Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Naitwa Richard M. Philemon, Mwaka 2008 baada ya kuhitimu form six, niliomba vyuo mbalimbali kikiwemo UDSM, lakini wakanipanga Mkwawa University College of Education (MUCE Iringa), sikwenda katika chuo hicho kutokana na sababu kadhaa za kifamilia na nilitoa taarifa.
Mwaka mmoja baadaye nikaomba nafasi UDOM nikafanikiwa kupata, nikaomba pia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) nikapata na nikaendelea na masomo hadi nilipohitimu Mwaka 2012.
Miaka kadhaa baadaye nilipopata kazi, nikaanza kukatwa mkopo wa chuo, nilipofuatilia nikaona kuna madeni mawili ambayo nayalipa kwa wakati mmoja.
Nikabaini kuwa nalipa mkopo wa MUCE ambao unaonesha nilisoma hapo kuanzia Mwaka 2008 pia nalipa mkopo wa UDOM ambao ndipo hasa niliposoma
Nilipofuatilia Bodi ya Mikopo kuhoji hawanipi majibu ya kueleweka, nikataka wanioneshe huo mkopo waliokuwa wanampa Mwanafunzi wa MUCE Iringa napo hawanioneshi
Bodi wanaishia kusema niende MUCE Iringa, chuo ambacho sijawahi hata kukanyaga, naendaje kwao kuwauliza wakati wao Bodi ya Mikipo ndio ambao walikuwa wanaingiza hela, hawataki kuonesha hizo hela zilikuwa zinaingiwa kwenye akaunti ya nani?
Nimesumbuka na Bodi ya Mikopo kwa zaidi ya mwaka sasa nikifuatilia kuhusu deni hilo lakini sipati msaada wowote, najiuliza kuna Watanzania wangapi ambao wanalipa madeni yasiyokuwa yao kama mimi na hakuna kinachofanywa na mamlaka?
Tena ukienda Bodi kuuliza wanakupa majibu ya ukali kweli, hii ni sawa.