Mgomo wa madaktari: Huu ni ugaidi

Mgomo wa madaktari: Huu ni ugaidi

Madaktari tunawaunga mkono,gomeni wananchi tupo nyuma yenu dhidi ya hi serikali legelege ya CCM ambayo imejaa mafisadi pande zote,ukienda hospital hakuna vifaa vya kuwahudumia wananchi,kila kukicha viongozi wa serikali wanakwenda nchi za nje.
 
SIASA ni mchezo mchafu.....nimeamini.....!

Rais weu alisema, Uwaziri hauna chuo! endapo watu unaowaongoza hawakutaki kwa nini usijiuzulu? mimi sioni sababu ya watu kufa kwa ajili ya uwaziri! mbona watanzania ni wengi tu ambao mheshimiwa Rais anaweza kuwachagua kuwa mawaziri na tukaendelea bila shida. tusianze kuitana majina yasiyofaa kulinda watu wachache katika Taifa. kumbuka maneno huumba!
 
Daktari wale wana vifaa vyote vya operation ikiwemo mikasi na hizo ni miongoni mwa silaha za magaidi so wasipovitumia kuwaponya wagonjwa si utani ni magaidi hawa.
Ugaidi wa Serikali ni nini hapo sasa? Kutomuajibisha Waziri eti kwa sababu BISIMBA na NAMALA wanachuki binafdsi naye? haina maana yoyote.

Punguani
 
kwani Tanzania haina viogozi wanaoweza kuongoza wizara mbali ya hao wawili? Naamini wafanyakazi au watendaji wako wakikukata hutaweza kutimiza malengo ya wizara kwani hawatatimiza maigizo yako ipasavyo.Je utaendelea kufanya kazi na watu ambao hawakotayari kufanya kazi na wewe? Achilia mbali sababu zingine zilizopo kukataliwa tu inatosha ku-step down.
 
Daktari wale wana vifaa vyote vya operation ikiwemo mikasi na hizo ni miongoni mwa silaha za magaidi so wasipovitumia kuwaponya wagonjwa si utani ni magaidi hawa.
Ugaidi wa Serikali ni nini hapo sasa? Kutomuajibisha Waziri eti kwa sababu BISIMBA na NAMALA wanachuki binafdsi naye? haina maana yoyote.

Unasema hivyo kwa kuwa hauko idara ya afya na hujui changamoto wanazokutana nayo na chanzo chake nani. Kinachotakiwa serikali iwasikilize maana sina hakika kama kuna mwanasiasa anayeza kujua matatizo yatokanayo na mazingira yao kazi kwani hayupo kwenye mazingira hayo. Msiwalaumu wataalam wakati hamthamini mawazo yao ya kitaalam, mnathamini mawazo ya mbumbumbu wa taaluma husika.
 
Sifa moja ya magaidi ni kutishia na ikiwezekana kutoa roho za binadamu wasio na hatia ili kutimiziwa malengo yao. Madaktari kuamua kugoma na roho za watu zipotee ili matakwa yao yatimizwe ni ugaidi. Kwa mfano, Magaidi wanaua mamia ya watu ili mwenzao mmoja atolewe gerezani na madaktari wetu wanataka kufanya hivyo hivyo kupoteza mamia ya maisha ya wagonjwa eti watu wawili tu waondolewe madarakani, hii inaingia akilini kweli? Hao watu wataendelea kuwepo hapo wizarani milele? Kwani wameona hakuna njia nyingine zaidi ya mgomo? Haki inaweza kupiganiwa kwa muda mrefu sio lazima anufaike yule anayedai na kutaka mabadiliko ya papo kwa hapo.
Sasa hivi napata picha kila nikimuona daktari namuona kama gaidi, watadharauliwa na jamii kwani ni wananchi wachache sana ambao hawataathirika kama mgomo kama ukitokea.

Nawasilisha.

Mkuu unaishi Dunia gani wewe? Umeulizwa swali tena kwa tafsiri yako hiyohiyo, nani ni Gaidi, Madaktari au Serikali?
 
Propaganda za magamba
Magamba halisi hawakuumizwa na mgomo ule. Mwakyembe, Mwandosya wako Apollo. Chami, Werema, Kombani, Zitto,..., walikuwa India. Hivi tunavyobishana humu, Lowasa yuko Ujerumani. MaDaktari hawa na familia zao, marafiki zao, hawaumizwi na mgomo huu ambao sasa unachukua sura ya KISIASA zaidi.
 
