28 Juni 2020
Soga, Pwani
Tanzania

MH. JOHN MAGUFULI ATEMBELEA MRADI WA SGR - RELI KIPANDE CHA DAR - MORO BAJETI TSHS. TRILIONI 7.2

Apanda treni maalum ya uhandisi, aridhishwa na kazi za kampuni Yapi Merkezi Dar Es Salaam - Morogoro RAILWAY mkandarasi toka Turkey . Ziara hiyo aliongozana na waziri Mh. Prof. Palamagamba Kabudi wa wizara mambo ya nje na Mh. mhandisi Isack Kamwelwe waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Suleiman Jafo Waziri ktk Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Kipande cha ujenzi reli-SGR cha Morogoro - Makutupora Dodoma ujenzi ni zaidi ya asilimia 30%. Watu zaidi ya 8,000 wameajiriwa ktk mradi huo wa reli Mpya ya SGR.

Source : TRC Reli TV

Yapı Merkezi is constructing the fastest railway in East Africa. The first phase of the 1,224 km total line, the 202 km long Dar Es Salaam - Morogoro Railway Project, is the most critical part of the project. When the 5-part line is completed, it will connect Uganda, Rwanda, Democratic Republic of Congo and Tanzania, and provide access to the Indian Ocean for all related countries.

The groundbreaking ceremony took place on on April 12, 2017 at Pugu with the participation of HE Dr. John Pombe Joseph Magufuli as President and Commander in Chief of the Armed Forces of the United Republic of Tanzania, Hon. Prof. Makame Mbarawa as Minister of Works, Transport and Communication, Mr. Yunus Belet as acting Ambassador of Republic of Turkey in Dar Es Salaam, Mr. Erdem Arıoğlu as Vice Chairman of Yapı Merkezi, Mr. Özge Arıoğlu as CEO of Yapı Merkezi, Mr. Emre Aykar as Yapı Merkezi Board Member and , Mr. Abdullah Kılıç as Yapı Merkezi East Africa Regional Manager.

All works pertaining to design, manufacture, assembly and operation startup of track superstructure, electrification, signaling, telecommunication, central control systems are being carried out by Yapı Merkezi.

202 km-long single line will be constructed at a design speed of 160 km / h between Dar Es Salaam and Morogoro. During the 30-month project, a total of 33 million cubic meters of excavation work will be undertaken; 96 pieces of 6,500 meter-long bridge and overpasses, 460 culverts, 6 stations and repair and maintenance workshops will be constructed. Source : Dar Es Salaam - Morogoro RAILWAY

28 Juni 2020
LIVE. MHE RAIS DKT. JOHN P. MAGUFULI AKIKAGUA MRADI WA RELI YA KISASA - SGR : DAR ES SALAAM - MOROGORO

Rais Dk. John Magufuli akifurahia jambo ndani ya Behewa la Treni ya Uhandisi alipokuwa akienda Mlandizi mkoani Pwani wakati akikagua kazi za ujenzi wa kipande cha Reli ya Kisasa kutoka Dar es salaam hadi Morogoro, leo. Ujenzi huo umefikia asililimia 80.

Na Mwandishi wa Ikulu
Rais Dk. John Magufuli leo 28 Juni 28, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge) kwa sehemu ya kwanza ya Dar es Salaam – Morogoro na kuelezea kuridhishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa.

Rais Magufuli amesafiri kwa gari kandokando ya reli hiyo kuanzia Kisarawe hado Soga Mkoani Pwani na kisha akapanda kiberenge kilichopita katika reli hiyo mpya kuanzia Soga hadi Kikongo kabla ya kuendelea na safari yake kwa gari kuelekea Morogoro.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Masanja Kadogosa amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa kazi ya ujenzi wa sehemu ya kwanza ya reli hiyo imefikia asilimia 82 ambapo Watanzania 13,000 wamenufaika na ajira na inatarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu (2020).

