Mishahara ya viongozi wa Tanzania

These wabunge must understand the issue is not about pay rise; it is about increasing productivity. Kuongeza mishahara bila tija, ni chanzo cha mfumuko wa bei katika uchumi. Every time, these wabunge will demand more and more pay rise as purchasing power falls since there is no TIJA. And if the government is not careful enough, this is a recipe for disaster--inflation spiral. TIJA,TIJA,TIJA ndio mbadala. Kuongeza mishahara isiyoendana na TIJA ni sawa na kubandika plasta juu ya donda ndugu.
Tatizo la wabunge wengi wanatumia pesa nyingi katika kampeni kwa kuonga ili washinde,hivyo huwa inasababisha wao kuwa na madeni mengi ambayo huwa hayalipiki kwa kipindi kifupi,ndio maana huwa wanakomaa sana na hili suala la posho.Mie nadhani kuna haja ya kuwa na wabunge wenye uwezo mkubwa kipesa,na wasio walafi wala mafisadi na wenyee nia njema na nchi yetu ndio wapewe madaraka.

wasiwe wabunge wanataka kufaidika na nchi yetu ila wawweze kuwafanya watanzania wafadike na nchi yao kwa ELIMU BORA,AFYA BORA NA MAISHA BORA.

sitaki Mbunge anyegombea ili aheshime,ili aweze kuchota vilowassa,ili aweze kutajirika.na ningependekeza posho ibaki pale pale ili kuwa na fare game wakati wa uchaguzi.

kwanza waliongezewa posho pindi walipoingia 2006/7 kisiri siri na sasa wanataka tena?huu ni Ulafi.
 
Yaani kanchi kenyewe ndo kama mkaonavyo,sasa posho zikiwa juu si itakuwa dhahma.

Ebu watoe justification za kuongezewa fungu.

Wakumbuke kuwa bungeni si sawa na investment,manake uko ndo twaelekea.

Mungu Ibariki Tz,mungu waongoze na viongozi wetu waache kuwa walafi bali waweke mbele maslai ya umma
 
mi nilidhani wanaomba wapunguziwe posho ambazo zinawapa mwanya wa kufanya starehe na kufuru na kusahau wananchi wao!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!...
Upuuzi huo wanataka shilingi ngapi hasa??? kwani sasa hivi wanalipwa bei gani???

msitusumbue bwana maana kazi ya ubunge ni wito sio ajira.. umeomba kura uwatumikie wananchi leo unaomba lundo la fedha eti kwa kisingizio cha kuwatumikia vyema wananchi....kama hamna uwezo kaeni pembeni waendelee kina Ndesapesa
 
Posted Date::3/27/2008
Wananchi wapinga wabunge kuongezewa mishahara
Na Muhibu Said
Mwananchi

SIKU moja baada ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kutaka waongezwe mishahara na posho, baadhi ya watu nchini wamepinga madai hayo.

Watu hao wamewataka wabunge kueleza bayana mahali zitakapopatikana fedha za kuwaongezea mishahara na posho, huku wengine wakiwataka kufikiria mara mbili matakwa yao kabla ya kuyawasilisha.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Nestory Ngulla alisema jana anawapongeza wabunge kwa kuona kile ambacho wafanyakazi wamekuwa wakikidai muda mrefu, huku wakipata upinzani mkali kutoka serikalini.

Hata hivyo, alisema wabunge wanapaswa kueleza wapi fedha za kuwaongeza mishahara na posho zitakapopatikana kwani serikali siku zote imekuwa ikishindwa kuwaongeza wafanyakazi mishahara kutokana na bajeti yake kuwa finyu.

"Tunawapongeza wabunge kwa kuona umuhimu wa kudai nyongeza ya mishahara na kwa kuanzisha hoja hiyo. Sasa watuambie pesa zitatoka wapi ili na sisi tuongezwe," alisema Ngulla.

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bob Makani alipinga wabunge kuiagiza serikali kuwaongezea mishahara na posho akisema kwamba, hatua hiyo siyo sahihi.

Makani ambaye pia ni mmoja wa waasisi wa chama hicho alisema wabunge hawapaswi kudai nyongeza ya mishahara kwa kuwa wao si wafanyakazi na kuwataka wafikirie mara mbili madai hayo.

