Mgogoro wa Zanzibar watinga Ikulu ya Marekani

Nimefuatilia huu uzi, nikichogundua ni kuwa huyu jamaa anayeitwa Kifyatu yupo shallow sana

Siasa za Zanzibar ni mchezo mchafu tokea uchaguzi wa 95

Ila mwaka huu Seif amewakamata vibaya ccm, amekataa kunyang'anywa ushindi wake

Ccm hawaandiki tena kanuni za mchezo, hata kwenye majadiliano CuF wanaonekana kuwa na msimamo uleule tofauti na miaka ya nyuma

CuF hawatakubali muafaka unaomrudisha Shein kuwa Rais wa Znz

CuF walikubali yaishe mwaka 2010 kwa kuunda SUK, mwaka huu ni zamu ya ccm

Rais wa Znz anaruhusiwa kikatiba kuhudhuria katika vikao vya baraza la mawaziri

CCM wanaogopa kuwa chama cha upinzani maana huo ndio mwanzo wa mwisho wake
Jack Daniel's Kifyatu

Ccm mtarimbo umewaganda,hawachomoki.
 
Last edited by a moderator:

Umeona lakini nilivyoshauri kitu kinachotokea sasa? Complete vindication. Muafaka uliofikiwa visiwani ni kuwa UCHAGUZI UNARUDIWA.

Wewe yero pamoja na Jack Daniel's huwa mna vichwa vigumu sana lakini kama mngekuwa mnasikiliza nasaha zangu mngeona kuwa siku zote niko sahihi. Mnakumbuka sakata letu la uchaguzi wa bara aliloanzisha JD - to his credit?

Muwe mnawasikiliza wazee wenu. Saa nyingine hawa wazee wanajua mengi kwa ajili ya kuona mengi.

Cheers.
 
Last edited by a moderator:
Wazanzibari waishio Marekani waliandamana mjini Washington mpaka White House ya MAREKANI, huku wakiwa na ujumbe kuwa kuwaomba Marekani na jumuiya zingine ziingilie kati kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi wa Zanzibar.

Licha ya hayo, pia katika nchi ya OMAN, raia walifurahi sana pale Maalim Seif alipoiomba Tume imtangaze mshindi wa Zanzibar.

Ikumbukwe Maalim Seif ameahidi kama atakuwa Rais wa Zanzibar basi baada ya siku 100 itageuka na kuwa Singapore.

Kama utakumbuka katika kipindi hiki cha miaka mitano akiwa kama MAKAMU WA RAIS aliweza kuinua zao la karafuu kutoka sh 300 hapo awali mpaka sasa ni sh 2500 kwa kilo.

Sitetei wala siungi mkono kinachoendelea Zanzibar ila haya ni mambo ya ndani sisi kama nchi huru tutatue matatizo yetu wenyewe
 
Umeona lakini nilivyoshauri kitu kinachotokea sasa? Complete vindication. Muafaka uliofikiwa visiwani ni kuwa UCHAGUZI UNARUDIWA.

Wewe yero pamoja na Jack Daniel's huwa mna vichwa vigumu sana lakini kama mngekuwa mnasikiliza nasaha zangu mngeona kuwa siku zote niko sahihi. Mnakumbuka sakata letu la uchaguzi wa bara aliloanzisha JD - to his credit?

Muwe mnawasikiliza wazee wenu. Saa nyingine hawa wazee wanajua mengi kwa ajili ya kuona mengi.

Cheers.

Huo muafaka wako ni ule wa Balozi Iddi ambao CUF wameshakanusha au mwingine?......

Wewe ulikuwa undecided voter, ulishakubali kumpigia kura Lowassa kabla hujabadilisha mawazo...lakini mda huo huo ulisema CDM wanashinda na kwamba CCM wanaogopa.....

Tatizo ulilionalo ni ukosefu wa kumbukumbu. yero alidhani ni uzee, mimi nadhani sio umri bali kushindwa kusimamia ukweli....unajua ukiwa muongo muongo huwezi kukumbuka uongo wako......

Wazee unaowazungumzia ni bora wasiwe wale waliopo CCM ambao hawana busara wala hekima.....
 
Wewe JD subiri tu kuhusu uchaguzi utaona, mbona kiherehere?

Nadhani yero ananifahamu vizuri sana. (The boy is smart ingawaje saa nyingine natamani nisafishe mdomo wake kwa sabuni ya magadi.) Ni kweli ni uzee!

