Fadhila zisipotoshe mila, utamaduni na desturi za Kiafrika

Black listed

Senior Member
Apr 6, 2023
182
252
Kumekuwa na kawaida ya kwenda kinyume na mila, utamaduni na desturi za kiafrika kunakotokana na harakati za kijamii miongoni mwetu.

Ni jambo jema watu kusaidiana, hasa tunapopata matatizo na hatuna uwezo wa kukabiliana nayo kwa wakati huo, lakini hilo lisiende kinyume na maadili yetu.

Baadhi yetu tumekuwa na kasumba ya kujipatia umaarufu kupitia kwa wenzetu wapatapo matatizo, bila kujali umaarufu tunaotaka utakuwa ni udhalilishaji kwa muhanga.

Hapa karibuni ndugu zetu wa Hanang wamekutwa na mafuriko, ambayo yameacha simanzi kubwa; maafa, majeruhi, uharibifu wa nyumba na miundombinu. Serikali, makampuni na watu binafsi, wamejitokeza kutoa misaada kwa hali na mali ili kuwakimu wenzetu hawa.

Hili ni jambo jema na tunawashukuru wote mliojitoa kwa moyo wa hali na mali. Tatizo ni namna ya kuiwakilisha/kukabidhi misaada hii; hili ndio lililonisukuma kuandika uzi huu.

Kuna misaada unapotoa, kuitangaza haina tatizo kusikia ikitajwa, lakini kuna vitu ukivitaja vinaleta ukakasi kuvisikia masikioni. Kama uko na watu mnaheshimiana, halafu ikatajwa, unajikuta unaimana chini kwa aibu!

Baadhi ya misaada iliyotolewa kwa wahanga wa mafuriko ya Hanang ni taulo za kike. Ni msaada mzuri kwa mama zetu na dada zetu, lakini ilivyowasilishwa, kwa watu wanaojali maadili ni jambo la kutia aibu!

Kwanza watoaji wenyewe wanatoa huku wakitaja, tena kwa kurudia rudia, huku wakionyesha wanavyoshusha kutoka kwenye lori! Watu wengine wanashukuru (akiwemo mkuu wa wilaya) kwa kutaja "tunashukuru kwa msaada wa taulo za kike!"

Najuwa wengine mtaniona mshamba; kwamba mbona hivi ni vitu vya kawaida sana; lakini jiulize (mfano mwanaume) unaweza kutaja neno hili kwa mtu unayemheshimu, kama mama yako?! Au linapotajwa neno hili, upo na mama, bibi na dada zako; utajisikiaje!

Mimi nadhani misaada mingine ikitolewa, sio lazima itajwe; inaweza kujumuishwa kwenye kundi la vitu vingine linalotolewa kama msaada. Au la, tafsida itumike. Ni kweli tupo kwenye dunia ya utandawazi, lakini hilo lisisigine mila, utamaduni na desturi zetu hivyo kumomonyoa maadili.
 
Kumekuwa na kawaida ya kwenda kinyume na mila, utamaduni na desturi za kiafrika kunakotokana na harakati za kijamii miongoni mwetu.

Ni jambo jema watu kusaidiana, hasa tunapopata matatizo na hatuna uwezo wa kukabiliana nayo kwa wakati huo, lakini hilo lisiende kinyume na maadili yetu.

Baadhi yetu tumekuwa na kasumba ya kujipatia umaarufu kupitia kwa wenzetu wapatapo matatizo, bila kujali umaarufu tunaotaka utakuwa ni udhalilishaji kwa muhanga.

Hapa karibuni ndugu zetu wa Hanang wamekutwa na mafuriko, ambayo yameacha simanzi kubwa; maafa, majeruhi, uharibifu wa nyumba na miundombinu. Serikali, makampuni na watu binafsi, wamejitokeza kutoa misaada kwa hali na mali ili kuwakimu wenzetu hawa.

Hili ni jambo jema na tunawashukuru wote mliojitoa kwa moyo wa hali na mali. Tatizo ni namna ya kuiwakilisha/kukabidhi misaada hii; hili ndio lililonisukuma kuandika uzi huu.

Kuna misaada unapotoa, kuitangaza haina tatizo kusikia ikitajwa, lakini kuna vitu ukivitaja vinaleta ukakasi kuvisikia masikioni. Kama uko na watu mnaheshimiana, halafu ikatajwa, unajikuta unaimana chini kwa aibu!

Baadhi ya misaada iliyotolewa kwa wahanga wa mafuriko ya Hanang ni taulo za kike. Ni msaada mzuri kwa mama zetu na dada zetu, lakini ilivyowasilishwa, kwa watu wanaojali maadili ni jambo la kutia aibu!

Kwanza watoaji wenyewe wanatoa huku wakitaja, tena kwa kurudia rudia, huku wakionyesha wanavyoshusha kutoka kwenye lori! Watu wengine wanashukuru (akiwemo mkuu wa wilaya) kwa kutaja "tunashukuru kwa msaada wa taulo za kike!"

Najuwa wengine mtaniona mshamba; kwamba mbona hivi ni vitu vya kawaida sana; lakini jiulize (mfano mwanaume) unaweza kutaja neno hili kwa mtu unayemheshimu, kama mama yako?! Au linapotajwa neno hili, upo na mama, bibi na dada zako; utajisikiaje!

Mimi nadhani misaada mingine ikitolewa, sio lazima itajwe; inaweza kujumuishwa kwenye kundi la vitu vingine linalotolewa kama msaada. Au la, tafsida itumike. Ni kweli tupo kwenye dunia ya utandawazi, lakini hilo lisisigine mila, utamaduni
na desturi zetu hivyo kumomonyoa maadili.
Hata wakitoa misaada ya kugawa Chupi watangaze tu, maana hapo ndipo nchi zetu hizi za Afrika zilipofikia.
 
Tokea nikiwa sekondari nilipopata uelewa wa maswala ya uzazi, sijawahi kuwa comfortable watu wanapozungumzia maswala ya hedhi au pedi waziwazi. Huwa nahisi fedheha sana. Af unakuta mtu anaongelea kwa mbwembwe dah! Upo sahihi mleta mada.
 
Maisha ya Sasa kuna vitu ukifanya kwa usiri utaonekana umekula au umeiba, Wakati mwingine watu waliotoa misaada yao wanahitaji kuona imewafikia walengwa. Tusiwalaumu sana wanaopigwa picha na kueleza hadharani.
 
Watu kama nyie ndo huwa mnaona kwenda na mke clinic ni mambo ya kike.....
Anyway misaada mingi inayotangazwa watu huwa wanakwepa fedheha za kuonekana wamepiga hela bila kufikishia walengwa
 
Back
Top Bottom