Mgogoro wa Zanzibar watinga Ikulu ya Marekani

Unajua JD, wakati wa utawala wa Mwalimu mimi na watu wengi sana tulikuwa tunamlaumu vibaya sana. Off course tulikuwa tunasemea chini chini, sio kama utandawazi wa siku hizi.

Angalia sasa. Kila mtu anasifu enzi ya Mwalimu. Wazee mtatudharau sana mpaka tukishaondoka ndio mnaangalia nyuma na kusema, "yule Kifyatu alikuwa na busara sana."

Najua jibu lako kwa sasa litakuwa, NEVER.

Nyerere alikuwa na mazuri yake lakini yeye ndiye chanzo cha kumfanya Rais wa JMT kuwa na mamlaka kupita kiasi.....lakini pia katiba kandamizi na mbovu alizidumisha yeye......

Uoga ni dhambi mbaya sana ambayo serikali ya CCM ilikuwa inawafundisha wananchi wake toka enzi za Mwalimu....Leo hii tunaambiwa wapinzani watageuza TZ kuwa kama Iraq, Libya, Misri na watu wazima wanashangilia.....
 
Hili la Maalim kuwa peke yake mimi pia sikulifurahia san lakini natumai kutakuwa na wasuluhishi independent toka AU, UN, EU, nk.

yero, hapa tujikite na kukuna vichwa vyetu kuhusu huu uchaguzi wa Zanzibar. Uchaguzi wa bara umekwisha. Najua wewe hukuridhika na matokeo. Kazi ya kufanya sasa ni kupata katiba mpya inayotoa kero zote zilizojitokeza na sio kulalamikia tena uchaguzi uliopita.

Mimi bado nina imani na hawa wanaojadili suluhu ya hili tatizo la Zanzibar. Wewe una matakwa yako, mimi nina matakwa yangu, lakini nakusihu tuwe na subira.
Hao wanaojadili wanajua fika kuwa hamna uchaguzi unaorudiwa

Ni jambo la aibu kwa taifa wala sio sifa kuwa AU, UN, EU wanasadia kutatua suala liliosababishwa na CcM kwenye kisiwa chenye wapiga kura Laki tano (500 thousand)

Wewe umekaa hapo unasubiri wengine watatue ugomvi wenu wa kipuuzi pamoja na kuwawashauri cha kufanya. Ni sawa na mtu anayetega bomu nyumbani kwake halafu anaita majirani waje wakune vichwa kumsaidia kulitegua kabla halijalipuka. Huo ni upimbi

Wapinzani wakisema nchii hii inahitaji katiba mpya maCcm yalivyo mambumbumbu yanaona wanapiga kelele bila kufikiria nje ya box la kijani na njano walimojifungia
 
Subiri kijana wewe.
Kwani lazima CcM ndo itawale Zanzibar? Au ndo zile hadithi kuwa wengine tofauti na CcM wakitawala amani na usalama unatoweka

Serikali ya CcM iache kuwafanya wazanzibari kama hawana akili
 
Sasa ikiwa hawataki kufata chanzo cha ushahidi unadhani wanania kweli ya kupata ufumbuzi wa tatizo?kimtazamo wangu ni ccm hawapo tayari kuitoa serikali kwa amani.naaamini wanachotafuta ipo siku watakipata
 
Hiyo sheria ya mtandao imeanza kukusumbua lini?.....wewe binafsi unadhani ina matatizo gani?....

Umesahau maana ya UKAWA?....waliopitisha hiyo wanayoita "katiba pendekezwa" ni nani kama sio CCM.....

Suala la katiba sio la upinzani tu kama unavyofikiri, wabunge wengi ni CCM na kinachowasumbua ni kuweka maslahi ya CCM mbele na ya Taifa nyuma......

Washauri wabunge wa CCM wakubali kuanza mchakato wa katiba mpya na sio kuwa na fikra mgando kuwa katiba mpya ni kwa faida ya wapinzani.....

Waachane na tabia ya kuweka vipengele katika katiba kwa kudhani CCM itatawala milele....angalia kinachowakuta Zanzibar sasa hivi wanaogopa Seif kuingia kwenye vikao vya BLW......

