Mila hizi za Kichaga mnazionaje wenzangu

Mila hizi za Kichaga mnazionaje wenzangu

Suala la kafara bado lipo na wazungu wanaendelea kutoa hadi kesho, Wahindi, wachina, waarabu nk, Tatizo lako umeamua kuwa limbukeni wa mila za kizungu kwa kuaminishwa kupitia biblia.

Familia maarufu Ulaya kwa kiasi fulani wanafanya haya haya wanayo fanya Wachagga na Makabila mengine. Achana na makapuku wa Kizungu na hawa wanaopata umaarufu kupitia Michezo,Uigizaji Sinema,Ubunifu,nk.
 
Kuna nyingine umesahau... kama mtoto amezaliwa nje ya ndoa, siku ya kukaribishwa nyumbani kwao, mbuzi mmoja anakatwa sikio na mtoto anachanjwa kutoa damu kisha damu ya mtoto na damu ya mbuzi zinachanganywa. Mi huwa najuliza, kwa nini wanachanganya damu ya mtu na ya mbuzi.. inamaana huyo mtoto ni mfugo pia? Kwa nini damu ya mtoto mgeni isichanganywe na damu ya watoto wengine wa familia kama ni lazima kuchanganya damu? Kifupi hii pia ni maneno mbofu mbofu tu.

Duh! kumbe Wachagga waliozaliwa nje ya ndoa ni mbuzi tu.

Kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Sijasema ni ushirikina ila ukishakufa umekufa uzikwe, uchomwe moto haitasaidia kitu. Unaweza liwa na mnyama hata mabaki ya maiti yasipatikane au kama wale waliopotea na ndege, waliokufa kwenye maji MV Bukoba n.k. Kuzika popote ulipowekeza na kuishi muda mrefu mi naona ni bora zaidi.

sasa kama wewe ndo waona si ubaki nayo rohoni mwako ya nini kulalama hapa sasa?
 
Inawezekana kweli, ndio maana nikasema mazingira ya makuzi yanaathiri, kama huna mchepuko, labda ulipokulia michepuko ilikuwa marfuku.


Pamoja na hayo, linganisha uchepukaji wa wanamme wa kisukuma na kichaga kwa mfano wengi wao. Ukipata jibu utajua nachosema, mazingira ya makuzi yana athari kuliko unavyofikiri.

Konie hebu nipe mwanga...wepi wanaongoza kuchepuka Kati ya hayo makabila mawili?
 
Ukisikia kutokuelemika ndiyo huku. Ebu jiulize kuna connection gani kufukia kitovu cha mtoto migombani ili asiugue au kutahiri msichana ili awe mzuri....wachagga wanafanya hivi.
 
Wewe tatito ni moja tu, you don't know the different between culture and traditional
 
Mila sio zote zenye nafasi, zipo baadhi hazifaikabisa kama kutoa kafara ya kuchinja mbuzi na kunyunyiza damu, kwa mfano umenunua gari mpya, umejenga nyumba unatakiwa ufanye, huu mi nauona ni ushirikina kwa nini msifanye sala tuu kwa jina la Yesu.

Nyingine kwa mfano kufukua kaburila marehemu na kutoa mifupa yote na kuiweka kwenye mgomba.

Nyingine kupelekangozi ya kitovu cha mtoto mchanga kinachokatikaga kwa Babu na Bibi eti ilimtoto asiwe anauguagua ovyo.

Au lazima kwenda kuzika Moshi wakati unakutamarehemu amejijenga na kushi sehemu nyingine miaka yote na kwao hata nyumba hana.

Rubish
 
hebu #misschagga njoo uhakiki haya ni ya kweli?

ni kweli wanachosema ila inategemeana na mchaga wa sehemu gani..... Lakuchimba mifupa ya marehemu ilikuwa kwa ajili ya kuweka ulinzi kwenyi mipaka ya mashamba na ukivuka pale lazima upate shida naomba kumkosoa mleta mada huwa inawekwa kwenye jiwe kubwa ambalo huwanje ya nyumba hapo linawekwa fuvu la babu au mtu mkubwa wa ile familia na si wote wanafanyiwa hivyo.......

Na sehemu nyingine ya mifupa huwekwa kwenye mipaka ambayo hutenganishwa na masale. huwa kuna majani fulani wanayaita masale ndipo wanapoweka ni hizi mila zilishakufa tokea kuja kwa dini ya kristo ...... Kwa miaka hii ni familia chache sana wanafanya huo mchezo..... Nimekulia kijijini nacho sema ndio ukweli kwenda kuzikwa nyumbani ni heshima kubwa sana ndio maana kama huna nyumba moshi au eneo katika ukoo uwezi enda zikwa huko wapo radhi wajenge hata nyumba ya tope alafu uzikwe la sivyo wanasema umezikwa pateni..... Pateni ni eneo huwa mara nyingi alizalishi na sehemu wanyanma wanakula nyasi huwa migomba haioti ni pakavu sana.......

Ila mkuu kutambika mara ya mwisho niliona wamefanya huo mchezo nilikuwa darasa la tano na nilikunywa kisusuio nikachapwa na mama sana kwa sababu nilienda kukaa na wanaume wakati wanachinja hairuhusiwi... Ila kwa kuwa mimi ni kpenzi cha baba yangu haikuwa shid kwake ila mama ilikuwa tabu nikapewa kibano vizuroi tokea hiyo siku sijaona tena wakichinja mbuzi sijauliza kwa nini lakini? Ila mimi nahisi ni mda wa kukutana haupo tupo bussy sana kutafuta hela,,,,, baa zetu hawjaependa tuendeleze hizo mila.... Kufa kwa mababu zetu waliokuwa wanpenda hizo mila..... Uchumi pia mbuzi bei yake kidogo ni nzuri kuchinja inaleta hasara...... Pia dini nayo imechangia kiasi kikubwa.......

Hope umeelewa kidogo... Kwa mimi hizi mila hazina ubaya hata kidogo ni nzuri sea zipo kwa eneo dogo na tunaziua kwa mila za wazungu tunzozitukuza na kuona hao ndio bora kuliko sis....... Kumbuka wenzetu nao zile ni mila kama zetu tu sema zao walikuwa na uwezo mkubwa wa kuambukiza dunia kuliko sisi.......
 
Mila sio zote zenye nafasi, zipo baadhi hazifaikabisa kama kutoa kafara ya kuchinja mbuzi na kunyunyiza damu, kwa mfano umenunua gari mpya, umejenga nyumba unatakiwa ufanye, huu mi nauona ni ushirikina kwa nini msifanye sala tuu kwa jina la Yesu.

Nyingine kwa mfano kufukua kaburila marehemu na kutoa mifupa yote na kuiweka kwenye mgomba.

Nyingine kupelekangozi ya kitovu cha mtoto mchanga kinachokatikaga kwa Babu na Bibi eti ilimtoto asiwe anauguagua ovyo.

Au lazima kwenda kuzika Moshi wakati unakutamarehemu amejijenga na kushi sehemu nyingine miaka yote na kwao hata nyumba hana.

Tuache na Mila zetu .....tunafurahia kudumisha mila na desturi zetu
 
Back
Top Bottom