Mihemuko siyo kigezo cha mtu kufaa kuwa rais

Mihemuko siyo kigezo cha mtu kufaa kuwa rais

Mkuu;
Hawa ni vijana wa mitandao ambao wanadhani Tanzania nzima inapatikana kwenye mitandao ya kijamii.

Ninakuhakikishia kwa wendo huu hata wabunge wa upinzani watapungua mwaka 2020.

Kumbuka Watanzania hawahitaji mambo makubwa kwa wanasiasa bali wanachotaka ni maji, barabara, umeme, afya na sehemu ya kuuzia mazao yao.

Mgosha kwa sasa anajitahidi sana kupeleka kwa wananchi orodha ya huduma niliyoorodhesha.
 
Nalisikitia tumbo lililo kubeba wewe nyani,
Kweli kabisa huyu ndugu anaboa na anakera mno.Ushauri wangu kwako Nyani Ngabu baki na USA yako tubaki na Tanzania yako we don't share the same pain please leave us NDUGU UNAKERA
 
Sasa kwa kauli mbovumbovu Lissu ana tofauti gani na Magufuli?

Lissu ni bonge la mropokaji, na hapo hana madaraka.

Akiwa nayo si ndo itakuwa balaa!!
Labda neno kuropoka lina maana nyingine. Kama lina maana yake ya asili basi unachofanya hapa ni uropokaji; alafu unamsingizia mtu mwingine kabisa kuwa na Tatizo lako.
 
Bado natatizika kujuwa kosa lipo wapi mnakuwa bado hamjatusaidia kosa lilipo ili tungundue.
 
Kweli kabisa huyu ndugu anaboa na anakera mno.Ushauri wangu kwako Nyani Ngabu baki na USA yako tubaki na Tanzania yako we don't share the same pain please leave us NDUGU UNAKERA

Kama nakukera chimba shimo ujifukie.
 
Aksante kwa kutuonyesha photos nzr za kazi za Govt.
Huo ndy wajibu wa Govt.
Toka enzi za Mkoloni, Barabara zilijengwa na zitaendelea kujengwa hata miaka 100 ijayo.

Govt ipo na kila siku inaendelea kuwepo.

Tanzania ni yetu sote.
 
Nawambia vijana ugoro sio kabisa tazama sasa nyani mzima oyoooooooooo kazi kula ugoro tu
 
Kama nakukera chimba shimo ujifukie.
Brother kama hutumiki na hiyo ndo reasoning yako basi nchi hii tuna hasara kubwa tunategemea kwa kuwa una exposure utakuwa na correct reasoning instead of such rubbish reasoning
 
Lowassa nae alisema atagombea! Ngoja moto uwake huko ufipa
 
HAKUNA JIPYA KTK ULIYOYAANDIKA,UNATUTHIBITISHIA UKEFLE ULIO NAO ,SIKU TUNDU LISSU AMEPIGWA RISASI, ULIANDIKA MANENO YA KIFEDHULI MNO, TANGU WAKATI ULE NIMEKUWA NAKUANGALIA KWA JICHO TOFAUTI, WEWE JAMAA UNA ROHO YA CHUKI MNO NA MWANASIASA HUYU,
 
wapinzani lazima wajue kukosoa tu hakumpi mtu sifa ya kuwa kiongozi bora!

vilevile uropokaji & kushinda unaponda wapinzani wako sio kazi ya kiongozi bora!
 
Brother kama hutumiki na hiyo ndo reasoning yako basi nchi hii tuna hasara kubwa tunategemea kwa kuwa una exposure utakuwa na correct reasoning instead of such rubbish reasoning
Mkuu, Thinking it is so hard for some.
.....
But common sense is not everyone's deodorant.
 
Haya unayesema kwa kuwa unajua ipo dola iitakayofanikisha ushindi kwa namna yoyote Ile.
Weka uchaguzi huru,ruhusu mikutano ya siasa kwa vyama vyote leo uone jinsi gani mmechokwa.
wapinzani lazima wajue kukosoa tu hakumpi mtu sifa ya kuwa kiongozi bora!

vilevile uropokaji & kushinda unaponda wapinzani wako sio kazi ya kiongozi bora!
 
Serikali haijawahi kusimama. Kwa hiyo hata ukiwa na Rais bogus kiasi gani, lazima kutakuwa na vitu anavyoweza kuonesha. Rais anayo dhamana kwa sasa na anakusanya kodi au anaweza kukopa kufanya chochote atakacho katika nchi yetu. Wengine wote hawana.

Sasa hawa wa vyama vya upinzani tunategemea watuoneshe barabara walizojenga kwa kodi zipi? Hata baadhi ya kodi za halmashauri tu serikali kuu imezichukua. Serikali za mitaa Tanzania nzima zinakusanya si zaidi ya bilioni 800 kwa mwaka. Serikali kuu inakusanya kutoka kodi karibu trilioni 17.

Nafikiri kama tunataka kulinganisha, then haiwezi kuwa ujenzi wa miundo mbinu maana hawa wengine hawana dhamana ya kukusanya kodi au kukopa ili kujenga miundombinu.

Tutafute vigezo vingine vya kupima.

Tukitumia kigezo cha miundo mbinu na mengine yanayofanywa kama sehemu ya wajibu wa serikali, then hakuna mtu yoyote nje ya Rais aliyepo madarakani anayeweza kushindana naye. Labda marais waliomtangulia.
Haswaaa, halafu mbona mnapata taabu sana kujinadi wakati majukwaa mmeyamiliki ninyi pekee yenu? Ninyi ndio mnao piga siasa wengine mmewapiga pini, shida nini? au ndiyo ile Kibaya chajitembeza! Mliaanda mazingira ya kuongea pekee yenu, lakini si mnayo fanya yanaonekana? Kwa nini mtumie nguvu kubwa kujinadi / kuomba msifiwe?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kuropoka maana yake nini?

1. Kuusema ukweli bila hofu?
2. Kuwa na ujasiri wa kusimama mbele ya dhalimu na kumwambia NO?
3. Kutetea haki za kiraia za wananchi?
4.Kutaka sheria za nchi na katiba viheshimiwe?
5. Kutaka mambo yafanyike vizuri badala ya kukurupuka?

Mleta mada naona umemshambulia Lissu personally (ad-hominem attack) badala ya kushambulia hoja zake kama vile katiba mpya, kutaka demokrasia, mikataba tunayoingia, miswada inayoletwa kwa hati ya dharura etc

Kifupi mleta mada umeshindwa kutoa mifano hata miwili kuonyesha huko kuropoka kwa Lissu ni kupi!!
 
Back
Top Bottom