Mgomo wa madaktari: Huu ni ugaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari: Huu ni ugaidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzeelapa, Mar 6, 2012.

 1. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Sifa moja ya magaidi ni kutishia na ikiwezekana kutoa roho za binadamu wasio na hatia ili kutimiziwa malengo yao. Madaktari kuamua kugoma na roho za watu zipotee ili matakwa yao yatimizwe ni ugaidi. Kwa mfano, Magaidi wanaua mamia ya watu ili mwenzao mmoja atolewe gerezani na madaktari wetu wanataka kufanya hivyo hivyo kupoteza mamia ya maisha ya wagonjwa eti watu wawili tu waondolewe madarakani, hii inaingia akilini kweli?

  Hao watu wataendelea kuwepo hapo wizarani milele? Kwani wameona hakuna njia nyingine zaidi ya mgomo? Haki inaweza kupiganiwa kwa muda mrefu sio lazima anufaike yule anayedai na kutaka mabadiliko ya papo kwa hapo.

  Sasa hivi napata picha kila nikimuona daktari namuona kama gaidi, watadharauliwa na jamii kwani ni wananchi wachache sana ambao hawataathirika kama mgomo kama ukitokea.

  Nawasilisha.
   
 2. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Kati ya madaktari na Serikali nani GAIDI?
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Sikulaumu sana kwa mawazo yako ila napenda uelewe tu kuwa hakuna maendeleo bila mapambano tena si ya vitabuni bali ni yenye kutoa jasho na mpaka damu kwa maana ya vifo.
  Unadhani haki inatafutwa kwa njia ya amani?Niambie ni wapi ambapo uliona kuna haki na watu hawakufa wakati wa kuipigania?
  Kma ni ugaidi basi nadhani tunaanza kuupotosha na kupoteza maana halisi ya neno lenyewe.
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja ya mzeelapa 100 kwa 100.
   
 5. Junior. Cux

  Junior. Cux JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 5,305
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  inaonekana mmetumwa wengi humu ndani lakini kesho ndo mtajua yote..
   
 6. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hatushangai kwa watu kama wewe kuunga mkono maana hata katiba mpya mliunga mkono hata mambo ambayo hayakuwa ya maana
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Madaktari naona wameboreka na kazi yao wanataka kuingia kwenye siasa kwa nguvu kama Kangwalangwala.

  Sijui nchi inaenda wapi!!
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu uko sahihi ila Gaidi namba moja ni HELLEN KIJO BISIMBA bila kumsahau NAMALA. Ni wauaji wa kweli hawa na ndiyo maana nimeanua kutumia maandishi mekundu.
  Is BISIMBA married? sidhani kama ana mtoto.


   
 9. vimon

  vimon Senior Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Nawaunga mkono madaktari 200%,madaktari hawa hoja moja wanataka hao watu waondoke ili waweze kufanya mzungumzo na serikali juu ya mstakabali wa afya za watanzania,unafikiri wanapenda watu wfe mikono mwao ili waendelee kukosa raha wao wamechoka juona watu wakifa mbele yao kwa sababu ya kukosa vifaa.
  Wamechoka juona watu wakifa kwa sababu ya kukosa dawa
  Wamechoka kuona viongozi wakienda India huku wagonjwa wanalala chini
  Wamechoka kuona Dawa na Vifaa muhimu vikikosekana mahospitalini
  Madaktari poleni na Mungu awatie Nguvu. Solidarity forever
   
 10. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #10
  Mar 6, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  mmetumwa.
   
 11. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Unajua kweli maana ya Ugaidi?
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Daktari wale wana vifaa vyote vya operation ikiwemo mikasi na hizo ni miongoni mwa silaha za magaidi so wasipovitumia kuwaponya wagonjwa si utani ni magaidi hawa.
  Ugaidi wa Serikali ni nini hapo sasa? Kutomuajibisha Waziri eti kwa sababu BISIMBA na NAMALA wanachuki binafdsi naye? haina maana yoyote.
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mawazo ya mtu aliyeshiba kodi ya wananchi wa Tanzania hayo.

  Unaogopa kuukabiri ukweli kiasi cha kuwabambika madaktari na sifa ya ughaidi?

  Ghaidi ni mtu anaye tumia silaha za moto na mbiu za kijeshi ili kutimiza malengo yake ya kiuchumi na kisiasa.

  Bunduki bado ziko mikononi mwa serikali na zinatumika kuua watu kia siku katika kona nyingi za nchi yetu.Lakini kwa upeo wako wa unene wa hewa Bado hujaiita serikali ya CCM ni ya Maghaidi.
  Bajeti ya Wizara ya Afya inatumiwa kama fedha ya kukidhi mahitaji binafsi ya Watendaji wa wizara na kusababisha wagonjwa kufa mikoni mwa Madaktari lakini bado serikali ya CCM huioni ni serikali ya kighaidi.

