Mgogoro wa Zanzibar watinga Ikulu ya Marekani

Mgogoro wa Zanzibar watinga Ikulu ya Marekani

Wazanzibari waishio Marekani waliandamana mjini Washington mpaka White House ya MAREKANI, huku wakiwa na ujumbe kuwa kuwaomba Marekani na jumuiya zingine ziingilie kati kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi wa Zanzibar.

Licha ya hayo, pia katika nchi ya OMAN, raia walifurahi sana pale Maalim Seif alipoiomba Tume imtangaze mshindi wa Zanzibar.

Ikumbukwe Maalim Seif ameahidi kama atakuwa Rais wa Zanzibar basi baada ya siku 100 itageuka na kuwa Singapore.

Kama utakumbuka katika kipindi hiki cha miaka mitano akiwa kama MAKAMU WA RAIS aliweza kuinua zao la karafuu kutoka sh 300 hapo awali mpaka sasa ni sh 2500 kwa kilo.

Magamba waache ung'ang'anizi wa madaraka na wamtangaze haraka maalim seif kama mshindi wa kiti cha urais wa zanzibar. nchi hii ikiingia kwenye machafuko CCM hawatakwepa lawama.
 
Unadhani Marekani wataifanya nini Tanzania kama imeamua kurudia uchaguzi wa Zanziabar? Yaani hujui maana ya nchi huru? Kila siku kulialia kwenye mataifa ya magharibi kwa vijitatizo vidogo vidogo?

Hapa sio kuwa Zanzibar imepinduliwa. Tume yao wenyewe (ZEC) imefuta uchaguzi na kutaka urudiwe. Marekani wanaambiwa hili ili wafanye nini?

Hivi haya mawazo ya kitumwa jamani bado wengine wanayo tu?

mpuuzi mkubwa wewe! zanzibar ni nchi huru tangu lini? jecha ana mamlaka ya kufuta uchaguzi wote? kama tume yenyewe hana mamlaka hayo jecha atafutaje uchaguzi? halafu mijitu mingine kwa kujitoa akili bhana!
 
Sioni point ya wao kwenda White House USA.
Marekani washatoa tamko inatosha kabisa, walichokifanya hawa jamaa ni pointless na very stupid.
Inazidi kuonyesha wabongo jinsi gani kichwani hazimo, siamini wamekaa wakakubaliana kabisa ati wakaandamane white house ya US..

acha kujitoa akili wewe. marekani ndiye baba wa dunia hii. akiamua kuichapa nchi yoyote bila kujali kama ni uhuru au la atafanya hivyo na hakuna wa kumuuliza. acha ubwege wewe. kama hujui ujeuri wa marekani muulize gadafi au sadam hussein.
 
Unachanganyikiwa kweli.....Hao jamaa hata bararaka ya karibu ya whitehouse hawawezi kukaribia wengi watakuwa waishi with false Identification....... ukitilia maanani ISIS wanavyoisumbua USA sasa hivi....Mr President hawezi kudili na taka taka hiyo....... waende huko oman kwa sultan!

mknd wk! lazima maCCM mpigwe tu! unakumbuka ujeuri wa gadafi na sadam ulivyowatokea puani? punguan wahed wewe!
 
wewe mpuuzi unayejiita Kifyatu kweli akili zako zimefyatuka sio bure.

kuna mgogoro gani zanzibar unaouongelea wewe? zanzibar hakuna mgogoro zaidi ya jecha wa CCM kuahirisha kutangaza matokeo baada ya kuona kwamba CCM yake imeshindwa uchaguzi. mwambie huyo jecha wenu arudi kazini ajumlishe matokeo na mshindi halali (maalim seif) atangazwe.

kuna kuna maeneo yanayolalamikiwa (na maruhani) kuna namna ya kulalamika lakini sio kufuta uchaguzi mzima bila mtu yeyote kulalamika.

hebu niambie mgombea yeyote aliyelalamikia rafu za uchaguzi. wewe uliona wapi refarii anaweka mpira kwapani kwa kisingizio cha kukuikwa kwa sheria 17 za mpira? kama sheria za mpira zimekiukwa kwanini asitoe kadi kwa mchezaji anayehusika badala ya kugawa kadi nyekundu kwa wachezaji wote 22? hata kama akifanya hivyo, kitakachovurugika ni mechi lakini matokeo ya mpira yatabaki kama yalivyo. unaipata hiyo picha au bado umejitoa akili? acha unafiki wako wa kike wewe!
 
Last edited by a moderator:
Jamani, kama watu wana uhakika kuwa ni nani mshindi, alieshinda, au atakaeshinda (na nitafurahi kama maalim akishinda) kwa nini CUF wanakataa kurudia huu uchaguzi? Ni vitu gani vilivyotokea/vilivyofanyika katika uchaguzi wa Octoba 25 ambavyo vitabalika kama huu uchaguzi ukirudiwa leo?

Kama madudu wanayoyasema ZEC kuwa yalitokea ni uzushi tu basi uchaguzi ukirudiwa matokeo yatakuwa yaleyale tu.