"Wao si wafanyakazi, walitaka Ubunge na Ubunge ni kujitolea. Sasa sidhani kama ni sahihi kuagiza waongezwe mishahara na posho. Wangefikiria mara mbili kabla ya kutoa agizo kwa serikali," alisema Makani.

Naye wakili maarufu nchini, Mabere Marando alisema wabunge kudai nyongeza ya mishahara ni haki yao akisema kwamba, wanastahili wanapaswa kulipwa mishahara kutokana na kazi yao.

Marando alisema ana uhakika fedha za kuwaongeza wabunge mishahara na posho zipo na kwamba, kinachotakiwa ni utekelezaji ili kuwawezesha kutembelea majimbo yao.

"Kama serikali inaweza kuwalipa matapeli Sh152 milioni kwa siku, itashindwaje kuwaongeza wabunge mishahara? Nasema wabunge waongezwe na wafanyakazi waongezwe," alisema Marando.

Wakichangia mada katika Semina ya Bunge iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar es Salaam International Conference Centre (DICC) jijini juzi, wabunge zaidi ya 10 kutoka vyama vyote walisema, sasa umefika wakati wa mishahara na posho zao kuongezwa ili kuwaepusha kujiingiza kwenye vishawishi.

Katika mjadala huo, Spika wa Bunge, Samuel Sitta ndiye aliyeanza kutoa hoja hiyo kwa kupendekeza kwamba, waongezwe mishahara na posho na kisha kuungwa mkono na kila mbunge aliyesimama kuchangia hoja hiyo.
 
Kwa kazi ipi waliyofanya Wabunge mpaka wastahili kuongezewa mishahara? Kama wanaostahili kuongezwa mshahara ni Slaa na Zitto tu kwa kuibua maovu chungu nzima kuhusiana na BoT, Richmonduli na mikataba ya madini, waliobaki wengi walikuwa wanachapa usingizi tu ili kuingiza posho zao.
 
Ebu jengeni hoja za maana na kulilia wananchi wenu na sio kukaa tu na kujifikilia wenyewe, shame on you, wabunge wote wenye hisia ya kuongezewa posho
Kwa hali ya sasa unaweza kuzungumzia mambo ya kuongezewa posho, wakati kima cha chini cha wafanyakazi wa kawaida serikali imetangaza na waajiri kibao bado hawatekelezi, na wanaotekeleza ni kwa mbinde, lakini hamsemi kitu mnataka nyie ndo muongezewe tuuuu, mnakaa kimya watu wanaendelea kuteseka na mabill kibao ya umeme.

Hivi mshahara wa mbunge ni kiasi gani? Posho zao nzao ni kiasi gani? Kwa mwezi mbunge wa kawaida anakipato gani ukijumuisha mshahara na posho? Wakimaliza muda wao wanastahili gani?

Wale wanaoteuliwa kuwa mawaziri mshahara wao na posho zao ni kiasi gani? Spika mshahara na posho zake ni kiasi gani? Viongozi wa serikali, makatibu wakuu, waziri mkuu, majaji, jaji kiongozi, jaji mkuu, makamu wa rais na rais mwenyewe mishahara yao na posho zao ni kiasi gani? wakistahafu nini haki zao? Yote haya yanatakiwa yawekwe wazi maana ni kodi ya mwananchi inayowalipa. Tukishajua hili, ndio tunajadili kama wanastahili nyongeza au la!

Kwa vile mishahara, posho n.k. itakuwa wazi, basi yule anayegombea nafasi hizi hatakuwa na sababu ya kulalamika mara anapofanikiwa unless katika kujinadi kwake aliwaeleza wazi kuwa sababu moja inayompeleka huko ni kuboresha maslahi ya wabunge!
 
Kama sijasahau nadhani serikali kupitia vyombo vya habari imekwishabariki ongezeko la bajeti ya Bunge.Sidhani kama kelele zetu zitakua na nguvu bado.Lakini hii peke yake yatosha kutupa picha jinsi serikali yetu inavyoendeshwa kibabe na imejaa rushwa.

Mimi nasema ni rushwa kwa sababu serikali inaogopa kukabwa koo na bunge kila wanapovurunda.Kwa hiyo ili maovu yao yasifichuliwe wameona ni vizuri kuepusha shari kwa kuwaongeza waheshimiwa.

Wabunge wetu na nyie badala ya kutetea bajeti nzima,nyie mmeona kifungu chenu tu,hivi kweli mnawakalisha wananchi au mnajiwakilisha wenyewe?Hivi nyie wabunge wetu niwaulize swali,kazi wanazofanya madaktari,police,walimu n.k,hivi mnaweza mkajilinganisha na kazi wanazofanya hao wapiganaji?

Yaani mmeshindwa kutetea maslahi ya Taifa halafu mnajitetea wenyewe,thinking that you are the best in this counry while you are nothing,wabunge oneni aibu
 
..jamani naomba kujua mishahara, na mafao[per diem] ya safari za ndani na nje ya nchi kwa watumishi wa umma wafuatao:

1.Raisi wa Jamhuri ya Muungano 2.Makamu wa Raisi 3.Waziri Mkuu 4. Mawaziri

5.Naibu Waziri 6.Makatibu wakuu wa wizara 7.Mabalozi 8.Maraisi wastaafu 9.Mawaziri wakuu Wastaafu
 
Mi nasikia tu kuwa kuna watu wana per diems za hadi 65,000/= mtumishi/officer wa kawaida, nadhani kwa makatibu wakuu wanaenda hadi 85,000 kwa siku

sasa kwen mafao ndo sijui

ila za wabunge zimekaaje hadi sasa?
 
Kwanini unataka kujua? Waraka wa mwisho wa serikali unaonyesha kila kitu. Fedha nyingi huwa si perdiem ni zile za dharula/incidentals. Ris na waheshimiwa wengine hulipiwa full board acommodation na hela kadhaa kwa ajili ya entertainment na dharula; how much siwezi kujua.
 
Kwanini unataka kujua? Waraka wa mwisho wa serikali unaonyesha kila kitu. Fedha nyingi huwa si perdiem ni zile za dharula/incidentals. Ris na waheshimiwa wengine hulipiwa full board acommodation na hela kadhaa kwa ajili ya entertainment na dharula; how much siwezi kujua.

Sasa kama kila kitu kiko wazi kwenye waraka wa mwisho wa serikali kwa nini haujui hizo hela kadhaa za entertainment na dharula?

Mishahara na mafao ya viongozi wa juu ni haki ya kila mtu kujua. Mbona jirani zetu, Kenya, iko wazi? Mbona Sauzi iko wazi? Sisi tunaogopa nini?
 
..jamani naomba kujua mishahara, na mafao[per diem] ya safari za ndani na nje ya nchi kwa watumishi wa umma wafuatao:

8.Maraisi wastaafu 9.Mawaziri wakuu Wastaafu


Briefly, ni 80% ya mishahara yao walipokuwa job, magari mawili SUV mapya kila mwaka, nyumba mbili za serikali Dar na Dodoma, Wafanyakazi wa ndani ya nyumba na nje wasiozidi watano, both Dar na dodoma, Askari wa kulinda nyumba zote mbili, safari za matibabu ulaya mara mbili kwa mwaka wao na wake zao na walinzi wakifuatana na mpishi mmoja na msaidizi wa karibu, free msosi wa government, walinzi wawili personal na mengineyo!

All this ni mpaka watakapoitwa kwenye haki.
 
Briefly, ni 80% ya mishahara yao walipokuwa job, magari mawili SUV mapya kila mwaka, nyumba mbili za serikali Dar na Dodoma, Wafanyakazi wa ndani ya nyumba na nje wasiozidi watano, both Dar na dodoma, Askari wa kulinda nyumba zote mbili, safari za matibabu ulaya mara mbili kwa mwaka wao na wake zao na walinzi wakifuatana na mpishi mmoja na msaidizi wa karibu, free msosi wa government, walinzi wawili personal na mengineyo!

All this ni mpaka watakapoitwa kwenye haki.

Kumbe... ndo maana watu wako radhi kuuza nchi kwa mafisadi alimradi waupate ukulu..

Ila sasa kama mambo ndo hivo kuku kwa mrija hadi uwe mgeni wa malaika, sasa che Nkapa uroho wa kujirundikia kiwira, benki, viwanda vya sukari ulikuwa wa nini?
 
Back
Top Bottom