Tatizo miluzi mingi humchanganya MBWA ndugu yangu unajua mpka sasa mimi sijui anayedai haki ni Daktari, BISIMBA ama ni nani? Serikali nayo itakuwa inajua kuwa inapambana na kundi zaidi ya moja so, uekelezaji lazima uende ngazi kwa ngazi. Kwani hawa LHRC wao wanaona mataktari wa Dar es salaam ndiyo wanaonewa? Mbona kule vijijini hapo? Sijawahi kusikia BISIMBA akiandamana kwa sababu eti ALBINO anauawa kikatili au yeye hana haki?. Tuache taratibu zifuatwe ili wagonjwa wetu wasiteseke tena kama ilivyokuwa awali kwa sababu ya external forces ambazo malengo yake ni ubinafsi na chuki binafsi.
mgogoro huu ni too high for your brain to analyse and understand utaishia kuchanganyikiwa tu.
 
Mimi nadhani kuwa serikali inajitahidi kuelewana na Madaktari na siyo jambo la busara kumlazimisha Rais kufanya kile wanachotaka wao. Kwa mfano akiteuliwa waziri mwingine ambao wao hawampendi , watagoma tena.
Serikali ingewaambia kuwa wale wasiyotaka kufanya kazi na Mponda na Nkya wana uhuru wa kuacha kazi na kwenda popote pale. Wasitumie Chama cha Madaktari kuleta vurugu hapa nchini.
Hata siku moja sijasikia Chama hicho kukemea utendaji mbovu wa madaktari. km operation ya kwicha badala ya mguu, mtoto kuparalyse,
 
Sifa moja ya magaidi ni kutishia na ikiwezekana kutoa roho za binadamu wasio na hatia ili kutimiziwa malengo yao. Madaktari kuamua kugoma na roho za watu zipotee ili matakwa yao yatimizwe ni ugaidi. Kwa mfano, Magaidi wanaua mamia ya watu ili mwenzao mmoja atolewe gerezani na madaktari wetu wanataka kufanya hivyo hivyo kupoteza mamia ya maisha ya wagonjwa eti watu wawili tu waondolewe madarakani, hii inaingia akilini kweli? Hao watu wataendelea kuwepo hapo wizarani milele? Kwani wameona hakuna njia nyingine zaidi ya mgomo? Haki inaweza kupiganiwa kwa muda mrefu sio lazima anufaike yule anayedai na kutaka mabadiliko ya papo kwa hapo.
Sasa hivi napata picha kila nikimuona daktari namuona kama gaidi, watadharauliwa na jamii kwani ni wananchi wachache sana ambao hawataathirika kama mgomo kama ukitokea.

Nawasilisha.

Mzeelapa tunashukuru kwa ujumbe wako ila utakuwa umetumwa na magaidi! haki yao ni ya msingi, makubaliano yaliofikiwa yafanyiwe kazi LA mgomo wao nami naunga mkono bila kujali athari. Viongozi/Serikali ndo magaidi-Wameua wangapi kupitia mikono ya polisi mbona hujawaita magaidi? kuwa macho na usipende kutumika na hawa majambazi wanaojinufaisha na raslimali za watanzania kuna siku yatawatokea puani! Watanzania hawatabaki kimya milele mkiendelea kuwadanganya na hotuba ya AMANI kila kukicha. WAPELEKEE UJUMBE KUWA WATANZANIA WATACHOKA KUSIKIA AMANI HUKU WAKIANGALIA RASLIMALI ZAO ZINAGAWIWA KWA WATAWALA WACHACHE NA MAJAMBAZI KWA MGONGO WA WAWEKEZAJI
 
kama CCM inajali watu basi ifanye hili imwachishe kazi WAZIRI NA NAIBU WAZIRI ili watu wapone.kwani kuna ugumu gani kwa mawaziri kuachishwa kazi ili kuokoa uhai wa watu?
 
Mandela alikuwa kwny list ya magaidi hadi 2008!
MaDaktari wetu watakuwa kwenye list hiyo milele kama watagoma tena kesho. Ziko namna nyingi na bora zaidi za kuhanikiza mabadiliko bila ya kuathiri mojakwamoja wasiokuwemo na wanyonge kabisa. Udaktari ni moja ya TAALUMA zinzolipa sana NCHI hii.
 
Sifa moja ya magaidi ni kutishia na ikiwezekana kutoa roho za binadamu wasio na hatia ili kutimiziwa malengo yao. Madaktari kuamua kugoma na roho za watu zipotee ili matakwa yao yatimizwe ni ugaidi. Kwa mfano, Magaidi wanaua mamia ya watu ili mwenzao mmoja atolewe gerezani na madaktari wetu wanataka kufanya hivyo hivyo kupoteza mamia ya maisha ya wagonjwa eti watu wawili tu waondolewe madarakani, hii inaingia akilini kweli? Hao watu wataendelea kuwepo hapo wizarani milele? Kwani wameona hakuna njia nyingine zaidi ya mgomo? Haki inaweza kupiganiwa kwa muda mrefu sio lazima anufaike yule anayedai na kutaka mabadiliko ya papo kwa hapo.
Sasa hivi napata picha kila nikimuona daktari namuona kama gaidi, watadharauliwa na jamii kwani ni wananchi wachache sana ambao hawataathirika kama mgomo kama ukitokea.