Kuzomea na kususia ni kutuma ujumbe kuwa viongozi wa juu serikalini washughulikie matatizo ya msingi haraka na sio kutumia mda mwingi kuzurura na kutalii maofisini.....

Sheria ya mtandao niliipigia kelele kabla haijapitishwa. Mimi ni researcher, kuniambia kuwa siwezi kupublish matokeo yangu mpaka nipate kibali kuhusu takwimu zangu kutoka serikalini ni kuwanyima uhuru scholars. Kama takwimu na maoni yangu yana mushkeli basi peers wangu watanilima na nitakufa scholastically kama nikiendelea na upuuzi huo. Sihitaji serikali inisimamie kwenye kitu ambacho pengine mimi pekee kama mtafiti ndie ninaekijua kiundani.

Pia, katika kipindi kifupi sana tumeona sheria hii inavyoweza kutumiwa vibaya na watawala na ikawa ya ukandamizaji. For God's sake watu humu JF wanakuwa waoga kutoa maoni yao wakichelea kuvunja sheria ya mtandao. Utapataje GREAT THINKERS kama unawatia watu gundi mdomoni? This is a regressive and not a progressive law.

UKAWA walisimamia katiba bora lakini sijui wana akili gani. Walitoka bungeni na kuzira na matokeo yake CCM waliendelea na mchakato wa katiba. Sasa eti unaniuliza maana ya UKAWA... Ndio, naifahamu maana ya UKAWA kuwa ni kuzira, kususia, kuzomea, na kelele tu. Elekezeni nguvu zenu kutatua matatizo na sio kutaka kupata umaarufu tu mnapoonekana kwenye runinga. Wabunge wa UKAWA wamekuwa wasanii wakitafuta sifa kwa wananchi wakati mambo ya muhimu wanayaacha yanaharibika. Ningefurahi katika bunge hili la 11 wangeacha kutangaza kwenye runinga hivi vikao vya bunge ili UKAWA watulie na wafanye kazi.

Usiniambie niwashauri wabunge wa CCM wafanye hiki au kile. Hiyo ndio kazi ya upinzani. Nilikwishasema awali kuwa ili Tanzania tusonge mbele tunahitaji upinzani mahiri. Hii ndio kazi yenu wapinzani. Wahamasisheni wananchi kulishinikiza bunge lilete katiba bora. Mnaweza kuanza kwa kusukuma ajenda ya kuwa mchakato mzima wa katiba uanze upya tena. Do your job guys.
 
Nyerere alikuwa na mazuri yake lakini yeye ndiye chanzo cha kumfanya Rais wa JMT kuwa na mamlaka kupita kiasi.....lakini pia katiba kandamizi na mbovu alizidumisha yeye......

Uoga ni dhambi mbaya sana ambayo serikali ya CCM ilikuwa inawafundisha wananchi wake toka enzi za Mwalimu....Leo hii tunaambiwa wapinzani watageuza TZ kuwa kama Iraq, Libya, Misri na watu wazima wanashangilia.....

Hapa hutapata ubishi wowote ule toka kwangu.
 
Heh heh heh kumbe muoga hivyo ,unaogopa sheria ya mtandao eh,watu husema msema kweli ni mpenzi wa Mungu usiogope Segerea ,ile imejengwa kwa ajili ya binadamu ingawa sio Sheraton

mbona umeanza kubabaika , ndio nyinyi mliopelekwa nje unamdanganya nani humu , mbona hujakataa
 
Hao wanaojadili wanajua fika kuwa hamna uchaguzi unaorudiwa

Ni jambo la aibu kwa taifa wala sio sifa kuwa AU, UN, EU wanasadia kutatua suala liliosababishwa na CcM kwenye kisiwa chenye wapiga kura Laki tano (500 thousand)

Wewe umekaa hapo unasubiri wengine watatue ugomvi wenu wa kipuuzi pamoja na kuwawashauri cha kufanya. Ni sawa na mtu anayetega bomu nyumbani kwake halafu anaita majirani waje wakune vichwa kumsaidia kulitegua kabla halijalipuka. Huo ni upimbi

Wapinzani wakisema nchii hii inahitaji katiba mpya maCcm yalivyo mambumbumbu yanaona wanapiga kelele bila kufikiria nje ya box la kijani na njano walimojifungia

Misimamo mikali kama huu wako ndio utakaotupoteza. Ndio maana wanaojadili ni wazee wenye busara na sio vijana kama wewe - mtaharibu. Kurudiwa uchaguzi au la ndio kinachojadiliwa. Tusubiri maamuzi.

