Mgomo wa madaktari: Huu ni ugaidi

Mgomo wa madaktari: Huu ni ugaidi

Wanachotaka kurudia kukifanya maDaktari wetu ni zaidi ya UGAIDI. Waliona madhara yaliwakumba akina nani wakati wa mgomo wao ule wa kwanza. Viongozi wakubwa serikalini hawakuumizwa na mgomo ule. Wao madaktari hawakuumizwa na mgomo ule. Wanataka kuurudia tena mgomo ule sio kwa sababu za KITAALUMA au KIMASLAHI kwao wala kwa TAIFA hili bali KISIASA kabisa! Wanatofauti gani na akina Osama waoelekeza mabomu kwa wasio na hatia tena kwa kutumia jina la Mungu?

Tumia kichwa kujibu swali kwenye 1 kwa mujiubu wa maelezo maelezo yako:
1. Kwa nini viongozi wa serikali hawakuumizwa na mgomo ule?
2. Hapo kwenye red naona umechanganyikiwa kama si tatizo la darasa. Ukipewa au kuahidiwa mshiko na wanaokutuma, usikurupuke hata kama kuna sharti la kutolipwa kwa sababu ya 'kuchelewa' kuingiza threads/coments zako, jipange angalau kiuongo uongo ili ionekane umefikiri kwa kutumia kichwa
.
3. Kama hautakubali kwamba mgomo wa madaktari una maslahi kwa taifa katika ulimwengu huu (Tanzania ya leo) basi utakubali katika ulimwengu ujao (Tanzania ya kesho). Mambo haya wamefunuliwa kuyajua wenye hekima tu.
 
Mkuu uko sahihi ila Gaidi namba moja ni HELLEN KIJO BISIMBA bila kumsahau NAMALA. Ni wauaji wa kweli hawa na ndiyo maana nimeanua kutumia maandishi mekundu.
Is BISIMBA married? sidhani kama ana mtoto.



Samahani naona unaanza kupotea mwelekeo. Jadili mada sio mtu. Yote uliyoyagusia ni mambo binafsi.
 
Madai yako yanaweza yakawa ni kweli lakini umetafsiri vibaya labda kwa kupenda au kwa uwezo mdogo wa akli yako...na hapa naona kwa asilimia 95 ni uwezo mdogo wa kufikiri...Kwani ni wapi madaktari wamesema kuwa wanataka watu wafe ili madai yao yatimizwe? Au ni wapi madaktari wameonyesha kufurahia kuangaika kwa watanzania kwasababu ya migomo yao inayosababishwa na serikali iliyochoka ya magamba? Unapaswa kutambua kuwa hawa madaktari wana wake/waume,watoto na watu wengi wanaowategemea..si busara serikali kuwakandamiza ati kwasababu wakigoma watu watakufa na wao wataonekana magaidi..huu ni mtazamo uharo kabisa...hivi mtoto wa dokta akishindwa kwenda shule kwasababu ya kukosa ada wewe utamsaidia,hivi madokta wanapokesha na wagonjwa usiku kucha wewe uwa unawasaidia? Tuache siasa kwenye mambo makini,huu uzi kwangu mimi nau-rate kama nyuzi uharo zilizowai kuletwa hapa JF.
 
Madaktari naona wameboreka na kazi yao wanataka kuingia kwenye

siasa kwa nguvu kama Kangwalangwala.

Sijui nchi inaenda wapi!!
ummejikojolea ndugu na hisi hata mdomo wako unatoa harufu kwa maneno uliyotoa.
 
Sifa moja ya magaidi ni kutishia na ikiwezekana kutoa roho za binadamu wasio na hatia ili kutimiziwa malengo yao. Madaktari kuamua kugoma na roho za watu zipotee ili matakwa yao yatimizwe ni ugaidi. Kwa mfano, Magaidi wanaua mamia ya watu ili mwenzao mmoja atolewe gerezani na madaktari wetu wanataka kufanya hivyo hivyo kupoteza mamia ya maisha ya wagonjwa eti watu wawili tu waondolewe madarakani, hii inaingia akilini kweli? Hao watu wataendelea kuwepo hapo wizarani milele? Kwani wameona hakuna njia nyingine zaidi ya mgomo? Haki inaweza kupiganiwa kwa muda mrefu sio lazima anufaike yule anayedai na kutaka mabadiliko ya papo kwa hapo.
Sasa hivi napata picha kila nikimuona daktari namuona kama gaidi, watadharauliwa na jamii kwani ni wananchi wachache sana ambao hawataathirika kama mgomo kama ukitokea.

Nawasilisha.

Haya ndo mlokuwa mnapanga na mama Nyoni pale hotelini ?
 
.......... kuwa wanapogoma wanaoathirika ni wananchi walalahoi wasio na mbele wala nyuma.......
.....wanatambua, hao unatuita walalahoi hatujatambua kuwa adui yetu sio madaktari bali ni serikali, mgomo ni njia mojawapo ya kuwafanya wamfahamu adui yao, ebo!!!!
 
Human progress is neither automatic nor inevitable.Every step toward the goal of justice requres sacrifice and suffering!
 
Hata Nyerere wakati anapigania UHURU wa Tangayika Wakoloni walimuita GAIDI.
Oops may be you were not born, lakini recently Nelson Mandela alipokuwa
anawapinga makaburu kuhusu ubaguzi wa rangi walimuita GAIDI na kumfunga ktk
kisiwa cha Robben.

