Waziri Mkuu Mwigulu, malalamiko ya Wananchi kuhusu ukosefu wa Dawa na Takwimu zisizo na ukweli yasipuuzwe

Waziri Mkuu Mwigulu, malalamiko ya Wananchi kuhusu ukosefu wa Dawa na Takwimu zisizo na ukweli yasipuuzwe

Megalodon

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
4,931
Reaction score
11,200
Katika Mkutano wako uliwahi kuhoji kwanini takwimu zinasema utoshelevu wa dawa ni 95% kwenye vituo huku asilimia 90 ya wananchi wanalalamika hakuna dawa.

Mkutano aliofanya Mchengerwa ulikuwa ni mkutano wa kujisafisha na yeye ndio waziri mwenye dhamana, as we speak, hapaswi kuendelea kuwa kwenye hiyo nafasi.

Hoja alizotoa kwenye mkutano wake ni kuwa madaktari wanaandika majina ya biashara , pia ameweka hoja wagonjwa wanataka kutibiwa hospital ambazo sio ngazi yao hivyo husababisha dawa kukosekana

Nadhani sasa Mwigulu unahitaji technical timu kwenye kundi lako vinginevyo unadanganywa.

Ishu ya madaktari kuandika majina ya biashara ni jambo la aibu hata kulitamka kwa sababu kwenye kila hospitali kuna hawa wanaitwa wafamasia kazi yao kubwa ni kutoa muongozo ya dawa , kama hii ni hoja basi tunapoteza hela kusomesha na kuajiri wafamasia. Pia suala la kuhakikisha madaktari hawaandiki majina hayo ni suala lipo chini ya Mchengerwa, inamaana ameshindwa kusimamia hilo eneo na watu wake wa chini. Mbona kwenye private hospitals hatusikii hayo malalamiko. Pia prescription zote mwisho wa siku zinaenda kwa mfamasia ambae yey ndio specialist wa kila kinachoitwa dawa , inamaana Daktari tujue jina la biashara mfamsia asijue? Unalishwa matango pori na mkaza mwana.

Nimefanya kazi Kagera hospital as fresh MD kabla sijaenda Ocean Road na kuhamia Canada. Ni ujinga mkubwa kusema utoshelevu ni asilimia 90 : Kama ingekuwa ni hivo basi hata famasi nje ya Hosp mnazopigia kelele zingekufa automatically.

Hata Canada nchi inayofanya production haina 75% ya utoshelevu wa dawa , nyie ambao mpo kwenye 90 % import depence muwe na 95% utoshelevu….. Hivi nyie ni wehu au ?

Endelea kuhoji Kwanini takwimu zinasema utoshelevu ni asilimia 90 huku wananchi wanapingana na hizo takwimu; wasikilize wananchi zaidi na Sio Mchengerwa na majambazi wa wizarani;

Ushauri . Unda kundi la watu ambao wataenda kujifanya wagonjwa kwenye kila kituo na Hospitali kulingana na ngazi ya ugonjwa.

Simulated patient A atoe dalili za ugonjwa ambao utamfanya atibiwe kwenye hiyo hospital , simulated patient B aende hosp za level ya juu atoe dalili za ugonjwa unaopaswa kutibiwa level hiyo , kusanya hizo prescription na dawa watakazopewa dhidi ya dawa walizokosa , asilimia ngapi ya simulated patient wamekosa dawa kwenye level za hospital zinazotibu ugonjwa husika - majibu utakayopata kwa asilimia 99 yataakisi malalamiko ya wananchi unayoyasikia.

Hakuna dawa kwenye hizo Hiospital amini wananchi na hizo takwmu zao ni kwa ajili yenu nyie watawala mpate kufurahi
Takwimu za mkaza mwana ni fake

Mwigulu fanya special audit kwenye takwimu anazokupa mchengerwa zote ni fake . Unda timu yako ya wataalam , mkaza mwana anakulisha matango pori.
Hospital hazina dawa , wananchi wanaangamia na out of pocket cost
Wananchi ndio wakusikiliza ….. utoshelevu wa 90% ni scam ….. hauna utofauti na ushindi wa Samia wa 98% while the country is bleeding and totally damaged —— ni scam

Dr Megalodon Mushi, MD, ( PhD)
Canada
Rue 52
 
Viongozi wote wa ccm waigizaji tu, wakiona tatizo watasema litatuliwe wakati wao ndio walio lisababisha.
 
Back
Top Bottom