Mimi ni Mlokole nataka kuoa Mroma

Mimi ni Mlokole nataka kuoa Mroma

Ee YESU wangu nisaidie!Kwahiyo RC hawataenda mbinguni.Mbona watu wanakariri majina ya dini kuliko mwokozi mwenyewe.
 
Inafaa sana kuishi bila kujitazama kuwa wewe ni bora zaidi kwa kuwa umeokoka! Suala hapa so kuokoka ama kutookoka mapenzi hayana hilo mpendwa wangu. Nakushauri kuwa msikivu kwa sauti ya mungu anayetuita sote kwake, mamoja umeokoka au laa! Kuokoka si kuwa ephata ama kuwa mkatoliki hata muislamu anayeishi vyema bila kuwadhuru wengine na kujali utu wa binadamu wengine anaweza kuwa ameokoka. Moyo wa mtuu ndo bwana anautazama! Kuwa makini na tabia ambazo walokole wengi wamekuwa wakizionesha, yaani mara nyingi wao hujiona bora kuliko wale wasiojiita wameokoka! Kujidhania mwenyewe umeokoka na kumwona asiye mwokovu ni mdhambi ni hatari sana maana mwenye kuhukumu mdhambi na mwenye haki ni mungu pekee! Sisi viumbe vyote ni mali yake na yatupasa kutohukumiana na kujiona sisi ni bora kuliko wengine!
 
wapendwa katika bwana
nimetatizwa na kitu hapa,mimi ni mlokole nasali Efatha bible,nimejaribu kuomba na ku connect na baadhi ya wapendwa wenzangu lakini nahisi sikufanikiwa
ila imekuja kutokea nikaonana na mwanamke ambaye anasali roman catholic na tumependana sana japo sikutarajia wala sikua na plan yoyote ya kumwoa
naomba ushauri kwa yafuatayo:
kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
je anaweza kuathiri wokovu wangu?
je naweza kwenda mbinguni?
je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?

Bora Mroma kuliko wewe unayesali Efatha.
 
Ee YESU wangu nisaidie!Kwahiyo RC hawataenda mbinguni.Mbona watu wanakariri majina ya dini kuliko mwokozi mwenyewe.

Asante sana. Maana hata na mimi nilikuwa najiuliza hili. Kumbe ndani ya Ukristu kuna classes? Mh
 
Inafaa sana kuishi bila kujitazama kuwa wewe ni bora zaidi kwa kuwa umeokoka! Suala hapa so kuokoka ama kutookoka mapenzi hayana hilo mpendwa wangu. Nakushauri kuwa msikivu kwa sauti ya mungu anayetuita sote kwake, mamoja umeokoka au laa! Kuokoka si kuwa ephata ama kuwa mkatoliki hata muislamu anayeishi vyema bila kuwadhuru wengine na kujali utu wa binadamu wengine anaweza kuwa ameokoka. Moyo wa mtuu ndo bwana anautazama! Kuwa makini na tabia ambazo walokole wengi wamekuwa wakizionesha, yaani mara nyingi wao hujiona bora kuliko wale wasiojiita wameokoka! Kujidhania mwenyewe umeokoka na kumwona asiye mwokovu ni mdhambi ni hatari sana maana mwenye kuhukumu mdhambi na mwenye haki ni mungu pekee! Sisi viumbe vyote ni mali yake na yatupasa kutohukumiana na kujiona sisi ni bora kuliko wengine!

Huu ushauri mzuri sana.
 
...mchungaji wako anasemaje,au hujui maana ya neno mchungaji...
 
wapendwa katika bwana
nimetatizwa na kitu hapa,mimi ni mlokole nasali Efatha bible,nimejaribu kuomba na ku connect na baadhi ya wapendwa wenzangu lakini nahisi sikufanikiwa
ila imekuja kutokea nikaonana na mwanamke ambaye anasali roman catholic na tumependana sana japo sikutarajia wala sikua na plan yoyote ya kumwoa
naomba ushauri kwa yafuatayo:
kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
je anaweza kuathiri wokovu wangu?
je naweza kwenda mbinguni?
je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?

