Duniani kuna matajiri wangapi? Ni wafanyabiashara wangapi wanaoishi maisha mazuri kuliko watumishi? Take home ya Laki3 kwa mwezi inabaki ziada ya sh.ngapi ili mtumishi aanzishe biashara? Biashara ni kitu rahisi kama unavyodhani? Vipi ufanisi katika utumishi wa umma utavyokua kila mtumishi akiwa mfanyabiashara? Kwa vile mshahara ni haki yake wacha aulize, ikiwa anakukera usifungue uzi wake au kucomment. Mawazo ya kipuuzi kama hayo kuona biashara ni kitu chepesi na kidogo tena kinachohitaji mtaji wa neno tu kuanzisha ni ya mtu mwenye umbilikimo wa fikra juu ya dhana ya biashara, mwenye kuchukua maneno ya vijiweni na kuyafanya ndio mwangi wake katika maisha halisi.
Tatizo kubwa kwa watu si kukosa mtaji bali ni kukosa uelewa na uthubutu! Hakuna mhindi aliyekuja bongo akiwa na mtaji! Wamekuja wakiwa maskini lakini wakiwa na mpango wa kujiendeleza! Si lazima uanze na mtaji mkubwa ila ni lazima uanze na akili kubwa!
Unamkuta kijana mwajiriwa analalamika mshahara kidogo ( ni kweli mshahara ni mdogo), sasa unafanyaje katika mazingira hayo? Suluhisho siyo kulalamika daima Bali ni kupambana! Atakwambia hana mtaji! Lakini ukimtazama ana Simu ya laki sita na kuendelea!, kavaa miraba ya bei mbaya etc! Vyote hivyo vingekuwa mtaji wa kuanzia halafu mdogo mdogo unajijengea tabia ya kuzalisha na kutumia na si kutumia tu! Bila tabia hiyo hata ilitokea MTU akapata pesa wazo LA kwanza ni kutumia na si kuzalisha kwanza! Kwa mwendo huo sahau kujikwamua!
Chanzo kikubwa cha mtaji si mshahara mkubwa Bali ni tabia ya kujiwekea akiba kwa malengo!
Hebu fikiri kidogo: kama angeamua kuweka akiba ya 50,000/= kwa mwezi na akawa na nidhamu hiyo kana kwamba si za kwake ( Ni kweli si zake bali za mtaji wa biashara yake tarajiwa). Kwa mwaka angekuwa na laki sita. Kwa miaka 5 angekuwa na milioni 3! Hizo zinatosha kama kianzio cha biashara!
Katika kipindi cha miaka 5 wakati anaandaa mtaji ni kipindi kizuri cha kufanya utafiti na kuchagua aina ya biashara utakayoimudu na utakuwa na taarifa zote muhimu za biashara hiyo!
Unaweza kusema: mshahara ni mdogo sana kiasi ambacho siwezi kuweka 50,000/= kwa mwezi! Siyo kweli! Ukweli ni kwamba unaweza lakini uamua kuacha vitu vingine ambavyo japo ni muhimu lakini si vya lazima! Mbona bodi ya mikopo imetoka huko ilikotoka na inakata watu 15% ya mshahara ambao ni zaidi ya 100,000/= na maisha yanaendelea! Ukweli ni kwamba japo maisha yanaendelea lakini kuna mambo ambayo umelazimika kuachana nayo! Kumbe ungeweza kuachana nayo kwa hiari na kujilimbikizia mtaji! Wako waliokuwa kwenye ajira kwa zaidi ya miaka 10 na hawana akiba ya pesa kabisa! Akaunti ni ya kupokelea mshahara tu! Bodi imewasaka na imeanza kuwakata! Hebu fikiri: Hizo unazokatwa na bodi kama ungekuwa umeamua kujilimbikizia akiba kwa miaka 10 uliyofanya kazi, saa hii ungekuwa na akiba takriban ya milioni 10! Huo ni mtaji wa kutosha kufanya biashara ya kukuingizia zaidi ya milioni moja kwa mwezi kama faida na huku ukiwa umeajiri mtu wa kukusaidia!
Kumbuka: 50,000/= kama zilivyo haziwezi kukusaidia! Lakini ukizilimbikiza kwa miaka 10 ni habari nyingine! Tunateseka kwa kukosa uelewa na malengo! Mtaji ni akili kubwa na si mshahara mkubwa! Mtaji alioanzia Bakressa haufiki 100,000/=! Leo yuko wapi?