KERO Mfumo wa kufuatilia deni kwa tuliokopa Bodi ya Mikopo (HESLB) una changamoto, haufunguki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi wanufaika wa mikopo ya Bodi ya Mikopo (HESLB) tuliomaliza deni na bodi tunaonewa na HESLB kwenye kipengele cha kuingia kwenye mfumo wa Account ya loan board ili kuweza kuona tathimini ya mwendelezo wa ulipaji mkopo ulivyo.

Ugumu unakuja kwenye Form Four Index Number hazikubali kabisa kwenye mfumo, tunataka kuingia kwenye Account ili kupata certificate kuonyesha kuwa tumemaliza makato, pia kujeshewa hela ambazo HESLB wamezidisha (refund).

Naomba hili lifanyiwe kazi ili Form Four Index ifanye kazi maana hawa jamaa wamefanya kusudi ili wadau tusirejeshewe fedha zinazozidi

Ni mimi mlalamikaji
 
Kama umemaliza kulipa deni ukienda ofisini kwao mbona wanatoa barua inayothibitisha kuwa umemaliza kulipia. Mm nimeenda ofisi ya hesb mwanza mwezi Dec mwaka jana na nilitumia siku moja tu kuipata hio barua
Na kwa Sasa sikatwi hata senti
 
Ukiwa mbali na ofisi msaada wao ni upi?
 
Wakuu msaada sawali hivi iwapo mtu Anataka kuomba mkopo wa elimu ya juu alaf mzazi wake mmoja amefariki je Kuna ulazima wa chetcha Kifo ikiwa cheti chat kuzaliwa kimebainisha kama mzazi amefarik
 
Hilo nalo lakuuliza. Ok inaonekana hujielewi. Cheti cha kifo ni lazima anza lukitafuta mapema. Utakuja kosa mkopo kipumbavu uanze kulaumu healsb

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
 
Hii Bodi ikiishiwa hela za kuwapa wanufaika wao, huwa haioni aibu kuwakata hata wale wafanyakazi ambao hawajawahi kukopa kwenye hiyo Bodi!

Au kuwaletea makato mapya wale wanufaika waliomaliza makato yao, kisa tu hawajachukua hiyo barua ya kumaliza mkopo.
 
Sisi wanufaika wa mikopo ya Bodi ya Mikopo (HESLB) tuliomaliza deni na bodi tunaonewa na HESLB kwenye kipengele cha kuingia kwenye mfumo wa Account ya loan board ili kuweza kuona tathimini ya mwendelezo wa ulipaji mkopo ulivyo.

Ugumu unakuja kwenye Form Four Index Number hazikubali kabisa kwenye mfumo, tunataka kuingia kwenye Account ili kupata certificate kuonyesha kuwa tumemaliza makato, pia kujeshewa hela ambazo HESLB wamezidisha (refund).

Naomba hili lifanyiwe kazi ili Form Four Index ifanye kazi maana hawa jamaa wamefanya kusudi ili wadau tusirejeshewe fedha zinazozidi

Ni mimi mlalamikaji
Watakuwa wanataka kuwapiga na kitu kizito chenye ncha kali
 
Kama umemaliza kulipa deni ukienda ofisini kwao mbona wanatoa barua inayothibitisha kuwa umemaliza kulipia. Mm nimeenda ofisi ya hesb mwanza mwezi Dec mwaka jana na nilitumia siku moja tu kuipata hio barua
Na kwa Sasa sikatwi hata senti
Hiyo dunia ya karne iliyopita mkuu. Kwanini aende ofisini wakati unaweza kufanya kila kitu nyumbani kwako kwa kutumia mfumo tu? ukaokoa muda na fedha....Wanatakiwa kubadilika haraka hii kero bado ipo hata sasa hivi ninapoandika huu ujumbe.
 
Back
Top Bottom