Ndugu Episodes, nimepitia kidogo hoja zilizototewa na wana jamvi na nina amini utapata nyingi za kukusaidia kufanya maamuzi. Nachangia na kuimarisha nyingine kama ifuatavyo:
  • Ukishasema kuwa wewe ni mlokole, maana ya haraka ni kuwa wewe umezaliwa mara ya pili na ni kiumbe kipya anayeongozwa na Mungu katika njia zako
  • Inapokuja swala la ndoa, hii ni "serious business" unahitaji uongozi wa Mungu kuliko tunavyoweze kueleza, kosa hapa linaweza kukutoa kabisa katika mpango mzima wa Mungu katika maisha yako
  • Kwa sababu ya ushauri wa kwamba watu wawili hawawezi kwenda pamoja pasipokupatana, na pia ushauri wa neno la Mungu kwamba "msifungiwe nira kwa jinsi isivyo sawasawa", ni vizuri huyo mwenzako akawa amezaliwa mara ya pili kama wewe na mnaongozwa na Mungu kwa Roho wake.
  • Hapa siyo swala la dhehebu gani hata kama ni wa dhehebu moja na wewe, mnaweza kuwa na mwelekeo usiosawa "spiritually"
  • Issue ya kila mtu ni "specific" lakini ushauri wa ujumla ni vizuri kuoana watu wawili wanaokiri na kuamini wokovu (hata kama ni mroma , mpentecoste etc) mradi ni Kitu Mungu ana wapa kibali kufanya
  • Kama watu wawili walikuwa hawaamini wokovu wakati wanaowana halafu baadaye mmoja akaamini akaokoka, ushauri ni kuwa waendelee wote kwenye ndoa kwa upendo na mbele ya safari yule wa pili anaweza kupata neema naye akaamini.
  • Mwisho ukimpata mwenzi wako wa maisha ambaye alikusudiwa kwa ajili yako ndoa inaweza kuwa paradiso duniani! (changamoto zinakuwa exciting) vinginevyo inaweza iwe jehanamu duniai!
 
wapendwa katika bwana
nimetatizwa na kitu hapa,mimi ni mlokole nasali Efatha bible,nimejaribu kuomba na ku connect na baadhi ya wapendwa wenzangu lakini nahisi sikufanikiwa
ila imekuja kutokea nikaonana na mwanamke ambaye anasali roman catholic na tumependana sana japo sikutarajia wala sikua na plan yoyote ya kumwoa
naomba ushauri kwa yafuatayo:
kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
je anaweza kuathiri wokovu wangu?
je naweza kwenda mbinguni?
je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?

Mtu ambaye hajaokoka ni mtu wa aina gani? Na mtu aliyeokoka ni wa wa aina gani? Nini tofauti za hao watu wawili? episodes
 
Last edited by a moderator:
wapendwa katika bwana
nimetatizwa na kitu hapa,mimi ni mlokole nasali Efatha bible,nimejaribu kuomba na ku connect na baadhi ya wapendwa wenzangu lakini nahisi sikufanikiwa
ila imekuja kutokea nikaonana na mwanamke ambaye anasali roman catholic na tumependana sana japo sikutarajia wala sikua na plan yoyote ya kumwoa
naomba ushauri kwa yafuatayo:
kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
je anaweza kuathiri wokovu wangu?
je naweza kwenda mbinguni?
je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?
Kwani Mungu anakuambia nini?Piga goti uombe.Mke mwema hatoki Efatha au Rc bali hutoka kwa Bwana.Sisi hatuna majibu ya moja kwa moja vinginevyo tutakudanganya hapa
 
ni sawa mkuu huyo dada sidhani kama hana hofu ya mungu. okey kama unawasiwasi piga goti kwa mungu muulize huyu ndiye mke wangua kwa imani yako nadhani mungu atakupa jibu.

