Miaka 8 bila kazi, tangu nimalize chuo kikuu

Miaka 8 bila kazi, tangu nimalize chuo kikuu

Dogo hakuna elimu isiyo na maana ila wewe ndo hauna maana[emoji419][emoji375].
Dogo ukisoma sio lazima kuajiliwa tuuuuu, kusoma ni kuondoa ujinga, ila wewe imesoma na hujaondoa ujinga, hivo elimu ulosoma haina msaada kwako
Sawa mkuu
 
Habari wanaJF....

Toka nko Primary school (PS), walimu wetu walipenda sana kutusihi kusoma kwa bidii ili tufanikiwe kimaisha. Toka mentality hiyo ya PS, niliwekeza mda wangu kwenye kusoma kwa bidii ili niyaishi maisha wanayosema walimu wetu.

Nmesoma shule kwa takilibani miaka 16 (toka Primary school mpaka nachukua degree yangu) kwa juhudi kubwa sana. Hatimae mambo yaligeuka toka pale nilipomaliza chuo na kurudi mitaani kufuata maisha yale walimu wetu walituambia, chakushangaza mambo yako tofauti kabsa.

Sasa na miaka 8 toka nmemaliza chuo, sjawahi kupata kazi ya maana. Tofauti na vibarua vidogo vidogo baada ya kumaliza chuo. Si kwamba skutafuta kazi, nmezunguka almost mikoa 8 Tanzania, nmefanya interviews za serikali zaidi ya 20, private sector zaidi ya 60. Nmerudi nyumban wale niliowaacha la 7 na F4, wana nyumba, biashara wengine magari.

Conclusion:
Tanzania [emoji1241] elimu haina maana.
hatari
 
Sijisifu lakini ndiyo ukweli.

Mjukuu wangu yupo "form three" Tanzania hii tena mbali na jiji, hajawahi kukaa bila kufanya kazi siku za Jumamosi, Jumapili, Holidays na Livu zao za shule.

Ni malezi tu. Huyo analelewa na FaizaFoxy toka ana mwaka mmoja na nusu. Nimemlea kwa mtindo wa "No free Lunch". Na sijam "influence" kabisa kumtafutia kazi za kufanya "connections" anazitafuta mwenyewe, mimi nampa ushauri tu inapobidi. Yupo huru kuufata au kuutosa.

Kuna ndugu yangu mmoja siku moja alinilalamikia mwanae kamaliza chuo mwaka juzi hana kazi, kama kuna mpango wowote nisimsahau. Nikamwambia mpango upo, amlete kwangu, akamleta, baada ya wiki tu, huyu kijukuu ambacho bado kipo "form three" ndiyo kinamtafutia kazi za kufanya "anko" wake.

Mie nawatazama tu, unaenda mwezi wa pili na zaidi huu.

Vijana mnaotafuta kazi, ulizeni niwape ushauri. Tanzania kuna kazi nyingi sana za kufanya na na zinakutafuta wewe, siyo wewe uzitafute.
Naomba ushauri mkuu...
 
IT za sasa hawajui hands on plus config....ndio maana hawaajiriki...hawajui chochote ni theory tu wamesoma kama notes....nani atakuajiri ukajifunze kazini ? Labda Govt sekta binafsi anataka kesho abakupa password unaingia kazini....sio uanze kufundishwa servers config au routers config.....database plus language zake.....nawaona IT wemgi siku hizi hawajui hands on wana depend suppliers kila kitu.......
Huu ni ukweli mchungu. Huyo dogo anasema ni website developer nikamuuliza kama ana website yoyote aliyodesign naona kimya
 
Elimu inasaidia Sana sema ukitaka kuifadi Elimu yako hakikisha unajua kiingereza vizuri then Anza kusoma vitabu vyenye self development utaanza kuona some changes in ur life circulation.

Honestly MAARIFA ni utajiri mkubwa Sana .

Unapoanza kupima Mafanikio yako na watu walioishia darasa la Saba au form your failure kuwa wameoa, wananyumba ..hapo lazima upate sonona kwa ajili ya wivu .

Maana hivyo vitu vyote u unaweza kuvipata even a single day so tafuta Sana Maarifa ili uwe mtu huru asiyelalamika Bali kushukuru kwa kila Jambo.
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Nakumbuka kipindi hicho hii fani ndiyo ilikuwa inaanza na watu wanasema ina dili sana hivyo wengi wakaikimbilia DIT na vyuo vingine kumbe famba tu!!!
Hapana sio famba. Hii fani bado ipo juu sema graduates wengi practically wako ovyo.. wale watundu watundu wote hawakosi kazi.
 