Hapa sio kama Dr. Shein anawekwa madarakani kwa mtutu wa JWTZ. Uchaguzi ukirudiwa wananchi hawatashikiwa mtutu kichwani wamchague Dr. Shein au Maalim. Kila mtu atapiga kura kama alivyopiga awali - tatizo liko wapi?

cc. Gavana

acha kujihemua bure mama. je, ni nani aliyelalamika kwamba uchaguzi haufanyiki vzr na kwa ushahidi upi? kama kuna mgombea/wagombea wanaodhani haki haikutendeka kwanini wasipeleke ushahidi wao mahakamani walalamike? ni kifungu gani cha katiba kinachomruhu jecha kufuta uchaguzi WOTE?kwanini ofc za tume zilizingirwa na JWTZ kabla?
 
Last edited by a moderator:
Daaah. Hii shida sana.

Labda Mfano Utasaidia:
Tuchukulie mfano kuwa wewe ni rafiki yangu na kila ninapokwama unanisaidia kifedha kujikimu mimi na familia yangu. Itokee mimi na mama watoto wangu tuna mfarakano wa kawaida nyumbani kwetu.

  • Hivi unategemea kuwa lazima tuje mlangoni kwako tukufahamishe kuwa tuna ugomvi?
  • Kama wazee wetu wakiwa wanaendelea kutusuluhisha, bado unadhani ni busara tupite kwa wahisani wetu wote tukilalamika kuwa tunagombana?

Kitendo hiki ndicho ninachokiona kinatudhalilisha sana sisi waTanzania lakini pia waAfrika wote kwa ujumla wetu. Hatujiamini kama tunaweza kutatua matatizo yetu sisi wenyewe. Kila likitokea tatizo tunakimbilia mataifa ya magharibi.

Kwa mwendo huu tusishangae wanapotudharau ingawaje sisi ni mataajiri wakubwa sana wa rasilmali.

Eee Mwenyezi Mungu tusaidie.

wewe sio mzima. kitendo cha kuomba misaada hakikudhalilishi ila kuandamana ndio kunadhalilisha?
 
kWELI WEWE UNAISHI UGHAIBUNIIIII ??

HIVI HAYA MAMBO YANAYOTOKEA WEWE HATA HUYAELEWI ??? HIVI JWTZ IMEENDA KUFANYA NINI PALE KITUO CHA ZEC , BAADA YA KUZINGIRA ???

MCHOCHEZI NI MIMI AU HIVYO VIFARU NA MAJESHI YALIYOMWAGWA MITAANI ?? MBONA DAR ES SALAAM HAMNA ???

HIVI TUAMBIE HUYU MKUU WA TUME YUKO WAPI ???

KUANDAMANA KWENDA IKULU YA MAREKANI NI VIZURI KWANI UBAYA WENU UNAONEKANA DUNIA NZIMA

HAKUNA MAZUNGUMZO YOYOTE YANAYOFANYWA YANAYOHUSISHA WANASHERIA AU WEWE UNADANGANYWA NA PENGO ???

mkuu achana hilo zezeta Kifyatu litakuumiza kichwa. majitu kama haya ndiyo yanayokwamisha demokrasia ya nchi hii.
 
Last edited by a moderator:
wewe mpuuzi unayejiita Kifyatu kweli akili zako zimefyatuka sio bure.

kuna mgogoro gani zanzibar unaouongelea wewe? zanzibar hakuna mgogoro zaidi ya jecha wa CCM kuahirisha kutangaza matokeo baada ya kuona kwamba CCM yake imeshindwa uchaguzi. mwambie huyo jecha wenu arudi kazini ajumlishe matokeo na mshindi halali (maalim seif) atangazwe.

kuna kuna maeneo yanayolalamikiwa (na maruhani) kuna namna ya kulalamika lakini sio kufuta uchaguzi mzima bila mtu yeyote kulalamika.

hebu niambie mgombea yeyote aliyelalamikia rafu za uchaguzi. wewe uliona wapi refarii anaweka mpira kwapani kwa kisingizio cha kukuikwa kwa sheria 17 za mpira? kama sheria za mpira zimekiukwa kwanini asitoe kadi kwa mchezaji anayehusika badala ya kugawa kadi nyekundu kwa wachezaji wote 22? hata kama akifanya hivyo, kitakachovurugika ni mechi lakini matokeo ya mpira yatabaki kama yalivyo. unaipata hiyo picha au bado umejitoa akili? acha unafiki wako wa kike wewe!

kuna mgogoro gani zanzibar unaouongelea wewe? zanzibar hakuna mgogorozaidi ya jecha wa CCM kuahirisha kutangaza matokeo baada ya kuona kwamba CCM yake imeshindwa uchaguzi. mwambie huyo jecha wenu arudi kazini ajumlishe matokeo na mshindi halali (maalim seif) atangazwe.

kuna kuna maeneo yanayolalamikiwa (na maruhani) kuna namna ya kulalamika lakini sio kufuta uchaguzi mzima bila mtu yeyote kulalamika.

hebu niambie mgombea yeyote aliyelalamikia rafu za uchaguzi. wewe uliona wapi refarii anaweka mpira kwapani kwa kisingizio cha kukuikwa kwa sheria 17 za mpira? kama sheria za mpira zimekiukwa kwanini asitoe kadi kwa mchezaji anayehusika badala ya kugawa kadi nyekundu kwa wachezaji wote 22? hata kama akifanya hivyo, kitakachovurugika ni mechi lakini matokeo ya mpira yatabaki kama yalivyo. unaipata hiyo picha au bado umejitoa akili? acha unafiki wako wa kike wewe![/QUOTE]

Hewala mkuu. Nakubali mimi ni mpuuzi.