Nawasilisha.

How do we gauge "ugaidi" in our society? Je anayelipia Dowans wakati wagonjwa hawana dawa wala pa kulala naye sio gaidi? Anayetembea kila kona ya dunia hii kwa hela ya walipa kodi wakati walimu hawajalipwa naye yuko kwenye kundi gani? Nionavyo mimi, mgomo sio kitu kizuri. Ila society yetu leo hii haiko sawasawa. Imejaa unafiki na uongo. Hakuna kitu au system yoyote dunia hii inayosimama kwa misingi ya uongo. Migomo kama hii inaleta ishara tu kwamba we are about to collapse kama hatufanyi mabadiliko na kuwa wazalendo katika kila nyanja.
 
kama CCM inajali watu basi ifanye hili imwachishe kazi WAZIRI NA NAIBU WAZIRI ili watu wapone.kwani kuna ugumu gani kwa mawaziri kuachishwa kazi ili kuokoa uhai wa watu?
MaDaktari hawa KIUTENDAJI wanaripoti kwa waziri? Dai lao hili ni la KITAALUMA? Dai hili lina MASLAHI kwao na kwa TAIFA hili? WanaJeshi wa nchi hii hawakugoma wala kushinikiza waziri wa ulinzi ajiuzulu kwa mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto. Wanafunzi mashuleni wanakaa chini madarasani na baadhi ya madaktari hawa walisoma katika mazingira haya.
 
Sifa moja ya magaidi ni kutishia na ikiwezekana kutoa roho za binadamu wasio na hatia ili kutimiziwa malengo yao. Madaktari kuamua kugoma na roho za watu zipotee ili matakwa yao yatimizwe ni ugaidi. Kwa mfano, Magaidi wanaua mamia ya watu ili mwenzao mmoja atolewe gerezani na madaktari wetu wanataka kufanya hivyo hivyo kupoteza mamia ya maisha ya wagonjwa eti watu wawili tu waondolewe madarakani, hii inaingia akilini kweli? Hao watu wataendelea kuwepo hapo wizarani milele? Kwani wameona hakuna njia nyingine zaidi ya mgomo? Haki inaweza kupiganiwa kwa muda mrefu sio lazima anufaike yule anayedai na kutaka mabadiliko ya papo kwa hapo.
Sasa hivi napata picha kila nikimuona daktari namuona kama gaidi, watadharauliwa na jamii kwani ni wananchi wachache sana ambao hawataathirika kama mgomo kama ukitokea.

Nawasilisha.

Unaonekana kujiunga karibuni sana na JF bila shaka kwa kazi maalumu. Umetumwa na nani na unalipwa kiasi gani? Kawaambie waliokutuma, kwamba huu sio ugaidi lakini gaidi ni wewe uliyetumwa na wale waliokutuma.
 
Kungekuwa kuna madaktari wa maana watu wangeenda India?
 
Gaidi ni huyo anayeweka watu kwa uswahiba katika vitengo nyeti kama afya.. hivi mponda na nkya wamezaliwa na huo uwaziri? kama unakiri watu walikufa mgomo uliopita huoni kwamba walipaswa kuachia ngazi hata kabla ya shinikizo la madaktari?
 
Sifa moja ya magaidi ni kutishia na ikiwezekana kutoa roho za binadamu wasio na hatia ili kutimiziwa malengo yao. Madaktari kuamua kugoma na roho za watu zipotee ili matakwa yao yatimizwe ni ugaidi. Kwa mfano, Magaidi wanaua mamia ya watu ili mwenzao mmoja atolewe gerezani na madaktari wetu wanataka kufanya hivyo hivyo kupoteza mamia ya maisha ya wagonjwa eti watu wawili tu waondolewe madarakani, hii inaingia akilini kweli? Hao watu wataendelea kuwepo hapo wizarani milele? Kwani wameona hakuna njia nyingine zaidi ya mgomo? Haki inaweza kupiganiwa kwa muda mrefu sio lazima anufaike yule anayedai na kutaka mabadiliko ya papo kwa hapo.
Sasa hivi napata picha kila nikimuona daktari namuona kama gaidi, watadharauliwa na jamii kwani ni wananchi wachache sana ambao hawataathirika kama mgomo kama ukitokea.

Nawasilisha.

Inawezekana wewe na serikali yako ni magaidi no. 1 badala ya madaktari. Mimi nawaunga mkono kwa sababu wao wanachodai si kwa manufaa yao tu bali kwa serikali, wananchi na taifa zima kwa ujumla.

Pole sana kwa kuwa na "closed mind"
 
Back
Top Bottom