Mgomo wa madaktari: Huu ni ugaidi

Nadhani Gaidi ni yule anayetutoza kodi ili awatimizia mahitaji yao madr waweze kufanyakazi kwa ukamilifu. Pili ahadi ni DENI hebu soma hii ili upunguze kulalama bila sababu za msingi

MSIMAMO JUU YA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI

KAMA TULIVYOTOA TAARIFA KWENYE KIKAO CHA MADAKTARI CHA MARCH
3, NI KWAMBA

MAKUBALIANO YALIYOFIKIWA NA HATIMAYE KUTIWA SAINI KATI YA
SERIKALI NA
MADAKTARI TAREHE 2/3/2012 NI KUWA, ILI MEZA YA MAZUNGUMZO YA KUJADILI
MADAI
YA MADAKTARI IWEZE KUENDELEA NA HATUA YA PILI NI LAZIMA WAZIRI WA AFYA
(DR MPONDA) NA NAIBU WAKE (DR LUCY NKYA) AMA WAJIUZULU AU WAWAJIBISHWE
KAMA

ILIVYOKUWA IMEAHIDIWA NA MH. WAZIRI MKUU FEBRUARY 9 ALIPOFANYA KIKAO
NA WATUMISHI WA AFYA PALE HOSPITALI YA MUHIMBILI.

AIDHA, KULINGANA NA MAKUBALIANO HAYA KIKWAZO KIKUBWA CHA
KUTOKUENDELEA KWA MAJADILIANO YA MADAI YA MADAKTARI (UBORESHAJI
WA HUDUMA WAPATAZO WAGONJWA,

MAZINGIRA MAZURI YA KUFANYIA KAZI NA MASLAHI KWA UJUMLA WAKE) NI
KUENDELEA KUWEPO KWA DR MPONDA NA DR LUCY NKYA KWENYE NAFASI ZAO ZA
KIUONGOZI.

HIVYO BASI, KWENYE HUO MKUTANO WA MARCH 3, BAADA YA MAJADILIANO NA
TAFAKARI ZA KINA, ILIKUBALIWA KWA PAMOJA KUWA WATU HAWA WAWILI
WANATAKIWA KUACHIA NGAZI MARA MOJA ILI HAKI ZA WAGONJWA
NA MADAI YA MADAKTARI YAWEZE KUJADILIWA NA KUTEKELEZWA.

HIVYO BASI, ILIAMULIWA KUWA KAMA MPAKA SIKU YA JUMATANO
(MARCH 7) BADO AKINA DR MPONDA NA DR LUCY NKYA WATAKUWA BADO WAPO
MADARAKANI WATAANZA MGOMO RASMI KUSHINIKIZA AMA WAJIUZULU AU
WAWAJIBISHWE ILI TARATIBU ZINGINE ZIWEZE KUANZA.

KAMA ILIVYO TARATIBU YA CHAMA KUTOA TAARIFA KWA WANACHAMA KOTE NCHINI,
IFAHAMIKE KWAMBA MKUTANO ULIAMUA KUWA MADAKTARI WOTE KUWA KUANZIA
JUMATANO (MARCH 7) WATASITISHA KUTOA HUDUMA ZOTE ZA AFYA KATIKA
HOSPITALI ZOTE NCHINI MPAKA HAPO SERIKALI ITAKAPOONESHA UTAYARI KWA
KUTIMIZA AHADI YAKE YA KUWAWAJIBISHA WATAJWA HAPO JUU ILI HATUA
ZINGINE ZA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI KWA MANUFAA YA TAIFA
YAWEZE KUANZA KUSHUGHULIKIWA.

IFAHAMIKE KWAMBA CHAMA KINASIKITISHWA SANA NA KITENDO
CHA VIONGOZI WAANDAMIZI WA WIZARA YA AFYA AMBAO WANAJUA
UMUHIMU WA KUWAJIBIKA. KWA MARA NYINGINE TENA WANAWAFANYA
MADAKTARI WAENDELEE KUTETEA HAKI ZA WATANZANIA

KATIKA NJIA NGUMU NA KWA NIA YA KUFANIKISHA MALENGO HAYA KWA FAIDA YA
WATANZANIA WOTE.

IMETOLEWA NA OFISI YA MAT MAKAO MAKUU.

