufanya vinginevyo kutondoa maudhui ya jamvi hili na kulifanya sehemu ya michapo. Mbaya zaidi itawafanya hata wale wenye mawazo yanayopingana na wengi wetu kuchelea kuyaweka humu kwa kuhofia hizo lugha za ubabe na kejeli!

Amandla........

Yanayotendwa yote kwa wastaafu hupatikana idara ya utumishi, nimesema kuwa wasaidizi wakuu wa wastaafu ni trined people wanajua kuwa zama hizi sio za kupindisha sheria tena, kama kawaida maneno mengi ukweli hakuna, mimi ndiye niliyesema kuwa sijawahi kuisoma katiba inasema nini kuhusiana na mafao ya marais wastaaafu, na mawaziri wakuu, lakini nimliyoyaona nimeyakwea hapa wazi,

Kama kuna mjane anyehudumiwa sasa hivi ni Mama Maria tu, na yeye ninaamini ni under special order kutoka kwa the sitting president, lakini pia kuna wakati under Mkapa, na yeye aliachwa nje mpaka walinzi kule Butiama waliondolewa, otherwise sidhani kama bongo tuna sheria ya kuwafaa wajane, lakini mashirika ya umma huwa yana hiyo kitu, director mpya anaweza kumaua hilo ninasema hivyo kwa sababu nimeona sana, kwa mfano BOT, Sigara, nimeona wastaafu wakipewa special treatment na the sitting directors,

Ukiuliza kwa ustaarabu nitakujibu kwa ustaarabu, lakini ukileta za kuleta nitakupa hizo hizo, hapa JF wako members wengi sana hapa tunakata ishus bila noma, ila nyinyi wawili ndio mmeamua mnataka a showdown mimi sina tatizo kwa sababu nimeona wengi sana hapa kama nyinyi, lakini my standing haiwezi kubadilishwa hata siku moja na msimamow angu ni ule ule, uamuzi ni wenu kusuka au kunyoa,

Mada imetolewa nimetoa maoni yuangu kwa sababu nmi haki yangu, ni haki ya kila mtu hapa JF kuni-challenge with facts kuliko zangu na ni haki ya kila member hapa kuni-challenge na ukweli zaidi ya wangu, lakini sio tatizo langu watu kuwa na ego finyu au insecure na hoja zao zisizo na facts wala ukweli, logic sio uwkeli it just logic.

Ninarudia tena kuwa nimeweka maoni yangu on mafao ya viongozi as I know binafsi, sasa kama una ukweli zaidi uweke hapa badala ya maneno mengi sana yasiyohusu topic kabisaa!

Ahsante Mkuu!
 
Na kwa heshima kwa wengi ambao malumbano kama haya yanawachefua, mimi naishia hapa. Niliyotaka kusema nimeyasema na sina haja ya kuendeleza ubishi usio wa msingi nje ya mada inayowa'interest' wengi.

I am out of here. For real.

Low Class Fundi Mchundo.
 
1.
Kiingereza, bwana mdogo, kiingereza. Ulizia kwanza kabla ya kupandisha munkhari! Flatter sio tusi. Sasa kama si mshari unataka nini nikutafute kwenye real life? Ili iwaje?

Kiingereza? Kiko wapi? Unitafute ili tuyamalize maana inawasumbua sana watu hapa JF malumbano yasiyo na kichwa wala miguu, wewe na ndugu yako mbona tukikutana hamsemi haya maneno yenu mengi ya chuki mnasubiri kwenye forum, ndio mankuwa vijogoo ndio maana ninakupa nafasi wewe na mwenzako, siwaogopi tukutane tumalize mambo, halafu tutakuja hapa tunaheshimiana, au?

2.
Haya, kumbe haunijui! Sasa mbona mara unaniita DJ, halafu unadai mimi ni low class kwa vile natongoza mke wa mdogo wangu, halafu mmeniletea hausgel, halafu ninatunzwa harlem, halafu kila nikikutana na wewe nainamisha macho! Yote hayo yalitoka wapi?

Nimekuita DJ kwa sababu unasema maneno mengi sana hapa kama ma-DJ, lakini huna ukweli wa ishu hata mmoja, hayo mengine unajua wazi yanayokuhusu na yasiyo kuhusu ndio maana pamoja na kwamba yamefichwa kiaina umeweza kujua kinachosemwa, na aliyeyaleta ya housegirls unamjua sana, au!

3.
Usichoelewa ni kuwa unapingwa na hoja na si vinginevyo. Kwa wengine kusema kuwa uliyasikia kutoka kwa mpishi wa Mkuu, au shemeji wa mke wako ambaye ameoa Mkuu, haitoshi. Ndiyo maana kwenye hili nika kwambia unayosema yanatofautiana na sheria inayotawala maslahi ya viongozi. Nikakuwekea sheria yenyewe lakini ukasema hauna haja nayo maana wewe unapata facts on the ground. Huo ni uamuzi wako lakini usitulazimishe wengine, hata kama ni wachache, kukubaliana na hizo anecdotal evidence. Kama hazitukalii vyema hata ukisema kuwa wewe ndiye mhusika na maslahi hayo! Unapodai kuwa dataz zako ni zaidi ya sheria ndipo panapoingia walakin. Hasa hapo inapodhiirika kuwa haujui tofauti ya katiba, sheria na waraka!

Amandla.............

Hakuna mtu anayeweza kuelewa sheria bila maneno hapa, mbona siku zote huwa unaweka maneno why kwenye hili umeweka namba tu, weka maneno yote ya sheria kama unaamini una ukweli, hayo ya shemeji na the rest sikuyasema na ndio ninapokudharau na kukuita low class kwa sababu ni pure nonesense,

Nimesema nina ukaribu sana na wakuu ninaowaongelea na nikaweka ukwelii ninaoujua kuhusu maisha yao as wastaafu, umesema maneno mengi sana ya kupinga lakini sijaona ukweli zaidi tu ya logic, naomba kurudia tena kua kama una uwkeli au sheria on your side yaweke maneno hapa kama nilivyoweka yangu ili wananchi wachambue ukweli na uongo au abuse ilipo, mimi niko radhi kuchambua na wewe at anytime, ninajua kwua Mkapa amepewa Range mbili mpya baada ya kutoka urais na ndizo anazozitumia sasa hivi, moja yake moja ya mkewe, sasa hizi sio SUV kama nilivyosema?

Mkuu kama kweli una ukweli zaidi uweke hapa tuuchambue acha hizi nonesense kwa sababu haziwasaididi wananchi hapa kuelimika.
 
Kiingereza? Kiko wapi? Unitafute ili tuyamalize maana inawasumbua sana watu hapa JF malumbano yasiyo na kichwa wala miguu, wewe na ndugu yako mbona tukikutana hamsemi haya maneno yenu mengi ya chuki mnasubiri kwenye forum, ndio mankuwa vijogoo ndio maana ninakupa nafasi wewe na mwenzako, siwaogopi tukutane tumalize mambo, halafu tutakuja hapa tunaheshimiana, au?

Mbona unakuwa mzito wa kuelewa! Sijawahi kukutana na wewe, period. Sikujui hata unaishi wapi! Wala sina haja ya kufahamiana na mtu yeyote humu ndani.

Sasa unataka tukutane wapi wakati pengine tunaishi bara tofauti? Hiyo lugha ya vitisho unajisumbua. Sihitaji kulazimisha heshima yako. Na vile vile sina haja ya kulazimisha uniheshimu.

Ninachosisitiza ni kuwa nitaendelea kukupinga kila pale utakapoleta vitu vilivyokaa kinamna. Sitabadilika.
 
Mkuu Yo-Yo,
Hawa watu wangu wawili ndio nina deal nao, maana ninawajua sana kuliko wanavyofikiri na walikuwa hawajui, na wameamua wenyewe kuwa wanataka personal hilo sina noma nao, kwa hiyo mkuu nimekusikia sana, lakini niachie hawa size yangu hawa nitakula nao sahani moja mpaka mwisho.
Mkuu hueleweki.....mara usema humjui mtu mara usema unawajua vizuri.....tukueleweje hapo??

Au swaumu mkuu?

Katika wanaonzaga personal hapa ni wewe.....umemuita mara kadhaa Fundi Mchundo mdini akikushinda kwa hoja unaanza personal......Kuhani nae umemuandama na hoja za majina mengi mpaka imekuwa wimbo.....nafikiri kuna watu wakikujua ni matatizo hata kama hawakujui watalazimisha kuwa wanakujua basi tu watafute cheap popularity......

Nakushauri tu achana na personal......utamuelimisha vipi mtu kwa kumuogopesha kuwa unamjua mara katongoza wake za watu.....hayo hayana maana katika kujenga taifa hili sana sana unaigalagaza personaity yako....

Ni hayo tu
 
Mbona unakuwa mzito wa kuelewa! Sijawahi kukutana na wewe, period. Sikujui hata unaishi wapi! Wala sina haja ya kufahamiana na mtu yeyote humu ndani. Sasa unataka tukutane wapi wakati pengine tunaishi bara tofauti? Hiyo lugha ya vitisho unajisumbua. Sihitaji kulazimisha heshima yako. Na vile vile sina haja ya kulazimisha uniheshimu. Ninachosisitiza ni kuwa nitaendelea kukupinga kila pale utakapoleta vitu vilivyokaa kinamna. Sitabadilika.

Mkuu siogopi kupingwa hata siku moja, sipokuwa nipinge kwa hoja na facts pia ukweli, kwa sababu ndio tabia yangu simpingi mtu hapa bila kuwa na uwkeli zaidi ya wa kwake, sileti maneno ya mitaaani na utoto, hapa ni mahali pa kubwa sana na pa heshima kuleta ujinga wa mitaaani na chuki za wanyama in binadamu, mengine yote ni nonesense!
 
1.
Mkuu hueleweki.....mara usema humjui mtu mara usema unawajua vizuri.....tukueleweje hapo?? Au swaumu mkuu?

Cha muhimu hapa ni hoja ya msingi nayo ni mishahara na mafao ya wakuu wetu wa taifa, be careful maana sio watu wote wasioeleweka kwa standard zako wawe wa-Islam wenye saumu infact hayo ni matusi makubwa sana kwa dini za wenzako hapa JF hatupendi hoja za namna hii, tunaheshimu dini zote na wananchi wote.

2.
Katika wanaonzaga personal hapa ni wewe.....umemuita mara kadhaa Fundi Mchundo mdini akikushinda kwa hoja unaanza personal......

angekuwa amenishinda kwa hoja kwenye hii topic tusingekwua hapa maana ningeshakubali kushindwa, nimetoa hoja zangu sijaona majibu zaidi ya nonesense!

Wamejaribu personal nimezijibu na bado niko tayari anytime kwa hoja au personal, ninarudia at anytime!


3.
Kuhani nae umemuandama na hoja za majina mengi mpaka imekuwa wimbo.....nafikiri kuna watu wakikujua ni matatizo hata kama hawakujui watalazimisha kuwa wanakujua basi tu watafute cheap popularity......

Huyo mtu wako nimemuandama na hoja ya uzushi aliyoileta hapa JF kuhusu DR. Masau, you know that sasa nashangaa unapojaribu kubadili ukweli, sina heshima na hayo majina yake maana ni utoto sana yeye anajua na wote wenye hiyo tabia huwa sizimii na huwa ninasema ukweli sina sababau ya kuficha, ukitaka kunijua sina noma ninaweza kukupa info zangu kwenye PM nione utafanya nini huwezi fanya anything, zaidi ya filimbi tu za hapa!

4.
Nakushauri tu achana na personal......utamuelimisha vipi mtu kwa kumuogopesha kuwa unamjua mara katongoza wake za watu.....hayo hayana maana katika kujenga taifa hili sana sana unaigalagaza personaity yako....
Ni hayo tu

Ni mpaka wewe na wenzako mkiacha personal ndipo tutakuwa na mjadala safi, unajua uzuri ni mmoja kwamba siwaogopi pamoja na vitisho vingi na maneno ya chooni all the time sina wasi wasi kabisa you know that, wewe unishauri nini labda mjishauri huko namna ya kunishambulia upya maana so far njia mnayotumia haifanyi kazi ndio maana m,nahangaika,

Ninawaona na maneno mengi sitishiki wala simuogopi any of you, hapa ni kukata ishus kama hamuwezi njia zipo lakini kunitisha mimi hamuwezi kabisa na maneno mengi ya kujifanya mnajau sana kumbe zero tupu, sio mimi na hii forum nimeapa haiwezi kuharibiwa na nyinyi watu watatu tu, hapana siku zote msimamo wangu ni firm na siwajahi kuyumba,

Kwa mimi sihitaji ushauri wako wala wa yoyote yule, whatever comes mimi sina noma wembe wangu ni kuchapa fimbo tu! au kwamba ninakuogopa wewe hata siku moja bro never!