Lakini Jecha kuahirisha kutangaza matokeo ya, au kufuta uchaguzi huo sio mgogoro mkuu?

Pia, kama Jecha akitia ngumu kuwa ni lazima uchaguzi urudiwe hivi nyie mtafanya nini? Mtafanya mapinduzi? Maana ndio ninachokisikia tu humu.

Mimi nawashangaa sana, kama mna uhakika ya ushindi kwa nini mnagomea kurudiwa uchaguzi. Mlifanya madudu gani siku ya Oktoba 25 ambayo mnaogopa hamuwezi kuyarudia tena kama uchaguzi utarudiwa?

Sijui unamaanisha nini na maruhani? Hilo nitakuachia mwenyewe.

Kuhusu aya yako tamati, mimi nitasema hivi:
Jecha ndie aliefuta uchaguzi; Sasa hivi Maalim, Dr. Shein na wasuluhishi wa UN, AU, EU wanajadiliana, hizi kelekele zako ni za nini? Kwa nini tusisubiri matokeo ya haya mazungumzo?

Kuna fitna hapa ya huu muungano. Hili varangati la uchaguzi ni kisingizio tu. Tumewaona na hila zenu tokea mko mbali sana lakini mlifikiri sisi ni wapuuzi tu. Tatizo la muungano litatuliwe kikatiba na sio kupitia hila za uchaguzi.
 
Test for Magufuri administration!! will he be like president Mugabe? let us wait and see! 1.2 Trilion grant might be a peanut to current position considering his efforts on cost cutting
 
mpuuzi mkubwa wewe! zanzibar ni nchi huru tangu lini? jecha ana mamlaka ya kufuta uchaguzi wote? kama tume yenyewe hana mamlaka hayo jecha atafutaje uchaguzi? halafu mijitu mingine kwa kujitoa akili bhana!

Mkuu huu utusi ni wa nini?
 
Swali tunalolijadili ni lipi?

1. Matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 yalikuwaje?
2. Je, huu muungano wa bara na visiwani ni halali kuwepo?

Swali la kwanza ndilo nililokuwa nimejikita nalo muda wote huu. Ni suluhu gani tuipate kuhusu ushindi wa CUF au CCM (ASP) kutokana na uchaguzi huu uliopita. Hili swali ni rahisi sana kulipatia suluhisho lake na nimeainisha suluhu zake hapo awali.
Suluhisho lako ni kurudia uchaguzi. Suluhisho lako RAHISI ni dhaifu sana:

Maswali ya msingi kuhusu kufuta uchaguzi wa Zanzibar hayajawahi kutolewa ufafanuzi......

Ripoti zote za waangalizi wa uchaguzi wa zenji zinasema uchaguzi ulienda vizuri.......

Dr. Shein kashindwa kwa kura 25,000.... CCM wamepoteza majimbo tisa (9) kisiwani Unguja. Cha ajabu jana Balozi Seif Ali Iddi (Aliyekuwa mwenyekiti wa kampeni CCM Zanzibar) anaropoka kwenye Radio France International kuwa CUF & CCM wamekubaliana kuwa uchaguzi Zanzibar urudiwe...CUF wamesema hakuna kitu kama hicho.....

Suluhisho pekee ni kumalizia kutangaza matokeo yaliyobaki na kumtangaza mshindi...kama wazee wako wenye busara hawataki hiyo, wanajidai ni wabishi, wanakaidi sauti ya wapiga kura, watawekewa vikwazo tu na MCC , hamna namna nyingine sasa, maana tushachoka sasa.....

Nchi hii ni lazima tukubaliane kuwa inaendeshwa kwa misingi ya sheria na haki......Kwa kiasi fulani ni bora tunategemea misaada ya Marekani maana inasaidia kuondokana na Ubabe wa CCM, biashara ya kujificha chini ya mwamvuli wa vyama vingi huku nchi inaendeshwa kama one party state haiwezekani tena Zanzibar.......
Swali la pili ni la kikatiba. Je huu muungano tuwe nao au la. Hatuwezi kutumia uchaguzi huu uliopita (2015) kutengua muungano. Nyote humu mnai-discredit CCM au ASP kuwa sio halali kuwepo Zanzibar. Hii sio sahihi. CCM na CUF wana nafasi sawa kugombea uongozi wa Zanzibar kufuatia ridhaa ya waZanzibari. Lakini nyie hoja zenu ni kuwa CCM ni wakoloni weusi na kuwa mnataka kuwaondoa visiwani. Sasa tukichukulia kuwa CCM ndio ASP na serikali asisi ya Zanzibar, kusema kuwa unataka kuing'oa visiwani ni uhaini, YES - TREASONOUS. Huwezi kusema unataka kutumia uchaguzi huu kama nyenzo tu ya kuing'oa CCM kwa kuwa hawa ni wakoloni weusi.
Kitendo cha CCM kuitwa kuwa ni wakoloni weusi ni changamoto wanayotakiwa kukumbatia kwa mikono miwili na sio kuleta ubabe na jeuri......