Lakini uzuri wa Historia inatufundisha kwamba kwakuwa watu hao wote walikuwa
wanapigana VITA ya HAKI finally WALISHINDA.

Wewe kibaraka wa SERIKALI DHALIMU kuwaita Madaktari Magaidi huna tofauti na
MAKABURU wa S. Africa na WAKOLONI wa Kiingereza. Lakini kitu kimoja ni kwamba
madaktari katika vita hii watashinda kwasababu wanapigania upande wa HAKI.
 
ni kweli kabisa madaktari wakigoma tunaoumia ni sisi wananchi walalahoi lakini je sisi walalahoi tunadai na kutetea vipi haki zetu kwa serikali? Wananch tukiamka na kuacha kulalamika hovyo mambo yataenda sawa. NAWAUNGA MKONO MADOCTOR
 
haya ni maneno ya pinda Leo


Pinda amekamilisha mkutano na waandishi wa habari hivi punde na meseji ya kubwa kwa madaktari ni kuwaambia kuwa serikali haiwezekani kushinikizwa na madaktari na kuwafukuza mawaziri Mponda na Nkya. Hivyo, kama wanataka kugoma, wagome tu
 
Pinda amekamilisha mkutano na waandishi wa habari hivi punde na meseji ya kubwa kwa madaktari ni kuwaambia kuwa serikali haiwezekani kushinikizwa na madaktari na kuwafukuza mawaziri Mponda na Nkya. Hivyo, kama wanataka kugoma, wagome tu[/QUOTE]

Ilikuwaje akamsimamisha kazi Blandina?sio shinikizo?
Bado kitambo kidogo atabadili upepo huyu anayejiita mtoto wa mkulima!!!!!
 
Sifa moja ya magaidi ni kutishia na ikiwezekana kutoa roho za binadamu wasio na hatia ili kutimiziwa malengo yao. Madaktari kuamua kugoma na roho za watu zipotee ili matakwa yao yatimizwe ni ugaidi. Kwa mfano, Magaidi wanaua mamia ya watu ili mwenzao mmoja atolewe gerezani na madaktari wetu wanataka kufanya hivyo hivyo kupoteza mamia ya maisha ya wagonjwa eti watu wawili tu waondolewe madarakani, hii inaingia akilini kweli? Hao watu wataendelea kuwepo hapo wizarani milele? Kwani wameona hakuna njia nyingine zaidi ya mgomo? Haki inaweza kupiganiwa kwa muda mrefu sio lazima anufaike yule anayedai na kutaka mabadiliko ya papo kwa hapo.
Sasa hivi napata picha kila nikimuona daktari namuona kama gaidi, watadharauliwa na jamii kwani ni wananchi wachache sana ambao hawataathirika kama mgomo kama ukitokea.

Nawasilisha.
Mkuu, umejitahidi kujenga hoja yako.
Lakini tukigeukia upande wa pili je? Yaani hao wanaolalamikiwa wakiachia madaraka ili madaktari wasigome na rohao za watu wasio na hatia zisipotee, haiwezekani?
Kama inawezekana, ni nani gaidi kati ya pande hizo mbili? Madaktari au mawaziri?
 
Mkuu uko sahihi ila Gaidi namba moja ni HELLEN KIJO BISIMBA bila kumsahau NAMALA. Ni wauaji wa kweli hawa na ndiyo maana nimeanua kutumia maandishi mekundu.
Is BISIMBA married? sidhani kama ana mtoto.



what is wrong with mwanaharakati Bisimba mpigania haki za binadamu...!!
 
Gaidi ni serikali yetu isiyotaka kuwasikiliza na kuleta suluhisho. Shame on you hayajakufika kaka/dada yakikufika utajuta viongozi wa nchi yako kutowajibika. Hivi huyu waziri hawezi kuwa kama A.H.Mwinyi whyyyyyyyyy anataka kutuletea matatizo sisi wagonjwa watarajiwa. Viongozi wako hawataathiriwa maana wao checkup apollo.
 
Serikali legelege inashindwa kuwawajibisha viongozi pale wanapokosea matatizo yake ndo haya madaktari wao ndo wanajua kwa kiasi gani hao nkya na mponda wanakwamisha utendaji wao wa kazi, mm naona serikali ingewasikiliza na kujua ni kwa kiasi gani hao wakuu wanavyokwamisha kazi! kuwaita madr magaidi tunakosea serikali ya magamba ndo magaidi no moja tena ndo chanzo cha migogolo mingi kwa watumishi kwasababu ya kuchanganya siasi na hali halisi.
 
kati ya madaktari na serikali nani gaidi?
inategemea tafsiri unayopenda maana mpaka leo hatuna tafsiri moja ya ugaidi. Kama unalenga kujua nani muovu au mkosefu katika hili basi ni selikali inyofanya danadana katika swala nyeti la uhai wa wananchi. Katika hili inapoteza uhalali wa kuongoza taifa. Nba ninakuomba uache utani katika mambo ya msingi. Hii "suicide" imeanzia kwenye elimu sasa imehamia kwenye afya.
 
Tanzania haiwezi kusonga mbele kwa dharau na vitisho kama wanavyotaka kufanya hawa madaktari,serikali ya Tanzania ni tofauti sana na ile ya Somalia ambapo kila mtu awazalo ndilo anataka lifanyike.Pengine hili kundi linalowaunga mkono hawa madaktari itabidi lijilaumu kwa kutofanya uamuzi sahihi pale tuliposhindwa kushikilia msimamo wetu wa KUTOITAMBUA serikali iliyopo madarakani.
 
Back
Top Bottom