Mimi ningekaribishwa nikatoe ushauri (haitatokea kamwe) ningetoa mchango wangu. Lakini kukaa huku nje na kuanza kusema wafanye hiki au kile ni kupoteza muda tu. Ni sawasawa na kukaa jukwaani kwenye mpira na kupiga kelele "wewe mkabe huyo, aaaah mbona umelikosa bao la wazi hilooo". Hali hii inaweza kukufarijisha lakini haitashinda mechi. Wacha wachezaji, refa na wapambe wake wasimamie mchezo. Kipenga cha mwisho kikipigwa tutaangalia matokeo.
 
Kwani lazima CcM ndo itawale Zanzibar? Au ndo zile hadithi kuwa wengine tofauti na CcM wakitawala amani na usalama unatoweka

Serikali ya CcM iache kuwafanya wazanzibari kama hawana akili

Mimi sipingani na wewe hapa yero. Ningependa sana CUF wangeshinda (kwa vyovyote vile CUF wameibeba Pemba yote). Ni muhimu upinzani nao uje ushike dola na CCM wawe wapinzani. Lakini tufanye hivi kwa taratibu nzuri na usalama. ZEC wamesema kuna vipengele vilivyokiukwa kwenye uchaguzi. Sasa kama hii ni kweli au sio mimi sijui. Ndio maana naweka matumaini yangu makubwa katika hili jopo linalojadili huu uchaguzi.
 
Sasa ikiwa hawataki kufata chanzo cha ushahidi unadhani wanania kweli ya kupata ufumbuzi wa tatizo?kimtazamo wangu ni ccm hawapo tayari kuitoa serikali kwa amani.naaamini wanachotafuta ipo siku watakipata

Mimi sijui uamuzi wa mwisho utakuwa nini lakini mkuu, nashindwa kuelewa kwa nini CUF hawataki uchaguzi urudiwe.

- CUF wanasema uchaguzi ulikuwa huru na wanataka matokeo yatangazwe.
- CCM wanasema kuna kamchezo kachafu kalichezwa na wanataka uchaguzi urudiwe.

Sasa sijui ukweli uko wapi na ndio maana nasubiri maamuzi ya hawa wasuluhishi.

Lakini kama ukiniuliza mimi maoni yangu ni kuwa:
1. Kama matokeo yakitangazwa kufuatia matakwa ya CUF ni kuwa mmepuuzia malalamishi ya CCM.
2. Kama uchaguzi ukirudiwa (na hasa kama ukisimamiwa na watu wengine na sio ZEC) basi tutaondoa huu utata.

Kosa langu ni lipi hapa?
 
Kosa lako ni kuamini malalamiko ya ccm na ukaacha ushahidi wa fomu za matokeo
 
Kwa hiyo wewe unapata habari wapi ? Wamarekani wenyewe wanategemea hizo media, itakuwa wewe uliyetembelea nchi yao ! Una waandishi wako binafsi wewe ? Una access na classfied information za Marekani kama alivyo Obama ? Hata Obama mwenye source nyingi za information za Marekani bado na yeye anategemea hizi media ! Itakuwa wewe ambaye ambaye umekaribishwa Marekani !??

Eti sikuwezi ! Nani amekwambia nashindana na wewe ?

By the way habari ni habari, analysis ya habari ndio inategemea itikadi na mtazamo wa media husika.....kilichotokea Florida ni habari iliyokuwa wazi hivyo media zote, CNN, BBC, Fox News, Aljazeera, Press Tv ya Iran CCTV ya Uchina zote zilireport facts kama ilivyotokea ila kwenye analysis inawezekana walitofautiana ila kwenye habari ni hiyo hiyo.....

Sasa mkuu mbona tunarukia udadavuzi wa siasa za Wamarekani? Waache wajadili yao na sisi tugange yetu.

Tuna zigo kubwa liko mbele yetu tulitatue hilo kwanza. Hili ndio linalotuhusu - tuelekeze nguvu zetu huko.

Ukitaka kuniingiza kwenye maswala ya marekani utapwelea kwani mimi sitegemei habari kutoka hivi vyombo vinavyoitwa "main-stream media" kama CNN, FOX, BBC, nk. Eti FOX News? Wewe unachekesha sana. Kama ndiko unakoaminia kutapa taarifa zako basi wala usinisumbue. Huniwezi.
 
Sheria ya mtandao niliipigia kelele kabla haijapitishwa. Mimi ni researcher, kuniambia kuwa siwezi kupublish matokeo yangu mpaka nipate kibali kuhusu takwimu zangu kutoka serikalini ni kuwanyima uhuru scholars. Kama takwimu na maoni yangu yana mushkeli basi peers wangu watanilima na nitakufa scholastically kama nikiendelea na upuuzi huo. Sihitaji serikali inisimamie kwenye kitu ambacho pengine mimi pekee kama mtafiti ndie ninaekijua kiundani.

Sijakuuliza kuhusiana na Sheria ya Takwimu.....anyway maelezo mazuri...
Pia, katika kipindi kifupi sana tumeona sheria hii inavyoweza kutumiwa vibaya na watawala na ikawa ya ukandamizaji. For God's sake watu humu JF wanakuwa waoga kutoa maoni yao wakichelea kuvunja sheria ya mtandao. Utapataje GREAT THINKERS kama unawatia watu gundi mdomoni? This is a regressive and not a progressive law.

Good. Nadhani pia unamaanisha imetumika vibaya kwenye uchaguzi wa mwaka huu......
UKAWA walisimamia katiba bora lakini sijui wana akili gani. Walitoka bungeni na kuzira na matokeo yake CCM waliendelea na mchakato wa katiba. Sasa eti unaniuliza maana ya UKAWA... Ndio, naifahamu maana ya UKAWA kuwa ni kuzira, kususia, kuzomea, na kelele tu. Elekezeni nguvu zenu kutatua matatizo na sio kutaka kupata umaarufu tu mnapoonekana kwenye runinga. Wabunge wa UKAWA wamekuwa wasanii wakitafuta sifa kwa wananchi wakati mambo ya muhimu wanayaacha yanaharibika. Ningefurahi katika bunge hili la 11 wangeacha kutangaza kwenye runinga hivi vikao vya bunge ili UKAWA watulie na wafanye kazi.
Nina wasiwasi kama ulifuatilia BMK...

Hivi huwa unafuatilia Bunge, maana kila mtu anajua kuwa wabunge wa Ukawa ndiyo wanaofanya kazi...hata Spika mstaafu A. Makinda anatambua hilo......

Kabla hujafikiria kuhusu matangazo ya bunge kutooneshwa kwenye TV, ungejiuliza ni kwanini yalianza kuoneshwa kwenye TV.......usiwe tu mropokaji.....
Usiniambie niwashauri wabunge wa CCM wafanye hiki au kile. Hiyo ndio kazi ya upinzani. Nilikwishasema awali kuwa ili Tanzania tusonge mbele tunahitaji upinzani mahiri. Hii ndio kazi yenu wapinzani. Wahamasisheni wananchi kulishinikiza bunge lilete katiba bora. Mnaweza kuanza kwa kusukuma ajenda ya kuwa mchakato mzima wa katiba uanze upya tena. Do your job guys.
Kwahiyo wewe unatoa ushauri kwa wabunge wa upinzani tu....wabunge wa CCM huwezi kuwashauri?.....

Bunge zima linafanya kazi ya kushauri serikali, kutunga sheria na kuwakilisha wananchi.....sio wapinzani tu....

CCM wasipokuwa na nia ya dhati ya kuleta katiba mpya, jitihada za wapinzani haziwezi kufanikiwa maana hawafanyi hiyo kazi peke yao....mbona huelewi kitu rahisi hivi

Unajua kwanini 'katiba pendekezwa' ilipotelea njiani?......
 
Mimi sijui uamuzi wa mwisho utakuwa nini lakini mkuu, nashindwa kuelewa kwa nini CUF hawataki uchaguzi urudiwe.

- CUF wanasema uchaguzi ulikuwa huru na wanataka matokeo yatangazwe.
- CCM wanasema kuna kamchezo kachafu kalichezwa na wanataka uchaguzi urudiwe.

Sasa sijui ukweli uko wapi na ndio maana nasubiri maamuzi ya hawa wasuluhishi.

Lakini kama ukiniuliza mimi maoni yangu ni kuwa:
1. Kama matokeo yakitangazwa kufuatia matakwa ya CUF ni kuwa mmepuuzia malalamishi ya CCM.
2. Kama uchaguzi ukirudiwa (na hasa kama ukisimamiwa na watu wengine na sio ZEC) basi tutaondoa huu utata.

Kosa langu ni lipi hapa?

Ni lini CCM walilalamikia uchaguzi wa Zanzibar? Walimlalamikia nani? Jibu haya maswali please.....

Au unamaanisha Jecha alivyozungumza upuuzi wake alifanya hivyo kwa niaba ya CCM?......

Sio CUF wanasema uchaguzi ulikuwa huru, maana ukisema CUF mtu anaweza kufikiri ni "biased".....waangalizi wote wa ndani na wa nje wanasema uchaguzi ulienda vizuri......

Kama huo utata ulijulikana, kwanini asingechaguliwa msimamizi mwingine kutoka nje kabla ya uchaguzi kuanza.....jibu ni kwamba hamna utata, hamna haja ya kurudia uchaguzi.....

Aibu ya mwaka ni kwamba mmefungwa wakati refa ni wa kwenu......
 
Mimi sipingani na wewe hapa yero. Ningependa sana CUF wangeshinda (kwa vyovyote vile CUF wameibeba Pemba yote). Ni muhimu upinzani nao uje ushike dola na CCM wawe wapinzani. Lakini tufanye hivi kwa taratibu nzuri na usalama. ZEC wamesema kuna vipengele vilivyokiukwa kwenye uchaguzi. Sasa kama hii ni kweli au sio mimi sijui. Ndio maana naweka matumaini yangu makubwa katika hili jopo linalojadili huu uchaguzi.
Kabla hujaweka matumaini yako kwenye hilo jopo, wewe kama mtu unayetumia akili zako mwenyewe kufikiri, ulipaswa kwanza kujiridhisha kama hayo yanayosemwa na ZEC ni ya kweli au sio ya kweli
 
Misimamo mikali kama huu wako ndio utakaotupoteza. Ndio maana wanaojadili ni wazee wenye busara na sio vijana kama wewe - mtaharibu. Kurudiwa uchaguzi au la ndio kinachojadiliwa. Tusubiri maamuzi.

Mimi ningekaribishwa nikatoe ushauri (haitatokea kamwe) ningetoa mchango wangu. Lakini kukaa huku nje na kuanza kusema wafanye hiki au kile ni kupoteza muda tu. Ni sawasawa na kukaa jukwaani kwenye mpira na kupiga kelele "wewe mkabe huyo, aaaah mbona umelikosa bao la wazi hilooo". Hali hii inaweza kukufarijisha lakini haitashinda mechi. Wacha wachezaji, refa na wapambe wake wasimamie mchezo. Kipenga cha mwisho kikipigwa tutaangalia matokeo.

Hao watu waendelee kujadili hicho kiini macho cha CcM, sisi huku tunasuport msimamo wa CuF na tunawakumbusha CuF kwamba wasifanye kosa kuruhusu huo uchaguzi urudiwe

Hatupotezi mda bali sisi kama mashabiki, wafuasi, wapenzi na wanachama, tunawaonyesha CuF kwamba tupo pamoja nao katika kudai haki yao inayotaka kuporwa na CcM

Wazanzibari sio watoto wadogo, tunawakumbusha CuF kuwa kwa vyovyote vile hatutakubaliana na uamuzi wa kurudia uchaguzi, matokeo yaendelee kutangazwa bado majimbo 24

Kama uchaguzi wa Zanzibar unarudiwa basi na wa Bara urudiwe maana angalau huku Lowassa alipeleka malalamiko yake NEC
 
Kwa hiyo wewe unapata habari wapi ? Wamarekani wenyewe wanategemea hizo media, itakuwa wewe uliyetembelea nchi yao ! Una waandishi wako binafsi wewe ? Una access na classfied information za Marekani kama alivyo Obama ? Hata Obama mwenye source nyingi za information za Marekani bado na yeye anategemea hizi media ! Itakuwa wewe ambaye ambaye umekaribishwa Marekani !??

Eti sikuwezi ! Nani amekwambia nashindana na wewe ?

By the way habari ni habari, analysis ya habari ndio inategemea itikadi na mtazamo wa media husika.....kilichotokea Florida ni habari iliyokuwa wazi hivyo media zote, CNN, BBC, Fox News, Aljazeera, Press Tv ya Iran CCTV ya Uchina zote zilireport facts kama ilivyotokea ila kwenye analysis inawezekana walitofautiana ila kwenye habari ni hiyo hiyo.....

Maana kama hauna waaandishi wako binafsi, access nyingine yeyote hata sisi tunayo ! Unless uniambie una access ya classified informtion za Marekani kama aliyokuwa nayo Obama......

Ndio, waMarekani wanapata habari zao kupitia vyombo hivyo vya habari na ndio maana hawajui chochote kuhusu nchi yao au za nje.

Hizi TV na magazeti makuu ya Marekani yanamilikiwa na mashirika makuu (corporate media) machache. Kutokana na fedha zao hawa ndio wanaowachagulia wananchi viongozi wao (lobbyists, super-pac, n.k.). Wabunge wa Marekani hawawakilishi wananchi wao bali wanawakilisha mashirika yaliowadhamini wakati wa uchaguzi. Taarifa zote za habari zinachujwa ili kuwapa wasikilizaji kile wanachotaka wakijue, na mara nyingi huo pia ndio msimamo wa serikali.

Kwa mfano ukitaka kujua ukweli kuhusu Israeli na Palestina, usikilize CNN, FOX, NBC, MSNBC nk. Ni vema wende ukasome magazeti ya Israel (kama Haaretz), au ukasikilize TV za Iran (kama Press TV) au kasome/kasikilize habari toka urusi (kama RT).

Kwa uchambuzi wa mambo ya dunia unaweza pia kusikiliza mihadhara (YouTube) ya watu kama Prof. Noam Chomsky, Illan Pappe (na wengineo) au kusoma habari mtandaoni kama Havard-Belfer Center, au New Eastern Journal.

Ukizoea kusoma New York Times, Washington Post, nk. hutapata undani wa mambo ya Marekani kwa sababu haya magazeti na TV viko karibu sana na serikali na haviwezi kutoa undani, na mara nyingi vinatumiwa kusambaza sera au propaganda za serikali.

Aljazera ilipokuwa independent ilikuwa inatoa habari nzuri mpaka Marekani wakawalalamikia. Sasa hivi ni sehemu ya main-stream media hapa Marekani na haina tofauti yoyote na CNN.

Press Tv bado imeimarisha objectivity yake kuhusu mataifa ya magharibi lakini ukitaka kujua undani wa Iran soma magazeti ya Israel.

CCTV ya Uchina imekaa kimaslahi sana. Hawataki kumuudhi mtu yeyote kwa habari zao. Na hasa sasa wana soko kubwa Marekani usitegemee critical analysis kutoka kwao.

Ninachokisema ni kuwa, kwa habari nzuri kuhusu Marekani, usisikilize maoni ya TV wala ya magazeti ya Marekani.

Mimi ni mTanzania (kila uchaguzi narudi nyumbani kuchagua) lakini ni mkazi wa Marekani kwa zaidi ya miaka 35 sasa. Ninapokuambia usitegemee kujua undani wa Marekani kwa kusikiliza CNN sifanyi mas-hara.

Kama unataka kusikia habari za kawaida kama, ajali, mafuriko, waliouana kwa risasi, au machafuko barani Afrika, basi CNN inatosha. Kwa mengine yote nenda kwengine.

