Mgogoro wa Zanzibar watinga Ikulu ya Marekani

Mgogoro wa Zanzibar watinga Ikulu ya Marekani

Freedom tommorrow

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2015
Posts
1,795
Reaction score
1,132
Wazanzibari waishio Marekani waliandamana mjini Washington mpaka White House ya MAREKANI, huku wakiwa na ujumbe kuwa kuwaomba Marekani na jumuiya zingine ziingilie kati kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi wa Zanzibar.

Licha ya hayo, pia katika nchi ya OMAN, raia walifurahi sana pale Maalim Seif alipoiomba Tume imtangaze mshindi wa Zanzibar.

Ikumbukwe Maalim Seif ameahidi kama atakuwa Rais wa Zanzibar basi baada ya siku 100 itageuka na kuwa Singapore.

Kama utakumbuka katika kipindi hiki cha miaka mitano akiwa kama MAKAMU WA RAIS aliweza kuinua zao la karafuu kutoka sh 300 hapo awali mpaka sasa ni sh 2500 kwa kilo.

Attachments

  • zanzibar.jpg
    zanzibar.jpg
    31.6 KB · Views: 3,602
Hapo ndio tutaona usiriasi wa mmarekani na jinsi anavyo iheshimu demomrasia.

Mara nyingi tumezoea kumsikia Mmarekani akitetea haki za mashoga zaidi hadi inafikia hatua kuziwekea vikwazo baadhi ya nchi kisa zimekataa ushoga na wakati huo amesahau maswala ya msingi kama demokrasia na inabidi Obama ajue umuhimu wa demokrasia na ndio iliyomfikisha hapo alipo na kuwa mtu wa kwanza mweusi duniani kuwa rais Wa Marekani.
 
Marekani walikuwa na mgogoro wao mkubwa sana wa kiuchaguzi (Al Gore vs. George W. Bush) mwaka 1999/2000.

Hivi waMarekani waishio Tanzania waliandamana mpaka Magogoni kwa Mkapa kushinikiza Al Gore apewe ushindi?

Mbona tunauendeleza huu utumwa jamani?

Mara tumekimbilia ikulu ya Marekani, mara ikulu ya Uingereza? Si afadhali haya maandamano yangekwenda Umoja wa Mataifa New York au Geneva ningeelewa? Tumekuwa kama watoto jamani. Ukisukumwa kidogo unakimbia kwa mama kulia na kulalamika.

Ya Rabbi, tutakuja jitawala lini sisi waMatumbi? Dooo!
 
Kifyatu

Unaweza kulinganisha kati ya Marekani na Tanzania? Ni lini USA ilishawahi kuomba misaada Tanzania? Halafu kikwete ameenda USA zaidi ya mara 20, yeye Obama alikuja mara ngapi hapa?
 
Enhee endeleeni na mjadala maana nafuatilia kwa ukaribu kujua haki ya wazanzibari kupata kiongozi waliomchagua kupitia sanduku la kura
 
Unaweza kulinganisha kati ya Marekani na Tanzania? Ni lini USA ilishawahi kuomba misaada Tanzania? Halafu kikwete ameenda USA zaidi ya mara 20, yeye Obama alikuja mara ngapi hapa?

Unadhani Marekani wataifanya nini Tanzania kama imeamua kurudia uchaguzi wa Zanziabar? Yaani hujui maana ya nchi huru? Kila siku kulialia kwenye mataifa ya magharibi kwa vijitatizo vidogo vidogo?

Hapa sio kuwa Zanzibar imepinduliwa. Tume yao wenyewe (ZEC) imefuta uchaguzi na kutaka urudiwe. Marekani wanaambiwa hili ili wafanye nini?

Hivi haya mawazo ya kitumwa jamani bado wengine wanayo tu?
 
Tume imefuta uchaguzi baada ya jeshi la kivamizi la Tanganyika JWTZ kuzingira kituo cha matangazo na kuondoka na mwenyekiti wa tume ambaye record ya video ya kuufuta uchaguzi ilionyeshwa kwenye tv .

Mpaka wakati huu Mwenyekiti wa Tume yuko chini ya ulinzi wa WAVAMIZI kutoka Tanganyika
 
Kukubali Demokrasia ya vyama vingi ni pamoja na kukubali matokeo ya uchaguzi.....haikubaliki demokrasia ya Zanzibar ni pale tu CCM inaposhinda kwamba wao wakishindwa wanafuta uchaguzi....

Ni sawa na watu wawili wanaocheza mchezo wa 'chess'.... halafu kwa sababu mmoja kati yao ameona ameshashindwa, yaan 'CHECKMATE', hana kete ya kuikwepa, anaona avuruge mchezo waanze upya......bila kujali maslahi ya watazamaji waliolipia mchezo(wapiga kura)......

Marekani kihistoria ni nchi inayosimamia misingi ya demokrasia nje ya mipaka yake.....na Wazanzibari wamefanya jambo la msingi kupeleka ujumbe kwenye jumuiya ya kimataifa kuhusu jaribio la ukiukwaji wa demokrasia Zanzibar.....

Ni watanzania wachache sana hasa ambao wanaongozwa na ushabiki sio fikra huru wanaoweza kukubaliana na kilichofanyika Zanzibar......
 
Sioni point ya wao kwenda White House USA.
Marekani washatoa tamko inatosha kabisa, walichokifanya hawa jamaa ni pointless na very stupid.
Inazidi kuonyesha wabongo jinsi gani kichwani hazimo, siamini wamekaa wakakubaliana kabisa ati wakaandamane white house ya US..
 
CCM wanasema busara zinatumika 'kutatua mgogoro wa Zanzibar'......vichekesho vya mwaka...Kuna busara gani zaidi ya kukubali matokeo kuwa wameshindwa uchaguzi?

Kama kuna mgogoro ni huo uliotengenezwa na CCM baada ya kushindwa uchaguzi Zanzibar.....Rasilimali zinapotea bila sababu za msingi 'kutatua mgogoro' ambao ni UJINGA wa CCM....

Tamko halitoshi bila utekelezaji, Jumuiya ya kimataifa inaombwa ishinikize serikali ya Magufuli 'kutatua mgogoro' wa Zanzibar haraka iwezekanavyo.....Wazanzibari wapate wawakilishi wao na Rais wao mpya (Seif).....
 
Sioni point ya wao kwenda White House USA.
Marekani washatoa tamko inatosha kabisa, walichokifanya hawa jamaa ni pointless na very stupid.
Inazidi kuonyesha wabongo jinsi gani kichwani hazimo, siamini wamekaa wakakubaliana kabisa ati wakaandamane white house ya US..

kuna wengi wamesikia kwenye vyombo vya habari baada ya haya maandamano na wanahamu kujua kuhusu zanzibar na tz na wanataka kujua ukweli kuhusu huu uitwao muungano ambao wameanza kugundua kuwa ni uvamizi
 
Hapo ndio tutaona usiriasi wa mmarekani na jinsi anavyo iheshimu demomrasia.

Mara nyingi tumezoea kumsikia Mmarekani akitetea haki za mashoga zaidi hadi inafikia hatua kuziwekea vikwazo baadhi ya nchi kisa zimekataa ushoga na wakati huo amesahau maswala ya msingi kama demokrasia na inabidi Obama ajue umuhimu wa demokrasia na ndio iliyomfikisha hapo alipo na kuwa mtu wa kwanza mweusi duniani kuwa rais Marekani.

Unachanganyikiwa kweli.....Hao jamaa hata bararaka ya karibu ya whitehouse hawawezi kukaribia wengi watakuwa waishi with false Identification....... ukitilia maanani ISIS wanavyoisumbua USA sasa hivi....Mr President hawezi kudili na taka taka hiyo....... waende huko oman kwa sultan!
 
Marekani walikuwa na mgogoro wao mkubwa sana wa kiuchaguzi (Al Gore vs. George W. Bush) mwaka 1999/2000.

Hivi waMarekani waishio Tanzania waliandamana mpaka Magogoni kwa Mkapa kushinikiza Al Gore apewe ushindi?

Mbona tunauendeleza huu utumwa jamani?

Mara tumekimbilia ikulu ya Marekani, mara ikulu ya Uingereza? Si afadhali haya maandamano yangekwenda Umoja wa Mataifa New York au Geneva ningeelewa? Tumekuwa kama watoto jamani. Ukisukumwa kidogo unakimbia kwa mama kulia na kulalamika.

Ya Rabbi, tutakuja jitawala lini sisi waMatumbi? Dooo!

Marekani ndo umoja wa mataifa,chunguza kiundani utaelewa tu.
 
Tume imefuta uchaguzi baada ya jeshi la kivamizi la Tanganyika JWTZ kuzingira kituo cha matangazo na kuondoka na mwenyekiti wa tume ambaye record ya video ya kuufuta uchaguzi ilionyeshwa kwenye tv .

Mpaka wakati huu Mwenyekiti wa Tume yuko chini ya ulinzi wa WAVAMIZI kutoa Tanganyika

Nani kawashikia waZanzibari mtutu kichwani kuwa uchaguzi ukirudiwa leo wasipige kura walivyofanya awali?

Mimi sijui sheria na KATIBA ya Zanzibar lakini nijuavyo mimi ni kuwa tume ya uchaguzi, ZEC, imesema imeona madudu kwenye uchaguzi uliopita na imetaka uchaguzi urudiwe.

Kwa sasa hivi pande zote zenye malalamiko ziko kwenye majadiliano ya usuluhishi. Hili la kuzungumzia majeshi ya kivamizi ya Tanganyika ni upuuzi mtupu. Yaani waZanzibari mnajisikia mpo karibu zaidi na Oman kuliko Tanganyika? - Eti raia wa Oman walifurahi sana!
  • Leo watu wanakwenda ikulu ya Marekani kuandamana ili Marekani iifanye nini Tanzania?
  • Je, mazungumzo ya usuluhishi yameshindikana kutatua hili tatizo?
  • Marekani ni nani katika muundo na Katiba ya serikali ya Zanzibar?
  • Ni kipi tusichoweza kukizungumza na kuelewana katika lugha yetu ya Kiswahili mpaka tuwaite waMarekani?
  • Kwa nini tusiwaite Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Ghana badala ya Marekani na Uingereza?
  • Hiki kiherehere cha kukimbilia nchi za magharibi chanzo chake ni kipi?

Nina maswali mengi najiuliza kwa hili na nakosa majibu. Matatizo tunayo - ndio, lakini hivi hatuwezi kukaa na kupata suluhu sisi wenyewe mpaka tukimbilie kwa "mabwana" zetu huko ulaya? This is pathetic.
 
Sioni point ya wao kwenda White House USA.
Marekani washatoa tamko inatosha kabisa, walichokifanya hawa jamaa ni pointless na very stupid.
Inazidi kuonyesha wabongo jinsi gani kichwani hazimo, siamini wamekaa wakakubaliana kabisa ati wakaandamane white house ya US..
Ila ccm sio stupid kwenda na bakuri USA kuomba misaada.Tumia ubongo kufikiri sio makalio
 
Marekani walikuwa na mgogoro wao mkubwa sana wa kiuchaguzi (Al Gore vs. George W. Bush) mwaka 1999/2000.

Hivi waMarekani waishio Tanzania waliandamana mpaka Magogoni kwa Mkapa kushinikiza Al Gore apewe ushindi?

Mbona tunauendeleza huu utumwa jamani?

Mara tumekimbilia ikulu ya Marekani, mara ikulu ya Uingereza? Si afadhali haya maandamano yangekwenda Umoja wa Mataifa New York au Geneva ningeelewa? Tumekuwa kama watoto jamani. Ukisukumwa kidogo unakimbia kwa mama kulia na kulalamika.

Ya Rabbi, tutakuja jitawala lini sisi waMatumbi? Dooo!

wamefanya hvo kwa sababu marekani ndio muasisi na msimamiz wa siasa za kidemokrasia
 
unachanganyikiwa kweli.....hao jamaa hata bararaka ya karibu ya whitehouse hawawezi kukaribia wengi watakuwa waishi with false identification....... Ukitilia maanani isis wanavyoisumbua usa sasa hivi....mr president hawezi kudili na taka taka hiyo....... Waende huko oman kwa sultan!

ndivyo anavyowadanganya pengo ??
 
Back
Top Bottom