Miezi sita ya Godbless Lema Bungeni

Mh. Lema anapambana kuongoza municipal. Hilo litamwezesha kupanga vizuri vipaumbele vya halmashauri. Akifanikiwa sote tutakuwa mashaidi wa maendeleo ya Arusha. Sasahivi hata bajeti inapitishwa kwa nguvu bila kufuata utaratibu. Ni vigumu kuyaona maendeleo katika hali kama hii!
 
Chama siyo kinachofanya kazi, kazi inafanywa na Mbunge husika kutokana na uelewa wa mambo na busara zake. Usikae kichama kwenye hii hoja kaa ki perfomance.

Mbunge hafanyi kazi ila anasimamia utekelezaji, kazi inafanywa na mwananchi mwenyewe, halafu lema kuwa mbunge siyo kuwa eti anabusara hapana wenye busara ni nyinyi mliomtuma kule bungeni akawasemee matatizo yenu.

Nikupongeze kwa speech yako nzuri kwa mbunge wako. Mimi mbunge wangu kaonesha nia ya dhati ya kuichukia posho kiasi kwamba imekuwa ni haramu kwake sijui huyu wako kama kaipenda hii ya ulaji wake kupunguzwa?
 
Kama mna mambo yenu binafsi na mbunge hukuwa na sababu ya kuficha hiyo checklist. Lakini kama ni suala linalohusu public, basi huna budi kuweka wazi hiyo checklist. Kama hiyo checklist ina mambo ya bafuni, basi tunaweza kukusaidia kupata cellphone number yake muwasiliane privately kwa urahisi kuliko hapa JF.
 
WanaJF la muhimu hapa tuanze kuwakumbusha hawa waheshimiwa wetu mara tu bunge la bajet hii litakapopita kwa sababu mipango iliyokuwa ikiendelea ilikuwa ile ya wabunge waliopita ambayo ilipitishwa bajet ya 2010 - 2011 others labda tuwe na ajenda nyingine.
 
do u teach u r husband how to sex or u give him sex??

batilda burian wewe''
Acha matusi mkuu......punguza munkari
Mbunge hafanyi kazi ila anasimamia utekelezaji, kazi inafanywa na mwananchi mwenyewe, halafu lema kuwa mbunge siyo kuwa eti anabusara hapana wenye busara ni nyinyi mliomtuma kule bungeni akawasemee matatizo yenu.

Nikupongeze kwa speech yako nzuri kwa mbunge wako. Mimi mbunge wangu kaonesha nia ya dhati ya kuichukia posho kiasi kwamba imekuwa ni haramu kwake sijui huyu wako kama kaipenda hii ya ulaji wake kupunguzwa?

Nadhani hii ina-apply pia Mpanda Mashariki, Bunda, Bagamoyo, Ulanga Magharibi, Singida Mjini, Igunga, Monduli, Chalinze, Kinondoni wote hawana busara isipokuwa wapiga kura wao tu..........
 
Chama siyo kinachofanya kazi, kazi inafanywa na Mbunge husika kutokana na uelewa wa mambo na busara zake. Usikae kichama kwenye hii hoja kaa ki perfomance.

ngoja nikuwekee check list ya babu yako kikwete hapa,mwenyewe utaichana
 
basi we baki na hizo akili zako za kizamani, serikali ni ccm sasa unataka walete maendeleo kwa mbunge wa upinzani? hii ni siasa bibie sio sindimba. Nyie mtarudi CCM 2015 lasivyo mtakiona cha moto.

Sioni sababu ya kuwarudisha ccm 2015, wakati kunawabunge wa ccm wamekaa miaka 30 na majimbo yao bado ni balaa

Barabara mbovu
Maji safi na ya uhakika hakuna,
Shule Hazina madawati, waalimu, vitabu nk,
Hospitali hakuna dawa, waganga na wauguzi,
Hakuna Umeme

Mbaya zaidi wabunge hao wa ccm hawana mawazo ya ubunifu kwa miaka yote na wanasinzia tu bungeni hata kusema hawaongei.

ukitaka tuwataje kwa majina na majimbo wanapotoka tutakwambia.

ila kwa upande wa Mh. Lema mimi naona amefanya vizuri sana, kwanza ameanza kwa kuwatoa uoga watanzania kwa ujumla wao, amewahamasisha kuwa wajasiri katika kudai haki, amekuwa mstari wa mbele katika kuwaonyesha jinsi amabavyo haki hudaiwa. hayo ni mafanikio makubwa sana kwa kipindi cha miezi sita.
 
Shikamoo Mh Mbunge, napenda kukumbusha kwamba sasa hivi imeshatimia miezi sita tangu uingie bungeni rasmi nafasi ambayo uliipigania sana na Mungu akakusaidia ukaipata. Nadhani umeshahudhuria vikao kama vinne hivi vya bunge ikiwemo hiki cha bajeti. Nimeona leo tuae chini mimi na wewe tupitie ile check list yetu yaani mimi mwananchi na wewe Mh Mbunge. Check list inajumuisha yote yale uliyoongea mwaka jana katika kipindi cha miaka mitatu ukiwa unapambana na Mama yetu Batilda. Mimi check list yote ninayo ila mwenzangu sijui kama ullitunza ili ikusaidie kwenye safari yako ya 2015. Kama hutojali naomba uniwekee check list yako hapa ili niangalie ni lipi umekwishalifanya ndani ya kipindi hiki cha miezi sita.

