Mgomo wa madaktari - Updates

Mgomo wa madaktari - Updates

nipo pamoja na madaktari 100%. Kwanini keki ya taifa letu wanufaike watu wachache?
 
Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa, mgomo huu ni wa kisiasa zaidi kuliko masilahi. Madaktari hawana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri, kazi yao ni kutibu. Inanisikitisha sana kuona madaktari wetu wanafanya upuuzi kama huu.
hivi madaktari huwa nao wanapiga kura!?

Kama ni ndio basi lazima wajue jema na baya. Ila ninachokukumbusha mkuu Kidatu ni kuwa kazi nyingi (kama si zote) sasa hivi hapa TZ zimeingiliwa na wababaishaji na sasa wanataka kujipenyeza kwenye hii fani ngumu, hivyo kufuatana na ubabaishaji kutowezekana kwenye udaktari ndio maana unaona haya yanayoendelea!

Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa, mgomo huu ni wa kisiasa zaidi kuliko masilahi. Madaktari hawana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri, kazi yao ni kutibu. Inanisikitisha sana kuona madaktari wetu wanafanya upuuzi kama huu.

vyama siasa ni vibaya,vimeiba gloves,asprin,mitungi ya oxgen. Vyama vya siasa ni wachonganishi,wameondoa umoja wa kitaifa.....Kipindi hiki cha Wosia wa Baba kimeletwa kwenu na sabuni ya Rumi! Teh teeeeeh...
 
vyanzo vya kuaminika yoyote anaweza kuandika hata mimi. Hicho sio chanzo makini.
 
Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa, mgomo huu ni wa kisiasa zaidi kuliko masilahi. Madaktari hawana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri, kazi yao ni kutibu. Inanisikitisha sana kuona madaktari wetu wanafanya upuuzi kama huu.

Ndio walewale, Sababu za serikali mbovumbovu.
Najua upo kazini.
 
Bila kujali maslahi ya upande wowote katika mgogoro huu, naomba mtu anaeunga mkono mgomo huu anijibu swali hili;- wagonjwa, ambao ni haki yao kupata matibabu, na ambao pia sio chanzo cha mgogoro, wana maslahi gani katika mambo yanayoendelea sasa hivi? Istoshe, katika kugoma kwao, ni makosa kusema madaktari wanawakomoa wagonjwa?
 
Wanatupa neti zenye matundu ambayo hata nzi anapita,alafu sisi tunawapa madini!bora hata wale waliochukua hizo neti na kufanyia uvuvi na ufugaji,maana angalau wanajiongezea kipato hata kama ni kidogo!
Kweli mkuu, na bado zinasumu inayoua taratibu..
 
Vp umewahi pata hati punguzo arif?
Sijawahi pata swahiba, naziogopa zile net kama ukoma!

Walipita mabalozi kugaia watu kwa nguvu, mamangu akachukua kama nne hivi, walivyompa mgongo tu akazitia kiberiti zote!
 
TANESCO nao wakituhujumu kwenye umme eti tu kudai haki zao...giza nene

TRA wagome kukusanya kodi eti wanadai haki zao.

TBS wagome kuthibitisha ubora wa vyakula eti wanadai haki zao.
 
Napata shida sana kuamini habari za mgomo wa madaktari.

I really dont understand the motive of being a politician...they fail to resolve petty issues and want to continue using public funds being in the office. Hawa wasaidizi wa Rais wanamuangusha sana...wameamua kutotaka kuona hili tatizo linafikia mwisho wake bila ya mgomo kuendelea.
 
Asante kwa kutuweka sawa. Lakini je kama Serikali ikikubali kuwatosa wapendwa wao Mponda na Nkya mamabo yataishia hapo? hakutakuja jipya? Hilo ndilo linalowafanya wakubwa hao wawe radhi kutoa kafara kubwa ya roho zetu sisi wagaagaa! Madakitari wakishinda Sirikali inajua pia kuwa walimu nao wanapasha! Wakulima wa korosho Mtwara na Lindi, wakulima wa mahindi yanayokosa soko la uhakika nao wanapasha! Watumiaji wa nishati ya umeme walikwisha pasha kitambo joto liko 100 degrees Celsius!
 
Nipo muhimbili,mama mkwe wangu amefariki,aliwekewa mashine ya oxgen usiku baada ya hapo dr hakuja tena,na mama ndo ametutangulia.migomo ina madhara,amefarik saa sita na nusu mchana huu.
 
Sijawahi pata swahiba, naziogopa zile net kama ukoma!

Walipita mabalozi kugaia watu kwa nguvu, mamangu akachukua kama nne hivi, walivyompa mgongo tu akazitia kiberiti zote!

Si angewaambia kwamba hataki hizo net ili wapewe watu wengine...
 
TANESCO nao wakituhujumu kwenye umme eti tu kudai haki zao...giza nene

TRA wagome kukusanya kodi eti wanadai haki zao.

TBS wagome kuthibitisha ubora wa vyakula eti wanadai haki zao.
Kama wana sababu ya kweli ya kuwafanya wagome, tutawaunga mkono kama tunavyowaunga madaktari.
 
Nimepata taarifa toka kwa ndugu yangu anayefanya kazi pale kama doctor kuwa mgomo umeeanza rasmi na hali si njema,kumbuka ile ni hospital kubwa inayohudumia wilaya nzima ya kilombero na sehemu za jirani.
 
Nipo muhimbili,mama mkwe wangu amefariki,aliwekewa mashine ya oxgen usiku baada ya hapo dr hakuja tena,na mama ndo ametutangulia.migomo ina madhara,amefarik saa sita na nusu mchana huu.

pole kwa kufiwa na mama mkwe..pumzika mama mkwe wangu....JK anaona sasa!!! kiburi hicho alikuwa nacho hata gadhafi lakini mwisho wake walimuingiza niiiiii kwenye nanihiiii.....
 
Back
Top Bottom