Mihemuko siyo kigezo cha mtu kufaa kuwa rais

Nyota ya kung'ara kisiasa kwa Tundu Lissu ilianza toka akiwa mwanachama wa Nccr Mageuzi miaka ya 1998 kipindi akipambana na mikataba ya kinyonyaji walioingia nayo akina John Pombe Magufuli wakati akiwa Waziri mwandamizi wa serikali ya ccm

Lissu anakubalika kwa awamu zote toka Mkapa, Kikwete na hata Magufuli ndio wakataka kumnyamazisha milele lakini kwa sababu Mungu siyo John wakashindwa kumzima

Kikwete wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010 akiwa Singida alisema 'ni bora Dr Slaa awe rais, lakini siyo Lissu kuwa mbunge' sasa kwa muktadha huo unaona kabisa kuwa Lissu anatishia utawala wa kiimla kwa awamu zote katika nchi hii

Na ili hoja yako isimame wima ungeleta takwimu za hali ya maisha ya wananchi wa nchi hii imeborekaje toka kuingia madarakani Magufuli katika nyanja za kiuchumi, kielimu, kibiashara, na katika huduma za kijamii katika ujumla wake

Ni jambo la aibu mno kutumia kigezo cha barabara pekee kama ndio kukubalika kwa kiongozi huku hali mbaya kiuchumi ikilikumba taifa
 
Upinzani walikuwa na hoja yenye mashiko sana [ufisadi wa CCM].

Wakaja wakaichezea shilingi chooni wenyewe.

Tokea 2015 umewasikia tena wakiutaja ufisadi?

Sasa hivi wamebaki kuwa watu wa kudandia matukio tu kwa sababu hawana tena ajenda ya maana na iliyo relatable kwa Watanzania.

Ajenda ya ufisadi ilikuwa relatable kwa Watanzania walio wengi sana. Hiyo ajenda iliwafanya hadi CCM wabadilike....
Mwambie JIWE hana uwezo hata wa kupambana na ABDUL NONDO kwa hoja. Aendelee kukomaa kutuia DOLA.

===========================
 
Attachments

  • 1545892078702.png
    1545892078702.png
    164.7 KB · Views: 21
Wewe kilaza unasikiliziga hoja na sera zinazongumziwa na wapinzani nchi za Ulaya na Marekani ambazo ufisadi sio tatizo kubwa kwao?
Matatizo ya nchi ni zaidi ya ufisadi,ni upuuzi na akili finyu kufikiri kwamba ufisadi ndio inatakiwa iwe hoja ya kudumu na kwamba daima ndio itakuwa ajenda ya upinzani hata pale ambapo mambo yanabadilika na kuibuka mengine.
Well
 
Wewe jamaa Lisu sijui alikugongea wife!!utake usitake jamaa ni smarter than you
 
Kwa hiyo Lisu alimsingizia tu eeh?
Kama alimsingizia au la inategemea na riport ya mwakyembe ilivyokuja. Je Lissu aliunda hiyo tume au JK? Na Lowasa si alikjuwa best wa Lowasa kwaninin hakumtetea badala yake akamwacha ajiuzulu. There was something which you and me do not know. Sisi ne lay people hivyo tunapokuwa hatuingii kwenye cabinet halafu tukatoka na conclusions ambazo hatujui vyanzo tunawakosea wanaohukumiwa. Upande wangu sijawahi dhani Lowasa ni mwizi ila ninachokijua kwa Lowasa ni wanawake na Pombe sababu niliishi Dodoma na nilikuwa karibu na watu waliomzunguka kwenye 80s. The rest kwangu ni story.
 
Lissu hakuwa na shida na Slaa wala hakuvutika na Lowasa,alichokifanya ni hesabu za kisiasa tu akilenga kuigawa na kuipasua ccm kama njia ya kuuingiza upinzani madarakani kwa mara ya kwanza.Ni kiasi gani alifanikiwa au alishindwa ktk mkakati huo ni swala lingine lenya kuhitaji mjadala mpana.
Iwapo Lowassa na upinzani ungefanikwa lazima mfumo mzima wa utawala na siasa ktk nchi ungebadilika na hicho kinachoitwa ufisadi wa Lowassa kingechukua sura mpya zaidi ktk bunge na mahakama.
Lissu angekuwa anakiamini anachosema basi asingekubali kumtosa Dr.Slaa na kumpokea ‘fisadi’ Lowassa.

Au umesahau mwandishi wa ile list of shame alikuwa nani?
 
Mbona umechefukwa sana? Magufuli hahitaji sanduku la Kura kumBakisha mamlakani Polisi wanatosha so punguza povu jamaa yako ataendelea kuwepo
Sijui sababu ni nini hasa. Yawezekana ikawa ni ombwe la kiuongozi. Si mnajua kuwa asili haiachi ombwe liwe hivyo hivyo tu. Ombwe likijitokeza sehemu, kama hakuna kitu cha kuliziba, basi asili itatafuta tu kitu cha kuliziba hilo ombwe.

Haya ngoja nizame sasa kwenye hoja.

Kutokana na kujizoea sifa kupitia mgongo wa rais Magufuli kwa kuwa mmoja wa wakosoaji wake wakuu, kamanda Tundu Lissu eti ndo anapigiwa chapuo na makamanda wenzake awe ndo mgombea urais wa CHADEMA 2020.

Hiyo yote kisa tu eti wenyewe makamanda wanaona kwa vile huyo kamanda wao anamkosoa sana Magufuli, basi kwao hiyo ndo sifa kuu ya uwezo alionao huyo kamanda.

Kiukweli mimi sijaona chochote kile kwa huyo kamanda kinachoonyesha kweli kazi ya kiuongozi anaiweza.

Kuwa tu mkosoaji, tena mwenye mihemuko, si uwezo wa kuongoza.

Kukosoa tu kwa kuhemuka hemuka ni kazi rahisi sana.

Manake wewe unakaa tu kusubiri wenzio wafanye ili nawe ndo upate nafasi ya kusema. Sasa kuna ugumu gani hapo?

Na hivi majuzi yule wanayemwita shangazi, eti naye baadhi ya makamanda washaanza kumpigia chapuo kuwa anafaa kugombea urais kisa tu anamkosoa sana Rais Magufuli huko Twitter!!!

Makamanda tafadhalini sana! Hamjielewi kabisa nyie watu. Punguzeni mihemuko.

Rais Magufuli hamtomshinda 2020 kwa kuweka mtu mwenye mihemuko.

Mkubali mkatae, kazi ya Rais Magufuli inaonekana sasa karibu Tanzania nzima.

Ukizunguka huko mikoani siku hizi unakutana na barabara za lami tena zenye ubora wa juu. Na mataa ya sola yamezipamba hizo barabara na yakiwaka usiku utadhani watu wapo Ulaya!

Mambo kama hayo ndo mtaji wa Magufuli 2020. Nyinyi mtaji wenu ni mihemuko.

Mtagaragazwa vibaya mno!!

Cheki baadhi ya mambo ya Rais Magufuli hayo.....huko ndo vijijini kulivyo siku hizi!
View attachment 978508View attachment 978509View attachment 978510
 
Hakuna mtu mpumbavu kama yule anayemchagua mtu amjengee bara bara au amjengee shule...Eti bara bara za Magufuli, mimi kila mwezi nilikua nakatwa zaidi ya milioni na point kisha mpuuzi aje asifie upuuzi hapa
 
Ukitumia vyombo vya usalama kukandamiza wanaokukosoa na wasiokupenda. Ukatumia vibaraka wako kutisha na kutesa.
Nakuhakikishia hata unge kuwa na uwezo kumleta Mungu Tanzania usingependwa.
Magufuli hapendwi kwa mengi, aliingia madarakani kimagumashi na ni MKABILA SANAAA. Hana tofauti na akiba Nkurunzinza, na Kagame anaowaita rafiki zake.
Ingekuwa Maombi/Dua zinafanya kazi nami ningemuombea Dua mbaya sana, lakini kwasababu hauana effect yoyote, I wish aondolewe kwanguvu na anyimwe hata pension kwa upuuzi anaoufanya.
Watu kama nyie Nyani Ngabu ndio huwa mnaona ni sawa mtawala mmoja anzalisha wakimbizi mamilioni kutoka nchini kwake na mkaona ni sawa tu. Ukimuuliza Kabila anakwambia mambo kwake safi, Ukimuuliza Nkurunzinza naye anasema nchi yake ni tulivu na demokrasia imetamalaki, hata Kagame hivyo hivyo. Lakini wanaokimbia nchi hizo wanaongea uhalisia na ukweli tofauti na wao. Tanzania ndio inaelekea huko, watu wachache kwa maslahi yao, unaona ukabila au siasa wanasema tuko vizuri sanaaa. Lakini naamini siku wananchi wakikubali kufa kama wenzetu kule Syria, hapa tutawachinha sana wasukuma. Na kwa chuki iliyopo sidhani kama patatulia tena. Mkuu Nyani Ngabu Magufuli hafai kuwa hata mwenyekiti wa mtaa. Ni bahati mbaya alipewa madaraka kwa nguvu na anayatumia vibaya na kwa faida yake. Mind you mimi sio mwanavyama.
 
Daah kijiji gani hiki nihamie maana mimi kijijini kwetu siwezi kwenda msimu huu, nasubiria mpaka mvua ziishe ndio kunapitika
Sijui sababu ni nini hasa. Yawezekana ikawa ni ombwe la kiuongozi. Si mnajua kuwa asili haiachi ombwe liwe hivyo hivyo tu. Ombwe likijitokeza sehemu, kama hakuna kitu cha kuliziba, basi asili itatafuta tu kitu cha kuliziba hilo ombwe.

Haya ngoja nizame sasa kwenye hoja.

Kutokana na kujizoea sifa kupitia mgongo wa rais Magufuli kwa kuwa mmoja wa wakosoaji wake wakuu, kamanda Tundu Lissu eti ndo anapigiwa chapuo na makamanda wenzake awe ndo mgombea urais wa CHADEMA 2020.

Hiyo yote kisa tu eti wenyewe makamanda wanaona kwa vile huyo kamanda wao anamkosoa sana Magufuli, basi kwao hiyo ndo sifa kuu ya uwezo alionao huyo kamanda.

Kiukweli mimi sijaona chochote kile kwa huyo kamanda kinachoonyesha kweli kazi ya kiuongozi anaiweza.

Kuwa tu mkosoaji, tena mwenye mihemuko, si uwezo wa kuongoza.

Kukosoa tu kwa kuhemuka hemuka ni kazi rahisi sana.

Manake wewe unakaa tu kusubiri wenzio wafanye ili nawe ndo upate nafasi ya kusema. Sasa kuna ugumu gani hapo?

Na hivi majuzi yule wanayemwita shangazi, eti naye baadhi ya makamanda washaanza kumpigia chapuo kuwa anafaa kugombea urais kisa tu anamkosoa sana Rais Magufuli huko Twitter!!!

Makamanda tafadhalini sana! Hamjielewi kabisa nyie watu. Punguzeni mihemuko.

Rais Magufuli hamtomshinda 2020 kwa kuweka mtu mwenye mihemuko.

Mkubali mkatae, kazi ya Rais Magufuli inaonekana sasa karibu Tanzania nzima.

Ukizunguka huko mikoani siku hizi unakutana na barabara za lami tena zenye ubora wa juu. Na mataa ya sola yamezipamba hizo barabara na yakiwaka usiku utadhani watu wapo Ulaya!

Mambo kama hayo ndo mtaji wa Magufuli 2020. Nyinyi mtaji wenu ni mihemuko.

Mtagaragazwa vibaya mno!!

Cheki baadhi ya mambo ya Rais Magufuli hayo.....huko ndo vijijini kulivyo siku hizi!
View attachment 978508View attachment 978509View attachment 978510
 
Hebu lala huko! Umesharudi bongo au bado upo na maboksi ya wateja? Taja barabara moja mpya aliyoijenga. Usivisemee viporo anavyomalizia vilivyoanzishwa na JK! Ni hakuna.

Cheki mambo ya Magufuli hayo....

C320790E-0F0C-43D7-9343-61D288298714.jpeg
 
Sijui sababu ni nini hasa. Yawezekana ikawa ni ombwe la kiuongozi. Si mnajua kuwa asili haiachi ombwe liwe hivyo hivyo tu. Ombwe likijitokeza sehemu, kama hakuna kitu cha kuliziba, basi asili itatafuta tu kitu cha kuliziba hilo ombwe.

Haya ngoja nizame sasa kwenye hoja.

Kutokana na kujizoea sifa kupitia mgongo wa rais Magufuli kwa kuwa mmoja wa wakosoaji wake wakuu, kamanda Tundu Lissu eti ndo anapigiwa chapuo na makamanda wenzake awe ndo mgombea urais wa CHADEMA 2020.

Hiyo yote kisa tu eti wenyewe makamanda wanaona kwa vile huyo kamanda wao anamkosoa sana Magufuli, basi kwao hiyo ndo sifa kuu ya uwezo alionao huyo kamanda.

Kiukweli mimi sijaona chochote kile kwa huyo kamanda kinachoonyesha kweli kazi ya kiuongozi anaiweza.

Kuwa tu mkosoaji, tena mwenye mihemuko, si uwezo wa kuongoza.

Kukosoa tu kwa kuhemuka hemuka ni kazi rahisi sana.

Manake wewe unakaa tu kusubiri wenzio wafanye ili nawe ndo upate nafasi ya kusema. Sasa kuna ugumu gani hapo?

Na hivi majuzi yule wanayemwita shangazi, eti naye baadhi ya makamanda washaanza kumpigia chapuo kuwa anafaa kugombea urais kisa tu anamkosoa sana Rais Magufuli huko Twitter!!!

Makamanda tafadhalini sana! Hamjielewi kabisa nyie watu. Punguzeni mihemuko.

Rais Magufuli hamtomshinda 2020 kwa kuweka mtu mwenye mihemuko.

Mkubali mkatae, kazi ya Rais Magufuli inaonekana sasa karibu Tanzania nzima.

Ukizunguka huko mikoani siku hizi unakutana na barabara za lami tena zenye ubora wa juu. Na mataa ya sola yamezipamba hizo barabara na yakiwaka usiku utadhani watu wapo Ulaya!

Mambo kama hayo ndo mtaji wa Magufuli 2020. Nyinyi mtaji wenu ni mihemuko.

Mtagaragazwa vibaya mno!!

Cheki baadhi ya mambo ya Rais Magufuli hayo.....huko ndo vijijini kulivyo siku hizi!
View attachment 978508View attachment 978509View attachment 978510
We Dada angu humu ni mkongwe,, lakini cha ajabu hunaga cha maana,, na ulivyo na nuksi haya maandiko yako kuna siku utakuja kuyakana AU utatamani yajifute, maana itakuwa kinyume chake,
 
Hizi ni baadhi kutoka ktk ilani yenu;
Milioni 50 kila kijiji,
Watoto wa kike waliopata mimba kurudi shuleni,
Kuendeleza mchakato wa katiba mpya,
Ajira kwa vijana,
Kuboresha maslahi ya watumishi
Viwanda,
Usalama
Ni kipi kati ya haya mnaweza kujivunia mmefanya vizuri?
Macho yako hayaoni? Au hausikii?
 
Back
Top Bottom