Mila hizi za Kichaga mnazionaje wenzangu

Mila hizi za Kichaga mnazionaje wenzangu

ndugu yangu? wewe ni kabila gani?
kabila lenu halina mila mpaka uanze kunyooshea mikono wachaga?
mi naona maisha yashakupeleka resiii, hao wachaga unaosema wanamila potofu wewe zinakudhuru nini?

Mi kabila langu jina linajieleza na huu ni uchambuzi tuu wa maswala mbalimbali hayana uhusiano na kashfa wala dharau kwa wachaga. Punguza hasira naona umesimama kaa chini utulie.
 
Before colonial era na hizi mila za kizungu mnazoziona za kistaarabu tulikuwa na tamaduni zetu...Hii western culture naona imewasweep wengi na soon mtajiona hata hizi rangi zenu hazifai tena, recommended rangi ni toka kwa weupe...Mimi najivunia kuwa nilivyo, najivunia utamaduni wangu hata kama ni wa kula nyau who care!
 
Ahsante mkuu Ndetirima kwa kuja kivingine. Kuna uzi niliuweka hapa wenye maudhui kama yako naona mods wameuondoa. Mila za kichagga mpaka sasa bado zina nguvu na ukizifanya unapata matokeo uliyokusudia. Matatizo mengi yaliyomsumbua mtu(mchaga) hupatiwa ufumbuzi kwa kufanya mila ambayo haina gharama. Gharama zake ni mbuzi au kondoo na mbege kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Mila sio zote zenye nafasi, zipo baadhi hazifaikabisa kama kutoa kafara ya kuchinja mbuzi na kunyunyiza damu, kwa mfano umenunua gari mpya, umejenga nyumba unatakiwa ufanye, huu mi nauona ni ushirikina kwa nini msifanye sala tuu kwa jina la Yesu. Nyingine kwa mfano kufukua kaburila marehemu na kutoa mifupa yote na kuiweka kwenye mgomba. Nyingine kupelekangozi ya kitovu cha mtoto mchanga kinachokatikaga kwa Babu na Bibi eti ilimtoto asiwe anauguagua ovyo. Au lazima kwenda kuzika Moshi wakati unakutamarehemu amejijenga na kushi sehemu nyingine miaka yote na kwao hata nyumba hana.

Hata hao waliokuletea dini ya Yesu wanatoa kafara, usiwe limbukeni wa mila za weupe, kwa taarifa yako tu hakuna watu ambao hawatoi kafara toka Marekani hadi Japan, India, Arabuni etc. Sasa wewe kuwa limbukeni wa mila za wazungu eti kisa wamekuaminisha kwa njia ya biblia wakati hata hiyo biblia yenyewe inakubali utowaji wa kafara.
 
Inawezekana kweli, ndio maana nikasema mazingira ya makuzi yanaathiri, kama huna mchepuko, labda ulipokulia michepuko ilikuwa marfuku.


Pamoja na hayo, linganisha uchepukaji wa wanamme wa kisukuma na kichaga kwa mfano wengi wao. Ukipata jibu utajua nachosema, mazingira ya makuzi yana athari kuliko unavyofikiri.

Kony hapa una-assume sana sasa, sio kila mtu amelelewa kwenye hizi tamaduni. Besides si kila mwanaume ana michepuko.
 
Watu hawajui kuwa hata kwenye dini kuna kafara au sadaka.

Zile habari zote za agano la kale walikuwa wanatoa sadaka za kuteketeza, na sadaka kuu na ya mwisho iliyoondoa sadaka za kuteketeza ni sadaya ya Yesu mwenyewe.

Hata hao waliokuletea dini ya Yesu wanatoa kafara, usiwe limbukeni wa mila za weupe, kwa taarifa yako tu hakuna watu ambao hawatoi kafara toka Marekani hadi Japan, India, Arabuni etc. Sasa wewe kuwa limbukeni wa mila za wazungu eti kisa wamekuaminisha kwa njia ya biblia wakati hata hiyo biblia yenyewe inakubali utowaji wa kafara.
 
Nyingine kwa mfano kufukua kaburi la marehemu na kutoa mifupa yote na kuiweka kwenye mgomba.

Mimi siifahamu malengo ya huu utaratibu, na kama kuna kingine huwa wanafanya.
Ila nimuulize mleta mada, shida ya huu utaratibu iko wapi? Hauoni faida ya desturi hii ikiboreshwa kidogo?
 
Hata hao waliokuletea dini ya Yesu wanatoa kafara, usiwe limbukeni wa mila za weupe, kwa taarifa yako tu hakuna watu ambao hawatoi kafara toka Marekani hadi Japan, India, Arabuni etc. Sasa wewe kuwa limbukeni wa mila za wazungu eti kisa wamekuaminisha kwa njia ya biblia wakati hata hiyo biblia yenyewe inakubali utowaji wa kafara.

Mkuu watu huwa hawaelewi. mimi sifagilii kafara kabisa, ila hakuna watu wanatoa kafara kama hao watu weupe. Tena bora wachaga wana chinja mbuzi, watu weupe kafara zao kubwa ni binaadamu wenzao. Naskia wachina walileta container lililojaa miili ya watu kwa ajili ya kafara ili waweze kufanya biashara Tanzania bila matatizo, na naskia pia miungu ya Tanzania imekubali kafara hizo ndio maana unaona wachina wamejaa Tanzania wanafanya hadi umachinga japo kiswahili hawajui. Chezea ngozi nyeupe wewe...
 
Mitoto ya siku izi inazaliwa mjini imeathiriwa na TV an fesibuku... haijui hata utamu wa mila!! ndio hawa hawa wanatetea mambo ya mwanaume kupumuliwa kisogoni a mwanaume mwenzie! Tudumishe mila zetu kama unaona hazifai zikaushie kivyako kuja kuuliza kama ni sawa haihusu,, its individual level

Burudika na Late Ebbo hapa Mr Ebbo - Mimmasai | Muziki.net
 
Ha ha haaaa.....Kwa hiyo kusoma ndio kuacha mila zako? Mie nashauri wataalamu waje watufafanulie hapa maana ya mila na desturi. Maana uelewa wetu wengi ni mdogo. Maana mambo mengine ni mila za wazungu sie tunaiga na tunaona zao ni nzuri. Mila zipo, na zitaendelea kuwepo
 
mimi huwa nachoga sana nikiangaliaga haya mafuvu na mifupa ya watu iliyowekwa huku kwnye masale baada ya kufukuliwa kweli kna mila nyngne daah bas tu hatunajins tumezikuta inabid tuziache zilivyo.
 
kiukweli, unaweza ona mila za wenzako kama zinakushangaza ila waache wazifanye kama hawavunji sheria.
 
Sijasema ni ushirikina ila ukishakufa umekufa uzikwe, uchomwe moto haitasaidia kitu. Unaweza liwa na mnyama hata mabaki ya maiti yasipatikane au kama wale waliopotea na ndege, waliokufa kwenye maji MV Bukoba n.k. Kuzika popote ulipowekeza na kuishi muda mrefu mi naona ni bora zaidi.

Sawa chasaka tumekuelewa nyumbani ni nyumbani hata kama ni porini.
 
Frankly speaking, hizo ni Kafara na zina wa cost sana sana. We angalia nguvu ya hao mizimu inavyowavuta kila mwisho wa mwaka wende kutoa sadaka za damu, na huwa wasipoenda wanakufa wenginewanapata ajali. hii ni chambo ibilisi anawamaliza kistaili kwa sababu shetani anapotaka damu baadaye anatake damu ya mtu. kama wewe ni mchaga fanya mpango ukawakomboe ndugu zako wamwamini Mungu wa Kweli. Seriouly sisi Tulijaribu kwenda kuzivunja hizo mila kwa njia ya maombi tukafanikiwa lakini vita ilikuwa kali mno. Mungu anaweza of course wanahitaji masaada wa haraka kwa kuwa wengi wao wanachanganya Mungu na miungu na matokeo yake Mungu amewaacha. Mf nasikia wanapotoa nywele wakati wa msiba ni mapango wa shetani kuandaa mtu mwingine atakayekufa next. inasikitisha na wanahitaji maombi. Tofauti na mikoa mingine ambao wengi wao hawamjui Mungu ni rahisa kuwahubiria juu ya Mungu wa kweli. Lakini hawa wanachanganya...kanisani mila na kwa waganga. Urgent need for intercession!
 
Mitoto ya siku izi inazaliwa mjini imeathiriwa na TV an fesibuku... haijui hata utamu wa mila!! ndio hawa hawa wanatetea mambo ya mwanaume kupumuliwa kisogoni a mwanaume mwenzie! Tudumishe mila zetu kama unaona hazifai zikaushie kivyako kuja kuuliza kama ni sawa haihusu,, its individual level

Burudika na Late Ebbo hapa Mr Ebbo - Mimmasai | Muziki.net

Hembu waambie hawa mboga saba za mawazo enzi za mababu kijana akitaka kuoa lazima ile familia anayotoka yule bint ichunguzwe pamoja na tabia za huyo chaurembo kuanzia maradhi, maadili na kadhalika mpaka uchawi kama kwenu wazazi wako wanga basi kijana,
Ataelezwa ukweli na akijifanya nunda unaachiwa kitakachotokea mbeleni usijemlaumu mzazi, na lazima bint akutwe ng'aring'ari siku ya ndoa basi utawajengea heshima kubwa sana wazazi waliokulea watapelekewa zawadi kemkem ,
Ukilala nje yaani kwa mwanaume basi huruhusiwi kurudi nyumbani ubaki hukohuko kinachofuata ni taratibu za mahari na faini,
Sio siku hizi vijana wanakutana face book usiku asubuhi wameshatangaza nia ya kuona ndio maana maadili hakuna ukichanganya na yale maradhi ya kurithi kama pumu, kisukari nk unapata bomu la iraki tudumishe tamaduni zetu zilizokuwa nzuri zilizo na vikwazo huna budi kuziweka kando kama kuzika mtu akiwa hai nk.
 
Mila na desturi haziishi. Hata huko ulaya zimejaa tele. Google ni bure kabisa we ingia tu. Walokole halisi hawadharau mila, wanaodharau ni walewasiojitambua.
 
Acha kujidai umeokoka kuliko mchungaji, mila zote mbaya? Mila ni nini na uchawi ni nini?

Ndio mila nyingi zinaambatana na imani potofu mf:kuzika watoto hai eti ili kufanya amani baina ya koo n.k ni ushilikina tu,huwezi kutenganisha ushilikina na uchawi. Nafikiri bwana Pembe hakujidai eti kwakuwa ameokoka isipokuwa ameeleza ile kweli,kweli tupu.
 
Back
Top Bottom