Lakini kuhusu uchaguzi wa rais wa JMT, tofauti yangu na nyie wawili ilikuwa tayari mlikwisha fanya maamuzi kuhusu Lowassa.

Mimi kwa kitambo sana nilikuwa mpenzi wa CDM, lakini umeona ukomavu wangu wa fikra? UKAWA walipomuingiza Lowassa tu nilianza kunusa kaharufu kabaya. Na kama mnakumbuka ule mjadala wetu nilianza kwa kufikiria pengine Lowassa sio mbaya, mpaka mwishowe (kutokana na utafiti wangu binafsi) nikamtosa Lowassa na kuanza kumpigia debe Magufuli. Hicho ndio kitu kinachoitwa OBJECTIVITY. Huanzi na mtu na kumtafutia sifa za kumuuza bali unaanza na sifa unazozitafuta halafu unaangalia kama mtu anaewekwa ana vigezo. (Hawakukufundisha hii Law School?).
 
Unaaminije taarifa zilizokwishakanushwa?....

Mimi ni mmoja wa wale Mwl. Nyerere alizungumzia kuwa wanataka mabadiliko nje ya CCM.......

Tatizo la CCM ni mfumo.....Magufuli anatambua hili vizuri sana......

Hapa tunazungumzia uchaguzi wa Zenji...... wa Bara kila mwenye uelewa mpana anajua ulivyomalizika....

Wazenji wanahitaji kumuona Rais wao mpya Seif anaapishwa......
 
Subira, my learned brother, subira. Mambo ya Zanzibar ni poa sana, utaona.

Kuhusu siasa za bara:
Ningependa kuona CCM ikipumzishwa, na sio tu ili kuwapa fundisho bali hasa katika kujenga siasa nzuri za ushindani. Kama upinzani hawatakuja chukua dola watakomaaje? Lakini JD, msije mkafanya upuuzi mlioufanya mwaka huu tena. Mmeniudhi sana.

Na katika miaka ijayo msijefanya muungano kama UKAWA wakati wa uchaguzi. Utamifarakanisha na kuanza kugombana wenyewe kwa wenyewe na mwishowe CCM watashinda. Ushauri wa bure huu. Mimi sina chama.
 
mmoja wao ni wewe tehtehtehhhh
Heh heh heh kumbe muoga hivyo ,unaogopa sheria ya mtandao eh,watu husema msema kweli ni mpenzi wa Mungu usiogope Segerea ,ile imejengwa kwa ajili ya binadamu ingawa sio Sheraton
 
Subira, my learned brother, subira. Mambo ya Zanzibar ni poa sana, utaona.

Kuhusu siasa za bara:
Ningependa kuona CCM ikipumzishwa, na sio tu ili kuwapa fundisho bali hasa katika kujenga siasa nzuri za ushindani. Kama upinzani hawatakuja chukua dola watakomaaje? Lakini JD, msije mkafanya upuuzi mlioufanya mwaka huu tena. Mmeniudhi sana.

Na katika miaka ijayo msijefanya muungano kama UKAWA wakati wa uchaguzi. Utamifarakanisha na kuanza kugombana wenyewe kwa wenyewe na mwishowe CCM watashinda. Ushauri wa bure huu. Mimi sina chama.

Subira ya aina gani hiyo hadi serikali itishiwe kunyimwa misaada ndo ina-act, mwezi mzima walikuwa wapi.....

Hayo mambo unayosema "poa sana" wakati wazanzibar sio tu hawana Rais bali pia wawakilishi ni kujipa matumaini hewa......

Kila mtu anajua jinsi CCM walivyo wababe and jeuri.....mpaka hapa tulipo, kila kitu wamesababisha wao......

Ubabe an jeuri yao wamaeutumia hata kwenye uchaguzi wa JMT, siuiti uchaguzi wa Bara maana maajabu kura za wagombea urais wa JMT kutoka Zanzibar zimechukuliwa kuwa ni halali na zimejumlishwa.......

Wakati kura za Wazanzibari zinaonekana sio halali....target ya CCM ilikuwa ni kuchakachua kura za Seif..wagombea wengine wamekumbwa tu mswahiba ilhali hawakulengwa........

CCM inaniudhi jinsi ambavyo inaweka maslahi ya chama mbele kuliko maslahi ya Taifa, hivi hiki chama cha Nyerere kitajifunza lini ukomavu wa kisiasa?......kitajifunza lini kuheshimu maamuzi ya wananchi?....

