Mishahara ya Marais wastaafu ipunguzwe

Ukaridayo

JF-Expert Member
Oct 8, 2012
508
470
Wakuu ningeomba kuwasilisha hapa mana Leo asubuhi nimeskia kwenye radio ktk magazeti ya Leo wakisoma moja ya kichwa hicho cha hbr!. Juu ya mishahara yao kupunguzwa, ningependa kufahaamishwa hivi hao maretired ni kweli bado wanalipwa kiwango kile kile cha utumishi.
 
Wanalipwa 80 percent ya chochote anachopata Magufuli. Hii ni pamoja na mishahara, Magari, Matibabu etc
 
Wapunguziwe tena hata nusu ya hiyo wanayoipata maana wengi wao ni mizigo tu kwasasa. huyu wa awamu ya tatu yeye ni mitusi tu kila wakati, sasa watu kama hao wanini ktk jamii? wanaifilisi nchi tu. Wanachokifanya ni kukumbatia madhambi tu!, ndicho wananchokiweza. mm naona kama wanataka wawapunguzie acha wapunguze sana tu!, Wanasingizia wanamshauri Rais wa sasa: wakati vipindi vyao wamevuruga. Wapunguze tu hiyo mishahara maana hayo ni MAJIPU MENGINE yanayolitafuna taifa letu!!!! thenkyuuuu
 
Katika utawala bora,kama wanasiasa wanavyojinadi wakati wa kampeni wakiwemo wagombea Urais,mishahara yao inafaa ijulikane kwa umma mbona inafanywa siri? Unapata mshahara ambao mwajiri wako haujui kweli? Kama kweli hao ni watumishi wetu tujue mishahara yao.
 
Inavyoonekana mpaka wadau kuanza kushauti kwenye media mbalimbali juu ya ishu ni kuwa mishahara wanayolipwa hawa watu bado ni mzigo mzito achilia mbali privileges kubwa wanazoendelea kupata... Privileges tu peke yake feva kubwa sana mbali na mavitege uchumi yao binafsi waliyowekeza.
 
460 milion kwa mwezi hapo kula kulala afya bure na malupulupu bdo
Nilipata kuwa somewhere nikapata kuliweka hilo mbele ya wadau nikiwaambia mshahara wa prezida tz ni zaidi ya mil400 mbali na posho mbali na overtime hapo... Huwezi kuamini walin'gaka wengine wakaniambia kiasi hicho hakipo raisi analipwa mil arobaini na tano.
 
China nasikia ili kupunguza mzigo wa pension wao wana njia mbadala. Eti ni kweli kuwa wao wanahakikisha kuwa hawapo?
 
China nasikia ili kupunguza mzigo wa pension wao wana njia mbadala. Eti ni kweli kuwa wao wanahakikisha kuwa hawapo?
Mhhh ninamashaka makubwa na hiyo nadharia sema China hawana mambo ya uwendawazimu ktk katiba yao.
 
David Cameron mwenyewe anapokea pauni 149,000 kwa mwaka ambayo ni million 300+ tzs kwa mwaka na ni Nchi tajir.

Speaker Wa bunge wa uingereza anapokea 150,000 sterling pounds kwa mwaka

Na liinchi limaskin bado linawalipa maparasites 400k + tzs kwa mwezi licha ya katafuna Nchi mithili ya mchwa
 
Wapunguziwe tena hata nusu ya hiyo wanayoipata maana wengi wao ni mizigo tu kwasasa. huyu wa awamu ya tatu yeye ni mitusi tu kila wakati, sasa watu kama hao wanini ktk jamii? wanaifilisi nchi tu. Wanachokifanya ni kukumbatia madhambi tu!, ndicho wananchokiweza. mm naona kama wanataka wawapunguzie acha wapunguze sana tu!, Wanasingizia wanamshauri Rais wa sasa: wakati vipindi vyao wamevuruga. Wapunguze tu hiyo mishahara maana hayo ni MAJIPU MENGINE yanayolitafuna taifa letu!!!! thenkyuuuu
Acha awatukane maana wanastahili hivyo
 
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.
 
Back
Top Bottom