Huu ni ukweli mchungu. Huyo dogo anasema ni website developer nikamuuliza kama ana website yoyote aliyodesign naona kimya
Website developer kila mtu anaweza .....vijana hawajui ukiwa chuo pambana sana usome certifications on line......maana zipe saaa ndio kazi....theory nani atakuajiri ?? Ccna ccnp ....security....database oracle .....sql etc...! Unakuja kuomba kazi hujui lolote .....mimi nianze kukufundisha hata ccna huna....nakupa router hata config basics hujui.....zamani mcse....ilikuwa must kupata assured job....banks telecom etc....course online bure .....tu badala kukaza huko wao wako insta.....nani atakuajiri na theory zako ??
 
Habari wanaJF....

Toka nko Primary school (PS), walimu wetu walipenda sana kutusihi kusoma kwa bidii ili tufanikiwe kimaisha. Toka mentality hiyo ya PS, niliwekeza mda wangu kwenye kusoma kwa bidii ili niyaishi maisha wanayosema walimu wetu.

Nmesoma shule kwa takilibani miaka 16 (toka Primary school mpaka nachukua degree yangu) kwa juhudi kubwa sana. Hatimae mambo yaligeuka toka pale nilipomaliza chuo na kurudi mitaani kufuata maisha yale walimu wetu walituambia, chakushangaza mambo yako tofauti kabsa.

Sasa na miaka 8 toka nmemaliza chuo, sjawahi kupata kazi ya maana. Tofauti na vibarua vidogo vidogo baada ya kumaliza chuo. Si kwamba skutafuta kazi, nmezunguka almost mikoa 8 Tanzania, nmefanya interviews za serikali zaidi ya 20, private sector zaidi ya 60. Nmerudi nyumban wale niliowaacha la 7 na F4, wana nyumba, biashara wengine magari.

Conclusion:
Tanzania [emoji1241] elimu haina maana.
Ulilazimishwa kutobaki na wenzio baada ya drs la saba?
 
Information Technology (IT)
Kweli penye miti hapana wajenzi, nimesomea degree tofauti na masuala ya IT lakini baada ya kumaliza chuo nikagundua fursa kwenye hizo nyanja za IT na nimeweza kutengeneza mpunga wa kutosha kwa kujiongeza na kujifunza vitu vidogo vidogo vya IT online ambavyo nimeweza kuvifanyia kazi na kupiga hela.

Mkuu kwa course uliyosoma haukuwa na haja ya kuzunguka na vyeti.
 
7yrs ukaanza shule. Ukasoma kwa 16yrs . Unatafuta kazi kwa 8yrs. Hivyo umri wako ni kati ya miaka 30-33. Bado Jua halijazama una muda wa kupambana ila kama hujapata mtoto umezingua.
Fanya hivi. Sahau kama ulisoma anza kupambana kwa namna zisizotegemea elimu yako. Elimu utaitumia ukifanikiwa bila elimu
Hajazingua kuhusu mtoto. Anatakiwa apate mtoto ndani ya ndoa. Kwa hapo unamuonea kijana.
 
IT za sasa hawajui hands on plus config....ndio maana hawaajiriki...hawajui chochote ni theory tu wamesoma kama notes....nani atakuajiri ukajifunze kazini ? Labda Govt sekta binafsi anataka kesho abakupa password unaingia kazini....sio uanze kufundishwa servers config au routers config.....database plus language zake.....nawaona IT wemgi siku hizi hawajui hands on wana depend suppliers kila kitu.......
Si kweli mkuu.

IT ni pana sana. Hata mim kuna sehem nmei-master sana na kuna sehem siko vizuri.
Si kila mwana IT anafanana na mwingine knowledge ya IT (Kama Account, Law, Business Administration, au Procurement.....). IT unachagua mwenyew wapi una-specialize (kama ni Networking, Database, Programming, Hardware, etc.).
Please don't generalised
 
Aisee! Inakuwaje msomi wa IT unalalamikia ajira! Kuna mwenzako nipo naye huku kijijini, ana degree yake ya IT kutoka Mzumbe! Aisee anapiga hela mpaka basi kupitia ofisi yake.

Jiajiri kijana. Maisha ya kujiajiri ni matamu sana kuliko yale ya kuajiriwa.
Asante sana mkuu...
 
Sina ajira, sijawahi kuajiriwa, ila kwa maelezo ya OP miaka 8 kazunguka mikoa karibu yote, kaomba kazi serikalini mpaka private ila holaaa, kwa experience yangu imebidi nishangae tena especially kama OP ni mwenyeji wa dar (born n raised)
Naomba kujua maana ya OP kwa humu JF mkuu.
 
7yrs ukaanza shule. Ukasoma kwa 16yrs . Unatafuta kazi kwa 8yrs. Hivyo umri wako ni kati ya miaka 30-33. Bado Jua halijazama una muda wa kupambana ila kama hujapata mtoto umezingua.
Fanya hivi. Sahau kama ulisoma anza kupambana kwa namna zisizotegemea elimu yako. Elimu utaitumia ukifanikiwa bila elimu
Asante sana mkuu.
 
Back
Top Bottom