Pengine wale jamaa wangeruhusiwa kujumlisha kura zao wakamaliza kama walivyopanga tusingekuwa na Magufuli kama Rais......Pengine kinachomfanya Magufuli atafute umaarufu ni ukweli kwamba hakushinda uchaguzi.......

Hicho kitu hakiwezi kusahaulika kwa kuzungumzia mchakato wa UKAWA kumpata mgombea wake wa Urais.....

Kinachoniudhi ni kwamba tuna demokrasia uchwara huku watu wazima wenye akili timamu wanaona kila kitu kiko "poa sana".....yote ni kwa sababu ya maslahi ya CCM .......
 
Wananchi tuna haki ya kujua kinachozungumzwa huko

Mazungumzo ya aina gani hayo ambayo uwakilishi wa CuF ni Sef peke yake

Suala la kurudia uchaguzi halitakiwi kupewa kipaumbele, huko ni kuturudisha nyuma kidemokrasia

Uchaguzi wa bara ulijaa magumashi sema Watanzania ni wavumilivu, pia viongozi wa UkAwA walitumia burasa

Suala la chama kupata mgombea wake sio ishu tena, kwani wanaCCM wengi tu walikerwa na namna ambavyo mgombea wao wa Urais alipatikana

Ishu muhimu ni kura za mgombea wa CDM zilizochakachuliwa kumbeba Magufuli, lakini sheria za Kidictator za CcM haziruhusu wagombea wa Urais kutafuta haki mahakamani

Ukitaka kujua kuwa uchaguzi wa Bara ulijaa mizengwe angalia idadi ya kesi zilizofunguliwa na wagombea za kutoridhishwa na matokeo

Wazanzibari wanahitaji kuona haki inatendeka hizo blah blah za CcM haziwasaidii wanzanzibari kuwapata wawakilishi wao pamoja na Rais waliyemchagua
 
Umeona lakini nilivyoshauri kitu kinachotokea sasa? Complete vindication. Muafaka uliofikiwa visiwani ni kuwa UCHAGUZI UNARUDIWA.

Wewe yero pamoja na Jack Daniel's huwa mna vichwa vigumu sana lakini kama mngekuwa mnasikiliza nasaha zangu mngeona kuwa siku zote niko sahihi. Mnakumbuka sakata letu la uchaguzi wa bara aliloanzisha JD - to his credit?

Muwe mnawasikiliza wazee wenu. Saa nyingine hawa wazee wanajua mengi kwa ajili ya kuona mengi.

Cheers.

Huo muafaka umeutoa wapi au umejitungia......

Unapimaje ugumu wa kichwa? Nec na Ccm wangeacha uwanja wa kuchezea uwe sawa (levelled) halafu ndo ungezungumza kuhusu nasaha zako.....

Ndio yaleyale ya kuamini kuwa wazee wana busara kuliko wengine wakati wazee wengi tu wanazidiwa busara na vijana....

Mda wa kusikiliza wazee ilikuwa enzi za Mwalimu......
 
Huo muafaka umetangaziwa wewe peke yako? Ungependa kuona uchaguzi unarudia lakini hutaki kujadili sababu za kuifuta in the first place

Unajua unaweza kufikiri mwenzako au wenzako wana vichwa vigumu kumbe wewe ndo mgumu kuelewa

Hizo nasaha zako zinaweza kumsaidia Seif kupewa ushindi wake? Kama haziwezi endelea kubaki nazo
 
Last edited by a moderator:
We kifyatu huna hoja ya msingi hapo.ivi nikuulize ni majadiliano gani yasiyofikia mwisho wakati ukweli upo wazi?cause kama ccm wanataka yaishe si warudi kwwenye fomu za matokeo waangalie kama kuna malalamiko yyte yalitolewa na wakala wao wa kila kituo ili yaonekane ni kweli uchaguzi ulikuwa na kasoro .bila ya hivyo hakuna maelewano zaidi
 
Subira ya aina gani hiyo hadi serikali itishiwe kunyimwa misaada ndo ina-act, mwezi mzima walikuwa wapi.....

Hayo mambo unayosema "poa sana" wakati wazanzibar sio tu hawana Rais bali pia wawakilishi ni kujipa matumaini hewa......

Kila mtu anajua jinsi CCM walivyo wababe and jeuri.....mpaka hapa tulipo, kila kitu wamesababisha wao......

Ubabe an jeuri yao wamaeutumia hata kwenye uchaguzi wa JMT, siuiti uchaguzi wa Bara maana maajabu kura za wagombea urais wa JMT kutoka Zanzibar zimechukuliwa kuwa ni halali na zimejumlishwa.......

