Miaka 8 bila kazi, tangu nimalize chuo kikuu

Miaka 8 bila kazi, tangu nimalize chuo kikuu

Na sio kulaumu... Lawama zetu sometimes zinaleta upofu
Ni kweli kabisa, lawama za kutaka mtu mwingine awe responsible kwa maisha yako sio sawa lazima upigwe upofu tu maana fursa zile zile wanazotumia F4& std 7 kutokea ungeweza kuzifanya vizuri kwa maarifa uliyotoka nayo huko chuoni unless ulitoka na cheti tupu. Pambana, future ipo kwa watu majasiri tu.
 
Nakazia hapa mimi pia ni muanga wa lile jamaa, nashukuru mungu humu jamiiforum kuna watu wana moyo wakusaidia wengine, baada ya kutoa kilio changu humu mmoja alikiona na kuamua kunisaidia kwa kunielekeza niende kwenye taasisi fulani ambayo walikuwa na uitaji wa mtu mwenye sifa kama zangu , kwasasa nipo huku nimejishikiza kupunguza japo ukali wa maisha lakin niseme tu mbaka sasa najioni kabisaa nipo nyuma ya muda na sijui kama mambo yatakuja kuwa sawa.
Mbaka = mpaka. Watu kama wewe ndo maana mnakosa kazi.
 
Mtu umesoma IT na bado unasema huna ajira kwa miaka 8 toka ulipohitimu chuo..Hiyo IT uliielewa vizuri kweli?..maana naamini usingeshindwa kujiariri hata kidogo na kuacha kulalamika.

Sasa waliosoma Education (Arts) watasemaje??
Sawa mkuu.
Comments zako zinaonesha hujua vizuri nini maana ya IT
 
Habari wanaJF....

Toka nko Primary school (PS), walimu wetu walipenda sana kutusihi kusoma kwa bidii ili tufanikiwe kimaisha. Toka mentality hiyo ya PS, niliwekeza mda wangu kwenye kusoma kwa bidii ili niyaishi maisha wanayosema walimu wetu.

Nmesoma shule kwa takilibani miaka 16 (toka Primary school mpaka nachukua degree yangu) kwa juhudi kubwa sana. Hatimae mambo yaligeuka toka pale nilipomaliza chuo na kurudi mitaani kufuata maisha yale walimu wetu walituambia, chakushangaza mambo yako tofauti kabsa.

Sasa na miaka 8 toka nmemaliza chuo, sjawahi kupata kazi ya maana. Tofauti na vibarua vidogo vidogo baada ya kumaliza chuo. Si kwamba skutafuta kazi, nmezunguka almost mikoa 8 Tanzania, nmefanya interviews za serikali zaidi ya 20, private sector zaidi ya 60. Nmerudi nyumban wale niliowaacha la 7 na F4, wana nyumba, biashara wengine magari.

Conclusion:
Tanzania [emoji1241] elimu haina maana.
Elimu ya Tanzania ni matakataka ambayo hayapo jalalani bali yapo kwenye vichwa vya watu.Tanzania ukitaka kutoboa weka vyeti vyako kabatini anza kupambana upya bila kutegemea vyeti vyako vya taaluma!
 
Kwa hiyo wewe ni IT halafu unalalamika eti huna kazi..?

Yaani umeshindwa hata kufungua banda la kuunguza CD au kurusha nyimbo/movies kwenye flash au kwenye simu hapo mtaani kwenu ?
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom