Basi la Shule ya Kemebos lapata ajali, laua mwanafunzi mmoja, 6 wajeruhiwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,537
8,547
Screenshot_2024-03-24-17-43-19-507_com.brave.browser-edit.jpg
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kemobos, Frank Makage (17) amefariki dunia na wengine 6 wamejeruhiwa kwenye ajali ya basi la shule hiyo.

Ajali hiyo imetokea leo Jumapili Machi 24, 2024 katika Kata ya Kimwani wilayani Muleba mkoani Kagera wakati wanafunzi 35 wa shule hiyo wakisafiri kwenda Kata ya Katoro wilayani Chato mkoani Geita kwenye mapumzikoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera, Bracius Chatanda amethibitisha kutokea ajali hiyo na kuwa bado uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo chake.

Mkuu wa Wilaya Muleba, Dk Abel Nyamahanga amesema ajali hiyo imetokea Saa 8 usiku wa kuamkia leo.

"Basi lilikuwa limebeba wanafunzi limepata ajali usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na wenzake sita wamepata majeruhi," amesema DC Nyamahanga.

Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, Asheri Mpango amethibitisha kupokea mwili wa mwanafunzi huyo na majeruhi sita, wakiwamo wanafunzi na watumishi wa shule hiyo.

"Umepokelewa mwili wa mwanafunzi mmoja, majeruhi sita ambao mmoja kati ya hao, amevunjika mkono ambaye ni matroni wa shule, jina lake ni Anitha Frederick, mfanyakazi mmoja aitwaye Ashraf Athman (21) na Magdalena Muhage (16) ambaye ni mwanafunzi," amesema Mpango.
 
Pole sana kwa wote waliofikwa na huu mkasa.
Inauma sana unajua mwanao yupo shule mara unaletewa taarifa amefariki au ameumia.

Inauma sana.

Mwenyezi Mungu awape tulizo na faraja. Ameen
 
Pole sana kwa wote waliofikwa na huu mkasa.
Inauma sana unajua mwanao yupo shule mara unaletewa taarifa amefariki au ameumia.

Inauma sana.

Mwenyezi Mungu awape tulizo na faraja
 
Back
Top Bottom