Mila hizi za Kichaga mnazionaje wenzangu

Ndetirima

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
1,008
Reaction score
790
Mila sio zote zenye nafasi, zipo baadhi hazifaikabisa kama kutoa kafara ya kuchinja mbuzi na kunyunyiza damu, kwa mfano umenunua gari mpya, umejenga nyumba unatakiwa ufanye, huu mi nauona ni ushirikina kwa nini msifanye sala tuu kwa jina la Yesu.

Nyingine kwa mfano kufukua kaburila marehemu na kutoa mifupa yote na kuiweka kwenye mgomba.

Nyingine kupelekangozi ya kitovu cha mtoto mchanga kinachokatikaga kwa Babu na Bibi eti ilimtoto asiwe anauguagua ovyo.

Au lazima kwenda kuzika Moshi wakati unakutamarehemu amejijenga na kushi sehemu nyingine miaka yote na kwao hata nyumba hana.
 
Kuna nyingine umesahau... kama mtoto amezaliwa nje ya ndoa, siku ya kukaribishwa nyumbani kwao, mbuzi mmoja anakatwa sikio na mtoto anachanjwa kutoa damu kisha damu ya mtoto na damu ya mbuzi zinachanganywa. Mi huwa najuliza, kwa nini wanachanganya damu ya mtu na ya mbuzi.. inamaana huyo mtoto ni mfugo pia? Kwa nini damu ya mtoto mgeni isichanganywe na damu ya watoto wengine wa familia kama ni lazima kuchanganya damu? Kifupi hii pia ni maneno mbofu mbofu tu.
 
Uamuzi unao mwenyewe umeenda shule unajua lipi baya na lipi jema. Fanya lililo jema na Mungu wako atakujazi. Sio wote ni Wakristu, wengina hawana dini wengine ni Waislamu.

Mila na desturi mara nyingi zililenga kupata mlo. Ukichinja wewe na nduguzo mtapata posho, ukitengeneza mbege kijiji kitakunywa etc! Sasa hiyo ya kuomba waliotangulia mbele ya Haki sijui umuhimu wake na ukweli wa matokeo yake.

Zamani nasikia mvua isponyesha kwa muda mrefu kijiji mnaitana mnchinja kondoo mnakula nyama lile tumbo mnaenda kulitumbukiza mtoni pale ambapo maji yametulia na wanasema kabla hamjafika nyumba mvua lazima inyeshe. Sasa sijui hiyo ni sayansi gani lakini maisha yalisonga mbele!

Mila mbaya ni ile ya kuzika watoto (sio wachanga) wakiwa hai kwenye mipaka kama ishara ya kutakiana amani kati ya koo au vijiji.

Iliyo kiboka zaidi ni ile mkishikwa mnafanya ngono kabla ya ndoa, mnapandishwa msitu wa mlima Kilimanjaro mnavua nguo mnalaliana halafu jiti linachomekwa kutoka mgongoni hadi ardhini mnaachwa hapo mpaka mnakufa! Hii nasikia ilileta nidhamu sana kwa Wachagga.
 
Nyingi ya hizi mila zimepitwa na wakati na kwa sababu ya dini na shule wengi wameshaziacha. Na ukiona anayengangania ujue huyo ni mchawi.
 
Acha kujidai umeokoka kuliko mchungaji, mila zote mbaya? Mila ni nini na uchawi ni nini?

Nyingi ya hizi mila zimepitwa na wakati na kwa sababu ya dini na shule wengi wameshaziacha. Na ukiona anayengangania ujue huyo ni mchawi.
 
Elimu na dini, ni kama mkorogo kwa mtu mweusi, hata ujichubue na kuwa mweupe kiasi gani, wakifukua kidogo tu ni mweusi.

Usi-underestimate utamaduni uliokukuza, unaathiri hata jinsi yako ya kutafakari mambo. Mfano, Babu yako alikuwa na wake 8, Baba yako akawa na wake 3. Wewe hata uwe mchungaji, mke mmoja hadi siku unakufa ni ndoto, usipooa vimchepuko vya hapa na pale vitakuwepo. Why? Deep down umeshaaminishwa mwanamme ni ruksa kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja.

Nigeria ni kati ya nchi zenye makanisa meeengi sana ya kiroho, watu wameokoka kukiko hata akiya Yuda Eskarioti, lakini wengi wao asubuhi kanisani, jioni kwa sangoma, why? Ushirikina ni sehemu ya maisha yao.

Uamuzi unao mwenyewe umeenda shule unajua lipi baya na lipi jema. Fanya lililo jema na Mungu wako atakujazi. Sio wote ni Wakristu, wengina hawana dini wengine ni Waislamu.
 
Nyingi ya hizi mila zimepitwa na wakati na kwa sababu ya dini na shule wengi wameshaziacha. Na ukiona anayengangania ujue huyo ni mchawi.
Kama ni shule wachaga ndiyo wenyewe..ni zaidi ya miaka mia sasa jamaa wanabukua lakn hadi mimi wa juzi nimezikuta maana yake ni kuwa elimu haijasaidia. Tena kuhusu dini ni vilevile pia.. Inahitajika mbinu nyingine au ustaarabu mpya tu ndo utaboresha hizi mila..
 
Kuzikwa kwenu ni ushirikina? Mie hata kama nimejijenga Manhattan, lazima nirudishwe Ihayabuyaga.
Sijasema ni ushirikina ila ukishakufa umekufa uzikwe, uchomwe moto haitasaidia kitu. Unaweza liwa na mnyama hata mabaki ya maiti yasipatikane au kama wale waliopotea na ndege, waliokufa kwenye maji MV Bukoba n.k. Kuzika popote ulipowekeza na kuishi muda mrefu mi naona ni bora zaidi.
 
ndugu yangu? wewe ni kabila gani?
kabila lenu halina mila mpaka uanze kunyooshea mikono wachaga?
mi naona maisha yashakupeleka resiii, hao wachaga unaosema wanamila potofu wewe zinakudhuru nini?
 
Kufa na maiti kutopatikana hilo ni jambo jingine, lakini kama maiti ipo, sioni kwa nini mtu asizikwe anakotaka.

Wewe unaweza ona kuzikwa kokote ni sawa, je inamaanisha kila mmoja anaona sawa?

Labda niulize, kila disemba wachaga wanaenda kusherehekea xmas na mwaka mpya Kilimanjaro, ina ulazima gani? Huoni ni kupoteza pesa tu? Mbona sie wengine tunasherehekea huku huku tulipo?

Kuna vitu vina sentimental values, nothing more.

Sijasema ni ushirikina ila ukishakufa umekufa uzikwe, uchomwe moto haitasaidia kitu. Unaweza liwa na mnyama hata mabaki ya maiti yasipatikane au kama wale waliopotea na ndege, waliokufa kwenye maji MV Bukoba n.k. Kuzika popote ulipowekeza na kuishi muda mrefu mi naona ni bora zaidi.
 
Kwani kabla wazungu hawajaja tulikua tunaishije kwanza hawa wazungu wametuletea shida tu !ametuuletea ushoga mila zetu zilikua zina ustaarabu wa hali yajuuu sana
 
Uamuzi unao mwenyewe umeenda shule unajua lipi baya na lipi jema. Fanya lililo jema na Mungu wako atakujazi. Sio wote ni Wakristu, wengina hawana dini wengine ni Waislamu.

Mila na desturi mara nyingi zililenga kupata mlo. Ukichinja wewe na nduguzo mtapata posho, ukitengeneza mbege kijiji kitakunywa etc! Sasa hiyo ya kuomba waliotangulia mbele ya Haki sijui umuhimu wake na ukweli wa matokeo yake.

Zamani nasikia mvua isponyesha kwa muda mrefu kijiji mnaitana mnchinja kondoo mnakula nyama lile tumbo mnaenda kulitumbukiza mtoni pale ambapo maji yametulia na wanasema kabla hamjafika nyumba mvua lazima inyeshe. Sasa sijui hiyo ni sayansi gani lakini maisha yalisonga mbele!

Mila mbaya ni ile ya kuzika watoto (sio wachanga) wakiwa hai kwenye mipaka kama ishara ya kutakiana amani kati ya koo au vijiji.

Iliyo kiboka zaidi ni ile mkishikwa mnafanya ngono kabla ya ndoa, mnapandishwa msitu wa mlima Kilimanjaro mnavua nguo mnalaliana halafu jiti linachomekwa kutoka mgongoni hadi ardhini mnaachwa hapo mpaka mnakufa! Hii nasikia ilileta nidhamu sana kwa Wachagga.
Eti... Aisee hebu leta ushahidi hapa maneno mazito sana haya.
 
Sijasema ni ushirikina ila ukishakufa umekufa uzikwe, uchomwe moto haitasaidia kitu. Unaweza liwa na mnyama hata mabaki ya maiti yasipatikane au kama wale waliopotea na ndege, waliokufa kwenye maji MV Bukoba n.k. Kuzika popote ulipowekeza na kuishi muda mrefu mi naona ni bora zaidi.

Ndetirima chunguza utabaini ukwel kichaga m2 asipozikwa nyumbani wanadai ni sawa na kupotea,pia mtoto yeyote awe wa ndoa au lazma akatiwe sikio b4 kuingia kwenye boma.hata wazungu,wahindi,wachina wana mila zao
 
Elimu na dini, ni kama mkorogo kwa mtu mweusi, hata ujichubue na kuwa mweupe kiasi gani, wakifukua kidogo tu ni mweusi.

Usi-underestimate utamaduni uliokukuza, unaathiri hata jinsi yako ya kutafakari mambo. Mfano, Babu yako alikuwa na wake 8, Baba yako akawa na wake 3. Wewe hata uwe mchungaji, mke mmoja hadi siku unakufa ni ndoto, usipooa vimchepuko vya hapa na pale vitakuwepo. Why? Deep down umeshaaminishwa mwanamme ni ruksa kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja.

Nigeria ni kati ya nchi zenye makanisa meeengi sana ya kiroho, watu wameokoka kukiko hata akiya Yuda Eskarioti, lakini wengi wao asubuhi kanisani, jioni kwa sangoma, why? Ushirikina ni sehemu ya maisha yao.
Kony hapa una-assume sana sasa, sio kila mtu amelelewa kwenye hizi tamaduni. Besides si kila mwanaume ana michepuko.
 
Kuna watu hapa Tanzania wana mila na desturi hao Wachagga ahata tone hawafikii...
 
Back
Top Bottom