DR. NAMALA MKOPI RAIS WA MAT

Mtalii yuko mlimani anakwea na kula bata Bata tu!!!!!!!!! Kama alidhani siku 30 ni mwaka basi wamechimba chini kwani Madr wako kikazi zaidi, in short they are truly and really walking their Talks!!!!!!!!!​
 
Inawezekana upo sahihi, ila ni vema sa utuambie kama madaktari ni magaidi, Je Serikali? Je waziri wa Afya? Na wewe je?
 
Sifa moja ya magaidi ni kutishia na ikiwezekana kutoa roho za binadamu wasio na hatia ili kutimiziwa malengo yao. Madaktari kuamua kugoma na roho za watu zipotee ili matakwa yao yatimizwe ni ugaidi. Kwa mfano, Magaidi wanaua mamia ya watu ili mwenzao mmoja atolewe gerezani na madaktari wetu wanataka kufanya hivyo hivyo kupoteza mamia ya maisha ya wagonjwa eti watu wawili tu waondolewe madarakani, hii inaingia akilini kweli? Hao watu wataendelea kuwepo hapo wizarani milele? Kwani wameona hakuna njia nyingine zaidi ya mgomo? Haki inaweza kupiganiwa kwa muda mrefu sio lazima anufaike yule anayedai na kutaka mabadiliko ya papo kwa hapo.
Sasa hivi napata picha kila nikimuona daktari namuona kama gaidi, watadharauliwa na jamii kwani ni wananchi wachache sana ambao hawataathirika kama mgomo kama ukitokea.

Nawasilisha.

Hao Mawaziri kama wao si magaidi kwa nini wasiondoke madarakani kunusuru roho za watu?
 
Madokta gomeni... Hoja yenu kuhusu mtatibu vipi wakati dawa hakuna ina mashiko.. afu kuhusu kuwatosa hao mawaziri wenyeji wa morogoro ninaunga mkono hoja. Kazeni mpaka JK akubali mziki. Taaluma yenu kiboko, hakuna kilaza hapo kama political science
 
Mwanangu lazima awe GAIDI hapa Tanzania ................. ahhhh Daktari.
 
Kama madaktari ni magaidi, Kikwete anafanya nini Kilimanjaro? Hebu fikiria kama siku Nduli Idi Amin alipoivamia ardhi yetu, Mwalimu Nyerere angeamua kupumzika kwa kutembelea Olduvai Gorge! Mlima Kilimanjaro upo Tanzania, Kikwete alizaliwa akaukuta na atakufa na kuuacha.
 