Hamna aliyesema CCM sio halali kuwepo Zenji, inaweza kuwepo kama chama cha Upinzani, kuwa mpinzani ni jambo zuri tu, mbona CUF wamekuwa kwa mda mrefu....inakupa mda wa kujipanda tena kuchukua dola....Labda kama CCM wana wasiwasi kuwa hawawezi tena kuwashawishi wapiga kura wa-Zanzibar.....

Kung'oa CCM visiwani sio Uhaini bali ni kuitoa madarakani kwa njia ya kura kama walivyokwishafanya Wazanzibari, kwa kufanya hivyo hakufuti mfumo wa vyama vingi Zanzibar bali demokrasia inaimarika zaidi.....

Kuhusiana na Muungano, kama Wazanzibari wengi hawahitaji muungano, wafanye referendum waamue....hiki sio kitu cha ajabu, kimefanyika sehemu nyingi duniani mfano Scotland (UK), Eritrea (Ethiopia), South Sudan (Sudan), Cremea (Ukraine-Russia), hata Barcelona (Spain)...karne ya 21 hivi vitu sio vya kulazimishana......
Kuna hoja tatu hapa za kutafakari:
  1. Je, Zanzibar irudishwe kwa Sultan (raia wa Omani) kwa kuwa ndie aliepewa uhuru na Muingereza mwaka 1964?
  2. Je, Zanzibar irudushwe kwa ASP na iwe nchi huru bila ya mfungamano wowote na Tanganyika?
  3. Je, tujikite kuuboresha muungano uliopo kwa kujibu kero za sasa za waZanzibari kupitia katiba mpya?

Sasa hoja ya kwanza na ya pili (kama ndio muafaka) ni rahisi sana kwa Tanganyika. Tanganyika ni kuwarudisha waPemba na waUnguja wote (raia wa kigeni) walioko bara kwenda kwao Zanzibar na waTanganyika wabaki na upweke wao. This can be really messy but easy to implement.

Hoja ya tatu ni ngumu sana kuitekeleza lakini ndio yenye tija kwa visiwani na bara - kwa maoni yangu. Nasema ni ngumu kuitekeleza (lakini haiishindikani) kwa sababu kuna hii kasumba kuwa matatizo yote ya visiwani yanaletwa na huu muungano. Na kwamba mara tu visiwani watakapokuwa huru na kujiunga na Oman au na other Arab (Islamic) countries, basi neema itawabubujikia.
Hoja yako ya kwanza na ya pili hazina mantiki......umeongozwa na mihemko.....

Hoja yako ya tatu, unazungumzia kero ambazo zimekuwapo kwa mda mrefu. Kama jambo dogo la kukubali matokeo halali ya wapiga kura wa Zanzibar linawashinda CCM, wataweza hayo makubwa ya kushughulika na kero sugu za muungano?

Kama wanapelekea Wazanzibari wanajeshi na vifaru katika uchaguzi uliofanyika na kumalizika kwa amani ni wazi hatuna viongozi wenye uwezo wa kusimamia misingi ya utawala bora, utawala wa sheria na demokrasia...kwa kifupi tuna tatizo la uongozi (leadership problem)....

Huu mgogoro upo kwa sababu ya maslahi ya CCM wala sio maslahi ya Zanzibar au Taifa...kama mtu anabisha aniambie kwamba tuliruhusu mfumo wa vyama vingi Tanzania Zanzibar kama geresha tu wala hatukuwa na dhamira ya kweli kusimamia hilo, nitamuelewa.........
Ndugu zangu, tafakarini sana. Be careful what you wish for.
Mkishashindwa hoja, mnakimbilia kuogopesha watu....ndio yale yale ya mkiwachagua wapinzani kutatokea machafuko, mara Tanzania itakuwa kama Iraq, Libya, Misri..... Siasa za kitoto sana.....
Cha mwisho.
Kama tutaendeleza huu mjadala kuhusu uchaguzi wa 2015, tafadhali sana tusiuchanganye na swala la MUUNGANO, hatutafikia muafaka.
Suala la muugano haliwezi kutenganishwa na huu mjadala......labda hujui, makada wa CCM wamejitokeza mara kibao kwenye vyombo vya habari kusema kuwa Maalim akipewa nchi atavunja muungano....CCM wanatafuta njia ya ku-sympathize na Wazanzibari kuwa huyo mtu hata kama ameshinda hana nia nzuri na Zanzibar...wanasahahu kuwa washapiga propaganda za aina hiyo kwenye kampeni zao, na Wazanzibari wamemchagua Maalim hivyo hivyo.....
 