Akizungumza na wananchi wa Soga na Kikongo, Rais Magufuli amewapongeza kwa kupata mradi huo na ametaka waendelee kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa ili waweze kunufaika zaidi na mradi huo.
 
29 Juni 2020
Kilosa, Morogoro
Tanzania

Uwekaji Jiwe La Msingi SGR Reli Mpya ktk Mahandaki Ya Kilosa

Mh. John Pombe Joseph Magufuli aweka jiwe la msingi na saini yake (graffiti ) ktk ujenzi wa mahandaki katika reli ya SGR Mpya sehemu ya Kilosa mkoani Morogoro Tanzania

Source : TRC Reli TV
 
29 Juni 2020
Kilosa, Morogoro
Tanzania

Shangwe na Nyimbo ndani ya Handaki SGR
Viongozi wa awamu ya 5 ya serikali ya CCM Mpya wakiongozwa na Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli wapongezana kwa nyimbo ndani ya handaki la reli Mpya SGR
 
Miaka 15 ni kuendelea kutumika baada ya kukarabati sio inakarabatiwa kwa miaka15 acha uzwazwa
Okay sawa tunaunga mkono juhudi... maana muda wa kukamilika ns kuanza kutumika SGR haujulikani kinyume na ilivyoelezwa awali!!!
Kwa mantiki hii... hadi mradi huu ukamilike!!!
Namkumbuka Kamuzu Banda...
 
16 Julai 2020
SGR-RELI SASA YAHAMIA MAONESHO YA SABASABA NA ZIARA WAKUU WA VYUO VIKUU BILA KUSAHAU SHANGWE LA WCB KWA MAFUNDI SGR !

Source : TRC RELI TV
 
30 July 2020
Dar es Salaam, Tanzania

TANZANIA NEW RAILWAY (SGR ) PROJECT PROGRESS REPORT FOR THE MONTH OF JUNE 2020 (WITH SUBTITLES)

The 1,224 km long SGR RAILWAY line construction in Tanzania
Yapı Merkezi is constructing the fastest railway in East Africa. The first phase of the 1,224 km total line, the 202 km long Dar Es Salaam - Morogoro Railway Project, is the most critical part of the project. When the 5-part line is completed, it will connect Uganda, Rwanda, Democratic Republic of Congo and Tanzania, and provide access to the Indian Ocean for all related countries.

The groundbreaking ceremony took place on on April 12, 2017 at Pugu with the participation of HE Dr. John Pombe Joseph Magufuli as President and Commander in Chief of the Armed Forces of the United Republic of Tanzania, Hon. Prof. Makame Mbarawa as Minister of Works, Transport and Communication, Mr. Yunus Belet as acting Ambassador of Republic of Turkey in Dar Es Salaam, Mr. Erdem Arıoğlu as Vice Chairman of Yapı Merkezi, Mr. Özge Arıoğlu as CEO of Yapı Merkezi, Mr. Emre Aykar as Yapı Merkezi Board Member and , Mr. Abdullah Kılıç as Yapı Merkezi East Africa Regional Manager.

All works pertaining to design, manufacture, assembly and operation startup of track superstructure, electrification, signaling, telecommunication, central control systems are being carried out by Yapı Merkezi.

202 km-long single line will be constructed at a design speed of 160 km / h between Dar Es Salaam and Morogoro. During the 30-month project, a total of 33 million cubic meters of excavation work will be undertaken; 96 pieces of 6,500 meter-long bridge and overpasses, 460 culverts, 6 stations and repair and maintenance workshops will be constructed.
Yapı Merkezi İnşaat ve Sanayi A.Ş.
Source : TRC RELI TV
 
30 July 2020
Dar es Salaam, Tanzania

TANZANIA NEW RAILWAY (SGR ) PROJECT PROGRESS REPORT FOR THE MONTH OF JUNE 2020 WITH SUBTITLE

Source : TRC RELI TV

Mwishoni kabisa eti imechukua muda mchache kumalika wakati walisema kufikia mwezi wapili ilitakiwa iwe imeisha mwaka huu, na wakaomba kuongezewa miezi sita sasa imeisha namzigo bado kabisa haujakamilika😀😀. Hichi kipande Cha Dar-Moro kitaisha 2022.
 
