Inashangaza!! Serikali ilipotangaza kupanda bei ya mafuta ya taa, walipandisha siku hiyo hiyo. Hawa wanatunishana misuri na serikali.
Mimi wakati mwingine nafikiri hii biashara ni ya watu wazito serikalini. Wanashindwaje kudhibiti hali hii kama kweli hawahusiki? Udhibiti unawashindaje akina IGP na Tiss kuhusu uchakachuaji? Halafu tunalalamika kuwa hatuendelei na ni maskini. Tutaendeleaje wakati mafuta tunayotumia yanaharibu magari, mitambo, matrekta na zana nyingine za kilimo na viwanda?
Hii ni hatari kuliko kuliko hata maandamano yanayoogopwa na serikali. Hali ya uchumi ikiwa mbaya, umaskini kadiri unavyotamalaki, pengo kati ya maskini na matajiri wachache linavyo kuwa kubwa watu wataandamana kuitaka serikali itoke madarakani. "They will have nothing to loose except their chains."