Madaktari Kenya Watishia mgomo kupinga karantini ya Ebola

Madaktari Kenya Watishia mgomo kupinga karantini ya Ebola

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,145
Reaction score
4,199
Madaktari nchini wameonya kuwa wako tayari kuanzisha mgomo wa kitaifa kupinga mpango wa serikali wa kuanzisha kituo cha karantini na matibabu ya Ebola katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Laikipia.

Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno (KMPDU), Davji Bhimji Atellah, amesema hatua ya serikali kuruhusu Kenya kuwa mwenyeji wa wagonjwa waliokumbana na virusi hivyo ni hatari kwa usalama wa wananchi na inalenga zaidi maslahi ya mataifa ya kigeni.

KMPDU imeitaka Wizara ya Afya na Wizara ya Mambo ya Nje kutoa maelezo ya wazi kwa nini Kenya ilichaguliwa badala ya mataifa jirani yaliyo karibu na kitovu cha mlipuko.

“Hatutakaa kimya tukitazama Kenya ikigeuzwa eneo la kudhibiti ugonjwa hatari ambao hatukuusababisha,” chama hicho limesisitiza.

Madaktari wamerejelea kipindi ambapo milipuko ya awali ilipotokea, kuwa Marekani ilikuwa ikiwahamisha raia wake nyumbani kwa matibabu, na si kuwasafirisha hadi nchi nyingine.
 
Wakenya wakikubali hii ujinga watanzania pia tutakuwa hatarini, tupo pamoja na wakenya, marekani ajenge hicho kituo huko kwao.
 
Back
Top Bottom