Tuheshimu mila za watu

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
785
1,139
Kukamatwa watu kula Mchana Zanzibar ~ Watanganyika wasio Waislamu wamezusha Mjadala.

Ni vyema tukafahamu ya kuwa MILA, DESTURI, SILKA na UTAMADUNI ni mfumo wa maisha kamili ya kila jamii. Zanzibar kwa karne nyingi imekuwa ikitajika na kusifika ikafikia kubandikwa jina Tolerance Country. Kwa miongo kadhaa iliyopita zimeanza kuja hizi nganu zenye sura ya udini kwa lengo lile lile kama unataka kumuua mbwa mpe jina baya. Hayo yamekuja kutoka kwenye kundi fulani la kisiasa na kudhani ni mtaji kwao kumbe ni kuizamisha Zanzibar.

Sina hakika kama katazo la kula HADHARI mchana wa RAMADHANI lipo kisheria au la. La muhimu, kuna watu wanadhani katazo la kula hadharani mchana wa mwenzi mtukufu wa ramadhani ni katazo makhsusi kwa Watanganyika na Wakiristo. Wasichotaka kukifahamu katazo linamlenga kila binaadamu wakiwemo Wazanzibari na Waislamu wenyewe.

Kwa faida ya anaetaka kufaidika mwanamke wa Kiisilamu hawezi kufunga mwezi mzima (29/30) kutokana na sababu za kimaumbile hivyo mwanamke huyu ndani ya nyumba yetu tumezaliwa, tumelelewa na kukua pamoja mimi huwa siijui ni lini yupo ndani ya siku zake (hedhi). Nakusudia kusema ndani ya myumba yetu wakati yeye anaudhuru wa kisheria anaruhusiwa kula siku hizo (baada ya ramadhani anakuja kuzilipa) basi pia huwa anakula kwa kujificha. Huwa hali mbele yetu tukimuona.

Kuna wagonjwa nao wanaruhusiwa kula kisheria (wakipona wanakuja kulipa na wasipopona wanatolewa fidia). Wakiwa ndani ya nyumba lakini mfumo wao wa kula unakuwa ni tofauti na miezi mengine yote.
Kuna watoto ambao hawajatimia umri wanaruhusiwa kula basi hawa watoto pia huwa hawali ovyo ovyo majiani wana utaratibu wameekewa wao wenyewe wanaifahamu na kuiheshimu ramadhani kupita kiasi.

Mfano ulio hai watoto wangu mimi binafsi wanakwenda skuli na chuoni huwa wanapewa fursa warudi myumbani kula kisha warudi tena skuli au chuoni kuendelea na vipindi, mwanangu mmoja anakwenda nyumbani kula na kurudi skuli mtoto mmoja haendi anaona aibu kuwa ataitwa KOBE (jina la utani kwa mtoto asiyefunga) jaribu kufikiria mtoto wa miaka 7 anaona aibu kugundulika kuwa hakufunga anahiyari abakie skuli asirudi nyumbani kula kwa kuchelea asijulikane kuwa ni kobe!

Tulio zaliwa na kukulia Zanzibar kwa miongo kadhaa tumewashuhudia wageni kutoka mabara ya mbali wakiuheshimu utamaduni huu. Ajabu iliyoje majirani zetu na ndugu zetu wa karibu tulitegemea wao ndio wawe sehemu kutoa elimu hii badala kuhoji kwani Zanzibar na Tanganyika ni nchi tofauti? Tanganyika kuna baadhi ya MILA na TAMADUNI hakuna Zanzibar. Kadhalika Zanzibar kuna baadhi MILA na TAMADUNI hazifanani kabisa na Tanganyika si ajabu.

Zanzibar wapo Wakiristo tumezaliwa nao na kucheza nao tumekuwa wote hakuna hata siku moja Mkiristo wa Zanzibar anaweza kufanya upuuzi wa kula hadharani mchana wa ramadhani.

Siungi mkono watu kujichukulia sheria mikononi lakini vile vile sikubaliani na watu ambao hawana tolerance ya kuheshimu utamaduni wa wengine na kudhani wao pekee wana haki ya kuingia kwenye nyumba ya mtu na kufanya anachoona yeye ni sawa kwake. Heshima ni kitu cha bure kwani mtu akichukuwa chakula chake na kuenda kula ndani kwake kuna tatizo gani? Karaha ya kula mchana wa mwezi mtukufu wa ramadhani watu wanadhani inawahusu Watanganyika na Wakiristo tu, haya yashawafika hata Wazanzibari na Waislamu. Kosa linalofanyika ni kule kujichukulia sheria mikononi na kupelekea kuumiza watu.

Sisi tulipo nchi za wamaharibi kuna mambo mengi tumezuiwa tusifanye na tunaheshimu hizo taratibu. Mfano sisi tuna msikiti lakini ni marufuku kuadhini kwa bomba (spiker) kwa hiyo tunaadhini kimya kimya na kusali kimya kimya tumepungukiwa nini kwenye imani yetu?

Assallam aleykum.
 
Mila zipo ni kawaida, lakini uwepo wa mila, desturi, na tamaduni zako, jitahidi zisiingilie uhuru wa wengine, kwasababu hata wale ambao mila zako zinaingilia uhuru wao, nao pia wana mila, desturi, na tamaduni zao.

Dawa ya hayo yote ni kuvumiliana tu, sio kuleteana ubabe kukamatana na kupelekana polisi. Zanzibar ni ya wote, wenye asili, rangi, imani tofauti, sio ya kikundi fulani cha imani moja peke yao.
 
Ukiona funga Yako inasumbuliwa na wanaokula! Ujue wewe ni mlafi na huna sifa ya kufunga' Umepatana na Mungu kwamba ufunge' unakutana na jaribu doogo la mtu anayekula' na wewe ukashindwa kuvumilia!! Wewe ni mpumbavu na haufungi kwa ajili ya Mungu' bali umefunga ili ujitwalie sifa tu machoni pako
 
🔹 Muda mrefu unaandika maujinga acha ujinga na upuuzi wewe

🔹 Kwa hiyo ni haki wahindi wanavyoua waislamu kule India kwa sababu Mila zao destiri na mautopolo yote kama mlionayo Zanzibar kwao ni dini na Mila za Kihindu ? Ninyi ni watu wa ajabu sana wenye mawazo mgando na yaliyopitwa na wakati kisa tuu ni minority Islam hivyo mnataka Kila mmoja afuate hayo mamila ya hovyo ya kiarabu

🔹 Jamii yoyote ya kistaarabu huwa Ina safeguard rights za minority na sio minority kujiona kuwa hawana haki

🔹Tena hata kitendo Cha KUFUNGA hoteli za Umma mchana ni kinyime kabisa na jamii xilizostaarabiks maana Kuna ,wageni, wagonjwa nk
 
Mila na tamaduni za kijinga ni za kupiga STOP ndiyo maana unaona ukeketaji unapigwa vita na ulikuwepo karne na karne!

BTW: Hao wamasai mnaowanyang'anya virungu na sime huko visiwani nao huo ni utamaduni na desturi yao kabla hata Sultan wa Oman kuja huko.
 
Nyie nanyi embu punguzeni hizi mada zakutulazimisha tuone sense kwenye kitu ambacho sio sensible!!!

Ukweli ni kwamba hamna self-control, mnaendeshwa na mihemko, na zaidi mmetawaliwa na tamaa ya chakula, ama sijui tuite ulafi...?😏 Yani mi nifunge, we ule, mimi niharibu funga yangu....??? Kama sio ujinga huo ni nini?

Ukifunga kwa imani hata kupikia wengine utawapikia, kisha utawetengea mezani na utakaa kutia nao stori wakiwa wanakula bila tatizo lolote. Jaribuni kukomaa kiimani badala ya kupiga kelele ili muonekane bora, matokeo yake mnaishia kuonekana vituko.
 
Mtoto wako ana nidhamu ya uoga. Mkanye mapema na umfunze kabla dunia haijamfanya kitu.
Mfano ulio hai watoto wangu mimi binafsi wanakwenda skuli na chuoni huwa wanapewa fursa warudi myumbani kula kisha warudi tena skuli au chuoni kuendelea na vipindi, mwanangu mmoja anakwenda nyumbani kula na kurudi skuli mtoto mmoja haendi anaona aibu kuwa ataitwa KOBE (jina la utani kwa mtoto asiyefunga) jaribu kufikiria mtoto wa miaka 7 anaona aibu kugundulika kuwa hakufunga anahiyari abakie skuli asirudi nyumbani kula kwa kuchelea asijulikane kuwa ni kobe!
 
Mila zipo ni kawaida, lakini uwepo wa mila, desturi, na tamaduni zako, jitahidi zisiingilie uhuru wa wengine, kwasababu hata wale ambao mila zako zinaingilia uhuru wao, nao pia wana mila, desturi, na tamaduni zao.

Dawa ya hayo yote ni kuvumiliana tu, sio kuleteana ubabe kukamatana na kupelekana polisi. Zanzibar ni ya wote, wenye asili, rangi, imani tofauti, sio ya kikundi fulani cha imani moja peke yao.
Zanzibar ni ya Wazanzibari wa Tanganyika acheni kujitoa ufahamu
 
Back
Top Bottom