Wakati kura za Wazanzibari zinaonekana sio halali....target ya CCM ilikuwa ni kuchakachua kura za Seif..wagombea wengine wamekumbwa tu mswahiba ilhali hawakulengwa........

CCM inaniudhi jinsi ambavyo inaweka maslahi ya chama mbele kuliko maslahi ya Taifa, hivi hiki chama cha Nyerere kitajifunza lini ukomavu wa kisiasa?......kitajifunza lini kuheshimu maamuzi ya wananchi?....

Pengine wale jamaa wangeruhusiwa kujumlisha kura zao wakamaliza kama walivyopanga tusingekuwa na Magufuli kama Rais......Pengine kinachomfanya Magufuli atafute umaarufu ni ukweli kwamba hakushinda uchaguzi.......

Hicho kitu hakiwezi kusahaulika kwa kuzungumzia mchakato wa UKAWA kumpata mgombea wake wa Urais.....

Kinachoniudhi ni kwamba tuna demokrasia uchwara huku watu wazima wenye akili timamu wanaona kila kitu kiko "poa sana".....yote ni kwa sababu ya maslahi ya CCM .......

Kutishiwa kwa serikali/misaada mimi nakukaribisha lakini sio kwa uchaguzi wa Zanzibar bali serikali/bunge iiangalie tena hii sheria ya mtandao. Mimi inanisumbua sana.

Kuhusu uchaguzi wa raisi wa JMT tusubiri sasa 2020. Kazi kuu ya upinzani ni kushinikiza ipatikane katiba inayoondoa kero za wananchi. Hii ni kazi yenu upinzani. Usije hapa kulialia tu, fanyeni kazi.

Seriously, hata kama upinzani wasipofanya kazi yoyote ile nyingine katika miaka 5 ijayo na wakashuhulikia katiba tu mpaka inyooke mimi nitasema watakuwa wamekidhi kiu ya wananchi. Kumbuka Magufuli (CCM) alipata 58% ya kura. Hii ina maana upinzani imebeba 42% ya nchi (karibia nusu) ambao wamesikia kilio chao. Kila mtu anajua mapungufu ya katiba ya 1977 na kama mtaweza kulitatua hili, you will be my heros. Msiwe mnasusia susia tu na kuzomea zomea. Wekeni vichwa chini mlishughulikie hili la katiba na wananchi watawakumbuka vizuri 2020 au 2025.
 
Wananchi tuna haki ya kujua kinachozungumzwa huko

Mazungumzo ya aina gani hayo ambayo uwakilishi wa CuF ni Sef peke yake

Suala la kurudia uchaguzi halitakiwi kupewa kipaumbele, huko ni kuturudisha nyuma kidemokrasia

Uchaguzi wa bara ulijaa magumashi sema Watanzania ni wavumilivu, pia viongozi wa UkAwA walitumia burasa

Suala la chama kupata mgombea wake sio ishu tena, kwani wanaCCM wengi tu walikerwa na namna ambavyo mgombea wao wa Urais alipatikana

Ishu muhimu ni kura za mgombea wa CDM zilizochakachuliwa kumbeba Magufuli, lakini sheria za Kidictator za CcM haziruhusu wagombea wa Urais kutafuta haki mahakamani

Ukitaka kujua kuwa uchaguzi wa Bara ulijaa mizengwe angalia idadi ya kesi zilizofunguliwa na wagombea za kutoridhishwa na matokeo

Wazanzibari wanahitaji kuona haki inatendeka hizo blah blah za CcM haziwasaidii wanzanzibari kuwapata wawakilishi wao pamoja na Rais waliyemchagua

Hili la Maalim kuwa peke yake mimi pia sikulifurahia san lakini natumai kutakuwa na wasuluhishi independent toka AU, UN, EU, nk.

yero, hapa tujikite na kukuna vichwa vyetu kuhusu huu uchaguzi wa Zanzibar. Uchaguzi wa bara umekwisha. Najua wewe hukuridhika na matokeo. Kazi ya kufanya sasa ni kupata katiba mpya inayotoa kero zote zilizojitokeza na sio kulalamikia tena uchaguzi uliopita.

Mimi bado nina imani na hawa wanaojadili suluhu ya hili tatizo la Zanzibar. Wewe una matakwa yako, mimi nina matakwa yangu, lakini nakusihu tuwe na subira.
 
Huo muafaka umeutoa wapi au umejitungia......

