Hii si hali ya kushangilia hata kidogo.Imagine uko hosp na hali mbaya then mgomo unatokea,then imagine unaumwa sasa na kuna mgomo!Imagine wagonjwa walioko hosp!imagine.
Lkn madoc c wakulaumiwa,kwani hii ndio njia ya kushinikiza kusikilizwa pale sirikali isiyojali watu wake inapopuuza walipakodi wake!Acha tufe kwa ukombozi wa watakaobaki.Huu ndio msimamo tuliotakiwa kuwanao watz wote,maana wengine tuna hali ngumu pia lkn eti tunaitetea serikali haina pesa!Nani kasema?wanazila wachache tu!
Serikali inawang'ang'ania waziri na naibu wake as if ni wao pekee ndo wanaweza kuongoza wizara.
This is so touching @Shansila, hata hivyo natamani watz wangekuwa proactive kidogo !!!
hata kujaribu kuja kudadisi nini kinaendelea katika mahospitali yetu haya
Ieleweke kuwa wagonjwa watakufa zaidi kwa sabb ya mgomo wala si uongo lakini
madaktari pia huwa tunashuhudia wagonjwa wengi sana wakifa hospitalini kwa ukosefu wa vitu vidogo vidogo sana, hivi unafikiri huwa tunajisikiaje? Tunafurahia sio????
Kwa mfano sasa hivi ninavyotype hapa MOI hakuna POP can u blv this hospitali ya MIFUPA ATI? Vipi Namtumbo huko?
MOI x-ray hazifanyi kazi sasa sisi madr tuna tofauti gani na waganga wa kienyeji???tuunge mifupa na ndumba basi
Muhimbili hakuna oxygen watu wanakufa tunawaona na hatuna la kufanya watu ambao tungeweza kuwaokoa!!! LAKINI SERIKALI INAPIGA TU POROJO ILI KUWAHADAA WANANCHI ETI MGOGORO UNASHUGHULIKIWA TUPO KWENYE MCHAKATO MAANA YAKE VIFO VYA WANANCHI KWAO SIO DHARURA HATA KIDOGO.
Muhimbili kwa ujumla vifaa tiba na madawa muhimu ya dharura na ya bei poa hakuna nenda pale kaulize upewe tathmini
na wala si vya bei kubwa! Kweli wewe mwananchi serikali yako inakupenda?
Serikali imebembelezwa na madr kuwa wajadiliane kuanzia tarehe 9 feb wanakuja kukubali tarehe 29 feb 2012 kwa kuwa wanajua madr watakutana tarehe 3 machi 2012......wana nia ya dhati ya kutatua matatizo hawa???
Walipokutana na madr wakafikiri wakitaja vijipesa bila ya kuongelea masuala ya msingi mahospitaini kwetu basi madr watasuuzika roho na kusahau madhira wanayokumbana nayo kila siku mawodini hapo ndio walipokosea na wakakosa hoja kabisa ....sasa wameanza tena propaganda ili kuwafanya madr waonekane kama vile wahuni hivi???
MFANO RAHISI
Katika vyanzo vikuu vya vifo vya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji muhimbili SEPSIS inashika namba tatu
"Sepsis" hutokana na uambukizo wa bacteria kwenda kwenye sehemu ya kidonda cha operesheni na kusababisha uambukizo, sababu yake kubwa ni uchafu mahospitalini kwetu...mara nyingine hupelekea mtu kupata uambukizo mkali ambao unaweza kwenda hadi kwenye mfumo wa damu na kusababisha "SEPTICAEMIA" na mara nyingi ikifikia huku nafasi ya kumuokoa mgonjwa inakuwa finyu zaidi....
Wananchi tuamke ......