  Serikali ya CCM imekosa umoja na uwiano miongoni mwa nguzo zake kuu na kwa ukosefu huo imekufa kiutendaji, iko ndani ya jeneza inasubiri kuzikwa tu.

  Polisi wanafanya kile kilicho ndani ya Utashi na Mapenzi. Wanapiga na kuua watu, wanadhurumu mali, wanabambika kesi za uongo, zaidi wanatishia usalama wa raia wa Tanzania

  Mahakimu na Majaji wanatumia sheria kama Combine Harvester na kujiwekea Gharani chochote kile wakipatacho.

  Bunge ni la Wapiga usingizi,wazomeaji na wangojea posho tu. Wabunge wanawajibika kwa Mafisadi na kwa Waume na wake zao tu.

  Baraza la Mawaziri na Rais ni Rubber Stamp kuu kuu, walio wengi ni mawakala wa majasusi wanaomiriki makampuni ya kigeni nchini Tanzania. Makampuni ambayo ni mali ya Vilembwe wa Karl Peters. Rais na Mwaziri wake wanajipendeza kwa maghaibu hawa kwa ujira ulio na thamani ya shanga za kiunoni.

  Ikulu imegeuzwa uchochoro wa kufanyia misheni za uovu na dangulo la kufanyiza na kufanyizwa.  Ughaidi Halisi nchini Tanzania unafanywa na viongozi wa serikai ya CCM kwa kuhakikisha kwamba huduma za jamii zinazoroteshwa kadri inavyowezekana ili kuwafanya Watanzania walio wengi kuiingia katika Utumwa mpya na kuwa wageni ndani ya nchi yao na katika makazi yao ya asili.

  Serikali ya CCM ndiye Gaidi mkuu.

  Huwezi kufanya ughaidi bila kuwa na bunduki.   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tatizo miluzi mingi humchanganya MBWA ndugu yangu unajua mpka sasa mimi sijui anayedai haki ni Daktari, BISIMBA ama ni nani? Serikali nayo itakuwa inajua kuwa inapambana na kundi zaidi ya moja so, uekelezaji lazima uende ngazi kwa ngazi. Kwani hawa LHRC wao wanaona mataktari wa Dar es salaam ndiyo wanaonewa? Mbona kule vijijini hapo? Sijawahi kusikia BISIMBA akiandamana kwa sababu eti ALBINO anauawa kikatili au yeye hana haki?. Tuache taratibu zifuatwe ili wagonjwa wetu wasiteseke tena kama ilivyokuwa awali kwa sababu ya external forces ambazo malengo yake ni ubinafsi na chuki binafsi.
   
 15. j

  jane_000 JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwanini mbona hakuna mandamano ?
   
 16. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  SIASA ni mchezo mchafu.....nimeamini.....!
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wanachotaka kurudia kukifanya maDaktari wetu ni zaidi ya UGAIDI. Waliona madhara yaliwakumba akina nani wakati wa mgomo wao ule wa kwanza. Viongozi wakubwa serikalini hawakuumizwa na mgomo ule. Wao madaktari hawakuumizwa na mgomo ule. Wanataka kuurudia tena mgomo ule sio kwa sababu za KITAALUMA au KIMASLAHI kwao wala kwa TAIFA hili bali KISIASA kabisa! Wanatofauti gani na akina Osama waoelekeza mabomu kwa wasio na hatia tena kwa kutumia jina la Mungu?
   
 18. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nchi ipo katika kupambana na njia zote kandamizi ambazo zimekuwa zikifanya na viongozi wetu,wote tunapambana bila kujali ni kutoka upande gani cha msingi malengo ambayo tunakusudia ya kupata maslahi kulingana na kazi ambazo kila mtu anafanya,kwa mfano chukulia u mwalimu ambaye umeajiliwa hivi karibuni na unaenda kuripoti katika kituo chako cha kazi ambako ni mbali na huna mwenyeji ambaye unaweza kumuomba msaada,kufika unaambiawa hakuna pesa,utapenda?Utakaa kimya?Mambo kama haya ndio yanayoleta misuguano katika nchi yetu ndugu.
   
 19. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Gaidi wa kwanza ni serikali ya baba mwanaasha inayoacha wagonjwa walale watatu watatu na kuambukizana. Wa pili ni wewe ambae umejilipua mwenyewe!
   
 20. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Propaganda za magamba
   
Loading...