Ninyi ndio wale wale msiojua hata Katiba ya nchi inasemaje kuhsu majukumu ya mbunge. Kasome ibara ya 63 (2) ili ufahamu majukumu ya mabunge, hayo umayotaka akueleze ni mifumo ya kwa euza wabunge kuwa matarishi wa vijimiradi kutoka Serikali kuu na zile za mitaa kuja kwa wananchi katika majimbo yao ilihali mbunge na kazi moja ya kuisimamia Serikali tu.
 
Pukudu thanks very much hili hata mimi nimeliona ila nataka yale ambayo yana impact kwa jamii nzima. Nina uhakika watu wenye shida ya ada ni zaidi ya mia nne hapa Arusha. So tuhesabu vile vitu vyenye impact kwa jamii nzima na siyo society yenye access na yeye.

Hili ni muhimu sana tena linahusu jamii kubwa, linahusu wale wenye hitaji, wewe unaweza ukaliona ni dogo kwa kuwa unaweza ukalipia ada wanao, au wazazi wako waliweza kukulipia. lakini kuna watoto, wanageuka kuwa watumishi wa ndani na hata makahaba kwa kuwa tu wazazi walishindwa kumlipia ada ya shule na kwa kuwa serikali haiwajali wasio kuwa nacho wanaishia huko.
 
Shikamoo Mh Mbunge, napenda kukumbusha kwamba sasa hivi imeshatimia miezi sita tangu uingie bungeni rasmi nafasi ambayo uliipigania sana na Mungu akakusaidia ukaipata. Nadhani umeshahudhuria vikao kama vinne hivi vya bunge ikiwemo hiki cha bajeti. Nimeona leo tuae chini mimi na wewe tupitie ile check list yetu yaani mimi mwananchi na wewe Mh Mbunge. Check list inajumuisha yote yale uliyoongea mwaka jana katika kipindi cha miaka mitatu ukiwa unapambana na Mama yetu Batilda. Mimi check list yote ninayo ila mwenzangu sijui kama ullitunza ili ikusaidie kwenye safari yako ya 2015. Kama hutojali naomba uniwekee check list yako hapa ili niangalie ni lipi umekwishalifanya ndani ya kipindi hiki cha miezi sita.

1. Amefanikisha CCM kujivua magamba; we kuangushwa mzee mzima Makamba unadhani mchezo?
2. Muswada feki wa sheria ya mabadiliko ya katiba umeshindwa bungeni
3. CCM imepoteza kabisa direction sasa wanakwenda kwa msaada wa upepo tu

Achana na cheki listi yako mjomba hiyo; hayo yote ni katika kipindi cha miezi sita tu sasa multiply by 10 utajua kitakacho watokea magamba 2015
 
Pukudu thanks very much hili hata mimi nimeliona ila nataka yale ambayo yana impact kwa jamii nzima. Nina uhakika watu wenye shida ya ada ni zaidi ya mia nne hapa Arusha. So tuhesabu vile vitu vyenye impact kwa jamii nzima na siyo society yenye access na yeye.

dada kufacilitate wanafunzi 400 kwenda shule ni impact kubwa sana dont underestimate it (kama kweli kafanya hivyo). Jiulize hao 400 wasingeenda shule si wangeongeza namba ya watu waliopo kijiweni au ombaomba!!.

Ni vema turudi kwenye JD ya mbunge, siamini kama mbunge ndo anajenga kitu fulani.. jukumu lake kubwa ni kutuwakilisha bungeni na at the same time kuhakikisha eneo analowakilisha linakuwa katika ramani ya maendeleo.
hebu soma hapa uone majukumu ya mbunge then jadili:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/26243-nini-majukumu-ya-mbunge-kwa-wapiga-kura-wake.html
Tunazifahamu kazi za mbunge?
 
basi we baki na hizo akili zako za kizamani, serikali ni ccm sasa unataka walete maendeleo kwa mbunge wa upinzani? hii ni siasa bibie sio sindimba. Nyie mtarudi CCM 2015 lasivyo mtakiona cha moto.

Inaonyesha uwezo wa ubongo kupambanua ni mdogo. Huduma kwa wananchi ipo vile vile hata awe nani yupo madarakani.
 
Anza na na huyu anayekusanya kodi kwanza.

Ahadi za Kikwete:
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  35. Kulinda haki za walemavu- Makete
  36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  42. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
  57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
 
Shikamoo Mh Mbunge, napenda kukumbusha kwamba sasa hivi imeshatimia miezi sita tangu uingie bungeni rasmi nafasi ambayo uliipigania sana na Mungu akakusaidia ukaipata. Nadhani umeshahudhuria vikao kama vinne hivi vya bunge ikiwemo hiki cha bajeti. Nimeona leo tuae chini mimi na wewe tupitie ile check list yetu yaani mimi mwananchi na wewe Mh Mbunge. Check list inajumuisha yote yale uliyoongea mwaka jana katika kipindi cha miaka mitatu ukiwa unapambana na Mama yetu Batilda. Mimi check list yote ninayo ila mwenzangu sijui kama ullitunza ili ikusaidie kwenye safari yako ya 2015. Kama hutojali naomba uniwekee check list yako hapa ili niangalie ni lipi umekwishalifanya ndani ya kipindi hiki cha miezi sita.

Akikuwekea hiyo list hapa ntavua hijab yangu na hiyo picha ya kwenye avatar yangu ntaitoa. Labda umuwekee wewe.
 
Back
Top Bottom