Tuanzie mbali kidogo kuhusu historia ya migomo nchini;
Wanafunzi wa vyuo vikuu waligoma wakapigwa, wakatishiwa wakafukuzwa vyuo wananchi wakaambiwa watoto wao hawana nidhamu, wakaamini wakaungana na serikali...wakubwa wakachukua chao mapema mgomo ukaisha....madai yao: posho za kujikimu kimaisha...mikopo ya elimu, nk... Matokeo yake serikali ikaonekana ina haki, wanafunzi wakaendelea kunyanyaswa wakubwa wakatumia vibaya fedha za mikopo ya wanafunzi...leo anayepewa mkopo si anayestahili...watoto wa maskini hawana haki na kodi za baba zao tena...ungepata nafasi kidogo ya kuwa maeneo waliyopo hawa watoto ungelia machozi! Wale wa kike wameopt umalaya na kuombaomba hawawezi tena kusoma, kiwango cha elimu kimeporomoka, ushahidi ni madhara tunayoona maofisini mwetu kwa graduates waliotoka vyuo vikuu, matokeo ya mitihani ya darasa la saba na sekondari kuporomoka...wananchi waliosapoti serikali wanamuona Ndalichako...Mwanaasha kapata nini?
Waalimu wakagoma kwa madai hayohayo...wakagawanywa na strategists kuwa waunde kamati, wakatishiwatishiwa na kikamati chao, wakanywea, wakubwa wanapeta wanafanya watakavyo na fedha zetu na maisha ya walimu yanazidi kuwa duni...wananchi wamedanganywa tena kuwa walimu wanadai kisichowezekana, wakaamini hizo propaganda wakaacha kuunga mkono walimu, madhara yake ni migomo baridi ya walimu na kufeli watoto. Walimu kwakuwa nao ni binadamu, wameopt viosk vyao viitwavyo tuition...darasani hawafundishi ili watoto waje tuition...mfumo wa elimu umeporomoka, wananchi wameacha kuilaani serikali, wanawalaani walimu kwa msaada wa serikali
Sasa madaktari. Wao wamejipanga. Serikali inaogopa kutumia nguvu kuwalazimisha warudi kazini kwa kuwa wanajua hawa jamaa wameshikamana na hawataki kamati inayoweza kununuliwa na mafisadi. Wanasimama kwa umoja wao dhidi ya dhuluma za serikali yao. Pinda katupiwa mzigo peke yake na mtalii anapiga propaganda akijua hawezi kushinda. Anajaribu kutafuta huruma za wananchi kupitia press. Tunawapata wananchi wachache wasioamini juu ya mabadiliko wanaona tu vifo iwapo madaktari watagoma na kuwatupia madaktari lawama. Hawaoni madhara ya mgomo huu kwa mbali...wanaishia kutetea serikali legelege.
Wasijue kuwa serikali hii ni kama punda asiyekwenda pasipo mjeledi...madaktari wasipoyumba, wagonjwa kweli watapata shida na wengine kupoteza maisha, lakini hatimaye serikali haiwezi kuwafukuza kwani haina mahali penginepa kupata madaktari na gharama yake serikali yetu haitaiweza. Kwa hiyo serikali itatekeleza tu matakwa ya madaktari...wakimaliza wao, wale watu wetu waoga -walimu, nao watadai, watapewa, askari wetu nao pamoja na kukubali kutumiwa vibaya, nao watadai, watapewa, na wengine. Hiyo ndiyo hofu kubwa ya mtalii.

Conclusion: pasipo mjeledi, punda huyu aitwaye serikali hatokwenda! Madokta wetu aluta continua, mapambano yaendelee, tuko nyuma yenu mpaka serikali hii dhalimu ianze kujirekebisha kwa kuweka vipaumbele vyake sawa na kuzuia matumizi mabaya ya fedha za umma ili wazielekeze kwenye mambo nyeti
 
You are absolutely right, there must be a hidden agenda. Sooner or later the truth will get necked.
 
Wala si madaktari wote wanaohusika na ushuzi huu unaoitwa mgomo. Ni kikundi kidogo cha cockups ndiyo kinaendesha ubazazi huu. Mikoani wagonjwa wanapata huduma kama kawa
 
Madaktari kuweni na huruma kwani wanaoumia nisisi wa hali ya chini na sio hao viongoz kwan wao wakiumwa kdogo wanaenda nje ndo maana hata awajali lakini ingekuwa pia na wao wanaenda hospital zetu hizi wangetekeleza waliyoyasema jamani wananchi tunalia kwa ajil ya hili tunapoteza maelfu ya ndugu zetu walioko hospital. Rais jakaya kikwete angalia ili kwani machozi ya watanzani yatakurudia.
 
Mkuu uko sahihi ila Gaidi namba moja ni HELLEN KIJO BISIMBA bila kumsahau NAMALA. Ni wauaji wa kweli hawa na ndiyo maana nimeanua kutumia maandishi mekundu.
Is BISIMBA married? sidhani kama ana mtoto.




Hao uliowataja si Magaidi bali wale wa upande mwingine!
kwanini kwenye list usimweke JK, PINDA, NKYA na MPONDA?
 
Mkuu uko sahihi ila Gaidi namba moja ni HELLEN KIJO BISIMBA bila kumsahau NAMALA. Ni wauaji wa kweli hawa na ndiyo maana nimeanua kutumia maandishi mekundu.
Is BISIMBA married? sidhani kama ana mtoto.



Mbona JK ana watoto kama Riz 1, na Mwanaasha? mbona naye kwenye mgomo anaikimbia nchi?
YOU SHOULD BE BALANCED!!!