Test for Magufuri administration!! will he be like president Mugabe? let us wait and see! 1.2 Trilion grant might be a peanut to current position considering his efforts on cost cutting

Magufuli kama yuko serious aanze kuzirudisha zile nyumba alizomuuzia hawara Wake alipokuwa waziri. Hapo yutamuona ni born again na yuko serious kwa lolote lenye manufaa kwa nchi
 
Suluhisho lako ni kurudia uchaguzi. Suluhisho lako RAHISI ni dhaifu sana:

Maswali ya msingi kuhusu kufuta uchaguzi wa Zanzibar hayajawahi kutolewa ufafanuzi......

Ripoti zote za waangalizi wa uchaguzi wa zenji zinasema uchaguzi ulienda vizuri.......

Dr. Shein kashindwa kwa kura 25,000.... CCM wamepoteza majimbo tisa (9) kisiwani Unguja. Cha ajabu jana Balozi Seif Ali Iddi (Aliyekuwa mwenyekiti wa kampeni CCM Zanzibar) anaropoka kwenye Radio France International kuwa CUF & CCM wamekubaliana kuwa uchaguzi Zanzibar urudiwe...CUF wamesema hakuna kitu kama hicho.....

Suluhisho pekee ni kumalizia kutangaza matokeo yaliyobaki na kumtangaza mshindi...kama wazee wako wenye busara hawataki hiyo, wanajidai ni wabishi, wanakaidi sauti ya wapiga kura, watawekewa vikwazo tu na MCC , hamna namna nyingine sasa, maana tushachoka sasa.....

Nchi hii ni lazima tukubaliane kuwa inaendeshwa kwa misingi ya sheria na haki......Kwa kiasi fulani ni bora tunategemea misaada ya Marekani maana inasaidia kuondokana na Ubabe wa CCM, biashara ya kujificha chini ya mwamvuli wa vyama vingi huku nchi inaendeshwa kama one party state haiwezekani tena Zanzibar.......

Sitakujibu kwa hili. Itoshe tu kusema Maalim, Dr. Shein, wasuluhishi wa UN, EU, AU, na maraisi wastahafu wanalizungumzia. Sitaki kuumiza kicha changu kwa jambo ambalo liko kwa watu wenye ujivi mkubwa zaidi kuliko mimi.

Kitendo cha CCM kuitwa kuwa ni wakoloni weusi ni changamoto wanayotakiwa kukumbatia kwa mikono miwili na sio kuleta ubabe na jeuri......

Hamna aliyesema CCM sio halali kuwepo Zenji, inaweza kuwepo kama chama cha Upinzani, kuwa mpinzani ni jambo zuri tu, mbona CUF wamekuwa kwa mda mrefu....inakupa mda wa kujipanda tena kuchukua dola....Labda kama CCM wana wasiwasi kuwa hawawezi tena kuwashawishi wapiga kura wa-Zanzibar.....

Kung'oa CCM visiwani sio Uhaini bali ni kuitoa madarakani kwa njia ya kura kama walivyokwishafanya Wazanzibari, kwa kufanya hivyo hakufuti mfumo wa vyama vingi Zanzibar bali demokrasia inaimarika zaidi.....

Kuhusiana na Muungano, kama Wazanzibari wengi hawahitaji muungano, wafanye referendum waamue....hiki sio kitu cha ajabu, kimefanyika sehemu nyingi duniani mfano Scotland (UK), Eritrea (Ethiopia), South Sudan (Sudan), Cremea (Ukraine-Russia), hata Barcelona (Spain)...karne ya 21 hivi vitu sio vya kulazimishana......

Nadhani wewe umeachwa nyuma kidogo na mambo. CUF wanachokizungumzia sasa ni kuwa CCM (ambayo visiwani ni Afro-Shirazi Party - ASP) ni chama batili na hakitakiwi visiwani. Hiki hakisemwi waziwazi bali ni kwa kutumia code words kama "wakoloni weusi", n.k. Soma katikati ya mistari na utakiona hich dhahiri kabisa. Haya sio maneno yangu bali fuatilia majadiliano kweye uzi huu na ukipata nafasi msome Bwana Harith Ghassany (Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!), au kama una muda zaidi basi wasikilize wahubiri wa Uamsho (ninaweza kukupa links za hizi video kama unazitaka).

Kutokana na hizi harakati ninazoziona, nafikiri kuwa maoni ya CUF ni kuwa CCM (au ASP) ni batili (is illegitimate) kule visiwani. Ndio maana nikasema sitashiriki tena mjadala unaozichanganya kero za uchaguzi (2015) na kero za muungano. Tutapotezeana muda na sitaruhusu hicho.