7 August 2020
Dar es Salaam, Pugu na Ruvu

Waziri mkuu atembelea vipande vya reli Dar Moro vilivyokamilika

Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw. Masanja Kungu Kadogosa amueleza Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa kipande hicho cha ujenzi wa SGR reli mpya Dar - Moro kimetumia zaidi ya shilingi trilioni moja za kiTanzania. Hii ni ziara ya tatu kwa waziri mkuu ili kukagua maendeleo ya ujenzi wa reli mpya ya SGR mara ya mwisho ilikuwa mwezi Mei 2020. Pia Mh. Rais John Magufuli aliutembelea mradi huo mwisho mwa mwezi Juni 2020 kukagua utekelezaji wake.

Waziri Mkuu ameelezwa kuwa ktk ujenzi wa vipande kwa awamu kati ya Dar - Morogoro, sehemu iliyokamilika ya reli kipande cha Pugu - Ruvu urefu wa 50 kilometa SGR reli kampuni ya Yapi Merkezi ya Turkey wanapitisha treni yenye kichwa ( locomotive ) chenye kuvuta behewa moja maalum la uhandisi kukagua kazi.

Pia Mkurugenzi Mkuu wa TRC anebainisha kuwa kuna mchakato wa kununua mabehewa na vichwa locomotive ili reli hiyo ikikamilika iweze kutumiwa na treni baina ya Dar - Moro SGR reli mpya.

Pia Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania Prof. John Kondoro amemueleza Waziri Mkuu Mh. Majaliwa kuwa shirika la reli kupitia mradi maalumu wa Reli ya Mkoloni MGR linaimarisha reli toka Dar es Salaam mpaka Isaka ili kuwezesha treni katika reli ya kati ya mkoloni kubeba uzito zaidi na kuongeza kasi ya mwendo wa treni.
Source : TRC Reli TV
13 Feb 2020
SERIKALI YAKOPA TRILIONI 3.3 KUENDELEZA UJENZI WA RELI | TBC1 SERIKALI imetia saini mkopo wa zaidi ya shilingi Trilioni Tatu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa reli ya kisasa katika kipande cha pili kutoka Morogoro hadi Makutupora Singida... Source : Tanzania yapata Mkopo wa Sh. Trilioni 3.3 toka Standard Chartered Bank kwa ajili ujenzi reli ya SGR

The 1,224 km long SGR RAILWAY line construction in Tanzania
Yapı Merkezi is constructing the fastest railway in East Africa. The first phase of the 1,224 km total line, the 202 km long Dar Es Salaam - Morogoro Railway Project, is the most critical part of the project. When the 5-part line is completed, it will connect Uganda, Rwanda, Democratic Republic of Congo and Tanzania, and provide access to the Indian Ocean for all related countries.

The groundbreaking ceremony took place on on April 12, 2017 at Pugu with the participation of HE Dr. John Pombe Joseph Magufuli as President and Commander in Chief of the Armed Forces of the United Republic of Tanzania, Hon. Prof. Makame Mbarawa as Minister of Works, Transport and Communication, Mr. Yunus Belet as acting Ambassador of Republic of Turkey in Dar Es Salaam, Mr. Erdem Arıoğlu as Vice Chairman of Yapı Merkezi, Mr. Özge Arıoğlu as CEO of Yapı Merkezi, Mr. Emre Aykar as Yapı Merkezi Board Member and , Mr. Abdullah Kılıç as Yapı Merkezi East Africa Regional Manager.

All works pertaining to design, manufacture, assembly and operation startup of track superstructure, electrification, signaling, telecommunication, central control systems are being carried out by Yapı Merkezi.

