Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,277
- 144,453
Sijui sababu ni nini hasa. Yawezekana ikawa ni ombwe la kiuongozi. Si mnajua kuwa asili haiachi ombwe liwe hivyo hivyo tu. Ombwe likijitokeza sehemu, kama hakuna kitu cha kuliziba, basi asili itatafuta tu kitu cha kuliziba hilo ombwe.
Haya ngoja nizame sasa kwenye hoja.
Kutokana na kujizoea sifa kupitia mgongo wa rais Magufuli kwa kuwa mmoja wa wakosoaji wake wakuu, kamanda Tundu Lissu eti ndo anapigiwa chapuo na makamanda wenzake awe ndo mgombea urais wa CHADEMA 2020.
Hiyo yote kisa tu eti wenyewe makamanda wanaona kwa vile huyo kamanda wao anamkosoa sana Magufuli, basi kwao hiyo ndo sifa kuu ya uwezo alionao huyo kamanda.
Kiukweli mimi sijaona chochote kile kwa huyo kamanda kinachoonyesha kweli kazi ya kiuongozi anaiweza.
Kuwa tu mkosoaji, tena mwenye mihemuko, si uwezo wa kuongoza.
Kukosoa tu kwa kuhemuka hemuka ni kazi rahisi sana.
Manake wewe unakaa tu kusubiri wenzio wafanye ili nawe ndo upate nafasi ya kusema. Sasa kuna ugumu gani hapo?
Na hivi majuzi yule wanayemwita shangazi, eti naye baadhi ya makamanda washaanza kumpigia chapuo kuwa anafaa kugombea urais kisa tu anamkosoa sana Rais Magufuli huko Twitter!!!
Makamanda tafadhalini sana! Hamjielewi kabisa nyie watu. Punguzeni mihemuko.
Rais Magufuli hamtomshinda 2020 kwa kuweka mtu mwenye mihemuko.
Mkubali mkatae, kazi ya Rais Magufuli inaonekana sasa karibu Tanzania nzima.
Ukizunguka huko mikoani siku hizi unakutana na barabara za lami tena zenye ubora wa juu. Na mataa ya sola yamezipamba hizo barabara na yakiwaka usiku utadhani watu wapo Ulaya!
Mambo kama hayo ndo mtaji wa Magufuli 2020. Nyinyi mtaji wenu ni mihemuko.
Mtagaragazwa vibaya mno!!
Cheki baadhi ya mambo ya Rais Magufuli hayo.....huko ndo vijijini kulivyo siku hizi!