Hao uliowataja si Magaidi bali wale wa upande mwingine!
kwanini kwenye list usimweke JK, PINDA, NKYA na MPONDA?
 
jina lako ni lakizee,mawazo yako ni yakizee kama ya ****** pale magogoni afu unavaa malapa kwenye mvua what do u expect?ungekua na mzazi dr usingethubutu kusema hayo hivi anayeshughilikia afya yako anadharaulika na hapati stakihiki yake asubuhi anaamka akiwa na mawazo afu unategemea amfanyia mtu operation akiwa na mawazo ya maslahi?fikiria kwa kutumia kichwa na siyo masaburi yako unayakalia na kusugua viti
 
Mkuu unaishi Dunia gani wewe? Umeulizwa swali tena kwa tafsiri yako hiyohiyo, nani ni Gaidi, Madaktari au Serikali?

MADAKTARI rpt MADAKTARI (infact sio wote ila wenye nia ya dhati kugoma). Kwa kuongezea hawa hawana huruma, wauwaji, wadhaifu kiimani (ya dini zao). Inaelekea hawana wito au wameingia kwenye fani hii kwa makosa hata kama wanaweza kufanya kazi zao.
Kuna dalili za wazi kwamba zoezi hili litakuwa la mara kwa mara hata kama mawaziri husika watajiuzulu. Kesho watasema Rais ajiuzulu (sio lazima awe JK) wasikilizwe kwa vile wagonjwa watakufa, kisa wameshika mpini. Nyie wana CDM mnaoshabikia,(kisa ni mawaziri wa Magamba), mfano mkiingia madarakani hawahawa watawageuka. My advice to the Gvt. NEVER GIVE UP TO TERRORISTS!!! Hata asiye na akili anajua kuwa wanatumiwa na watatumiwa na wanasiasa kwa njia hii.
 
mawazo ya mtu aliyeshiba kodi ya wananchi wa tanzania.
Unaogopa kuukabiri ukweli kiasi cha kuwabambika madaktari na sifa ya ughaidi?

Ghaidi ni mtu anaye tumia silaha za moto na mbiu za kijeshi ili kutimiza malengo yake ya kiuchumi na kisiasa.

Bunduki bado ziko mikononi mwa serikali na zinatumika kuua watu kia siku katika kona nyingi za nchi yetu.lakini kwa upeo wako wa unene wa hewa bado hujaiita serikali ya ccm ni ya maghaidi.
Bajeti ya wizara ya afya inatumiwa kama fedha ya kukidhi mahitaji binafsi ya watendaji wa wizara na kusababisha wagonjwa kufa mikoni mwa madaktari lakini bado serikali ya ccm huioni ni serikali ya kighaidi.

Serikali ya ccm imekosa umoja na uwiano miongoni mwa nguzo zake kuu na kwa ukosefu huo imekufa kiutendaji, iko ndani ya jeneza inasubiri kuzikwa tu.

polisi wanafanya kile kilicho ndani ya utashi na mapenzi. Wanapiga na kuua watu, wanadhurumu mali, wabambika kesi za uongo zaidi wanatisha usalama wa raia wa tanzania

mahakimu na majaji wanatumia sheria kama combine harvester na kujiwekea gharani chochote kile wakipatacho.

Bunge ni la wapiga usingizi,wazomeaji na wangojea posho tu. Wabunge wanawajibika kwa mafisadi na waume na wake zao tu.

Baraza la mawaziri na rais ni rubber stamp kuu kuu, walio wengi ni mawakala wa majasusi wanaomiriki makampuni ya kigeni nchini tanzania. Makampuni abayo ni mali ya vilembwe wa karl peters. Rais na mwaziri wake wanajipendeza kwa maghaibu hawa kwa ujira ulio na thamani ya shanga za kiunoni.

Ikulu imegeuzwa uchochoro wa kufanyia misheni za uovu na dangulo la kufanyiza na kufanyizwa.



ughaidi halisi nchini tanzania unafanywa na viongozi wa serikai ya ccm kwa kuhakikisha kwamba huduma za jamii zinazoroteshwa kadri inavyowezekana ili kuwafanya watanzania walio wengi kuiingia katika utumwa mpya na kuwa wageni ndani ya nchi yao na katika makazi yao ya asili.

Serikali ya ccm ndiye gaidi mkuu.

Huwezi kufanya ughaidi bila kuwa na bunduki.

tuna sisitiza kuwa hoja ya madaktari kutaka mawaziri wajiuzulu huku wananchi wasio na hatia wakifariki dunia.....madaktari hawa ni magaidi sana...hili halikubaliki!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom