Bodi ya Mikopo: Tunafuatilia Madai ya matokeo ya Wanafunzi wa UDOM kuzuiwa kisa kuchelewa kwa malipo ya ada

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Ufafanuzi wa Awali:

Malipo ya Ada ya Mafunzo (Tuition Fee) ya mwanafunzi-mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu unaotolewa na serikali hulipwa kwa baada ya masuala yafuatayo kukamilika:
  1. Chuo kuwasilisha HESLB madai (invoice) sahihi na kwa wakati;
  2. 'Invoice' sahihi ni ile yenye kiwango (amount) sahihi kama kinavyoonekana kwenye mpango wa mkopo wa mwanafunzi (Loans Allocation). Hivyo, kama mwanafunzi amepangiwa ada ya TZS 1,000,000.00, inategenewa 'invoice' itakayowasilishwa iwe ya kiwango hicho;
  3. Kuwasilishwa kwa 'invoice' kwa wakati maana yake ni kuwa katika mwaka wa masomo, ada hulipwa mara mbili, kila baada ya 'semester' moja kwa kuwa utaratibu wa kibajeti ni kwa mwaka. Hivyo, wanafunzi wanapangiwa ada na zinalipwa ndani ya mwaka husika;
  4. Suala jingine, ni dhana ya wajibu. Tunapenda kuhakikisha kuwa hakuna tatizo la fedha na kuwa bajeti ya mikopo ya TZS 654 bilioni kwa mwaka 2022/2023 imetolewa yote na Serikali. Serikali imetimiza wajibu wake.
Dhana ya wajibu nayo inakwenda kwa wanafunzi-wanufaika ambao wana wajibu wa kujitokeza na kuthibitisha wapo vyuoni- masomoni kwa kusaini nyaraka muhimu kwa wakati ili kuviwezesha vyuo kuandaa madai halali na sahihi kwa wakati.

Tunaendelea kufuatilia kwa kuwasiliana na ongozi wa UDOM ili kupata ufafanuzi wa kina.

UDOM WAFAFANUA
Aidha, Ukurasa rami wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) nao umetoa maelezo kwa kuandika:

"Ukweli ni kwamba fedha zao zilikuja kutoka Bodi ya Elimu ya Juu (HESLB) na hawakwenda kusaini kwa muda waliwekewa mpaka fedha zikarejeshwa Bodi, kwa hiyo wanapashwa kufuatilia Bodi ili fedha hizo zirejeshwe chuo."

Pia soma: DOKEZO - Uongozi wa UDOM unazuia matokeo ya mitihani kwa Wanafunzi ambao tumecheleweshewa malipo ya ada kutoka Bodi ya Mikopo
 
hizi pesa za mikopo zimulikwe sawasawa kuna chuo x kinatabia ya kukata pesa za wanafunzi bila ya sababu tayari dawa yao inachemka
 
hizi pesa za mikopo zimulikwe sawasawa kuna chuo x kinatabia ya kukata pesa za wanafunzi bila ya sababu tayari dawa yao inachemka
Si ungekitaja hapa Mkuu kuliko kuandika kwa password tatizo linaendelea kuwepo hao Udom wana matatizo sana ..
 
Utaratibu wa kuwalipia ada kwa 100% wanafunzi wote waliofanikiwa kujiunga na elimu ya juu kabla ya kuanzishwa kwa hii takataka inayoitwa HESLB, ulikuwa ni mzuri sana.
 
Back
Top Bottom