Wazo lako la kura ya maoni (referendum) kama visiwani wanataka muungano au la mimi naliunga mkono. Lakini swala hili tusilichanganye na uchaguzi huu wa 2015. Haya ni maswala mawili tofauti kabisa.

Hoja yako ya kwanza na ya pili hazina mantiki......umeongozwa na mihemko.....

Hoja yako ya tatu, unazungumzia kero ambazo zimekuwapo kwa mda mrefu. Kama jambo dogo la kukubali matokeo halali ya wapiga kura wa Zanzibar linawashinda CCM, wataweza hayo makubwa ya kushughulika na kero sugu za muungano?

Kama wanapelekea Wazanzibari wanajeshi na vifaru katika uchaguzi uliofanyika na kumalizika kwa amani ni wazi hatuna viongozi wenye uwezo wa kusimamia misingi ya utawala bora, utawala wa sheria na demokrasia...kwa kifupi tuna tatizo la uongozi (leadership problem)....

Huu mgogoro upo kwa sababu ya maslahi ya CCM wala sio maslahi ya Zanzibar au Taifa...kama mtu anabisha aniambie kwamba tuliruhusu mfumo wa vyama vingi Tanzania Zanzibar kama geresha tu wala hatukuwa na dhamira ya kweli kusimamia hilo, nitamuelewa.........

JD, Hoja yangu ya kwanza na/au ya pili ndio haswa zinazopendelewa na CUF. Kama hili hulijui then hatupo kwenye ligi moja na nitaiachia hapo.

Naona tunakubaliana kuwa muungano ni kero moja na madudu ya uchaguzi (2015) ni kero nyingine. Ninachosema mimi ni kuwa wakati tunajadili nini kifanyike kuhusu uchaguzi, tusiingize kero za muungano hapa tutashindwa kupata suluhu.

JD, hivi unafikiri watu walikuwa hawajui mikakati yenu UKAWA ya kuleta machafuko bara wakati wa uchaguzi huu? Hii ni siri bayana mkuu. Sasa sitashangaa kama mikakati kama ile yenu bara ilikuwa inapangwa visiwani. Majeshi yako pale kulinda amani na sio kupindua. ZEC inasema uchaguzi urudiwe na tunachokisikia kutoka CUF ni kila aina ya hoja (kisheria, kikatika, kiutu, kutosumbua watu, n.k.) kupinga uchaguzi usirudiwe. Mlifanya nini wakati ule mnaokificha tusikione wakati sasa kila mtu ataangalia?

Huu mgogoro haupo kwa ajili ya maslahi ya CCM. Kama ni kwa ajili ya CCM basi wangetangaza tu kuwa Dr. Shein ameshinda. Na wewe unajua sheria kuwa kama ZEC ikisema tu kuwa CCM imeshinda uraisi basi hakuna cha kukata rufaa popote pale. CCM wamekubali agizo la ZEC kuwa uchaguzi urudiwe. Ni CUF tu ndio ving'ang'anizi wanaokataa. Hebu fikiria wewe mwenyewe. Hapa kuna kajiharufu ka ujanja-ujanja.

Mkishashindwa hoja, mnakimbilia kuogopesha watu....ndio yale yale ya mkiwachagua wapinzani kutatokea machafuko, mara Tanzania itakuwa kama Iraq, Libya, Misri..... Siasa za kitoto sana.....

Suala la muugano haliwezi kutenganishwa na huu mjadala......labda hujui, makada wa CCM wamejitokeza mara kibao kwenye vyombo vya habari kusema kuwa Maalim akipewa nchi atavunja muungano....CCM wanatafuta njia ya ku-sympathize na Wazanzibari kuwa huyo mtu hata kama ameshinda hana nia nzuri na Zanzibar...wanasahahu kuwa washapiga propaganda za aina hiyo kwenye kampeni zao, na Wazanzibari wamemchagua Maalim hivyo hivyo.....

Kama hutaki kutenganisha swala la muungano na matatizo ya uchaguzi katika kutafuta suluhu ya uchaguzi huu basi usini-tag unapoleta huo uzi wako. Sitakuwa na muda wa kuzuunguukia kitu hicho hicho mara nenda mara rudi.

JD, nilikustahi sana tulipokuwa tukijadili uchaguzi wa Lowassa na Magufuli na ndio maana sikukata kijeuri. Umeona nilivyokuwa sahihi katika maoni yangu juu ya raisi wa JMT.

Katika mjadala huu sitakuwa na simile hata kidogo na wewe. Ukileta yale mambo yalioniudhi awali nitakutaka kijeuri sana. Cha kwanza ni kuwa kama una swali basi aya moja au mbili zinatosha. Sitaki gazeti. Ukileta gazeti sitalijibu.

Nakupa onyo mapema.
 
Usipanic
Sitakujibu kwa hili. Itoshe tu kusema Maalim, Dr. Shein, wasuluhishi wa UN, EU, AU, na maraisi wastahafu wanalizungumzia. Sitaki kuumiza kicha changu kwa jambo ambalo liko kwa watu wenye ujivi mkubwa zaidi kuliko mimi.
Wakati hayo unayoita mazungumzo ya kutatua "mgogoro wa Zanzibar" yanaendelea , Meneja wa Kampeni-CCM Balozi Seif Ali Iddi anapotosha umma kuwa CUF & CCM wamekubaliana kurudia uchaguzi wakati ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho......

Uliponda Wazanzibari walioenda ikulu ya Marekani kwamba matatizo yetu tutatue wenyewe, hayo maandamano naona yamezaa matunda.....serikali sasa imeshatishiwa kunyimwa misaada ya MCC Phase 2 kwa sababu ya hicho unachoita "mgogoro wa Zanzibar" pamoja na ile ishu ya wale jamaa zetu wa LHRC kuhusiana na ile sheria ya CCM ya mtandao......

Nilifikiri kutatua matatizo yetu wenyewe kunakuwa hamna haja ya UN, EU au UN kuwepo......hasa hasa EU...kumbe watanzania wakienda kulalamika kwenye nchi zenye ushawishi mkubwa duniani wanaweza kupata haki yao inayominywa na CCM?......
Nadhani wewe umeachwa nyuma kidogo na mambo. CUF wanachokizungumzia sasa ni kuwa CCM (ambayo visiwani ni Afro-Shirazi Party - ASP) ni chama batili na hakitakiwi visiwani. Hiki hakisemwi waziwazi bali ni kwa kutumia code words kama "wakoloni weusi", n.k. Soma katikati ya mistari na utakiona hich dhahiri kabisa. Haya sio maneno yangu bali fuatilia majadiliano kweye uzi huu na ukipata nafasi msome Bwana Harith Ghassany (Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!), au kama una muda zaidi basi wasikilize wahubiri wa Uamsho (ninaweza kukupa links za hizi video kama unazitaka).

Kutokana na hizi harakati ninazoziona, nafikiri kuwa maoni ya CUF ni kuwa CCM (au ASP) ni batili (is illegitimate) kule visiwani. Ndio maana nikasema sitashiriki tena mjadala unaozichanganya kero za uchaguzi (2015) na kero za muungano. Tutapotezeana muda na sitaruhusu hicho.

Wazo lako la kura ya maoni (referendum) kama visiwani wanataka muungano au la mimi naliunga mkono. Lakini swala hili tusilichanganye na uchaguzi huu wa 2015. Haya ni maswala mawili tofauti kabisa.
Hata CHADEMA wamewaita CCM 'wakoloni weusi' na hamna cha code wala mdogo wake code...

Wazanzibari wanaifananisha CCM na ukoloni, halafu hii hata haihitaji Phd kugundua....angalia kwa mfano uchaguzi wa Zanzibar uliomalizika, Jecha amefuta matokeo bila kufuata sheria zilizopo na CCM wanamuunga mkono 100% pamoja na kuwa hawakuwahi kupeleka malalamiko yoyote ZEC...CUF peke yao ndio wanaonekana kusimamia haki......

Umefikiri kuwa kwa maoni ya CUF, CCM ni batili....hizo ni fikra zako wala sio fact...CCM ingekuwa batili, CUF wasingejiunga nao kutengeneza serikali ya umoja wa kitaifa 2010.....

Nasisitiza kuwa masuala ya muungano yanaendana sana na hicho unachoita mgogoro wa Zanzibar...pengine unajifanya hujui au hujui kabisa....Haya masuala mawili yanaendana wala hayapo tofauti na hayajawahi kuwa tofauti......
JD, Hoja yangu ya kwanza na/au ya pili ndio haswa zinazopendelewa na CUF. Kama hili hulijui then hatupo kwenye ligi moja na nitaiachia hapo.

Naona tunakubaliana kuwa muungano ni kero moja na madudu ya uchaguzi (2015) ni kero nyingine. Ninachosema mimi ni kuwa wakati tunajadili nini kifanyike kuhusu uchaguzi, tusiingize kero za muungano hapa tutashindwa kupata suluhu.

JD, hivi unafikiri watu walikuwa hawajui mikakati yenu UKAWA ya kuleta machafuko bara wakati wa uchaguzi huu? Hii ni siri bayana mkuu. Sasa sitashangaa kama mikakati kama ile yenu bara ilikuwa inapangwa visiwani. Majeshi yako pale kulinda amani na sio kupindua. ZEC inasema uchaguzi urudiwe na tunachokisikia kutoka CUF ni kila aina ya hoja (kisheria, kikatika, kiutu, kutosumbua watu, n.k.) kupinga uchaguzi usirudiwe. Mlifanya nini wakati ule mnaokificha tusikione wakati sasa kila mtu ataangalia?