202 km-long single line will be constructed at a design speed of 160 km / h between Dar Es Salaam and Morogoro. During the 30-month project, a total of 33 million cubic meters of excavation work will be undertaken; 96 pieces of 6,500 meter-long bridge and overpasses, 460 culverts, 6 stations and repair and maintenance workshops will be constructed.
Yapı Merkezi İnşaat ve Sanayi A.Ş.
 
11 August 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Wastaafu watembezwa ujenzi SGR Reli

Wastaafu watembelea kipande cha sehemu iliyokamilika ya SGR Reli, wapakizwa katika treni ya uhandisi kuona reli iliyokamilika kati ya stesheni za Pugu na Ruvu katika ujenzi unaoendelwa wa kipande cha Dar - Moro.

Source : TRC Reli TV
 
20 August 2020
Mpanda, Katavi
Tanzania

Kipande kipya cha reli kwenda Pwani ya Ziwa Tanganyika kujengwa bajeti shilingi 60bn

Ujenzi wa reli mpya kilometa 120 ya meter gauge rail (MGR) toka Mpanda mkoani Katavi mpaka bandari ya Karema katika Pwani ya ziwa Tanganyika, Tanzania kuanza

Kuhudumia nchi za maziwa makuu za DR Congo kupitia bandari ya Kalemie nchini DR Congo na Zambia kwa njia ya meli toka bandari ya Karema, Tanzania hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa TRC Masanja Kungu Kadogosa.

Ujenzi wa bandari ya Karema nchini Tanzania utachukua miaka miwili hivyo TRC nao wanataka kuhakikisha reli hiyo ya MGR inakamilika mapema ili bandari ya Karema ifanya kazi kwa ufanisi kwa kuunganishwa na moja kwa moja na bandari ya Dar es Salaam iliyopo ktk Pwani ya Bahari ya Hindi kupitia Tabora, Kaliua, Mpanda mpaka Karema.

Masanja Kungu Kadogosa amesema tuta la reli ya MGR toka Mpanda mpaka Karema litakuwa la SGR ili siku za baadaye mfumo wa reli ya SGR ukifika Mpanda kutakuwa hakuna haja ya kujenga tuta jipya.

Source : TRC RELI TV
 
TRC YAJA KATAVI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS,ZAIDI YA BIL 60 ZATENGWA UJENZI WA RELI MPANDA - KAREMA

Published on 20 Aug 2020
#NEWS Kufuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa maagizo wakiwa ziarani Mkoani Katavi kuhakikisha Reli ya kutoka Kaliuwa-Mpanda na Mpanda-Karema inaimarika, Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa amefika Mkoani ili kuanza utekelezaji.

Kadogosa amesema mantiki hasa kubwa ni kufungua uwezo wa kibiashara kati ya Tanzania na Nchi zilizotuzunguka hususani nchini Congo ambapo amesema sehemu kubwa ya Bandari nchini Tanzania mizigo inayopatikana ni kutoka Congo.

Hata hivyo Kadogosa amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa Juma Homera kuwa Serikali imetenga Bajeti zaidi Bilioni 60 za kuanzia. Vilevile amezungumzia changamoto ufinyu uliopo Sehemu ya abiria na wafanyabiashara kukosa sehemu ya kuhifadhia mizigo yao kwa ajili ya kusafirisha wakiwa stesheni ya Mpanda ambapo kama kamati ya Miundombinu wameahidi mwaka huu kujenga kituo kizuri kwa ajili ya abiria na ghala la kuhifadhi mizigo mingi zaidi huku akisema bajeti ya ujenzi huo imeshatengwa.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera amesema kama Mkoa watashirikiana vizuri kuhakikisha Mradi unatekelezeka kwa wakati na hakuna kikwazo chochote kitakachojitokeza huku Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Mhando ambaye Mradi huo unatekelezwa katika Wilaya yake amesema Mradi huo umekuja muda muafaka katika wakati ambao Mkoa na Wilaya unakwenda kwenye mfumo wa Viwanda na kuahidi kutoa ushirikiano.
Source : Sitetvtz
 
Kuna time huwa namuelewa sana JPM nikifikia wakati huo wa kumuelewa huwa nahakikisha natafuna hindi la kuchoma 👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾
Kuna vimambo vizuri anavifanya tunaviona kabisa sema tu ni vile ametia kutu vyuma ndio tunakosa hamu. Ila anafanya tuvitu vitu tuzuri. 😜
 
23 Agosti 2020
Mpanda, Tanzania

Mkurugenzi Mkuu abanwa na wananchi, mradi utakamilika lini ?

Wananchi wa vijiji kama Msasani, TambukaReli n.k wamembana mkurugenzi mkuu wa TRC Bw. Masanja Kungu Kadogosa kwa maswali lini mradi utaisha, reli mpya itafika kwao lini , fidia ya nyumba zao zilizopigwa alama ya X n.k kwani ni muda wa miaka miwili wanasikia stori zile zile.
 
..Mchina alijenga reli ya Tazara toka Dar mpaka Kapirimposhi kwa miaka mitano.

..Mturuki huu ni mwaka wa 4 hajamaliza kipande cha Dar kwenda Morogoro.
 
..Mchina alijenga reli ya Tazara toka Dar mpaka Kapirimposhi kwa miaka mitano.

..Mturuki huu ni mwaka wa 4 hajamaliza kipande cha Dar kwenda Morogoro.

Ngoma nzito sasa wanakuja kivingine kimya kimya hawasemi tena SGR reli mpya bali wanaanza kuboresha reli ya jeremani na kufikiria kuongeza reli zingine zisizo za SGR maana wamebaini kazi hii siyo mchezo alisema mhandisi angalau siyo chini ya miaka 15 kama fedha zipo, feasibility studies itaonesha lilikuwa jambo jema na pia kama nchi jirani watatia / kuchangia pesa ujenzi wa SGR.

Ukweli mradi huu walikurupuka hautaisha mradi huu wa SGR Mpya reli utakuwa wa kipande cha kilometa chache kati ya 1,200 kilometa walizojidai wanataka kukamilisha.
 
..Mimi na-support sgr.

..wasiwasi wangu ni gharama zake, na kama itaendeshwa kibiashara.

..pia sina uhakika kama uchumi wa waTz, our purchasing power, unaturuhusu kutumia treni za mwendo kasi za umeme.

..labda SGR iishie Isaka na kuwe na bandari kavu ya nchi za Rwanda, Burundi, na Eastern Congo.

NB:

..Mjapani aliwahi kushauri kwamba tuikarabati reli ya meter gauge inatosha.

..Rwanda au Burundi hawana uwezo wa kuchangia mradi huu.
 
Yaani hii pesa iliyotumika mpaka sasa ingetumika kuimarisha reli ya mkoloni ibebe mzigo mzito, iwe na kasi na kukwepa mafuriko ya Mto Mkondoa kupitia mahandaki yanayojengwa Kilosa na kule Manyoni , Ruvu kurekebisha tuta la reli / madaraja mambo yange kuwa safi upande wa usafiri wa reli nchini Tanzania. Na kubwa zaidi mradi ungekamilika ndani ya miaka mitano na kuleta mafanikio tajika. Lakini huu mradi wa full SGR Reli Mpya wa kilometa 1200 na mbwembwe nakshi zake hautaisha kabisa.
 
13 September 2020
Morogoro, Tanzania

MRADI WA SGR RELI MPYA WAPAMBA MOTO, WAHAMISHA MAKABURI MGOLOLE PANGAWE MOROGORO

Jumla ya makaburi 342 katika Vijiji vya Mikese, Kidugalo, Pangawe yatahamishwa ili kupisha mradi huu mkubwa wa reli mpya ya SGR mkoani Morogoro ambao ujenzi wake unaendelea kwa vipande unaoanzia pwani ya bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam kuelekea mpaka jijini Mwanza katika fukwe za Ziwa Victoria nchini Tanzania.
 
Back
Top Bottom