Mishahara ya Marais wastaafu ipunguzwe

Mishahara ya Marais wastaafu ipunguzwe

Hata kama hujasoma hesabu ama hisabati, tumia akili ndogo tu hii ifuatayo. Kwa mjibu wa TRA, kuna miezi makusanyo huishia milioni 800, ukitoa milioni 400+ ya rais aliye madarakani tu, unapata salio la milion 300+, hapo hujawalipa marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu, waziri mkuu aliye madarakani na wastaafu wengine, je maendeleo ndiyo kusema yatategemea misaada tu?
 
Mnataka kuleta matatizo nchini. Viongozi wakuu wotee, kuanzia Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu. Majenerali wote wanapata mafao yao kwa mwenzi ni 80% ya aliyeko kazini. Kama ni hivyo wote hao wapunguziwe mafao yao. Ni pamoja Na Lowassa. Kama mnadhani ni marais tu
 
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.

Mkuu kuwa mpole, umetumia namba IPI kupata hiyo 1.564 Trillion!?
 
460 milion kwa mwezi hapo kula kulala afya bure na malupulupu bdo

Kwa taarifa nilizo nazo Mshahara wa Raisi ni 400M kwa mwaka na si kwa mwezi.

Bado kuna utata ktk taarifa sahihi za Malipo ya Raisi.
 
Mkuu kuwa mpole, umetumia namba IPI kupata hiyo 1.564 Trillion!?
Kwa hiyo hesabu za kujumlisha huzifahamu mkuu?. Pitia tena bandiko langu, na wadau waliosema mshahara wa Rais ni milioni 460 kwa mwezi. Hivyo nimetumia hesabu ya darasa la kwanza tu kufikia hitimisho hilo hapo juu.
 
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.

Hii ni akili ya shule za kata. Hujui kutofautisha BILLION na TRILLION. Rudi kwanza shule ndio ukimbilie ku comment humu JF
 
Kwa hiyo hesabu za kujumlisha huzifahamu mkuu?. Pitia tena bandiko langu, na wadau waliosema mshahara wa Rais ni milioni 460 kwa mwezi. Hivyo nimetumia hesabu ya darasa la kwanza tu kufikia hitimisho hilo hapo juu.

Mkuu wewe hujawahi kusikia kabisa kuhusu Billion!?
 
Wapunguziwe tena hata nusu ya hiyo wanayoipata maana wengi wao ni mizigo tu kwasasa. huyu wa awamu ya tatu yeye ni mitusi tu kila wakati, sasa watu kama hao wanini ktk jamii? wanaifilisi nchi tu. Wanachokifanya ni kukumbatia madhambi tu!, ndicho wananchokiweza. mm naona kama wanataka wawapunguzie acha wapunguze sana tu!, Wanasingizia wanamshauri Rais wa sasa: wakati vipindi vyao wamevuruga. Wapunguze tu hiyo mishahara maana hayo ni MAJIPU MENGINE yanayolitafuna taifa letu!!!! thenkyuuuu

Wanamshauri kufanya yale waliyofanya na mnalipia ushauri huo.
 
Kwa taarifa nilizo nazo Mshahara wa Raisi ni 400M kwa mwaka na si kwa mwezi.

Bado kuna utata ktk taarifa sahihi za Malipo ya Raisi.
Angalau hiyo ina sound kuliko hao mapopoma wanaodai rais kwa mwezi anakula milioni 400+.
 
Tukiambiwa katiba mpya ndio mpango mzima hatuelewi!
Kweli kifo ndio mpango mzima alioubuni mwenyezi Mungu.
 
Kimsingi hao wastaafu hawana uhalali wa kulipwa huo mshahara mkubwa kiasi hicho kwani kupitia vipindi vyao vya uongozi mbaya na usiozingatia maadili ya kiuongozi ndio waliosababisha nchi kufikia hapa pamoja na utitiri wa rasilimali....tena mmoja wapo ana kashifa mnbali mbali za kujimilikisha mashirika ya umma na familia yake......wengine wamebinafsisha mashirka yetu ya umma kwa bei ya kutupa.....

Hao ni miongoni wazembe walioshindwa kusimamia sera za kimaendeleo badala yake nchi inarudi nyuma baada ya kusonga mbele......hebu tuweni wakweli wandugu pamoja na madudu yaliyoibuliwa katika uongozi uliopita ulioisababishia serikali hasara ya matrilioni ya shilingi bado ana uhalali wa kulipwa pesa hiyo kama mstaafu...???

Kuwalipa hao wastaafu hiyo mishahara ni moja ya matumizi mabaya ya kodi zetu kwa kuwa watanzania hatuna cha kujivunia kupitia uongozi wao......

Na wengine tumewasikia wakitutukana hadharani sie ambao tumetofautiana kimawazo....baada ya kulishauri taifa kuleta mshikamano badala yake kupitia kauli zao kumezua mgawanyiko mkubwa sana wa kitaifa....na wamekuwa wakimshauri ujinga raisi aliyepo madarakani....kwa kifupi hawana tija kwenye taifa hili changa....

Kupitia vipindi vyao vya uongozi tumeshuhudia huduma mbovu za afya...tumeshuhudia miundombinu mibovu isipokuwa kuelekea kwenye makasri yao tu huko wanakoishi....tumeshuhudia mdororo mkubwa wa kiuchumi pamoja na kuzidi kiporomoka kwa thamani ya shilingi huku kukikosekana na mipango madhubuti ya kujinasua.....

Kwa kifupi hawana uhalali wa kulipwa hata buku au buku mbili....wengine tumewashuhudia wakisafiri tu kwa kipindi chote cha uongozi wao...sasa mtu kama huyo alipwe ili iweje...???
 
Hivi bado wanalipwa kumbe?..kwa kawaida wastaafu si hua wanapata kiinua mgongo chao kisha wanaelekea nyumbani au?
 
Hiyo ml 460 nina mashaka nayo. Hesabu kidogo, 80% ya ml 460 ni ml 368. Chukua ml 368 zidisha kwa marais watatu wastaafu walio hai unapata 1.104 trilioni, kisha jumlisha na ml 460 ya rais aliyepo madarakani unapata 1.564 trilion. Makusanyo ya mwezi yakizidi sana ni Trilioni 1.3, ambayo iko chini ya mishahara ya marais hao. Je, makusanyo yote ndiyo kusema huishia kwenye kulipa mishahara ya marais? Acheni usengerema.
.....Umekurupuka....Hesabu zako za Kayumba....! milioni....then billion...halaf ndo trillion...ebu rekebisha
 
Back
Top Bottom