Mishahara ya Marais wastaafu ipunguzwe

Mishahara ya Marais wastaafu ipunguzwe

80%ya mshahara haipo kwa marais wastaafu pekee ipo pia kwa mawaziri wakuu waastafu na viongozi wengine waandamizi wa serikali ukweli ni mzigo kwa mlipa kodi.sheria hii iangaliwe upya.hebu UKAWA liangalieni hili kwakuwa nyie sio wanufaika mnaweza.
 
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.
Kweli Mathematics ni tatizo kwa walio wengi Tz,hivi kweli milioni 400 Mara tatu unapata 1.104 Trilioni!????
 
Hata kama wangefanya kilichotarajiwa.Wanapumua kama watu wengine,wanachopata ni kikubwa mno,wawahurumie watanzania.
Formula hiyo ya kulipa marais wastaafu iliwekwa kwa mategemeo kwamba punde rais akiwa madarakani aongoze nchi vizuri bila kujitumbukiza katika ufisadi kwa kuwa ana uhakiki marupurupu yake baada ya uongozi yanamuwezesha kuishi kwa raha mustarehe. La kujiuliza ni je marais hao wamefanya kilichotarajiwa?
 
Hata kama hujasoma hesabu ama hisabati, tumia akili ndogo tu hii ifuatayo. Kwa mjibu wa TRA, kuna miezi makusanyo huishia milioni 800, ukitoa milioni 400+ ya rais aliye madarakani tu, unapata salio la milion 300+, hapo hujawalipa marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu, waziri mkuu aliye madarakani na wastaafu wengine, je maendeleo ndiyo kusema yatategemea misaada tu?
Nawewe ni Ripoti ipi ya TRA inasema makusanyo ni Milioni mia nane?
Mbona tunaonyesha udhaifu mkubwa kiasi hicho?????
 
Mimi naona ni busara zaidi kuondoa 80% wanayopata Mawaziri Wakuu wastafu sababu wengine wamekiri kuwa katika vipindi vyao vya Uwaziri mkuu serikali haikufanya jambo lolote la maendeleo kwa wananchi wa Tanzania, inamaana walikuwapo Kama sanamu sasa kwa nini tuendelee kuwatunza.
 
Hata kama hujasoma hesabu ama hisabati, tumia akili ndogo tu hii ifuatayo. Kwa mjibu wa TRA, kuna miezi makusanyo huishia milioni 800, ukitoa milioni 400+ ya rais aliye madarakani tu, unapata salio la milion 300+, hapo hujawalipa marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu, waziri mkuu aliye madarakani na wastaafu wengine, je maendeleo ndiyo kusema yatategemea misaada tu?
hakuna kitu kama hiki...hivho kiasi si faida ya bakhresa kwamwezi!!umechanganya bilioni na milioni
 
Watu hata hamjui mshahara wa rais ni kiasi gani halafu bado mnajadili mishahara ya marais wastaafu kupunguzwa!

Marais wastaafu wanalipwa mishahara? Kama wanalipwa, wanalipwa shilingi ngapi?
 
Hata ukipunguzwa hawataniongezea mimi na sitajua hata uliopunguzwa umeenda wapi.... acha wachukue tu
 
Watu hata hamjui mshahara wa rais ni kiasi gani halafu bado mnajadili mishahara ya marais wastaafu kupunguzwa!

Marais wastaafu wanalipwa mishahara? Kama wanalipwa, wanalipwa shilingi ngapi?
Ukitaka Kujua Mshahara Wa Mtu Unaweka Wazi Kwanza Wa Kwako.Piga Picha Salary Slip Yako Weka Hapa Halafu Ulizia Mishahara Ya Wengine.
 
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.

Tofautisha trilion na bilion
 
Ukitaka Kujua Mshahara Wa Mtu Unaweka Wazi Kwanza Wa Kwako.Piga Picha Salary Slip Yako Weka Hapa Halafu Ulizia Mishahara Ya Wengine.

Mimi siyo mtumishi wa umma.

Mshahara wangu hautokani na pesa za walipa kodi.

Hivyo silazimiki wala siwajibiki kukidhi hitaji la uwazi juu ya matumizi ya pesa za walipa kodi.

Kwa vile nipo kwenye sekta binafsi, ni bosi wangu tu ndiye mwenye kujua mshahara wangu ni kiasi gani.

Hakuna bosi asiyeujua mshahara wa mtumishi wake.

Kwa mantiki hiyo basi, bosi wa watumishi wa umma ni umma wenyewe.

Hivyo, umma una haki zote za kujua mishahara ya watumishi wake.

Hivi unaelewa hata nilichokiongelea hapo?
 
Hata kama hujasoma hesabu ama hisabati, tumia akili ndogo tu hii ifuatayo. Kwa mjibu wa TRA, kuna miezi makusanyo huishia milioni 800, ukitoa milioni 400+ ya rais aliye madarakani tu, unapata salio la milion 300+, hapo
hujawalipa marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu, waziri mkuu aliye
madarakani na wastaafu wengine, je maendeleo ndiyo kusema yatategemea misaada tu?

Unashindwa kutofautisha milioni, bilioni na Trilioni halafu unataka sisi tutumie akili kidogo tu, acha dharau. Makusanyo ya TRA, ni bilioni 800 na si milioni 800 kama unavyosema wewe.
 
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.
Unachokataa ni nini wewe kenge? umekariri makusanyo tu, unadhani serikali inaishi kwa makusanyo? kama unakataa hawalipwi hivyo Wewe hapo ulipo unapata huduma gani nzuri ya jamii?, kila kitu Ni hovyo nchi nzima sasa pesa zinaenda wapi? na bado bajeti ya nchi ni tegemezi nyie wa Lumumba ubongo wenu umejaa tope.
 
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.
Mmmmh! Are you sure?
 
Mnataka kuleta matatizo nchini. Viongozi wakuu wotee, kuanzia Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu. Majenerali wote wanapata mafao yao kwa mwenzi ni 80% ya aliyeko kazini. Kama ni hivyo wote hao wapunguziwe mafao yao. Ni pamoja Na Lowassa. Kama mnadhani ni marais tu

Nadhani sasa ni wakati muafaka wa kuangalia upya ile sheria ya mafao ya viongozi kwani kwa wakati uliopo haiendani na uhalisia wa hali tuliyonayo nchini. Achilia mbali kuwa hao wanaohusika na sheria hiyo kuwa ni wengi sana wakiwemo marais, mawaziri wakuu, makamu wa rais, wakuu wa majeshi, maspika wa bunge etc. Kuwahudumia wastaafu wote hawa kufuatana na sheria ile ni mzigo mkubwa sana kwa Taifa kwani wengi wao bado wana umri mdogo hivyo muda mrefu wa kuishi!!

Kuna mafao mengine kwa kweli hayana uhalali wowote hasa kwa marais wastaafu. Kuna maana gani kwa serikali kuwajibika kumjengea nyumba ya kuishi baada ya kustaafu Rais ambaye akiwa katika utumishi wa umma aliuziwa nyumba na serikali? Mfano mzuri ni marais wastaafu Mkapa na Kikwete hawa tunajua kuwa waliuziwa nyumba na serikali sasa kuna uhalali gani wa kujengewa nyumba nyingine ya kuishi baada ya kumaliza muda wao? Marais wastaafu wajengewe nyumba pale tu kama hawatakuwa na mahala pa kuishi wao na wake zao baada ya kustaafu na nyumba hizo zilirudishwe seriklini mara wake zao au wao wenyewe watakapo itwa na muumba wao. Ni makosa makubwa kuwarithisha watoto wa Marais wastaafu nyumba za serikali baba zao walizojengewa kwa sababu ya wadhifa wao kwani hizo nyumba zinaweza kutumika kama mapango ya mafisadi!! Lazima sheria ya mafao ya viongozi iwe na uwiano na hali wa uchumi ya chi kuweza kuubeba mzigo wao!!!
 
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.
Rudi while boss.
 
Back
Top Bottom