Tuanzie mbali kidogo kuhusu historia ya migomo nchini;
Wanafunzi wa vyuo vikuu waligoma wakapigwa, wakatishiwa wakafukuzwa vyuo wananchi wakaambiwa watoto wao hawana nidhamu, wakaamini wakaungana na serikali...wakubwa wakachukua chao mapema mgomo ukaisha....madai yao: posho za kujikimu kimaisha...mikopo ya elimu, nk... Matokeo yake serikali ikaonekana ina haki, wanafunzi wakaendelea kunyanyaswa wakubwa wakatumia vibaya fedha za mikopo ya wanafunzi...leo anayepewa mkopo si anayestahili...watoto wa maskini hawana haki na kodi za baba zao tena...ungepata nafasi kidogo ya kuwa maeneo waliyopo hawa watoto ungelia machozi! Wale wa kike wameopt umalaya na kuombaomba hawawezi tena kusoma, kiwango cha elimu kimeporomoka, ushahidi ni madhara tunayoona maofisini mwetu kwa graduates waliotoka vyuo vikuu, matokeo ya mitihani ya darasa la saba na sekondari kuporomoka...wananchi waliosapoti serikali wanamuona Ndalichako...Mwanaasha kapata nini?
Waalimu wakagoma kwa madai hayohayo...wakagawanywa na strategists kuwa waunde kamati, wakatishiwatishiwa na kikamati chao, wakanywea, wakubwa wanapeta wanafanya watakavyo na fedha zetu na maisha ya walimu yanazidi kuwa duni...wananchi wamedanganywa tena kuwa walimu wanadai kisichowezekana, wakaamini hizo propaganda wakaacha kuunga mkono walimu, madhara yake ni migomo baridi ya walimu na kufeli watoto. Walimu kwakuwa nao ni binadamu, wameopt viosk vyao viitwavyo tuition...darasani hawafundishi ili watoto waje tuition...mfumo wa elimu umeporomoka, wananchi wameacha kuilaani serikali, wanawalaani walimu kwa msaada wa serikali
Sasa madaktari. Wao wamejipanga. Serikali inaogopa kutumia nguvu kuwalazimisha warudi kazini kwa kuwa wanajua hawa jamaa wameshikamana na hawataki kamati inayoweza kununuliwa na mafisadi. Wanasimama kwa umoja wao dhidi ya dhuluma za serikali yao. Pinda katupiwa mzigo peke yake na mtalii anapiga propaganda akijua hawezi kushinda. Anajaribu kutafuta huruma za wananchi kupitia press. Tunawapata wananchi wachache wasioamini juu ya mabadiliko wanaona tu vifo iwapo madaktari watagoma na kuwatupia madaktari lawama. Hawaoni madhara ya mgomo huu kwa mbali...wanaishia kutetea serikali legelege.
Wasijue kuwa serikali hii ni kama punda asiyekwenda pasipo mjeledi...madaktari wasipoyumba, wagonjwa kweli watapata shida na wengine kupoteza maisha, lakini hatimaye serikali haiwezi kuwafukuza kwani haina mahali penginepa kupata madaktari na gharama yake serikali yetu haitaiweza. Kwa hiyo serikali itatekeleza tu matakwa ya madaktari...wakimaliza wao, wale watu wetu waoga -walimu, nao watadai, watapewa, askari wetu nao pamoja na kukubali kutumiwa vibaya, nao watadai, watapewa, na wengine. Hiyo ndiyo hofu kubwa ya mtalii.
Conclusion: pasipo mjeledi, punda huyu aitwaye serikali hatokwenda! Madokta wetu aluta continua, mapambano yaendelee, tuko nyuma yenu mpaka serikali hii dhalimu ianze kujirekebisha kwa kuweka vipaumbele vyake sawa na kuzuia matumizi mabaya ya fedha za umma ili wazielekeze kwenye mambo nyeti