Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 484
- 2,642
Wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa wilaya sita (6) za Mkoa wa Ruvuma. Wilaya ya Tunduru ina majimbo mawili Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini.
Jana tar 3 Oktoba 2022 Mkuu wa Wilaya @julius_mtatiro na OCD wa TUNDURU. Wamethibitisha rasmi ya kwamba Tunduru kuna UGAIDI kupitia Barua hii waliyoiandika kuzuia ziara ya katibu Mkuu wa @actwazalendo_official @adoshaibuado . Kwamba Magaidi watamdhuru .
Hii ina maana ya kwamba Mh.@julius_mtatiro na OCD wa TUNDURU wametoa tahadhari kwa watalii wanaotaka kwenda Mbuga ya Selou kutalii kwamba Sasa hivi hali sio shwari , naona kuna haja sasa mamlaka Police @polisi.tanzania @policetanzania , IGP na Mheshimiwa Rais @samia_suluhu_hassan kuona namna Sasa ya kutoa amri ya watu wa TUNDURU na Ruvuma kwa ujumla kutotoka nje (Curfew) ili wananchi wasihatarishe maisha yao kwa uwepo wa Magaidi.
Tunduru ina vivutio vingi sana kama mbuga ya wanyama selous, mapori ya akiba ya sasawala na muhuwesi, masalia ya majengo ya wapigania uhuru wa msumbiji kupitia chama cha Frelimo, makaburi ya viongozi wa kimila, Miti inayogeuka kuwa mawe, mapango ya ajabu na nyayo za wanyama katika mwamba vyote hivi ni sehemu ya utalii na vinapatikana katika wilaya ya Tunduru pekee. Ila kwa taarifa hii ya DC na OCD maana yake Watalii hawapaswi kwenda sio sehemu salama kwao tena
Tunduru huko Ruvuma kimkoa kuna vivutio vingine vingi pia kama mapori ya akiba ya Selous,Mwambesi,ziwa Nyasa lenye samaki wa mapambo,visiwa,fukwe za kuvutia na vuvutio vingine lukuki, mto Ruvuma wenye maporomoko ya Nakatuta,Tulila na Sunda.
Pia kuna utalii wa kiutamaduni kama majengo ya kihistoria yakiwemo makanisa makongwe ya Peramiho,Lituhi na Lundu, makumbusho ya vita ya Majimaji,historia ya machifu wa kiyao,wangoni na historia ya biashara ya utumwa.Jiwe la Mbuji,mapango ya wamatengo na pango la mlima Chandamali ambalo lilikuwa maficho ya Nduna Songea Mbano wakati wa Vita ya Majimaji.
Vyote hivi vimekuwa vivutio vya watalii wengi wa ndani na nje ya nchi. Kwa kauli hii ya Mkuu wa Wilaya @julius_mtatiro na OCD ni kwamba huko TUNDURU -Ruvuma hali sio shwari kuna UGAIDI ni tangazo na hali ya hatari kwa watalii kwamba hawapaswi kwenda huko.
Serikali ituambie UGAIDI huu huko TUNDURU hali ipoje, usalama wa watu upoje nini chanzo cha UGAIDI huu.
Abdul Nondo.