Ahsante Mkuu!
__________________
 
...................Kwa sababu inawezekana kuwa kati ya ninalioyaona kwenye hawa wastaafu kuna wanayovuka mipaka kisheria, na ni wajibu wetu JF siku zote kukemea maovu ya viongozi wetu kisiasa, lakini badala yake nimeanza kushambuliwa kuwa ni uongo, sasa ukweli uko wapi hauletwi badala yake imegeuka personal, lakini ninasimamia pale pale kwenye hoja yangu kuwa niliyoyasema kuhusiana na mafao ya hawa wakuu ni ukweli niliuona na ninaweza kuurudia tena na tena, sasa kama kuna mwenye sheria inayosema tofauti na niliyoyaona ina maana kuna kiongozi anavunja sheria, kazi yetu JF ni kurekebisha!.............

FMES,
..........hiyo paragrapgh yako hapo juu ni murua kabisa........na naomba hii ndio spirit yetu hapa JF

Wazee JF............naona tunasahau moja ya mambo muhimu sana tunayoyafnaya hapa JF na hata huko mtaani JF kuonekana kimbilio la wengi wanaotaka ushauri pamoja na kujifunza ili kuliendeleza Taifa letu

Mndundu,...
.........you have raised very good points..........hapa hatuhitaji ubingwa wa nani anajua nini..........hapa JF always tunaweka record straight.......kumkoma nyani giladi...........

Fundi Mchundo.......
..........shukrani sana kwa vipengele kuhusu mafao ya wastaafu wazi...................sasa basi usiwaite wenzako waongo pale wanapokuambia experience zao........kwani experience kama hizo anazozungumzia FMES hatimaye huja kujenga facts.......kwani mambo mengi aliyosema nakuhakikishia kuwa ni sahihi...........kinachoshangaza ni kwanini hizo taratibu..........ulizotuwekea hazifuatwi........

......once again JF at work....i.e...........kuwafungua watu macho mjue kuwa........waraka wa mafao unasema hivi.........however facts on the ground are different........

Otherwise hii mada ni nzuri........kwani tukishajua mafao yao yanatakiwa kuwa vipi.......na facts on the ground are different.....then we have grounds to querry......na most likely utakuta kuna some sort of abuse ktk mafao..........
...............namkumbuka Mwl JKN (RIP) alipoletewa ile benzi mpya alilalamika sana kuwa ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi.........na alitaka ile benzi yake ya kustaafu itengenezwe ili aendelee kuitumia........it took a while ku-convince aikubali ile Benzi mpya.........sasa huyo alikuwa Mwl JKN sijui wastaafu wengine inakuwaje.........maana mengi aliyosema FMES kuhusu wastaafu ni kweli.............na si uongo

.....NOTE.....tulikuwa na dhamira nzuri ya kupata umeme wa dharura....but the fact on the ground kila mtu anajua..................what i mean ni kuwa tunaweza kuwa na paper works swaaafi kabisa kuonyesha mlolongo wa mambo.........lakini at the end of the day tunacho-evaluate ni what has been effectively achieved within justifiable means under our rule of law......
 
ninajua kwua Mkapa amepewa Range mbili mpya baada ya kutoka urais na ndizo anazozitumia sasa hivi, moja yake moja ya mkewe, sasa hizi sio SUV kama nilivyosema?

Mtoto wa Mkapa anaendesha Range Rover, nayo tuseme kwamba mpaka watoto wa wastaafu wanapewa magari? Tunachozungumzia ni stahili iliyoandikwa kwenye katiba na si kitu unachokiona. Unataka kuniambia kuwa Mkapa kakwambia kuwa amepewa hizo Range kama stahili yake? Kwani uwezo wa kujinunulia alikuwa hana? Ninachokuambia ni kuwa haiwezi kuwa stahili katika sheria kuwa hawa wakuu wapewe gari aina gani.

Litatajwa gari kwa uwezo wake (specifications) na kutokana na matakwa ya mstahili kuamua ni lipi anataka. Hata kama Mkapa amepewa Range, haimaanishi Kikwete nae atapewa Range. Kwa mfano, kiongozi au mtumishi wa serikali wa ngazi fulani anastahili kupewa fanicha lakini haisemi fanicha aina gani bali inatoa kinachoitwa specifications.

Mstahili kwa kukubaliana na Fanicha Ofisa wa serikali ndiyo wanaokubaliana ni fanicha ipi atapewa kulingana na viwango vilivyowekwa.

Kusema kuwa ni stahili ya Rais mstaafu kuongozana na mpishi ( kwa vile umemuona Mkapa au Sumaye akiongozana nae) vile vile ni uongo maana sheria inachozungumzia ni assistant. Aina gani ya assistant ni makubaliano kati ya mstaafu na hao wanaosimamia maslahi yake.

Nimemuita FMeS muongo baada ya yeye kujaribu kupindisha aliyoyasema. Amesema kuwa viongozi wana stahili ya safari mbili nje za matibabu ( si kweli) na nilipombana kwenye hili akadai kuwa hakusema alichosema ni safari za kawaida ! Muungwana anakiri anapokosea na muongo ni yule hata pale anapoteleza waziwazi anaendelea kukana kilichotokea.

Mfano mwingine ni hiki anachokizungumzia sasa hivi. Cha Mkapa na mke wake kupewa Range alipostaafu na kuwa hadi sasa ndiyo hizo wanazozitumia. Huyu ni mtu aliyedai wanapewa SUV mpya kila mwaka. Ikiwa aliyosema ni kweli, kwa nini Mkapa anaendelea kutumia alilopewa wakati anastaafu ( kama alivyotuambia FMeS)? Au mwaka haujapita toka astaafu?

Au ya mwaka huu ndiyo hiyo aliyompa mtoto wake? Madai kama haya ndiyo yanayotufanya wengine tupingane nae.

Sasa mtu ambae anakiri kuwa hajasoma sheria inayoongoza maslahi anapoendelea kudai kuwa kile anachosema amekiona ndiyo sahihi, nimwite nini?

Ogah. Bila shaka kuna mambo ambayo FMeS anayaleta humu kutokana na anachokiita experience yake ni ya kweli lakini kwa maoni yangu kwenye hili alidanganya ( kwa kuendelea kushikilia kitu ambacho dhahiri kilikuwa si kweli). Ninaamini kuwa ni haki yangu ku'question' kila kitu kinacholetwa humu. Si FMeS peke yake ambaye nimepingana nae.

Wengi tu na wengine wamenidhiirishia kuwa ni mimi ambae nilikuwa sielewi. Inapotokea hivyo sisiti kukubali kuwa kweli nilikosea. Si kwenye hili. Pengine atakapokuja mtu na kubandika sheria ( au amendment yake) inayothibitisha aliyoyasema FMeS. Nitapinga hata kama ataniambia ndivyo alivyoambiwa na mstaafu, acha hii ya kuona.
Amandla.
 
Kwamtazamo wangu hii hoja ingerudi kwawatu kuleta proven data au references kwenye hati sahihi za kiserikali au kikatiba, maana naona hoja hii (kama nyingi siku hizi hapa kwenye forum) inaelekea kwenye personal attacks kati ya pande mbili ambazo aidha zinajuana au wanavisa vyao.

... kungekuwa na objectivity au watu kuheshimiana mawazo yao wakipingana na kuto lete (drag) visa vyao kwenye threads nyingine.

Kumbe kuna watu wanagombana kikwelikweli humu ndani! Tufike mahala tudhibiti hali kama hii maana inatupotezea muda na mwelekeo wa mijadala yetu. Mtu unakuta kuna post mpya kwenye mjadala unaofuatilia, ukifungua unakuta si mwendelezo wa mjadala na badala yake ni ugomvi binafsi. Hii inachefua sana.

Wakubwa Mnundu na Kithuku, na Wakuu wengine,

Habari za Jumapili na za kusali ? Swaumu inaendeleaje ? Tukazane, tukazane, Iddi yakaribia.

Naomba kuleta senti mbili zangu kidogo hapa, kuhusu concern yenu. Hakuna wanaojuana, visa, wala ugomvi. Kwa nini mimi ndio nijifanya najua kinachoendelea? Kwa vile na mimi nimepitia hayo hayo anayoshambuliwa mwingine sasa hivi.