Unapimaje ugumu wa kichwa? Nec na Ccm wangeacha uwanja wa kuchezea uwe sawa (levelled) halafu ndo ungezungumza kuhusu nasaha zako.....

Ndio yaleyale ya kuamini kuwa wazee wana busara kuliko wengine wakati wazee wengi tu wanazidiwa busara na vijana....

Mda wa kusikiliza wazee ilikuwa enzi za Mwalimu......

Unajua JD, wakati wa utawala wa Mwalimu mimi na watu wengi sana tulikuwa tunamlaumu vibaya sana. Off course tulikuwa tunasemea chini chini, sio kama utandawazi wa siku hizi.

Angalia sasa. Kila mtu anasifu enzi ya Mwalimu. Wazee mtatudharau sana mpaka tukishaondoka ndio mnaangalia nyuma na kusema, "yule Kifyatu alikuwa na busara sana."

Najua jibu lako kwa sasa litakuwa, NEVER.
 
Huo muafaka umetangaziwa wewe peke yako? Ungependa kuona uchaguzi unarudia lakini hutaki kujadili sababu za kuifuta in the first place

Unajua unaweza kufikiri mwenzako au wenzako wana vichwa vigumu kumbe wewe ndo mgumu kuelewa

Hizo nasaha zako zinaweza kumsaidia Seif kupewa ushindi wake? Kama haziwezi endelea kubaki nazo

Subiri kijana wewe.
 
We kifyatu huna hoja ya msingi hapo.ivi nikuulize ni majadiliano gani yasiyofikia mwisho wakati ukweli upo wazi?cause kama ccm wanataka yaishe si warudi kwwenye fomu za matokeo waangalie kama kuna malalamiko yyte yalitolewa na wakala wao wa kila kituo ili yaonekane ni kweli uchaguzi ulikuwa na kasoro .bila ya hivyo hakuna maelewano zaidi

Hawarudi kwenye fomu za matokeo kwa sababu Sheikh Jecha ameona madudu wakati wa uchaguzi. Mimi simtetei Jecha lakini naweka imani yangu kwa hawa wakubwa anaokutana. Nategemea watatuletea ufumbuzi wa hili tatizo.

Subiri mkuu.
 
Kutishiwa kwa serikali/misaada mimi nakukaribisha lakini sio kwa uchaguzi wa Zanzibar bali serikali/bunge iiangalie tena hii sheria ya mtandao. Mimi inanisumbua sana.

Kuhusu uchaguzi wa raisi wa JMT tusubiri sasa 2020. Kazi kuu ya upinzani ni kushinikiza ipatikane katiba inayoondoa kero za wananchi. Hii ni kazi yenu upinzani. Usije hapa kulialia tu, fanyeni kazi.

Seriously, hata kama upinzani wasipofanya kazi yoyote ile nyingine katika miaka 5 ijayo na wakashuhulikia katiba tu mpaka inyooke mimi nitasema watakuwa wamekidhi kiu ya wananchi. Kumbuka Magufuli (CCM) alipata 58% ya kura. Hii ina maana upinzani imebeba 42% ya nchi (karibia nusu) ambao wamesikia kilio chao. Kila mtu anajua mapungufu ya katiba ya 1977 na kama mtaweza kulitatua hili, you will be my heros. Msiwe mnasusia susia tu na kuzomea zomea. Wekeni vichwa chini mlishughulikie hili la katiba na wananchi watawakumbuka vizuri 2020 au 2025.

Hiyo sheria ya mtandao imeanza kukusumbua lini?.....wewe binafsi unadhani ina matatizo gani?....

Umesahau maana ya UKAWA?....waliopitisha hiyo wanayoita "katiba pendekezwa" ni nani kama sio CCM.....

Suala la katiba sio la upinzani tu kama unavyofikiri, wabunge wengi ni CCM na kinachowasumbua ni kuweka maslahi ya CCM mbele na ya Taifa nyuma......

Washauri wabunge wa CCM wakubali kuanza mchakato wa katiba mpya na sio kuwa na fikra mgando kuwa katiba mpya ni kwa faida ya wapinzani.....

Waachane na tabia ya kuweka vipengele katika katiba kwa kudhani CCM itatawala milele....angalia kinachowakuta Zanzibar sasa hivi wanaogopa Seif kuingia kwenye vikao vya BLW......

Kuzomea na kususia ni kutuma ujumbe kuwa viongozi wa juu serikalini washughulikie matatizo ya msingi haraka na sio kutumia mda mwingi kuzurura na kutalii maofisini.....
 
Back
Top Bottom