Huu mgogoro haupo kwa ajili ya maslahi ya CCM. Kama ni kwa ajili ya CCM basi wangetangaza tu kuwa Dr. Shein ameshinda. Na wewe unajua sheria kuwa kama ZEC ikisema tu kuwa CCM imeshinda uraisi basi hakuna cha kukata rufaa popote pale. CCM wamekubali agizo la ZEC kuwa uchaguzi urudiwe. Ni CUF tu ndio ving'ang'anizi wanaokataa. Hebu fikiria wewe mwenyewe. Hapa kuna kajiharufu ka ujanja-ujanja.
Ligi niliyopo sio ya kulishwa propaganda....hoja yako ya kwanza na ya pili kuhusiana na Sultani na ASP respectively hazina mashiko....mfano hiyo ya Sultani CCM ndio wanaitumia sana kumponda Maalim...CUF wanachotaka ni kuona haki inatendekeka na kwamba mshindi haporwi ushindi wake kwa visingizio visivyo na kichwa wala miguu....

Hiyo unayoita 'mikakati ya UKAWA kuleta machafuko bara' ni sawa zile propaganda za CCM walivyokuwa wanasema 'Tanzania kutatokea machafuko na vita wapinzani wakishinda'....naona CCM wamehamishia huo upuuzi Zanzibar.....

Kuhusu uchaguzi kurudiwa, naona unapenda kuongelea hisia fulani ya kizushi kwamba labda kuna kitu CUF walikifanya kwenye uchaguzi ulioisha ndio maana hawataki kurudia uchaguzi......unarudi kulekule...hizo hoja za kisheria zina maana kwa sababu hii nchi inaendeshwa chini ya utawala wa Sheria....

Kifyatu bana, unanifurahisha....sio kwamba CCM wamekubali agizo la ZEC kuwa uchaguzi urudiwe, ila CCM ndio wamemuagiza Jecha kufuta uchaguzi na kupanga kuurudia.....Unawezaje kumtenganisha Jecha na CCM? mtu anayefuta uchaguzi mwenyewe bila kushirikisha wajumbe then CCM wanaunga mkono uamuzi huo......Hilo hata mtoto wa Form 4 anaelewa kwamba ni changa la macho, sasa wewe unazidiwa na mtoto wa Form 4 kuelewa jambo rahisi hivyo?....BTW unajua kwanini alichukua huo uamuzi peke yake?
Kama hutaki kutenganisha swala la muungano na matatizo ya uchaguzi katika kutafuta suluhu ya uchaguzi huu basi usini-tag unapoleta huo uzi wako. Sitakuwa na muda wa kuzuunguukia kitu hicho hicho mara nenda mara rudi.

JD, nilikustahi sana tulipokuwa tukijadili uchaguzi wa Lowassa na Magufuli na ndio maana sikukata kijeuri. Umeona nilivyokuwa sahihi katika maoni yangu juu ya raisi wa JMT.

Katika mjadala huu sitakuwa na simile hata kidogo na wewe. Ukileta yale mambo yalioniudhi awali nitakutaka kijeuri sana. Cha kwanza ni kuwa kama una swali basi aya moja au mbili zinatosha. Sitaki gazeti. Ukileta gazeti sitalijibu.

Nakupa onyo mapema.
Masuala ya uchaguzi na muungano hayapo tofauti, kama huna habari imekula kwako.....

Rais wako mstaafu alisema kero za muungano zitatuliwa na katiba mpya, hiyo inayoitwa 'katiba pendekezwa'....aliyeshinda Urais Zanzibar (Seif) ni muumini wa Serikali tatu (katiba ya wananchi) wala sio mbili kama CCM....

Kuna ishu ya Rais wa Zanzibar kuhudhuria vikao vya Baraza la mawaziri la JMT (katiba ya JMT 1977)...CCM wanaogopa Seif kuingia katika vikao hivyo.....

Kuna utata kuhusiana na mamlaka ya Rais wa JMT na Rais wa Zenji juu ya masuala ya Muungano.....

Uchaguzi wa bara ulishaingiwa na dosari kitambo toka poliCCM walivyowakamata wale jamaa waliokuwa wanajumlisha matokeo ya CDM, kwa kutumia sheria uchwara ya CCM ya mitandao....

Haukuwa sahihi kuhusu Rais wa JMT...nimezoea kuona mtu anasema maneno tofauti tofauti bila kuwa na kumbukumbu....

Unagopa kifyatu?...usiogope sikuchomi sindano......
 
Nimefuatilia huu uzi, nikichogundua ni kuwa huyu jamaa anayeitwa Kifyatu yupo shallow sana

Siasa za Zanzibar ni mchezo mchafu tokea uchaguzi wa 95

Ila mwaka huu Seif amewakamata vibaya ccm, amekataa kunyang'anywa ushindi wake

Ccm hawaandiki tena kanuni za mchezo, hata kwenye majadiliano CuF wanaonekana kuwa na msimamo uleule tofauti na miaka ya nyuma

CuF hawatakubali muafaka unaomrudisha Shein kuwa Rais wa Znz

CuF walikubali yaishe mwaka 2010 kwa kuunda SUK, mwaka huu ni zamu ya ccm

Rais wa Znz anaruhusiwa kikatiba kuhudhuria katika vikao vya baraza la mawaziri

CCM wanaogopa kuwa chama cha upinzani maana huo ndio mwanzo wa mwisho wake
Jack Daniel's Kifyatu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom