Nani kawashikia waZanzibari mtutu kichwani kuwa uchaguzi ukirudiwa leo wasipige kura walivyofanya awali?
Mimi sijui sheria na
KATIBA ya Zanzibar lakini nijuavyo mimi ni kuwa tume ya uchaguzi,
ZEC, imesema imeona madudu kwenye uchaguzi uliopita na imetaka uchaguzi urudiwe.
Kwa sasa hivi pande zote zenye malalamiko ziko kwenye majadiliano ya usuluhishi. Hili la kuzungumzia majeshi ya kivamizi ya Tanganyika ni upuuzi mtupu. Yaani waZanzibari mnajisikia mpo karibu zaidi na Oman kuliko Tanganyika? - Eti raia wa Oman walifurahi sana!
- Leo watu wanakwenda ikulu ya Marekani kuandamana ili Marekani iifanye nini Tanzania?
- Je, mazungumzo ya usuluhishi yameshindikana kutatua hili tatizo?
- Marekani ni nani katika muundo na Katiba ya serikali ya Zanzibar?
- Ni kipi tusichoweza kukizungumza na kuelewana katika lugha yetu ya Kiswahili mpaka tuwaite waMarekani?
- Kwa nini tusiwaite Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Ghana badala ya Marekani na Uingereza?
- Hiki kiherehere cha kukimbilia nchi za magharibi chanzo chake ni kipi?
Nina maswali mengi najiuliza kwa hili na nakosa majibu. Matatizo tunayo - ndio, lakini hivi hatuwezi kukaa na kupata suluhu sisi wenyewe mpaka tukimbilie kwa "mabwana" zetu huko ulaya? This is pathetic.