Mimi naomba niuseme ukweli mchungu kwa watanzania wenzangu, Watanzania tulio wengi huwa tunakwenda kazini kama mazoea (Kwenye siasa, wana ccm wanaongoza) ili hali wenzenu huwa wanakwenda kazini so that they may get different results everyday; Hii ndo tofauti yetu, hebu nitaje mifano michache, mnakumbuka siku za nyuma wakati hakuna simu za mkononi (au ilipokuwepo kampuni moja au mbili za simu, yaani Mobitel na Traitel) jinsi ambavyo TTCL walivyo kuwa wanasumbua kwa wewe kupata just line, ilikuwa inachukua zaidi ya siku 45, ushindani ulipoingia wote nadhani ni mashahidi, angalia jinsi ya ufunguaji wa Account Bank enzi hizo, shida tupu, kama sio kufanya kazi kwa mazoea, inakuaje leo bado tuwe na mgao wa umeme? yote haya ndio udhaifu mkubwa tuliokuwa nao Watanzania wengi, nimefanya kazi na watu tofauti (yaani watu wa mataifa mbalimbali duniani) ipo tofauti kubwa sana kati yetu sisi na wao (hasa Watanzania wa wenye umri mkubwa na kutokea Serikalini, kila kitu anataka kikae kwanza till kesho hata kama kinachotakiwa ni sahihi tu). Tujiulize, inakuwaje hadi leo nchi yetu iwe na njaa, how comes tuwe na upungufu wa madaktari ili hali kila mwaka Muhimbili, Bugando, IMTU, KCMC n. k wanamwaga wadokta wengi mtaani? jibu ni jepesi sana, "Wanasiasa wetu, ambao kimsingi ndio watunga sera, wanafanya kazi kwa mazoea' sio watu ambao wapo after results, it is just mazoea, nimeonda kazini, bila kujali umepata ulicho kitaka au laa."
Hili ndilo lilimtokea Dr Migiro, though kuna watu humu ndani wanaweza kudhani kasingiziwa lakini hii ndo hali halisi tulionayo wengi, mwangalie hata mkuu wa nchi leo, hivi alipo faiti kwa miaka 10 ili aingie Ikulu, wengi tulidhani ana solution ya matatizo mengi ya nchi yetu, hata wengine walifikia hatua na kuandika kitabu kiitwacho, Kikwete, tumaini lililo rejea, sina hakika kama mwandishi wa kitabu kile kama bado anayaaminiyale aliyoaandika leo? Kizazi hiki tulicho nacho (hasa kilicho zaliwa na kulelewa wakati wa sera za Ujamaa) hadi kipite ndo ninadhani twaweza badiri nchi yetu, changamoto zinazoletwa na akina Zitto Kabwe, Mnyika Halima Mdee n. k kinaonekana kama ni kizazi kilicho kosa adabu kwa wakubwa wao, wakati sehemu zingine za dunia ndivyo ambavyo wanafanya, but lengo ni kuona matokeo ya kazi unayo ifanya. Niseme kitu cha mwisho, hivi Watanzania walio wengi wanapo enda kupiga kura, huwa wanajua uhusiano wa Kura hiyo na maisha yao ya kila siku? kuto kujua ndio inasababisha wengie hata kura wasiende kupiga eti wanadai ni kupoteza muda, why, because tumezoea kufanya kazi kwa mazoea na sio kupata matokeo ya kile unacho kifanya.