Na mimi "ni low life, nililetewa housegirl, nikampeleka cinema, nikatongoza mke wa mdogo wangu, nikapata nae ajali, juha, tukakimbia from the scene of the accident, nikakutwa kwenye basement DC, nikatunzwa Harlem, nikamtumia private message kuomba undugu..." ..all that nimefanya. Leo na jana ni "low life" mwingine anaambiwa ameyafanya haya.

Ndugu Mnundu na Kithuku, katika kujuana nadhani pia mna refer kwenye posti ambazo mimi na mwingine tumeitana bosi, juha etc..Kama inaonekana kama tunajuana, yale mambo tunayo ya parody hapa ni njia tu ya ku absorb na kuvumilia matusi tunayorushiwa hapa all the time tunapo shwalisha "dataz" zinazoletwa. Sio visa vya kweli vile, ila tumetungiwa. Apparently kuna mtu ambae alifanya hivi visa vya housegirl na huyu mleta matusi anamjua, lakini kila mtu anabandikwa hivyo visa. Ndio maana sasa tunayachukulia kama vichekesho. Sio ya kweli yale, ndugu zangu. Hatujuani na mtu hapa.

Ikitokea kuna ka pointi ka watu wawili kanafanana na hivyo wale watu wanateteana basi mmoja ataitwa bosi wa mwingine. Very condescending. But what do you do, get bent out of shape and try to prove kwamba mimi sio mfanyakazi wa fulani? No. You take it easy. Ndio hapo kwa mfano mimi nimesimikwa Ubosi wa mtu. Lakini huyo aliyedhihakiwa kwamba ni kijakazi wangu didn't get all exercised about that "bosi" crap. Took it easy. Again, the idea being to deal with the belligerent language in an even-tempered manner. Vinginevyo hapa pangekuwa hapatoshi.

Na hata huyo rafiki yangu ninaetaniana nae kuhusu hayo ma dhihaka tunayorushiwa, hata yeye simjui hata kidogo, na labda ni vizuri ikabaki hivyo hivyo, japo ni mtu ambae, kama wengine wengi hapa jamvini, ningependa sana sana sana kukutana nae maishani mwangu maana anaoneka ni mtu mzima unaeweza kumwendea kwa ushauri. Lakini kwa kuheshimu ile spirit ya anonymity ya JF nashindwa hata kumuuliza intro/whereabouts zake (anadai anaishi Bongo lakini vi stori vyote vya ndani vya kina McCain na Sarah Palin havimpiti...!, sijui kama ni kweli ni Mzee fulani yuko Tanzania. I mean ni Watu wangapi Bongo walifuatilia au kukumbuka debate ya Lloyd Bentsen na Dan Quayle back then?)

Huyo anaetutukana nae simjui hata kidogo, japo keshanitungia eti tumekutana kwenye basement Washington, DC! On the other hand, yeye mwenyewe kesha jichoresha hapa, anajulikana ni nani in real life. Sasa kila siku anavyonitukana hapa na mimi ningekuwa fidhuli ningekuwa namrushia vi personal inuendo vya chini chini hapa, lakini najaribu kumuheshimu yeye, kujiheshimu mwenyewe, na kuheshimu ile basic understanding ya JF kwamba hata kama unamjua mtu, hapa tuna assume kutokujuana. Kujuana juana na kutongozana kunaenda aidha Facebook au kwenye Private Messages huko. Najaribu kuheshimu hilo.

Sasa, unajizuia vipi, how do you deal with that, I mean hakuna anaefurahia kutukanwa. Ndio tunaishia ku make light of it, ku absorb hayo ma dhihaka all the damn time kwa kuyageuza utani. Na wakati ukiona yanageuka serious ni katika kuepusha fikra za watu kwamba ni kweli huyu mtu anatujua au "tumewekwa ndani Harlem." Maana kuna makumi ya watu humu ndani wanakuwa kweli swayed na huyu Mja wa dataz, ambao wanaweza kufikiri kweli mtu uko hapa kama mnafiki unaebinjukia ma house girl halafu baadae unajifanya kuwa lambast mawaziri wenye shutuma za ufuska. Kwa hiyo, zaidi ya kuweka the records straight, huwa matusi yake hayajibiwi.

And really, kwa kutokumjibu na kuyageuza matusi yake mzaha mi nadhani ni tunawapunguzia mzigo ma mods, ambao kwa kweli hawajui nini wafanye na watu kama huyu mtusi. Oh yeah, they know it. I mean, yeye (kama wengine wachache fulani hapa jamvini) huwa hapati adhabu kwa chochote atakachokisema ( JF Mtandao), kwa sababu sijui alishaifanyia favor JF zamani huko, (hili la nafasi ya huyu mtu na mchango wake kwa JF nimelitoa kwenye discussion aliyoandikwa na moderator mmoja Mkuu, way back, kwenye mada ya kui support JF). Na kwa sababu huyu mtu hafungiwi ningeweza kutukanana nae hapa mpaka liamba tuone itakuaje. But, really, that's kinda tacky though. Tushapita u teenager long effing time ago, na wengine tayari wenyewe wanasema wana vi teenager tayari vyenye "Mama wa Ubatizo Asha Rose Migiro"). Sasa kwa nini tukae tunatukanana hapa watu wazima?

Kwa hiyo, Mndundu na Kithuku, najaribu kuchangia ka idea ka kinachoendelea hapa. Hapana, hatujuani na mtu hapa, na visa unavyovisoma sio vya kweli, ni matusi tuliyorushiwa tumeyageuza utani, ili tusirukwe akili, au kufanana na huyo huyo mrusha matusi. Mngekuwa kwenye hiyo situation labda na nyinyi mngebuni njia yenu ya ku deal na hayo mashambulizi ya dhihaka na matusi. Nyinyi mngefanyaje? Nyinyi, waheshimiwa Mndundu na Kithuku, mngefanyaje?

Tatizo la msingi ni kwamba FMES anatoa taarifa ambazo ni outlandish and bizzare but he doesn't wanna be questioned about it, and ends up cursing and disparaging everybody who dares to buck him. Anataka kila mtu awe mpambe. Hapana.
 
....NOTE.....tulikuwa na dhamira nzuri ya kupata umeme wa dharura....but the fact on the ground kila mtu anajua..................what i mean ni kuwa tunaweza kuwa na paper works swaaafi kabisa kuonyesha mlolongo wa mambo.........lakini at the end of the day tunacho-evaluate ni what has been effectively achieved within justifiable means under our rule of law......

Mkuu, Ogah! Hapa unakosea. Kilichowashika wakina Richmond na maswahiba wao ni kutokufuatwa kwa taratibu za procurement na si kutuletea mashine mbovu.

Wale waliotakiwa kusimamia taratibu walizipindisha kwa sababu zao. Hili ndio tatizo na si kuwa tuliona mashine mbovu. Wamebanwa na sheria na si hearsay. Utaratibu ungefuatwa, hata kama wananchi tusingeridhika na kilichofanywa, wangeendelea kupeta. Richmond hakutemwa kwa sababu alikuwa ni dobi ( si wote tuliona picha ya laundry yake?) bali alikiuka taratibu ambazo zimewekwa kwenye sheria.

Hebu tuangalie upande mwingine wa haya madai. Tunajua Mkapa hapendwi na wengi. Sasa wanaposikia kuwa anapewa nyumba Dar (kweli) na Dodoma (si kweli), anapewa Range mpya kila mwaka (si kweli), anaenda kutibiwa nje kwa kodi yetu kila mwaka mara mbili hata kama haumwi (si kweli)., analipiwa mpishi wakwenda nae nje kila akisafiri (si kweli) si watazidi kuongeza chuki dhidi yake?

Sasa hapa kuna tofauti gani na tunayomtuhumu Kuhani kuyafanya dhidi ya Masau? Au kwa vile yule ni Kuhani ndio maana tukadai vithibitisho lakini huyu ni FMeS hatudiriki kudai kithibitisho? Kwani kwa kumpinga Kuhani kwenye ishu ya Masau mnataka kusema yote aliyowahi kuyaleta (na ninatumaini ataendelea kuleta) Kuhani humu yana walakin? Lazima tuwe consistent.
 
Naona bosi wangu Kuhani amesema wazi yanayoendelea humu ndani. Kwa uthibitisho, mnaweza kuangalia insinuations anazoanza kupachikiwa Mkuu Yo Yo ( ambaye naye hatufahamiani) kwa kudiriki kumpinga FMeS.

Pole ya swaumu ( usemi wa kwaida) unageuzwa kuwa ni mashambulizi dhidi ya waislamu! Ni hatua fupi kabla hajaitwa mdini. Yote haya ni kwa sababu kadiriki kuwatetea Low Class, watembea na mahausgeli, vi'gigolo' Fundi Mchundo na Kuhani!
 
Briefly, ni 80% ya mishahara yao walipokuwa job, magari mawili SUV mapya kila mwaka, nyumba mbili za serikali Dar na Dodoma, Wafanyakazi wa ndani ya nyumba na nje wasiozidi watano, both Dar na dodoma, Askari wa kulinda nyumba zote mbili, safari za matibabu ulaya mara mbili kwa mwaka wao na wake zao na walinzi wakifuatana na mpishi mmoja na msaidizi wa karibu, free msosi wa government, walinzi wawili personal na mengineyo!

All this ni mpaka watakapoitwa kwenye haki.

This is absurd!

Why pay for two cars a year, two homes, five servants, police, security and all other stuff?

Huu ni unyonyaji na wala si "kuenzi" au kusema ni marupurupu!

Only in Tanzania!
 
Naomba utoe reference, Field Marshall ES. Hizo data ulizotoa zinapatikana wapi na je, ziko public kwa watanzania wote?

Hizi data zilipitishwa (sheria ya 1999 ilifanyiwa mabadiliko na nyongeza) na kama sikosei Bunge la mwisho la Mkapa kabla yajabwaga manyanga!
 
Kwa hiyo mshahara wa raisi ni kiasi gani? Mbona hakuna anayejibu hili swali moja kwa moja?

Mishahara ya viongozi wa juu haiko wazi. Hakuna nje ya watu wa utumishi na wengine wa karibu nao wanaoijua. Kuna mmoja huko nyuma ali'qouote' gazeti la Uganda lakini kwa vile mshahara wa rais wetu uliwekwa kwa Ugandan Shillings ilikuwa vigumu kwa wengine kuuelewa. Kinachotakiwa ni uwazi kiasi kuwa tuweze ku'google' tu na kuujua. Lakini si kwetu. Tunapenda mno siri. nadhani kuna wakati hata kuuliza tu kungeweza kukutia matatizoni ingawa nakumbuka Nyerere aliwahi kutaja mshahara wake( Sh 4,000 kama sikosei) zamani sana.
 
Mishahara ya viongozi wa juu haiko wazi. Hakuna nje ya watu wa utumishi na wengine wa karibu nao wanaoijua. Kuna mmoja huko nyuma ali'qouote' gazeti la Uganda lakini kwa vile mshahara wa rais wetu uliwekwa kwa Ugandan Shillings ilikuwa vigumu kwa wengine kuuelewa. Kinachotakiwa ni uwazi kiasi kuwa tuweze ku'google' tu na kuujua. Lakini si kwetu. Tunapenda mno siri. nadhani kuna wakati hata kuuliza tu kungeweza kukutia matatizoni ingawa nakumbuka Nyerere aliwahi kutaja mshahara wake( Sh 4,000 kama sikosei) zamani sana.

Angalau wewe umesema hujui...maana wengine wanajifanya wanajua lakini ukiwauliza hawajibu swali moka kwa moja na wanaishia kukuambia kasome hiki na kile....oh well, ndiyo Tanzania hiyo....
 
Kama sikosei, mpaka wakati Mzee Mwinyi anaondoka madarakani, mshahara wa Rais ulikuwa ni Public Information na si ajabu unaweza kuupata kwenye kumbukumbu za Bunge ingawa sikumbuki ulikuwa ni kiasi gani!

Ni jambo la kushangaza sana kuwa uwajibikaji na uwazi unakosekana kwa kitu kama mshahara wa Rais wa Tanzania na marupurupu yake!

Same can be said kuhusu mishahara ya Makamu, Mawaziri na hata Wabunge.

Kwenye kumbukumbu za Bunge kuna hii act ya 1988 iliyosainiwa na Warioba, lakini hakuna act au bill iliyofuata inayoonyesha mishahara. http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/4-1988.pdf

May be tukipata access kwenye government gazzette tutapata takwimu sahihi!
 
Back
Top Bottom