Mimi ni Mlokole nataka kuoa Mroma

Mimi ni Mlokole nataka kuoa Mroma

hivi ukipanda na daladala na mtu asiye okoka una athilika nini?
kuna tatizo hapa katika sisi walokole ni kwamba tunaamini katika kujitenga kwetu ndio tunamwabudu MUNGU vizuri na watu wengine ni wapuuzi.
tunashindwa kuelewa kuwa watu wote wameokolewa kwa DAMU YA YESU.
tunashindwa kukumbuka kuwa wajibu wa mtu aliyeokoka ni kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wa YESU. bali tunajiona dhamira yetu kuwa wanafunzi wa YESU peke yetu na wengine hawastahili.
japo si mahala pake lakini naimani naelekezwa niyaseme haya. na wengi tutakubaliana imefika wakati walokole hata tukienda magerezani kuwatendelea wafungwa tunaenda kutoa msaada si kwa kadri na shida na mahitaji ya watu bali tunatoa kwa walokole wenzetu tu.
hii ni shida.
back to major topic
kutoka rohoni ningekushauri ni bora usimuoe kwakuwa hofu ya ndoa yako naiyona ipo kwenye uroma wake, huu unaweza kuwa mlango katika kutotulia na ndoa yako kwni hujiamini na kibaya zaidi unaonekana unataka kuingilia uhuru wake wa kuabudu bila kushiriki zaidi katika maombi na roho wa MUNGU akamwongoza.
umeweka shaka kubwa kuhusu imani yake na unaonyesha ubaguzi na hauko tayari kumtayarisha kuwa mnyenyekevu kwa MUNGU akiwa ndani ya dhehebu lake na unaamini kwako ndio kuna wokovu zaidi kwahiyo hii ni shida umekwenda zaidi na akili zako na sio roho anavyokuongoza.
hivyo ingia kwenye maombi upate kibali usije ukarudi hapa ukatusumbua ili hilo gereza la dhehebu linalokuletea hofu liondoke.
pole inawezekana nimeonekana nimekuhukumu lakini halikuwa lengo langu na MUNGU anisamhe kama nimefanya hivyo lakin lengo ni kutoa mawazo ambao pia yanaweza kuleta upana wa uchangiaji.
 
Ndugu mlokole unaoa mwanamke au uroma? Oa mwanamke anayefaa. Inaonekana wewe unataka kuoa dhehebu. Kasome Mithali 31:10-31 uone aina ya mwanamke wa kuoa. Usioe dhehebu hutapata mwanamke anayefaa kwani si wote hapo kwenu (kwenye ulokole) wana tabia inayofaa. Yesu alisema imani iendane na matendo. Kusema tu mimi ni mlokole wakati matendo ni tofauti si sawa. Angalia matendo zaidi kuliko ulokole au uroma. Namjua mtu mmoja alioa mwanamke akidhani ni mlokole kumbe balaa. Hiyo ndoa ilisambaratika na huyo bwana kaoa tena baada ya kuvumilia muda mrefu. Yule mwanamke alitoroshea watoto kenya. Alihangaika sana na sikumbuki kama aliwapata wote. Mtu anaweza akajifanya mlokole ili tu aolewe au aoe akibaini kuwa ulokole ni muhimu katika mada ya ndoa. So take your time and choose a good and intelligent wife not otherwise. By the way I am also a believer!! Read James 2:14-26.

Mkuu umegusa pale nilipotaka kumwambia, kwa kumuongezea asome 2Wakorinto 14:18. Ningekuwa karibu na Biblia ningemwandikia.
 
Unajua mkuu katika watu ambao huwa nawadharau kwa kiasi kikubwa ni Walokole...Hawa watu ni waajabu sana....Lakini nilichogundua ni kuwa hawa viumbe wa ajabu kichwani ni watupu mno..Wangekuwa na elimu ingewakomboa angalau...

Mkuu, Mwalimu Mwakasege hajasoma?
 
namwona ni mwanamke mnyenyekevu sana KULIKO WENGI NILIOKUTANA NAO MAKANISANI[/QUOTE]

kumbe walokole hamna kitu,ndomana mapepo hayawaishi kila kukicha. nimejifunza kitu.
 
Inategemeana na maamuzi yenu wawili, kama mmeafikiana kuhusu hilo la imani sidhani kama kuna tatizo.
 
hivi ukipanda na daladala na mtu asiye okoka una athilika nini?
kuna tatizo hapa katika sisi walokole ni kwamba tunaamini katika kujitenga kwetu ndio tunamwabudu MUNGU vizuri na watu wengine ni wapuuzi.
tunashindwa kuelewa kuwa watu wote wameokolewa kwa DAMU YA YESU.
tunashindwa kukumbuka kuwa wajibu wa mtu aliyeokoka ni kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wa YESU. bali tunajiona dhamira yetu kuwa wanafunzi wa YESU peke yetu na wengine hawastahili.
japo si mahala pake lakini naimani naelekezwa niyaseme haya. na wengi tutakubaliana imefika wakati walokole hata tukienda magerezani kuwatendelea wafungwa tunaenda kutoa msaada si kwa kadri na shida na mahitaji ya watu bali tunatoa kwa walokole wenzetu tu.
hii ni shida.
back to major topic
kutoka rohoni ningekushauri ni bora usimuoe kwakuwa hofu ya ndoa yako naiyona ipo kwenye uroma wake, huu unaweza kuwa mlango katika kutotulia na ndoa yako kwni hujiamini na kibaya zaidi unaonekana unataka kuingilia uhuru wake wa kuabudu bila kushiriki zaidi katika maombi na roho wa MUNGU akamwongoza.
umeweka shaka kubwa kuhusu imani yake na unaonyesha ubaguzi na hauko tayari kumtayarisha kuwa mnyenyekevu kwa MUNGU akiwa ndani ya dhehebu lake na unaamini kwako ndio kuna wokovu zaidi kwahiyo hii ni shida umekwenda zaidi na akili zako na sio roho anavyokuongoza.
hivyo ingia kwenye maombi upate kibali usije ukarudi hapa ukatusumbua ili hilo gereza la dhehebu linalokuletea hofu liondoke.
pole inawezekana nimeonekana nimekuhukumu lakini halikuwa lengo langu na MUNGU anisamhe kama nimefanya hivyo lakin lengo ni kutoa mawazo ambao pia yanaweza kuleta upana wa uchangiaji.
Mkuu umemaliza kila kitu.
 
wapendwa katika bwana
nimetatizwa na kitu hapa,mimi ni mlokole nasali Efatha bible,nimejaribu kuomba na ku connect na baadhi ya wapendwa wenzangu lakini nahisi sikufanikiwa
ila imekuja kutokea nikaonana na mwanamke ambaye anasali roman catholic na tumependana sana japo sikutarajia wala sikua na plan yoyote ya kumwoa
naomba ushauri kwa yafuatayo:

kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
je anaweza kuathiri wokovu wangu?
je naweza kwenda mbinguni?
je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?
Nakushauri uonane na Nabii Mwingira umuulize suala hilo nadhani ndiye mchungaji wako, atakusaidia kiroho zaidi kuhusu hilo na hiyo ndiyo njia sahihi ndg yangu, hata sisi tukikushauri namna gani mwisho wa siku mchungaji ndiye atafungisha ndoa yenu, kwa hiyo tafadhali usifanye siri yoyote kwa mchungaji wako mwambie kwa uwazi na atakusaidia kiroho, na ukitaka kufuata njia iliyo sahihi ni LAZIMA mchungaji wako ajue hilo
 