Ni vizuri ujenge utamaduni wa kupata habari zako kutoka pande nyingi hasa zinazokinzana. Ukisoma nusu-uongo hapa na nusu-uongo kule utajua ukweli uko wapi.

Nimesema huniwezi kwa sababu mwenzio nina vyanzo vingi sana vya habari wakati wewe ukisikiliza CNN na FOX. Kama unataka tulumbane na mimi itabidi ufanye homework yako kwanza ya kupata ukweli uko wapi. Usiisikilize kabisa Fox News. Hii ni tabloid TV ya chama kimoja hapa marekani na wao ni uongo na udaku mtupu.
 
Mimi sijui uamuzi wa mwisho utakuwa nini lakini mkuu, nashindwa kuelewa kwa nini CUF hawataki uchaguzi urudiwe.

- CUF wanasema uchaguzi ulikuwa huru na wanataka matokeo yatangazwe.
- CCM wanasema kuna kamchezo kachafu kalichezwa na wanataka uchaguzi urudiwe.

Sasa sijui ukweli uko wapi na ndio maana nasubiri maamuzi ya hawa wasuluhishi.

Lakini kama ukiniuliza mimi maoni yangu ni kuwa:
1. Kama matokeo yakitangazwa kufuatia matakwa ya CUF ni kuwa mmepuuzia malalamishi ya CCM.
2. Kama uchaguzi ukirudiwa (na hasa kama ukisimamiwa na watu wengine na sio ZEC) basi tutaondoa huu utata.

Kosa langu ni lipi hapa?

Kulalamikiwa uchaguzi kupo popote hata huku Bara.Kama kuna mtu au chama hakijaridhika na Matokeo kiende Mahakamani.Ndivyo alivyofanya hata Kafulila.Kama ni upande wa Rais matokeo yatangazwe ambaye anahisi kudhulumika atalalamika kwenye vyombo vya habari.Ndivyo alivyofanya hata Lowasa.Cha msingi matokeo yatangazwe watu wasonge mbele.
 
Kwa kifupi hoja zako zinatetea kile kile ninachokisema !

Issue ni kwamba hizo sources zote ulizozitaja yeyote anaweza kuzi-access na hiyo ndio hoja yangu tangu mwanzo kwamba kwa wewe kuwa Marekani (katika age hii ya utandawazi) hakukupi advantage ya kupata taarifa za Marekani zaidi ya mtu mwingine aliyepo sehemu nyingine as long as huyo mtu ana interest na muda wa kufuatilia hizo taarifa. hivyo hakuna mtu mwenye advantage ya information kutokana na location yake........Kwa mfano, kwa mimi, miaka ya mwishoni mwa 90 na mwanzoni mwa 2000 nilikuwa na interests sana na habari za Israel na nilikuwa nasoma Haaretz na Jerusalem post kuliko hata nilivyokuwa ninasoma magazeti ya Bongo. Press Tv nayo nilikuwa naiangalia sana miaka ya 2010, 2011, 2012 ingawa kwa mtazamo wangu mimi wana propaganda za wazi kabisa na tena mara nyingine ni za kipuuzi. Sasa hivi siiangalii sana Press Tv, ingawa mara chache huwa navist website yao na kuna wakati hata nachangia mijadala kwenye hiyo website.......FOX News (especially kipindi kinachoitwa "The FiVe") naangalia mara nyingi ikiwa ni pamoja na Aljazeera na BBC News. CNN huwa naangalia mara chache........

Vile vile kwa mtu yeyote ambaye haziangalii moja kwa moja, anaweza akavisit websites zao wakati wowote akasoma na kuangalia video za habari na analysis mbali mbali......Youtube ipo wazi kwa yeyote aliye na muda na interest..............

Kwa kifupi, vyanzo vyote vya habari ulivyovitaja, mimi au yeyote anaweza aka-viaccess wakati wowote 24/7.....sasa unawezaje kujiona wewe ni zaidi wakati hizo access kila mtu (whether yupo US, Europe or Africa) anazo ?

Back
Top Bottom