Mgomo: Madaktari waiangukia serikali!

Haahaahaaa! chezea baba Riz1 weye?!
Nani alisema ni dhaifu? amuulize mama Riz1, Uli na nanii aliyenanii kule Nyilolo (sorry)
Hakuna serikali dhaifu duniani. Serikali siku zote INAJUA imeshika mpini bahati mbaya sana sisi mafala HATUJUI tumeshika makali
Na mbwembwe zote zile?! poleni sana madaktari
Adui yako mwombee njaa..
 


Wanaodaiwa kuwa ni Madaktari wanaofanyakazi chini ya usimamizi wa madakatari bingwa (Intern Doctors), wamemwangukia Rais Jakaya Kikwete huku wakimwomba radhi kwa ushiriki wao katika mgomo wa madaktari uliosababisha maafa kwa baadhi ya wagonjwa.


Poleni interns! Ila naona hammjui JK vizuri. Ni mtu asiyegeuka nyuma, na akiamua ameamua
 
watafute vp kazi mkuu wakati bado walikuwa hawajahitimu.
Ni uzembe wao wa kufanya mambo bila kufikiria, waliweka maslahi yao mbele badala ya maslahi ya wagonjwa, wakawaacha wakateseka, wakafa na wengine kupata ulemavu.
Dhambi waloifanya itawagharim sana mpaka watakapo tubia kwa dhati ya nafsi zao.
Walisahau wanashindana na serekali ambayo imeshika mpini nao wameshika makali kwani walikuwa bado hawaja hitimu na kuwa madaktari kamili.
Leo ndo wanakumbuka walipo jikwaa baada ya kusota mtaani.

Wasikate tamaa, waendelee kuiomba serekali na kuwaomba radhi watanzania.naamini watasamehewa na kurudishwa japo kwa masharti magumu.
Hawafai kuwa madaktari hawa serikali iwafutilie mbali maana thinking capacity yao ndogo sana! maana walipaswa kujua kuwa hawajahitimu na je wanachokisimamia ni sawa kama ni sawa wangeelea nacho hadi mwisho, hii inareflect kwenye tiba wanatotoa unampa mgonjwa dawa huna uhakika katikakati unabadilishabadilisha anakufa!
 
Nawaunga mkono. Wa kwanza kulaumiwa zaidi ni dr.ulimboka kwa kukaa kimya na taarifa mhimu juu ya kutekwa kwake.!
 
Hawa si madaktari bali wanganga njaa wanaoweza kuramba matapishi yao. Kama walikuwa wakijua wanachofanya hawakuwa na haja ya kumwangukia mtu aliyepaswa kuwaangukia. Njaa ni mbaya hasa inapoingia kwenye vichwa vya wale tunaodhania kuwa wamesoma ingawa hawakuelimika kama hawa madaktari uchwara wetu. Heri wangenyamaza wakaongeza kipato kwa kunyofoa mimba ingetsoha kuliko kuramba matapishi yao.

Kila mwanadamu kuna wakati hutakiwa kufanya/kuchukua hatua katika maamuzi magumu. Kila maamuzi tunayofanya huwa ni SAHIHI, matokeo ya maamuzi hilo ni jambo jingine. Na kila mmoja wetu kuna wakati aliamua vibaya na akapata tofauti na alivyotarajia; HAYO NDIO MAISHA........!!!, TUWASAMEHE NA MAISHA YANASONGA MBELE....!!!
 
Naichukia sana mijitu mioga, mioga inayopenda kujipendekeza pendekeza kwa wamagamba!
Ingekuwa amri yangu ningeamuru wote walioomba msamaha wapigwe risasi tatu za kichwa!
 
teh teh teh...nani aliwaambia wagome kama hawajui wanachofanya?

Hehehe kumbe waliyemtegemea ndiyo alikuwa adui yao namba moja. Lakini imetulia kuvaa makoti yenu meupe. Timu moja wengine wavae kaki na wengine kijani lazima kinuke tuu. Siku nyingine kabla ya kugoma mupite kwa wapiga ramli wawachekie mchezo mzima
 
OSOKONI kumbuka wewe hata ukienda nje bado ndugu zako watabaki Tanzania. kwa nini mimi nisomee hela ya masikini ndugu zangu Watanzania halafu nikawahudumie raia wa nchi nyingine? tuweni wazalendo jamani fikirieni kidogo nje ya box

kwanini wengine waibe hela tanzania wakazifiche uswiz,,,,????NADHAN HUKO NDO KWENYE MASLAH,NA HAWA NAO WANAKIMBILIA ,MASLAH
 
Sisi wengine tulionekana maadui tulipotoa ushauri wa nini kinatakiwa kufanyike. Tulipochambua wapi makosa yamefanyika.

Hata hivyo kulaumiana hakuleti manufaa yoyote. Sasa hivi tuangalie zaidi wapoi kwa kuelekea.

Hawa interns wako katika mafunzo. Mafunzo siyo jinsi ya kutibu tu, bali pia jinsi ya kudeal na situation mbalimbali sehemu ya kazi. Kukosea kwao ni sehemu ya kujifunza. Kwa bahati mbaya seniors wao badala ya kuwafunza, waliwapotosha.

Naungana nao kumuomba mheshimiwa Rais kuwasamehe hawa madaktari wetu moyoni kwake. Hata hivyo kwa vile walisimamishwa kisheria na si kisiasa, basi Rais aangalie jinsi sheria inavyoweza kumpa fursa ya kutoa msamaha ili waweze kuendelea kutiabia watanzania wenzao.

Personally najua hawa interns wana nia njema na waliamini mwongozo wanaopewa na wakubwa wao na hilo ni swala la kawaida kabisa katika fani ya udaktari. Kuwaacha na makovu ya kudumu bila kuwapa fursa ya kujirekebisha itakuwa ni adhabu kubwa mno kwa madaktari wa ngazi ya internship.

Kuhusu jinsi MAT inavoendesha mambo yake kishaghalabaghala nimeshaongea sana na sitaongea zaidi...
 
Jamani madaktari kugoma ni haki yao. Ila cha maana wanatakiwa wawe na utu. Kusomea somo lolote kwa mtu mwenye akili anajua anafanya nini. Yafuatayo ni mambo yanaowakuta watu kwa kadri ya kazi yake.
1. Walimu, wanaishi katika mazingira magumu, hawana mishaara mizuri, wanaona kwamba hawathaminiwi, wameanza migomo siku nyingi kabla sijazaliwa
2. Wanasiasa, wanaishi mazingira mazuri, mishaara minono, wanaamini wanaeshimiwa, si wakweli hata kidogo. Sikuzote wanajiangalia wao tu
3. Wanajeshi, magereza, polisi, wanaishi mazingira mabaya kuliko wote, watiifu kwa yeyote aliyepo madarakani, mishaara sio mizuri, hawaheshimiki na wengi
4. Madaktari, mishahara sio mizuri, mazingira mabaya, wahaheshimika unapoumwa tu au ukiwa na mgonjwa, wanataka kuonekana wa maana kuliko mtu yeyote duniani kisa tu eti ukiugua yeye atakuokoa, wanatabia ya kugoma mara kwa mara
sasa wewe una mtoto wako anataka kusomea udktari unamruhusu vipi kwa historia hii. Kwanini asisomee wanasheria, biashara, uhasibu, sijawahi kusikia wamegoma.
 
Nijuavyo mimi,

Kati ya madaktari zaidi ya 350, waliofukuzwa ..jumla ya madaktari 160 walisaini majina ili kuomba msamaha, ..waliobaki kati ya waliofukuzwa wakiwa nje ya nchi na baadhi katika sekta binafsi hapa nchini.

Hii ikiwa na maana kwamba madaktari 160,
1. Hawakuwa na madai ya msingi(halali)
2.Walionesha utovu wa nidhamu kwa uongozi wa hospitali tofauti tofauti nchini, mahakama
3.Ilikuwa ni halali kwa Dr. Ulimboka kuteswa na kuumizwa kwani madai hayakuwa na mantiki

na hivyo kusababisha vifo vingi ambavyo vingetibika kwa kuwa walikuwa na uwezo wa kuokoa maisha hayo..walitakiwa kuomba msamaha walikataa..leo hii kwanini warudi kuuomba?.. Je, ni kushindwa kwenda nje kama wenzao? Je, ni hali ngumu ya maisha huko mtaani? Je, ni kuona kuwa walipotoka na kurudi njia salama sasa??

USHAURI:
-Ingawa sababu kuu ya kuomba msamaha ni kudai kuwa wametelekezwa na wakubwa "specialist" na hawakupata kikao..bado tatizo liko miongoni mwao, ubinafsi kati ya madaktari wenyewe.

-Sidhani kama leo hii kesi itavunjwa mahakamani na MCT, iwaruhusu kurudi makazini..nadhani bado kusubiri kutakuwa pale pale na ndilo jambo "daktari wa kitanzania" aliyesoma under stressful condition and working under same enviroment asiloweza..kwani muda wote alishazoea kuwa "occupied/scheduled"..na ndilo jambo gumu liliposababisha kufika hatua hii.

2. Kuwapo na mgomo au jamvo kama hilo ni vizuri kupambanua kama utafika mwisho au la..nikimaanisha kwa kuwa hakukuwa na vitisho kwa mtu ambaye yeyote ambaye hatagoma atafanyiwa jamvo baya ni vizuri kujitathmini na aibu kwa mama wa familia au baba wa familia kufanya jambo kwa mkumbo..esp.unapokuwa msomi...

OMBI: "KAMA" Serikali ikiwaruhusu kurudi na wafanye kazi kwa moyo wote, wakiwatumikia watanzania.
 
Back
Top Bottom