napata mashaka kidogo kama we ni mlokole kweli uliyesimama katika neno sawa sawa, nadhani huwa mnaamini mke /mume hutoka kwa mungu basi yawezekana wewe hukumwomba mungu wakati unamtafuta huyo binti.

pili mawazo ya mwanadamu si ya mungu mrudie mungu wako anza upya na bwana katika uhusiano wako huu uone jibu la mungu ni lipi. akisema endelea fanya hivyo akisema mwache fanya ivyo katika bwana.
 
kuhusu kumwoa tumeongea sana na yupo tayari,mahusiano alikuwa nayo kwa sababu ana mtoto mmoja na hawajawahi kuishi pamoja,kuhusu usumbufu mbele ya safari nahisi ndugu inaweza kuwa hivyo lakini namwona ni mwanamke mnyenyekevu sana kuliko wengi niliokutana nao makanisani
Ungefanya jambo la maana sana kama ungekuja kuomba ushauri kuhu hapo kwenye red.
kwani hilo ndilo jambo kubwa litakaloleta effect kubwa kuliko issue unayoomba ushauri.
 
kuokoka ni kumkiri Yesu kwa kinywa chako ya kua ni Mungu..na Kuacha dhambi
wewe uko Efatha yeye yuko RC sioni kama kuna shida yoyote kiroho hapo..as long as wote mnaamini katika Mungu mmoja kwa jina la Yesu kristo hayo mengine hayawazuii nyie kua pamoja na kujenga familia..
 
aliyekwambia kuokoka ni kusali Efatha nani? wokovu uko kwa m2 aliyeamua kuacha matendo maovu na kutenda yanayompendeza Mungu ww husemi uongo? huna wivu? husengenyi? hutharau? hupuuzi baathi ya wa2 wanaokushauri mema? hujawahi kuhukumu wengine kwa matendo yao?unawasaidia wenye shida mbalimbali ie;wajane,mayatima na maskini?una upendo kwa wote bila kujali hali, kabila au dini? unaheshimu wakubwa na wadogo? hujivuni kwa jinsi ulivyo? unafurahi kwa kila aliepata mafanikio?na mengine mengi bs ww umeokoka na kama mmekubaliana oaneni hakuna mtakatifu duniani!
 
Hao ni wazinzi na waasherati wenzako hawamjui Mungu na wala hawajawahi kuokoka. Kumbuka siyo kila anayesali kanisa la walokole ameokoka. Mtu haingii mbinguni kwa kusali kwenye kanisa la kilokole. La hasha. Wanaoingia mbinguni ni wale waliotubu dhambi na kumwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yao na kuacha dhambi. Full stop.
Unajifanya unaijuwa sana Biblia ehehee!! Yesu alikufa msalababani kwa ajili ya dhambi zetu sasa utasemaje sisi tuache dhambu ni dhambi zipi hizo?

Na hata kama zipo kuna mlokole yeyote mwenye kipima dhambi ambacho kinaonesha hii ni dhambi na hii siyo dhambi?
 
wapendwa katika bwana
nimetatizwa na kitu hapa,mimi ni mlokole nasali Efatha bible,nimejaribu kuomba na ku connect na baadhi ya wapendwa wenzangu lakini nahisi sikufanikiwa
ila imekuja kutokea nikaonana na mwanamke ambaye anasali roman catholic na tumependana sana japo sikutarajia wala sikua na plan yoyote ya kumwoa
naomba ushauri kwa yafuatayo:
kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
je anaweza kuathiri wokovu wangu?
je naweza kwenda mbinguni?
je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?

MMIE PIA NAOMBA NIKUJIBU KAMA IFUATAVYO-
1-kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
JE NI MADHARA AU ATHARI ZIPI NULIZIPATA KABLA YA KUWA MLOKOLE..KAMA ZIPO ZITAJE NA NINI UNADHANI KILIKUWA CHANZO?

2-je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
NAINGIWA WASIWASI NA ULOKOLE WAKO..MAAANA MPAKA SASA HUJUI VITU VINAVYOMUUDHI MUNGU..NA PIA KUMBUKA MUNGU WETU YU MWEMA KIASI KWAMBA YUPO PALE KUKUOKOA KILA MARA UNAPOANGUKA KATIKA DHAMBI NA UKIMWOMBA MSAMAHA HUKUSAMEHE BILA KINYONGO. TAFAKARI KATIKA AMRI KUMI ZA MUNGU KAMA KUNAKITU UTAKUWA UMEKOSEA KWA KUMUOA MKATOLIKI BASI USIMWOE UTAMUUDHI MUNGU.

3-je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
KWANI MAISHA YENU "HUKO MBELE" MUMEPANGA YAFIKE WAPI?..NA KWANINI HUJAMSHIRIKISHA MWENZIO KUHUSU HILI LA MAISHA YENU HUKO MBELE NA UMEKIMBILIA KUTUULIZA SIE AMBAO HATA HATUJUI MUNA-MPANGO GANI HUKO MBELE..HUJACHELEWA MSHIRIKISHE MWENZIO MIPANGO YA UKO MBELE UMSIKIE NA YEYE ANASEMAJE NDIO UJUWE KAMA MTAFIKA MBALI.

4-je anaweza kuathiri wokovu wangu?
WOKOVU WAKO UMEJENGEKA KATIKA MISINGI IPI UNAYOHOFIA KUIVUNJA AU KUIATHIRI?..KAMA KWELI WOKOVU WAKO UMEJENGEKA KATIKA AMRI KUU YA MUNGU NAYO NI UPENDO BASI UKIMWOA HUYU NA HASA AKIWA NI CHAGUO LA MUNGU KWAKO UTAKUWA UNAIMARISHA ULOKOLE WAKO.

5-je naweza kwenda mbinguni?
KUNA WIMBO UNAIMBA"MBINGUNI HATUENDI KWA...........BALI WENYE MOYO SAFI WATRAENDAAAAA" TAFUTA HUO WIMBO USIKILIZE UJUWE JINSI UNAVYOTAKIWA KUFANYA ILI UUPATE UFALME WA MBINGU.."UZA KILA ULICHONACHO WAPE MASIKIN KISHA UNIFUATE".

6-je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?
HUWA HAKUNA TOFAUTI KUBWA KATI YA WALOKOLE NA WAKRISTO WA MADHEHEBU MENGINE MAANA WOTE HUTUMIA KITABU KIMOJA CHA BIBLIA...NI TOFAUTI TU YA MITAZAMO NA UCHAMBUZI WA MAFUNDISHO YA MUNGU UNAOTUTOFAUTISHA NA PIA TAMAA ZA BAADHI YA VIONGOZI KUJITOA NA KUTAKA KUWA NA "MAKANISA YAO ILI WAPATE KUILA SADAKA YA BWANA"

ANGALIZO...MAMA AKIWA ANAIJUWA DINI VIZURI KULIKO WEWE(KITU AMBACHO UMEONYESHA HUUJUWI UKRISTO WALA ULOKOLE) JIANDAE KUMFUATA HUKOOO ROMAN CATHOLIC..ATAKURUDISHA KUNDINI WEWE ULIYEPOTELEA KWA MJASIRIA MALI MWINGIRA.

MASWALI YANGU KWAKO MKUU:-
1- KWANINI UMEOKOKA?
2- UNA MUDA GANI TOKA UOKOKE?
3- UNAIJUWA BIBLIA VIZURI?
5- USHAWAHI KUSOMA MAANDIKO HAYA "MKE MWEMA HUTOKA KWA MUNGU" "KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA" "WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA...NA MENGINEYO MENGI TU
6- UNA UMRI GANI KWA SASA?
7- HUYU MKATOLIKI ULIMPATAJE?
8-HAUDHANI KAMA ULITENDA DHAMBI WAKATI UNAMTONGOZA MKATOLIKI WAKO
9-UMEJUWA LINI KAMA HUYU MTARAJIWA WAKO NI MKATOLIKI?
10- KABLA HUJAOKOKA ULIKUWA DHEHEBU GANI?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom