Milipuko yatikisa Zanzibar

Milipuko yatikisa Zanzibar

Spring Doctors wako kazini sasa, Issue ya Posho ndo inasahaulika hivyo!!!!
 
Halafu hawajui kuwa vitendo hivi vinazidi kuitenga Zbar na jumuiya ya kimataifa.

Na ndio maana anti - Zanzibar wanafanya hivi ili kuitia doa Zanzibar na watu wake kwa mwamvuli wa uislamu. Tangu Wazanzibar waamke na kudai zanzibar yao ndipo matokeo haya yanafanyika na utaona media za upande wa pili wa muungano ukizidisha chumvi katika matokeo yanayotokea zanzibar kana kwamba Tanganyika watu hawamwagiwi tindikali, kupigwa risasi, milipuko ya mabomu na kadhalika.
 
Milipuko hii kama kweli ni mabomu basi wenye makosa ni serikali kutokuwa makini na matatizo hayo toka mwanzo.Sijaona kilichofanyika ili kuwapata wahalifu,na sijui wanaona furaha gani watanzania wakirumbana kwa mihemuko ya udini wakati huo ni uhalifu na auhusiani na dini yoyote.Sipendi na sitaki kuaminishwa kwamba ni usilamu bali huyo aliyeweka mabomu hayo ni mhalifu tu na wala si kuweka dini mahali penye uhalifu ambao unaweza kutolewa majibu sahihi na wakosaji wakaadhibiwa.Rai yangu kwa Wanzanzibar bila kujali dini zao inabidi wafanye doria wenyewe ili kuwakamata wahalifu hawa.Kwa kweli wanaudhi.



...mkuu' ni wahuni tu, kama wale walio haribu, kuvunja na kuchoma Makanisa mbalimbali hapa Tanzania (hasa kama wale wa Mbagala, baada ya kukojolewa kitabu)
 
Usemacho Barubaru ni kweli kabisa.
Kanisa katoliki limeshadai hizo repoti hadi basi. Kinachotakiwa ni Uwazi wa repoti hizo na hatua za kisheria zilizochukuliwa.
 
Mmh! Kila siku kukiwa na issue HOT ndiyo matukio yanatokea!Siyo janja ya MaCCM kutupotezea concentration ili yajiongezee posho na kulazimisha serikali mbili kwenye bunge la katiba kweli? Hasa kama hakuna maafa nitapata maswali mengi zaidi.
 
Usemacho kama kinakaukweli fulani vile ndani yake :suspicious:
 
...mkuu' ni wahuni tu, kama wale walio haribu, kuvunja na kuchoma Makanisa mbalimbali hapa Tanzania (hasa kama wale wa Mbagala, baada ya kukojolewa kitabu)

Nitapingana na wewe viongozi wetu wanapenda kutumia lugha nyepesi hivi muhuni anapata wapi mabomu?Hawa ni wahalifu wanaoharibu amani na upendo tulionao watanzania.Serikali inatakiwa iwatafute ili tuapate amani.
 
Wakati haya yanazidi kutokea.je waandish wa habar wa zanzibar ni mara ngap mmeendesha kampeni ya kupinga hivi vitendo,maana wananchi wanawasikiliza vyombo vya habar sana.Home work kwenu tafuteni hata wimbo mpya wa afande sele unaitwa Africa dini zimeletwa muwapigie hao ndugu zetu baadhi wanaojiona wao ndio wako sahihi.
 
Watu wanataka kujitenga na wameonyesha dhahir kutuchukia, sasa sijui tunawang'ang'ania wa nini?

Sisi wa chama cha mapinduzi tunataka serikali mbili na muungano ni lazima.ukibisha tunakuvua ubunge kama yule jamaa wa zenji sawa wewe? Mtu mwenyewe CCM umevamia bila kukaribishwa unatuletea za kuleta hapa? Huu ni mda wetu wa kula so tupishe. Mmxxxiiiu
 
Duh!! Kanisani tena kumbe ndio maana katika wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar kati ya 67 Wakristo ni 2 na wote wametoka katika kipengere cha vikundi vya Kidini. inamaanisha kama kungekuwa hakuna kipengere cha dini Kutoka Zanzibar kusingekuwepo na Mkristo.
Mkuu unastuka leo kwani kwenye safu za viongozi wa serikali ya Zanzibar wakristo ni wangapi?
ndo maana nashangaaga nikisikia watu wanasema mfumo kristo huwa sielewi.
 
Solution ya hawa magaidi hapo unguja ni kuwajazia wabongo wanne kwa kila mzenji mmoja tunapeleka wabongo milion sita hapo unguja. Case inakuwa closed
 
Nitapingana na wewe viongozi wetu wanapenda kutumia lugha nyepesi hivi muhuni anapata wapi mabomu?Hawa ni wahalifu wanaoharibu amani na upendo tulionao watanzania.Serikali inatakiwa iwatafute ili tuapate amani.
Aliyemuua yule padri si alipatikana,ulishasikia habari zake tena? hizi ni move za kuchonga,msimamo wa CDM wa kujilinda uigwe na makanisa kule Zanzibar.
 
Hapa wakuu ndiyo ninapo ona umhimu wa wale wanao taka serikali tatu.Hawa jamaa wana ona wana dhulumiwa na muungano.Hawawataki wa bara kule.Ole wako useme una itwa John au Peter umekwisha.Tenda tu dhambi sema unaitwa Seleman Bin Hemed Bin Jumaa hapo utakaribishwa hata kahawa
 
Nimbinu ya Ccm kutuhamisha kutoka kwenye katiba mpya tukalie kujadili magaidi halafu wapate mwanya wowote hata kwa Rushwa hao wajumbe alafu wampitishe Mzee wavijisent kuwa Spika
 
itakuwa ni mazoezi ya kijeshi tu, mbona mimi naangalia TBC1 sasa hivi sijaona breaking news na TBC1 ndiyo tv ya umma, lazima kwa jambo kama hili wasingeachia vyombo vingine pekee ndiyo vitoe habari. ikiwa hivyo nitaamini kweli TBC1 sio ya umma.
TBC1 bado wanaifanyia utafiti habari hii na kusubiri tamko la polisi.Wasubiri watakujulisha.
 
Back
Top Bottom