Mihemuko siyo kigezo cha mtu kufaa kuwa rais

Mihemuko siyo kigezo cha mtu kufaa kuwa rais

Sijui sababu ni nini hasa. Yawezekana ikawa ni ombwe la kiuongozi. Si mnajua kuwa asili haiachi ombwe liwe hivyo hivyo tu. Ombwe likijitokeza sehemu, kama hakuna kitu cha kuliziba, basi asili itatafuta tu kitu cha kuliziba hilo ombwe.

Haya ngoja nizame sasa kwenye hoja.

Kutokana na kujizoea sifa kupitia mgongo wa rais Magufuli kwa kuwa mmoja wa wakosoaji wake wakuu, kamanda Tundu Lissu eti ndo anapigiwa chapuo na makamanda wenzake awe ndo mgombea urais wa CHADEMA 2020.

Hiyo yote kisa tu eti wenyewe makamanda wanaona kwa vile huyo kamanda wao anamkosoa sana Magufuli, basi kwao hiyo ndo sifa kuu ya uwezo alionao huyo kamanda.

Kiukweli mimi sijaona chochote kile kwa huyo kamanda kinachoonyesha kweli kazi ya kiuongozi anaiweza.

Kuwa tu mkosoaji, tena mwenye mihemuko, si uwezo wa kuongoza.

Kukosoa tu kwa kuhemuka hemuka ni kazi rahisi sana.

Manake wewe unakaa tu kusubiri wenzio wafanye ili nawe ndo upate nafasi ya kusema. Sasa kuna ugumu gani hapo?

Na hivi majuzi yule wanayemwita shangazi, eti naye baadhi ya makamanda washaanza kumpigia chapuo kuwa anafaa kugombea urais kisa tu anamkosoa sana Rais Magufuli huko Twitter!!!

Makamanda tafadhalini sana! Hamjielewi kabisa nyie watu. Punguzeni mihemuko.

Rais Magufuli hamtomshinda 2020 kwa kuweka mtu mwenye mihemuko.

Mkubali mkatae, kazi ya Rais Magufuli inaonekana sasa karibu Tanzania nzima.

Ukizunguka huko mikoani siku hizi unakutana na barabara za lami tena zenye ubora wa juu. Na mataa ya sola yamezipamba hizo barabara na yakiwaka usiku utadhani watu wapo Ulaya!

Mambo kama hayo ndo mtaji wa Magufuli 2020. Nyinyi mtaji wenu ni mihemuko.

Mtagaragazwa vibaya mno!!

Cheki baadhi ya mambo ya Rais Magufuli hayo.....huko ndo vijijini kulivyo siku hizi!
View attachment 978508View attachment 978509View attachment 978510

1. Wewe mwenyewe mleta hoja ni full mihemuko maana umesema mwenyewe

"....Kiukweli mimi sijaona chochote kile kwa huyo kamanda kinachoonyesha kweli kazi ya kiuongozi anaiweza..."

Kama hujaona wewe na macho yako hayo mawili, ndiyo unadhani na wengine hawajaona chochote?.....pathetic!!

2. Unapachika vipande vya sakafu ya barabara sijui ili iweje maana hata wakoloni wa Kijurumani na Kiingereza nao waliacha vipande vya sakafu vya barabara but yet they did not stop us to tell them to quit....

And you know what?

Baba yako Magufuli haja initiate then kujenga kisha kukamilisha hata kilometa moja ya miongoni mwa sakafu hizo za barabara in his three years in office!!

Hiyo yote ni kazi za watangulizi wake mainly Mkapa and Jakaya respectively.....

3. Kama ambavyo wewe hujaona, huoni uwezo wa Tundu Lissu na badala yake kuona elements za leadership emotions tu kwa kamanda huyu, basi, vivyo hivyo sisi wengine kwa huyo msukuma mwenzako Pombe hatuoni mtu timamu bali tunaona "mtu kichaa" tu aliye pewa rungu na mundu akizunguka zunguka sokoni kudhuru kila mtu...!!

4. Ni wazi sasa, ngoma imekulalia na ukilazimisha sana, basi mimi nakupa "draw game results" na kama ndivyo, then bebeni na nendeni na "kichaa" wenu hadi ktk ballot box 2020 na wengine (me, inclusive) tutaenda na wa mihemuko wetu TAML

Nakuhakikishia kabisa leo na uliweke hili moyoni na ktk akili zako kuwa, usidhani kuwa nyakati hizi ni nyakati zile ama mkadhani kwa kuwa leo nikuandikiapo hiki ni ijumaa, basi kila siku itakuwa ni ijumaa..... Never ever!!
 
Back
Top Bottom