Miaka 40! Mtambuzi naelekea uzeeni sasa

Mkuu nakuzidi mwaka mmoja,ebu niambie ulaji wako ukoje,je una kitambi,beer vipi unakunywa sana?nyama choma?mazoezi ya viungo,mastrees yanakusumbua?

Niliacha pombe na Sigara miaka 10 iliyopita, na ulaji wangu ni wa kawaida tu, huwa napenda vyakula vya asili hususan mbogamboga. kama nikiumwa napendeelea zaidi kujitibu kwa dawa za miti shamba kuliko za Hospitali, kwetu kuna hazina kubwa sana ya dawa za mitishamba, kwa hiyo huwa sipati shida. kuhusu mazoezi, huwa nafanya jogging siku za weekend na huwa napendelea kutembea kwa miguu niikiwa na safari zangu za hapa na pale kuliko kutumia daladala....................
 
Haaah! Mtambuzi na hizo threads zako, nikadhani uko over 40 kumbe mpaka jana hata 40 ulikuwa hujaifikisha.....lol! Heheheheheee! Hongera yako mkuu, hata hivo umesogea!

Age is nothing but a number my dear...................... nilianza kujifunza mambo hayo hata kabla sijaoa.....................
 
Tarehe kama ya leo, ndio siku ambayo nilizaliwa na kuongeza idadi ya watu hapo Duniani. Si haba, namshukuru muumba kwa kunifikisha hapa nilipo. Pia nawashukuru wazazi wangu, mke wangu mpendwa mama Ngina, na Wanangu Ngina, Ngano na Ngadu, bila kuwasahau wana JF, mahali ambapo pananisaidia kupunguza stress zangu za maisha…………..LOL

Tupo pamoja………………….

Happy birthday Dady Mtambuzi!!!!,Mungu akupe umri mrefu na afya njema mpaka uozeshe wajukuu zako!shuhuli wapi na saa ngapi mkuu?
 
Haaah! Mtambuzi na hizo threads zako, nikadhani uko over 40 kumbe mpaka jana hata 40 ulikuwa hujaifikisha.....lol! Heheheheheee! Hongera yako mkuu, hata hivo umesogea!

Kazini kwangu leo wamebisha sana kuhusu umri wangu, wanadai muonekano wangu uko tofauti na umri wangu, yaani eti ninaonekana kama ndio niko kwenye early 30s hivi...................... Bosi wangu Mzungu, yeye yuko 30 something lakini anaonekana mkubwa kunizidi.............Unajua hii miili iliyokulia vijijini ugali wa dona na wa muhogo na maziwa kwa wingi vinasaidia sana kuboresha afya...............LOL
 
Duh...una bahati sana mkuu. Wengine hili 'dongo' letu kila wakati watu wanakuongezea miaka mitano mbele....unapewa 'shikamoo' mpaka unaona noma!
 
Happy birthday! Mungu akupe maisha marefu zaidi... 40yrz sio mchezo, hadi nakuonea wivu jamani...lol..
 
HONGERA SANA MKUU; HONGERA KWA KUTIMIZA 40!
Ninakushauri uondoe mawazo kichwani mwako kuwa kwa kutimiza 40 unaelekea uzeeni. Ni utu-uzima, mwanzo wa maisha, mwanzo wa busara. Hata mitume wengi walipewa utume katika umri huo. Jivunie kwa kufikisha, kumbuka kuwa mbele kuna 40+ inakusubiri.
 
Hongera sana Mkuu!
Hayo majina ya watoto wako mkuu Ngina, Ngano na Ngadu ni ya kiukweli au ya kutumika hapa jamvini! Maana yamenichekesha, hasa huyo Ngano, nikasema kama ni kweli huyu Mkuu anataka kuharibia wenzake majina. Au na la kwako na la mama Ngina yameanza na Ng....
Msalimie sana Mama Ngina, mpe hongera zake kwa kukuwezesha kufikisha umri huo ukiwa na furaha. Katika msg zako naona kuna furaha na amani katika ndoa ila huyo Ngina inaonekana kakuzidi maujanja. Hata hivyo Mungu atakusaidia. Big Up, Wishing You All the Best
 
Ha ha ha haaaaaa...... Hayo majina ni ya kutumika hapa Jamvini mkuu, ila huyo Ngina, jina hilo ni nickname yake kwa sababu nilizoea kumuita my wife kwa jina la Mama Ngina kabla hajapata mtoto....................
Ni kweli kanizidi Maujanja.....................kule Arusha tunasema ni Pasua Kichwa....................
 
kwa umri huo ndio maana ukawa mvumbuzi,congrs sana afu nimependa mtiririko wa kmajina ya wanao!!!uwe na cku ya heri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom