mgunga pori
JF-Expert Member
- Jul 23, 2016
- 4,093
- 4,930
Mkuu hii ndio inaitwa reasoning sasa shangaa v8 zinagharimu mabilioni tunashindwa wekeza kwenye vitu muhimuMie pia nimependa hoja yake na ndio maana nikajiuliza maswali haya.
Maswali yangu ni:
Mpaka lini tutaendelea kulalamika kuhusu kuuziwa/kupewa vitu visivyo bora?
Kwa nini tusitengeneze vipimo vyetu wenyewe kwa ushirikiano wetu wa Umoja wa nchi za Afrika?
Hatuna mahabara? Kuna mahabara ya Umoja wa nchi za Africa hili iwe ina shughulikia magonjwa yetu na ya mlipuko pamoja na kuendelea kufanya utafiti?
Hatuna wana sayansi? Kama wapo serikali zetu lini zitawapa ushirikiano?
Hatuamini mfumo wa elimu zetu?
Kwanini kila kitu tutegemee wengine?; alafu wakitaka kujaribu dawa, chanjo, vipimo vyao kwetu tunakuwa wakali na kulalamika na kusema ni ubaguzi. Mchango wetu kwenye sayansi barani kwetu na duaniani huko wapi?
Mbona wana sayansi wetu wanatumiwa na hizo nchi za nje ambazo tunawategemea kila kitu? Kwa nini sisi tusiwatumie?
Sent using Jamii Forums mobile app