Mishahara ya Marais wastaafu ipunguzwe

Mishahara ya Marais wastaafu ipunguzwe

Kwa mujibu wa Zitto, mshahara wa raisi ni millioni 33 kwa mwezi. Hiyo milioni 400 wengi wenu mnayodai ni mshahara wa mwaka mzima.
 
Mnataka kuleta matatizo nchini. Viongozi wakuu wotee, kuanzia Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu. Majenerali wote wanapata mafao yao kwa mwenzi ni 80% ya aliyeko kazini. Kama ni hivyo wote hao wapunguziwe mafao yao. Ni pamoja Na Lowassa. Kama mnadhani ni marais tu
Mkuu, matatizo gani?! Hao wastaafu si nao ni raia wa Tanganyika na Zanzibar? Raia wenzao kule dodoma wanakula viwavi jeshi... Halafu kwa hili hakuna haja wala sababu ya kujificha kwenye kivuli cha Lowassa, kama unakumbuka wakati wa kampeni aliahidi kuwa kama angeshinda angeushusha mshahara wa rais hadi milioni mbili kwa mwezi.
Na kwa wale mnaouliza tuliambiwa kuwa rais aliyepita alikuwa analamba siyo chini ya milioni thelathini na tano kwa mwezi, mshahara tu....
 
Elimu Elimu Elimu! Tangu lini tshs 368 milion x 3 = 1. 104 trilion? Jibu sahihi ni 1.104 billion. Elimu elimu elimu!

Ndo maana tulitaka tuboreshe shule za Kata....ili Elimu Elimu Elimu iwe Elimu Elimu Elimu kweli....Na sio kanyaga twende...
 
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.

kumbe wacha hesabu iendelee kuwa janga la taifa. Eti ukitoka MILLION unaingia TRILLION? ???????

Ama BILLION? ????

Leo great thinker anatwambia marais wanalipwa TRILLION 1.5
Yaani Bilioni elfu moja mia tano...

NI KWELI MNA LENGO JEMA ??????
 
Kama sijakosea..... hesabu hizo za mishahara ya kutunga zilikanushwa na serikali
 
Kwa hiyo hesabu za kujumlisha huzifahamu mkuu?. Pitia tena bandiko langu, na wadau waliosema mshahara wa Rais ni milioni 460 kwa mwezi. Hivyo nimetumia hesabu ya darasa la kwanza tu kufikia hitimisho hilo hapo juu.
Duh.. Kweli hesabu zako ni za darasa la kwanza!! Yani ukitoka milioni unaingia trilioni, tehe teh..
 
Angalau hiyo ina sound kuliko hao mapopoma wanaodai rais kwa mwezi anakula milioni 400+.
Usiendekeze sana kutoka povu wakati hujui hata unachoongea!! Kwa taarifa yako Tanzania iko katika top 10 ya marais wenye mishahara minono!! Not so sure ni kiasi gani lakini nakumbuka si 400+ mil.. Fanya utafiti ndio uje ukanushe!!
 
Wapi naweza kupata taarifa sahihi kuhusu mshahara wa rais wa Tanzania?
 
Hiyo makala niliisoma mwaka jana sikumbuki ni jarida gani (sio la Tanzania) lakini nahisi laweza kuwa African Ventures Magazine..

Hiyo makala ilikanushwa na ikulu ya Kikwete.

Kwa hiyo bado mshahara wa rais wa Tanzania haujulikani.
 
Hiyo makala ilikanushwa na ikulu ya Kikwete.

Kwa hiyo bado mshahara wa rais wa Tanzania haujulikani.
Unajua haya majarida mpaka wanachapa habari kama ile wanakuwa na sources za uhakika.. Na kuhusu ikulu kukanusha sishangai maana ndio utamaduni walio jijengea .
 
Unajua haya majarida mpaka wanachapa habari kama ile wanakuwa na sources za uhakika.. Na kuhusu ikulu kukanusha sishangai maana ndio utamaduni walio jijengea .

Hizo habari za uhakika wao wamezitoa wapi?

Manake waliandika tu bila kutoa vyanzo.

Sasa wewe una uhakika gani kuwa hawakutunga, kuongeza chumvi, au kupunguza?

Mshahara wa rais wa Tanzania bado haujulikani.

Hebu jaribu kutafuta mishahara ya marais wa Kenya na Afrika Kusini uone...
 
Majaji nao wakistaafu wanakula 80% ya mshahara aliokua analipwa kila mwezi...Nchi inatafunwa hii balaa kodi kubwa inakwenda kulipa viongozi waliostaafu..ndio maana fedha za kujenga bara bara kidogo tuu lazima tukope na wao hawatuambii punguzeni mishahara kwa kuwa akikuposha anakupa na masharti ambayo yanafavour upande wa mkopeshaji..
 
Wapunguziwe tena hata nusu ya hiyo wanayoipata maana wengi wao ni mizigo tu kwasasa. huyu wa awamu ya tatu yeye ni mitusi tu kila wakati, sasa watu kama hao wanini ktk jamii? wanaifilisi nchi tu. Wanachokifanya ni kukumbatia madhambi tu!, ndicho wananchokiweza. mm naona kama wanataka wawapunguzie acha wapunguze sana tu!, Wanasingizia wanamshauri Rais wa sasa: wakati vipindi vyao wamevuruga. Wapunguze tu hiyo mishahara maana hayo ni MAJIPU MENGINE yanayolitafuna taifa letu!!!! thenkyuuuu
Hii itaongezaje kipato chako?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Nilipata kuwa somewhere nikapata kuliweka hilo mbele ya wadau nikiwaambia mshahara wa prezida tz ni zaidi ya mil400 mbali na posho mbali na overtime hapo... Huwezi kuamini walin'gaka wengine wakaniambia kiasi hicho hakipo raisi analipwa mil arobaini na tano.
Hivi ulipwe mshahara wa Tzs 400M na overtime? Kwanza kwa level ya raisi kuna kitu kinaitwa overtime?
 
A
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.

Magazijuto...460+(0.8*460*3)=
1564
Hahahahahahahahaahahaaa
 
Hivi ulipwe mshahara wa Tzs 400M na overtime? Kwanza kwa level ya raisi kuna kitu kinaitwa overtime?
Unashangaa nini sasa? Afrika kuna mambo mengi sana ya ajabu na ya kutisha tuko mbali na dunia ya wenzetu wanayoishi.... Mimi huwa sishangai kabisa pale ninaposikia vitu visivyoniingia akilini ktk serikali za kiafrika na Afrika kwa ujumla... Nakuambia kabisa Afrika ina safari ndefu sana ya ukombozi wa kifikra kutoka hapa tulipo mpaka kuwafikia wenzetu wa dunia hii.
 
Back
Top Bottom