Mikumi: Basi Standard Coach lililokuwa likitokea Iringa kwenda Dar es Salaam lapata ajali

Medecin

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
7,896
21,305
Ajali ya basi la Standard Coach kutokea Iringa kwenda Dar.

Saa tatu asubuhi hii imetokea ajali ya basi la Standard Coach lenye namba za usajili T543 CSF lililokuwa likitokea mkoani Iringa kwenda Dar es Salaam. Ajali imetokea maeneo ya Mikumi wilayani Kilosa eneo maarufu kama kona za Iyovi.
Ajali hiyo imehusisha magari mawili, basi na lori ambalo halikupata madhara yoyote.

Chanzo cha ajali kulingana na mashuhuda ni uzembe wa dereva wa lori kukosa umakini barabarani, dereva wa basi alijaribu kukwepa lori lililoingia upande wa basi na kusababisha basi kwenda kugonga mti uliopo pembezoni mwa barabara.

Nimeshuhudia majeruhi kadhaa kwa kuwasaidia kuwatoa kwenye basi na kuwakimbiza hospitali ndogo ya Mikumi na majeruhi wengine wamebebwa na madereva wa malori kwenda zahanati ya Ruaha Mbuyuni kwa ajili ya matibabu. Mpaka natoka eneo la tukio hakuna kifo chochote ila majeruhi watano hali zao si nzuri. Mmoja kavunjika mguu (mwanaume), mwingine kapasuka kichwani (mwanaume) na wengine wamepata majeraha sehemu mbalimbali za mwili.

Mpaka natoka eneo la ajali bado jeshi la Polisi lilikuwa halijafika eneo la tukio kutokana na ukosefu wa mtandao eneo la ajali hivyo taarifa kuchelewa kufika lakini tumewapa taarifa kwa kuwafuata hapo Ruaha Mbuyuni.

Nawaombea majeruhi wapate nafuu haraka.

20210729_085829.jpg

20210729_091331.jpg

20210729_092439.jpg

20210729_092450.jpg

20210729_092825.jpg
 
Kwa muonekano wa kwenye picha, inaonekana hii ajali ilikuwa mbaya sana. Pole Kwa majeruhi wote.

Mola awape uponyaji Wa haraka.
 
Polen sana wahanga.Mungu atawapa nafuu haraka

Ni kweli maeneo hayo hayanaga network.halafu ni hatari sana hizo kona.ukipata shida maeneo hayo si rabisi kupata msaada wa haraka
 
Ajali ya basi la Standard Coach kutokea Iringa kwenda Dar.

Saa tatu asubuhi hii imetokea ajali ya basi la Standard Coach lenye namba za usajili T543 CSF lililokuwa likitokea mkoani Iringa kwenda Dar es Salaam. Ajali imetokea maeneo ya Mikumi wilayani Kilosa eneo maarufu kama kona za Iyovi...
Dah ....Poleni abiria..... Kongole nyingi kwa mtuma mpicha....umetuma picha za ajali bila kuonyesha tone la damu...ila hujatutendea haki tunaopenda kuona damu.....Nadhani Profesa Mchana Junia atakuwa ananung'unika huko aliko.... 🤣 🤣🤣
 
Ajali ya basi la Standard Coach kutokea Iringa kwenda Dar.

Saa tatu asubuhi hii imetokea ajali ya basi la Standard Coach lenye namba za usajili T543 CSF lililokuwa likitokea mkoani Iringa kwenda Dar es Salaam. Ajali imetokea maeneo ya Mikumi wilayani Kilosa eneo maarufu kama kona za Iyovi...
Shida kubwa. Poleni sana Abiria na poleni wote kwa ajali.
 
Ajali ya basi la Standard Coach kutokea Iringa kwenda Dar.

Saa tatu asubuhi hii imetokea ajali ya basi la Standard Coach lenye namba za usajili T543 CSF lililokuwa likitokea mkoani Iringa kwenda Dar es Salaam. Ajali imetokea maeneo ya Mikumi wilayani Kilosa eneo maarufu kama kona za Iyovi.
Ajali hiyo imehusisha magari mawili, basi na lori ambalo halikupata madhara yoyote.
Alhamdulillah mungu kanusuru Roho za wapendwa wetu.
 
Back
Top Bottom