Tatizo la walikole ndio hili..kujifanya wao ni watakatifu na mbinguni ni kwao..ss km kwa style hii ya ubaguzi mbinguni mtafika.??? Umejihakikishiaje au kwa kujifanya umeokoka huku unabagua..yesu mwenyewe aliwapenda wabaya kwa wema..tena wale wabaya aliwapenda zaidi ili apate kuwakomboa na waweze kumpenda muumba..iweje nyinyi mnaoabudu/kutumikia kina mwingira mjione boora....maana ukiuliza unasali wapi..nasali kwa mwingira. .kwa rwakatale..kwa mzee wa upako..fungukeni enyi misukule mnatumiwa bila kujijua..KANISA NI MOJA TU NALO NI LA YESU KRISTO...sasa kanisa la fulani fulani..ndo ushetani wenyewe pendaneni muache kubagua wakristo wenzenu..mm nawapenda sana wasabato huwa wanaishi maisha yao..hawakebehi wenzao...hawadharau..hawakulazimishi uwafate km hizi dhehebu za kibiashara zinavyofanya kuutwa
 
AMOSI 3:3 je watu 2 waweza kutembea pamoja wasipokuwa wamepatana? mkioana mtakuwa mnasali wapi? romani au efatha?

Tokeni kati yao mkatengwe nao. Kuna uhusiano gani kati ya Kristo na beliari au kati yake yeye aaminiye na asiyeamini?
 
Ndugu mlokole unaoa mwanamke au uroma? Oa mwanamke anayefaa. Inaonekana wewe unataka kuoa dhehebu. Kasome Mithali 31:10-31 uone aina ya mwanamke wa kuoa. Usioe dhehebu hutapata mwanamke anayefaa kwani si wote hapo kwenu (kwenye ulokole) wana tabia inayofaa. Yesu alisema imani iendane na matendo. Kusema tu mimi ni mlokole wakati matendo ni tofauti si sawa. Angalia matendo zaidi kuliko ulokole au uroma. Namjua mtu mmoja alioa mwanamke akidhani ni mlokole kumbe balaa. Hiyo ndoa ilisambaratika na huyo bwana kaoa tena baada ya kuvumilia muda mrefu. Yule mwanamke alitoroshea watoto kenya. Alihangaika sana na sikumbuki kama aliwapata wote. Mtu anaweza akajifanya mlokole ili tu aolewe au aoe akibaini kuwa ulokole ni muhimu katika mada ya ndoa. So take your time and choose a good and intelligent wife not otherwise. By the way I am also a believer!! Read James 2:14-26.

Mke mwema hutoka kwa Bwana.
 
Kwahiyo ujui kuwa roma ndiyo kanisa kristu aliloacha? Ujui kuwa roma ndiyo ukristu wa kweli? Achana na conspiracy theories , tena fanya research juu ya catholic church...nenda catholic.com, whyimcatholic.com utapata majibu juu ya imani ya kikatoliki na siyo mataptap ya wasabato na wapteotestanti aka waasi...

Acha kujidanganya. Ingekuwa hivyo mapapa wasingewauwa mitume wa Bwana Yesu.
 
je naweza kwenda mbinguni?

kwanini usiende?hata kama ungemuoa mjahidina,ungeenda tu.
si utakuwa umetimiza amri ya mapendo ambayo ndiyo kubwa kuliko amri zote?
ila tu kumbuka,mbinguni hawaendi wawili,wawili.
unaweza ukaenda wewe na kiburudisho chako kikaenda kupigwa kiberiti,au kiburudisho kikaenda mbinguni na wewe ukaenda kusota.
au wote wawili,mkaenda eitha mbinguni au kula stiki kwa Shaitwan
 
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je naweza kwenda mbinguni?

Je, Wakatoliki ni chukizo kwa Mungu?
Je,Wakatoliki hawatakwenda mbinguni?
Kama nimekuelewa vizuri,maswali yako yana-suggest kuwa Wakatoliki ni wakosefu hivi...naomba maelezo hapo ili niweze kushauri
 
Unajua mkuu katika watu ambao huwa nawadharau kwa kiasi kikubwa ni Walokole...Hawa watu ni waajabu sana....Lakini nilichogundua ni kuwa hawa viumbe wa ajabu kichwani ni watupu mno..Wangekuwa na elimu ingewakomboa angalau...

Wewe unawadharau kwa kuwa una roho ya Ibilisi baba yako. Wao wanakuombea ili upate fahamu uokoke uingie mbinguni. Bwana Yesu alikuja kutafuta na kuokoka kilichopotea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom