Migiro leaves UN post; forced out or chose to leave?

Migiro leaves UN post; forced out or chose to leave?

Narudia, kwakuwa taifa letu linaongozwa na mzee zaifu:

ijapokuwa mama Asha Migiro anasema kuwa anarudi chuo kikuu kufundisha. Mimi natabiri kuwa moja kati ya haya mawili yatatokea.Either, Mr Mukandara atapewa kazi ya ubalozi na mama Migiro kufanywa mkuu wachuo kikuu cha Dar es salamu (muendelezo wa teuzi zisizoelewaka za kikwete. Teuzi zenye lengo la kuleta usawa fulani anaoutaka Kikwete – siutaji huo usawa ila kila atakaesoma hapa ataelewa naongelea nini). Kama si hivyo basi mama huyu atapewa ubunge na uwaziri fulani nyeti utakao msogeza karibu na kiti cha urais na kumsogeza mtu fulani mbali na urais. Atakaesogezwa mbali atakuwa anatishia malengo fulani ya Kikwete ya kumuachia mtu fulani urais kwa malengo ya kuleta usawa fulani anaoutaka Kikwete – siutaji huo usawa ila kila atakaesoma hapa ataelewa naongelea nini).
 
Incompetence is what makes her loose her job at UN...ban ki moon yuko very bright na focused asingeweza kuendelea kukaa na migiro
 
Unazungumzia ile ya biashara yake na Riziwani?
Jasusi mkuu,huo sasa uchoyo wa habari.Mwageni hapa,maana huko mbeleni tutalaumiana kwa kuficha habari na kubaki na tungejua?
 
deputy_secretary-general.jpg

Takriban wiki moja baada ya Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Dkt Asha-Rose Migiro, kurejea nyumbani Tanzania baada a kukitumikia chombo hicho cha kimataifa kwa kipindi cha miaka mitano, vyanzo vya habari ndani ya Umoja huo vinadokeza kuwa utendaji kazi dhaifu na kushindwa ku-fit katika 'taasisi hiyo kubwa na ngumu' ndio sababu zilizopelekea Mtanzania huyo kunyimwa fursa ya kurefusha mkataba wake wa kazi.

"Wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu ni mgumu na wenye mahitaji mengi; unahitaji mtu mwenye uzoefu wa kuongoza Sekretariaeti (ya Umoja huo).Changamoto kubwa kwake ilikuwa kutofahamu siasa za chombo hicho na kutengeneza 'marafiki' (alliances)," kilieleza chanzo kimoja kwa Vox Media kupitia maongezi ya simu.

Imefahamika kuwa Dkt Migiro alijaribu kulishawishi Kundi la Afrika (Africa Group),linalounda asilimia 28 ya wanachama wote wa Umoja wa Mataifa,kuomba limsaidie 'kumpigia debe' ateuliwe tena,ombi ambalo lilikataliwa.

"Hakuwa maarufu miongoni mwa wanadiplomasia, kwahiyo hakuna aliyemsikliza. Pia ukumbuke kuwa uteuzi wake ulipingwa sana," kilieleza chanzo hicho.

Jijini Dar es Salaam, mjumbe mwandamizi wa zamani wa Sekretarieti ya chama tawala CCM aliyewahi kufanya kazi na Dkt Migiro kabla hajateuliwa kushika wadhifa huo wa Umoja wa Mataifa alieleza kuwa uteuzi huo katika chombo hicho cha kimataifa ulitokana na ukaribu wa Dkt Migiro na Rais Jakaya Kikwete.

Inafahamika kuwa Rais Kikwete na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon walijenga urafiki katika kipindi wote wawili walipokuwa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa mataifa yao.

Ilipofika wakati kwa Ban Ki-moon kuomba kura kushika wadhifa wake wa sasa, Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kumsapoti,na kura ya Kikwete ilisaidia Migiro kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Lakini Ki-moon alipoamua hivi karibuni kufanya mapitio ya timu yake nzima kwa minajili ya kukabiliana na upinzani mkubwa dhidi ya timu hiyo, ililazimika Dkt Migiro 'atoswe' kutokana na "utendaji kazi dhaifu na ukosefu wa uzoefu unaohitajika kwa watendaji wa ngazi za juu katika Umoja wa Mataifa."

CHANZO: Chanzo cha Dkt Asha-Rose Migiro KUPOTEZA Unaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ~ Kulikoni Ughaibuni Habari hii imetafsiriwa kutoka Vox Media.Shukrani za pekee kwa mdau @mactemba kwa kunitumia kiungo (link) cha habari hii

Huyu mama alikuwa anafikiri hizo gpa zake za kukariri ndio zitaweza kuendesha chombo kikubwa namna hiyo duniani alitimuliwa Kama gadafi
 
Asha Rose did a good job, period!! watu mnapenda majungu na maneno yasio na maana. Ban ki moon alishasema yeye kuwa anetegemea kufanya mabadiliko makubwa second term yake na kubadili team nzima, and that's what he did. Sio Asha Rose pekee bali karibu team nzima ambayo UNSG anamandate ya kuchagua kaibadilisha.

Ni lazima muelewe kuwa kwa body kama UN ambayo ina siasa kibao na mtu hasa UNSG inabidi muda wote ajaribu kubalance na kurudisha favour toka mataifa mbalimbali ni muhimu kubadili na kuchagua watu toka mataifa tofauti. Ndio ni kweli walijaribu kulobby for a second term lakini SG stand firm, na vilevile kawaida huyu Deputy SG huwa anaserve only one term, wote waliomtangulia ARM waliserve one term. Ni kweli Ban ki moon was returning some favour na fadhila ya Tz kulobby kupata kwake ukatibu mkuu, favour returned now he needs to return other peoples favours as well hasahasa waliomsaidia kupata kipindi cha pili.
Life goes on, karibu nyumbani dada yetu you did us proud, hopefully atapatiwa nafasi nzuri ya kusukuma mbele maendeleo yetu kwa udhoefu wake.
 
ni lazima uweke bookshelves varandani si dhani kama huyu mama anayo.. panua mawazo kwa kusoma matukio mbali mbali na biograph za watu mashuhuri ili ujifunza ujanja walioutumia kufikisha nchi zao hapo zilipo. Kweli kama waziri wa mabo ya nje ili apate ujuzi mzuri lazima utumie akiri yako na mawazo ya watu mbali mbali mashuhuri waliwahi kufanya kazi yako.Mgogoro wa syria ungetakiwa ushikwe na Mama Migiro na siyo Kofi Anan.
 
Tutayajua mengi,,,,bora arud kuiunga mkono serikali yake dhaifu na legelege
 
deputy_secretary-general.jpg

Takriban wiki moja baada ya Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Dkt Asha-Rose Migiro, kurejea nyumbani Tanzania baada a kukitumikia chombo hicho cha kimataifa kwa kipindi cha miaka mitano, vyanzo vya habari ndani ya Umoja huo vinadokeza kuwa utendaji kazi dhaifu na kushindwa ku-fit katika 'taasisi hiyo kubwa na ngumu' ndio sababu zilizopelekea Mtanzania huyo kunyimwa fursa ya kurefusha mkataba wake wa kazi.

"Wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu ni mgumu na wenye mahitaji mengi; unahitaji mtu mwenye uzoefu wa kuongoza Sekretariaeti (ya Umoja huo).Changamoto kubwa kwake ilikuwa kutofahamu siasa za chombo hicho na kutengeneza 'marafiki' (alliances)," kilieleza chanzo kimoja kwa Vox Media kupitia maongezi ya simu.

Imefahamika kuwa Dkt Migiro alijaribu kulishawishi Kundi la Afrika (Africa Group),linalounda asilimia 28 ya wanachama wote wa Umoja wa Mataifa,kuomba limsaidie 'kumpigia debe' ateuliwe tena,ombi ambalo lilikataliwa.

"Hakuwa maarufu miongoni mwa wanadiplomasia, kwahiyo hakuna aliyemsikliza. Pia ukumbuke kuwa uteuzi wake ulipingwa sana," kilieleza chanzo hicho.

Jijini Dar es Salaam, mjumbe mwandamizi wa zamani wa Sekretarieti ya chama tawala CCM aliyewahi kufanya kazi na Dkt Migiro kabla hajateuliwa kushika wadhifa huo wa Umoja wa Mataifa alieleza kuwa uteuzi huo katika chombo hicho cha kimataifa ulitokana na ukaribu wa Dkt Migiro na Rais Jakaya Kikwete.

Inafahamika kuwa Rais Kikwete na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon walijenga urafiki katika kipindi wote wawili walipokuwa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa mataifa yao.

Ilipofika wakati kwa Ban Ki-moon kuomba kura kushika wadhifa wake wa sasa, Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kumsapoti,na kura ya Kikwete ilisaidia Migiro kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Lakini Ki-moon alipoamua hivi karibuni kufanya mapitio ya timu yake nzima kwa minajili ya kukabiliana na upinzani mkubwa dhidi ya timu hiyo, ililazimika Dkt Migiro 'atoswe' kutokana na "utendaji kazi dhaifu na ukosefu wa uzoefu unaohitajika kwa watendaji wa ngazi za juu katika Umoja wa Mataifa."

CHANZO: Chanzo cha Dkt Asha-Rose Migiro KUPOTEZA Unaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ~ Kulikoni Ughaibuni Habari hii imetafsiriwa kutoka Vox Media.Shukrani za pekee kwa mdau @mactemba kwa kunitumia kiungo (link) cha habari hii

Unafikiri kukosa uzoefu ni udhaifu? Jipange upya kumchafua mama huyu ambaye ameiletea Tanzania sifa kubwa. Watanzania na hasa wenye wivu na maisha ya watu badala ya kuwa na wivu wa maendeleo kama wewe hamtufai kwa sasa.
 
Nilifikiri kiu ya kutaka urais 2015 ndiyo iliyomwondoa kule.
 
Translation:

Kama juma moja baada ya aliyekuwa naibu katibu mkuu, Dr Asha rose Migiro kurejea Tanzania baada ya kutumikia kwa muda wa miaka mitano wa kutumika Chombo cha umoja wa mataifa, vyanzo vya ndani vya umoja huo vimedokeza kwamba, udhaifu wake katika utendaji na kupwaya kwake katika kazi ni baadhi ya sababu zilizoletelezea akataliwe kuweka mkataba wa pili.

Nafasi ya naibu katibu mkuu ni ngumu na inahitaji mtu mzoefu na mwenye ufanisi katika kuendesha sekretarieti. Changamoto kubwa iliyomkabili ilikuwa ni kukosa uelewa katika siasa za kimataifa na kujenga mshikamano, kimedokeza chanzo cha habari cha Vox Media katika mazungumzo ya simu.

Imedhihirika pia kwamba, Dr Migiro alijaribu kujipigia debe kwa kundi la Afrika ambalo lina asilimia 28 ya wanachama wote wa umoja wa mataifa, akiwashawishi wamuunge mkono katika uteuzi wake mpya, lakini harakati zake zikakataliwa.
Hakuwa na umaarufu wowote miongoni mwa wanadiplomasia, na hivi hakuna aliyemsikiliza. Pia ikumbukwe kwamba uteuzi wake wa awali ulikosolewa na wengi.

Huko Dar es salaam, kiongozi mmoja mwandamizi wa zamani katika chama tawala aliyefanya kazi kwa karibu naye alisema kuwa uteuzi wa Dr Migiro ulisukumwa na uhusiano wake binafsi na rais Jakaya Kikwete.

Inafahamika kwamba rais Kikwete na katibu mkuu Ban Ki-moon walikuwa na mahusiano ya karibu walipokuwa wote wakihudumu kama mawaziri wa mambo ya nje katika serikali zao.

Hivi ulipofika wakati wa Ban Ki-moon kutazama sifa ya waombaji, ikaonekana kuwa mwombaji wa Tanzania yuko juu kwa sababu alisindikizwa na debe la rais Kikwete mwenyewe.

Lakini hivi karibuni, Ban Ki-moon aliamua kupitia upya timu yake yote kwa nia ya kudhibiti malalamiko yaliyojitokeza katika timu yake, ndio maana ikabidi Dr Migiro aondoke kwa sababu ya utendaji mbovu na ukosefu wa uzoefu ambao unahitajika kwa wafanyakazi wa mamlaka ya juu ya umoja wa mataifa.
 
Dr. Asha-Rose Migiro ni mfano halisi wa uwezo wa wanawake wengi wa Tanzania. Kwanza mwanamke akishaweka tu mawigi au minywele bandia kichwani kwake au minywele kuwa kama ya kihindi, kizungu, kiaarabu basi ujue huyo ni bomu yaani ajitambui, na kama ajitambui atatambuaje wajibu wake kwake mwenyewe na kwa jamii?!!
 
Unafikiri kukosa uzoefu ni udhaifu? Jipange upya kumchafua mama huyu ambaye ameiletea Tanzania sifa kubwa. Watanzania na hasa wenye wivu na maisha ya watu badala ya kuwa na wivu wa maendeleo kama wewe hamtufai kwa sasa.

yani kama huyu mama kashindwa kufanya kazi umoja wa mataifa tusiseme kwakuwa unadai anaonewa wivu lol.... Kiukweli ameonekana kuwa na udhaifu mkubwa sana, siku zinavyozidi kwenda tutasikia mengi kuhusu huyu mama. Asitudanganye kuwa kaamua kupumzika' ukweli ni kwamba hajaweza kufanya kitu chochote kwenye taasisi ile. Kwanza hajaweza hata kujenga umaarufu wa jina lake mwenyewe hata jina la nchi hii. Ngoja atakayechukua nafasi yake uone atakavyoonekana kuwa tofauti kiutendaji na huyo 'Muishiwa Asha Rose Migiro'.
 
Hahahahahahahahahahahahahah!kazi kwakweli
Dr. Asha-Rose Migiro ni mfano halisi wa uwezo wa wanawake wengi wa Tanzania. Kwanza mwanamke akishaweka tu mawigi au minywele bandia kichwani kwake au minywele kuwa kama ya kihindi, kizungu, kiaarabu basi ujue huyo ni bomu yaani ajitambui, na kama ajitambui atatambuaje wajibu wake kwake mwenyewe na kwa jamii?!!
 
Wakuu, kuna mtu yeyote atakua na picha ya Mama Migiro akiwa hana wigi kichwani akatutundikie hapa ukutani?
 
Back
Top Bottom